ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 26, 2011

BONGO FLEVA NA DJ FETTY

Ni show ya muziki wa kizazi kipya iliyosimama hakuna mfanowe, inayo ruka kila jumamosi saa sita kamili mchana hadi tisa alasili ndani ya Clouds fm, hakuna ubishi kuwa hii ni namba wani show ya bongo fleva nchini: TUKOMEE HAPO:: pichani mdadada anaitwa Dj Fetty.

On the one and two anasimama Dj Steve B' aka skillz

VIP SIDE THE PLACE YOU CAN FIND ME 2night....

Wajua ninachozungumzia Yes! ni Hicho hicho Tukutane pale! pale!

HAPA WAPI-zzZZZ?

Ni usiku ndani ya jiji la Dar es salaam je waweza nambia niko wapi au barabara gani eneo hili pichani?

HUKO LIBYA HAPATOSHI MAADUI WAVAMIA MIJI MUHIMU MAJESHI YA GADDAFI HAPUMUI

Walioshuhudia wamesema waasi wa Libya wanakaribia kupambana na majeshi yanayomtii Kanali Gaddafi kwenye mji wa Ajdabiya.Ndege za Ufaransa na Uingereza zimerusha mabomu karibu na mji ulio mashariki mwa nchi hiyo wakati wa usiku, yakiwemo makombora ya serikali.

Waasi walijaribu kuwashambulia wanajeshi wanaomwuunga mkono Gaddafi baada ya kufanyika mashambulio ya ndege, lakini walisema ilibidi waghairi.

Mji huo umezingirwa kwa siku kadhaa sasa. Wakazi waliokimbia walisema mitaa ilibaki mitupu, na majeshi ya serikali yalikuwa yakifyatua risasi kiholela.

Majeshi ya nchi za magharibi yalianza kushambulia kwa mabomu wiki iliyopita kwa nia ya kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa lililozuia majeshi ya Libya kuwashambulia raia kwa ndege.Majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato yanatarajiwa kuongoza harakati hizo za kijeshi badala ya Marekani kwa siku zijazo.

Maafisa wamesema uvamizi huo umedhoofisha majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi kwa kiwango kikubwa, lakini mapigano yameendelea Misrata kwa upande wa magharibi na Adjabiya huko mashariki.

ALIYEKIRI KUUWA WATU SABA AUHUKUMIWA KIFO

Mwanaume mmoja nchini Japani aliyekiri kuwaua watu saba jijini Tokyo, mwaka 2008 kwa kuendesha gari kwa kasi kwenye mtaa wa watu wengi na baadaye kutumia kisu kikali kuwamaliza wengine amehukumiwa adhabu ya kifo.

Tomohiro Kato aliendesha gari kwa kasi katika eneo la watembea kwa miguu katika mji wa kibiashara wa Akihabara uliopo katikati ya jiji la Tokyo na kupoteza maisha ya watu watatu pale pale. Kisha akatoka garini akiwa na kisu kikali na kuanza kuwachoma watu ovyo na kuwauwa watu wengine wanne .Wakati wa kesi yake, Kato mwenye miaka 28 alisema kuwa alichukizwa na unyanyasaji uliokuwa ukifanywa kwenye mtandao lakini kilichofanya Mahakama Kuu ya wilaya ya Tokyo imuhukumu kifo ni matamshi yake kuwa “Yeye anahusika na alifanya kwa makusudi shambulizi hilo lililouwa watu.

Jaji Hiroaki Murayama alisema kuwa mtu huyo aliwashambulia kwa kisu mtu yoyote aliyemsogelea baada ya kuzungukwa na hivyo kuleta mazingira yaliyohatarisha maisha ya watu ambao hawana hatia.Alisema kuwa ni tendo la jinai lililo na ukatili mkubwa.
“Sina kingine cha kuchagua zaidi ya kumuhumu adhabu ya kifo” , alisema Murayama.


KWAHISANI YA MIRINDIMO.

Friday, March 25, 2011

MKUTANO WA ELIMU YA URAIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI WAFANYIKA DAR ES SALAAM HII LEO NA KUJA NA MAAZIMIO MAPYA YA MSINGI.

Mkutano juu ya elimu ya uraia kupitia vyombo vya habari hususani Radio na Luninga za vijijini umefanyika leo katika ukumbi wa Hotel Blue Pearl, jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau wakutosha toka pande na pande hapa nchini.

Juma Nyumano wa Radio Maria/Jogoo toka Mtwara.

Mkutano huo umeazimia kuanzishwa kwa mtandao wa kupashana habari na wanajamii, pia mkutano Umeshauri kuwa wataalam wa sheria wahusishwe kutoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya jinsi ya kuchambua mapungufu ya katiba katika mchakato uliopo sasa wa marekebisho ya katiba.

Rachel Mabihya Mwakilishi wasikilizaji toka Sengerema, Mwanza.

Kutokana na mvuto walio nao Wasanii watumike katika kutoa elimu kuhusu katiba, wanawake wajiendeleze kiuchumi, vilevile vipindi maalum vya masuala ya jinsia vianzishwe kwenye radio na tv za jamii.

Wawasilisha mada kutoka kushoto Rose Haji na Sebastian Sanga.

Inatajwa kuwa asilimia 1 ya wananchi wanatumia mtandao wa Internet, asilimia 5 television na kuna maeneo mengine magazeti yanachukuwa zaidi ya siku mbili kufikia wasomaji hivyo kuchelewesha upatikanaji wa taarifa na habari hali inayopelekea wananchi kuishi katika mazingira ya habari za uvumi.

Kamati ikijadili mara baada ya mkutano kumalizika.

Mmkutano huo ulihitimishwa kwa kuundwa kamati ya kufuatilia na kuhakikisha yanafanyiwa kazi mambo yaliyoibuka ndani ya mkutano huo.

Thursday, March 24, 2011

MAADHIMISHO YA KIFUA KIKUU KITAIFA MKOANI MARA LEO

Blogu hii inaongeza kuwa;-"Kufahamu mambo mbalimbali kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu ni msingi thabiti katika kupambana na kifua kikuu"

KUTOKA PEMBA - KUTANA NA MPEMBA HALISI.

Kama u-mmoja kati ya wahudhuriaji wa mara kwa mara wa mikutano na makongamano mbalimbali hata ile ya kisiasa jina 'Mpemba Asili' bila shaka utakuwa unalipata.Huyu ni mshairi kutoka Wete Pemba kijiji cha Ole nae akiishi na kufanya kazi mjini Dodoma kama mwelimishaji kwa njia ya mashairi kwa kuzingatia majanga kama Ukimwi, Rushwa, Umaskini, Madawa ya kulevya, Afya bora kwa jamii, Utunzaji mazingira na Kuelimisha wa Tanzania kujitambua.

Anasema amejitahidi sana kuwarithisha vijana wengi kipaji alichonacho cha utunzi wa ushairi lakini wengi imekuwa UTATA...

MPEMBA ASILI ANAKETI NA WATU WA RIKA ZOTE USISHANGAE KUMWONA KWENYE VIJIWE VYA:-

WATOTO = kujua ladha ipendwayo na njia fupi ya kuifundisha haraka jamii ikaelewa.

VIJANA = dunia na maendeleo yake.

MASELA = misemo ya kisasa ya mtaani inayopenyeza ujumbe kirahisi.

WAZEE = hekima, busara na lugha fasaha.

Huyo ni 'Mpemba Halisi'

Wednesday, March 23, 2011

UJUMBE WA LEO LEO....

tEHe...gUSa uNATe!

SERENA LODGE ....

Serena Hotel na vyumba vyake asili ya mwafrika vyenye huduma zote.

Swimming pool iliyotengwa karibu na bonde ambako kwa kutumia kiona mbali aka darubini utapata fursa kujionea wanyama ndani ya hifadhi.

Wataalam wanauita Baobab tree kwa lugha ya mama (kiswahili) twauita Mbuyu ...

Habari yake ndiyo hii.

Nikichungulia kubaini...

Na hiyo ndiyo njia kutoka jijini arusha inayopita vijiji kadha wa kadha mpaka kufika hoteli hii ya kitalii.

Hapo hapo hotelini kuna hawa ndugu.

HAPPY BIRTHDAY YA KUZALIWA REUBEN NDEGE

Leo ni siku ya kuadhimisha miaka kaadha ya kuzaliwa kwake Reuben Ndege wa Clouds Media Group, Wengi wakimtambua kama Nchakali aka Mzeeeyaa!! anayesomeka mwanzo mwisho ndani ya program lenye fuul ditelZ za Mastaa, Muziki na wanamuziki duniani Soso Fresh, at the same time ndiye anayeng'arisha kipindi cha kijanja ndani ya clouds radio XXL katika segment ya 255.

Blogu hii inaomba mkono wa baraka toka kwa Mwenyezi Mungu kwa kila kilicho chema ukigusacho.
HAPPY BIRTHDAY BROTHER.

MAADHIMISHO WIKI YA MAJI KITAIFA MWANZA

MAKAMU wa Rais , Dk. Mohamed Ghalib Bilal, jana alimezindua mradi wa maji vijijini wenye thamani ya Sh. Bilioni 19 utakaowanufaisha wakazi wa vijiji 44 vilivyopo katika mikoa ya Mwanza na Mara .

Awali akizindua mradi wa maji vijijini ambao umefadhiliwa na Serikali ya Japan, katika kijiji cha Hungumalwa kilichopo katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, amesema wananchi watakaofaidika nao wautunze ili kuhakikisha unakuwa endelevu kwa ajili yao na vizazi vijavyo.

Mh.Bilal akipata maelezo ya nyenzo maalum ya kuchuja maji kwa gharama ndogo (Tulip Water Filter) toka kwa mtaalam wa USAID.

SIMBA PIPE LINE.
Serikali ya Japani imetoa Yen bilioni 1.022 sawa na Sh. Bilioni 19.012 za Kitanzania kwa ajili ya kufanikisha mradi huo wa maji vijijini,na utaongeza watumiaji wa maji safi na salama katika vijiji 44 vilivyopo katika mkoa wa Mwanza na Mara.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya amesema hadi mradi huo utakapokamilika jumla ya visima virefu 182 vinavyotumia pampu za mikono vitachimbwa, hadi sasa vimeshachimbwa visima 116, ambavyo vimeshakamilika.

Maswi Drilling co.ltd nao waliwakilisha vyema viwanjani hapo.

Nje ya banda hili "Za sahizi" Kisha akasepa....

Tanzania breweries ltd (TBL) katika maadhimisho haya wameziwezesha shule nyingi mkoani Mwanza kupata maji safi na salama kwa kuchimba visima na kutoa mashine mbalimbali kwaajili ya urahisishaji wa upatikanaji maji.

Anaitwa Victor Maleko, Blogger maarufu toka rock City, Hapa inasakwa engo.....

Samaki ndani ya maji katika siku ya maji kwenye banda la Uvuvi.

Maadhimisho ya 23 ya wiki ya maji yamehitimishwa jana katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo Dk. Bilal ametoa vyeti na vikombe kwa washiriki na washindi mbalimbali waliokuwa na mabanda kwenye uwanja huo kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa kwa jamii.

Tuesday, March 22, 2011

HATIMAYE MAJINA YA WANAMUZIKI FIVE STAR MODERN TAARAB YAFAHAMIKA.

Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini .

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini. "Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed (27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma (25), Rajabu Kondo(25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa (22).

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.


KWA HISANI ya John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

MCHUNGAJI MWASAPILE KUHAMISHA UTOAJI TIBA

Na:Kizitto Noya na Venance George,Loliondo
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapile amesema hivi karibuni atahamisha utoaji wa tiba katika eneo analoishi sasa na kwenda sehemu ambayo itakuwa na nafasi kubwa zaidi, kwa lengo la kupanua huduma na kubadilisha mazingira anayoishi.
Akizungumza juzi mchana kijini hapo, mchungaji huyo alisema yeye si mganga wa kienyeji, bali anatibu kwa miujiza ya Mungu na kusisitiza kwamba ili mgonjwa apone anatakiwa kuwa na imani katika huduma hiyo.

“Kwa wale wanaoumwa Ukimwi wanapokunywa dawa hii wanapona kabisa. Tiba itaanza kujidhihirisha ndani ya siku saba. Lakini wadudu hata kama bado watakuwapo, hawatakuwa na nguvu na katika kipindi cha miezi mitatu, wadudu wote watakufa kabisa.

Kwa wale wenye kansa, dawa inamaliza kabisa tatizo hilo, dawa hii inaponya kichaa, kifafa na magonjwa mengine ambayo mgonjwa atataka apone."Idadi ya wagonjwa wanaomiminika kwa Mchungaji Mwasapile inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Wengi wanailalamikia Serikali kwa kushindwa kumsaidia mchungaji huyo kuboresha mazingira ya utendaji kazi wake. Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri tiba hiyo, Sara Ibrahim alisema: "Huduma ni nzuri lakini hakuna ulinzi wa maana. Hakuna 'ambulance' (gari la wagonjwa), watu wanafia kwenye magari kwa kukosa msaada wa karibu kuwafikisha kwa mchungaji. Tunaiomba Serikali isaidie huduma hiyo pia kwa kujenga vyoo, kusambaza maji na kutoa jenereta."

Licha ya malalamiko hayo, barabara ya kufika huko inazidi kuharibika na kusababisha mamia ya wagonjwa na jamaa zao kukwama porini. Zaidi ya abiria 600 waliokuwa wanatoka Arusha kwenda huko wamekwama umbali wa kilometa 306 kutokana na ubovu huo.

Barabara ya Arusha kwenda Loliondo, hasa katika Kijiji cha Samunge anakofanyia matibabu mchungaji huyo itaendelea kuwa mbaya kiasi cha kukosa mawasiliano kabisa katika siku za hivi karibuni kama hakutakuwa na jitihada za kuitengeneza.

Mmoja wa wagonjwa, Anna Ibrahim alisema: "Kila gari linalofika Samunge linatozwa Sh2,000 lakini barabara bado ni mbovu na hatujui fedha hizo zinakwenda wapi? Serikali inatakiwa itumie kodi yetu kutuletea maendeleo,” alisema. Hadi kufikia juzi, idadi ya magari yanayopeleka wagonjwa kwa Mchungaji Mwasapile yanakadiriwa kufikia 40,000.

Akizungumzia ongezeko hilo la wagonjwa wanaokwenda kwake kupata tiba, Mchungaji Mwasapile alisema hiyo ni sehemu tu ya watu watakaotoka maeneo mbalimbali duniani kuifuata huduma hiyo kwake... "Watu wataendelea kufurika hapa kutoka kila pembe ya dunia na maajabu ya Mungu yataendelea kujionyesha."


KWA HISANI YA www.mwananchi.co.tz

KUNDI LA MUZIKI WA TAARAB FIVE STARS LAPATA AJALI MBAYA WANAMUZIKI 13 WAFARIKI DUNIA.

Ajali mbaya ya gari imetokea jana usiku katika Mya Mikumi. Ajali hiyo imehusisha gari aina ya coaster lililokuwa limewabeba wanamuziki wa bendi ya muziki wa Taarab ya Five Star Morden Taarab na kusababisha vifo vya wanamuziki 13 wa kundi hilo akiwemo muimbaji maarufu wa kiume Issa Kijoti.

Marehemu Issa Kijoti enzi za uhai wake.

Gari hilo lilikuwa na jumla ya watu 22. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali inadaiwa kuwa gari hilo lilikuwa kwenye mwendo mkali likijaribu kuovateki na hatimaye kugonga roli lililokuwa limepakia mbao pembeni mwa barabara. Miili imeheribika vibaya sana kiasi cha kusababisha zoezi la utambuzi kuwa gumu.

Mwanahawa Ally yu mmoja kati ya wanusurika wa ajali hiyo aliye ambatana na kundi hilo kama msanii mwalikwa wakitokea mjini Songea ambako walikuwa kwenye ziara yao ya kimuziki na walifanya onyesho lao juzi hivyo jana wakawa wakirejea jijini Dar. Anasimulia kuwa kwa bahati mbaya walipofika maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro basi lao likapata ajali, naye akijeruhiwa mkono na kupata majereha kadhaa kichwani na sehemu nyingine za mwili.

Taarifa zaidi tutaendelea kukupatia kadri zinavyotufikia,
Pole 5stars Morden Taarab Pole Tanzania.
@ALBERT G. SENGO.

Monday, March 21, 2011

NDIYO MAANA AJALI HAZIISHI.

Huku gari ikiwa katika mwendo, macho kwenye simu akichati na simu mbili, Ni dereva wa basi dogo la abilia maarufu kama daladala inayotoa huduma njia ya Nyasaka hadi Igoma kupitia Nyakato Mecco jijini Mwanza .

BARABARA YA SINGIDA, ARUSHA KIMEO

Tumetumia muda wa zaidi ya masaa mawili kupisha matengenezo ya daraja la eneo la Kaeteshi ili tupate kuvuka upande wa pili.Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini hali ya usafiri na usafirishaji kwa magari yatumiayo barabara kuu ya Singida – Babati hadi Minjingu mkoani Arusha imekuwa tete kwa baadhi ya vipande kuwa na utelezi wa tope jingi pamoja na baadhi ya madaraja kuharibika vibaya na hivyo kukwamisha shughuli za usafirishaji na uchumi.

Baadhi ya madereva wametoa ushauri kwa wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kuyakarabati maeneo korofi nyakati za usiku kwani muda huo kunakuwa na magari machache hivyo kuepusha adha ya msongamano wa magari inayojitokezwa nyakati za pilika, mazungumzia mchana.

Barabara halisi kama inavyoonekana ipo kwenye matengenezo kufikia kiwango cha lami hivyo inayotumika kwa sasa ni ya muda mfupi imechongwa tu kwa katapila pembeni yake.

HALI HALISI
Aidha wameiomba serikali kuidhibiti mapema hali mbaya ya barabara hiyo kabla mvua zaidi kunyesha hali inayoweza kusababisha zoezi la ukarabati kuwa gumu zaidi, Mpaka sasa maeneo yaliyoathiriwa vibaya na mvua hizo ni pamoja na Katesh na Dareda.

Benki ya Maendeleo ya Afrika imetenga shilingi bilioni 210 kukamilisha ujenzi wa barabara hii ulioanza mwaka 2008 na unaotegemewa kukamilika mwezi wa 8 mwaka huu, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kugharamia ujenzi wa barabara zetu kwa nia ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, kuondoa umaskini na kuboresha hali ya maisha .