ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 21, 2011

BARABARA YA SINGIDA, ARUSHA KIMEO

Tumetumia muda wa zaidi ya masaa mawili kupisha matengenezo ya daraja la eneo la Kaeteshi ili tupate kuvuka upande wa pili.Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini hali ya usafiri na usafirishaji kwa magari yatumiayo barabara kuu ya Singida – Babati hadi Minjingu mkoani Arusha imekuwa tete kwa baadhi ya vipande kuwa na utelezi wa tope jingi pamoja na baadhi ya madaraja kuharibika vibaya na hivyo kukwamisha shughuli za usafirishaji na uchumi.

Baadhi ya madereva wametoa ushauri kwa wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kuyakarabati maeneo korofi nyakati za usiku kwani muda huo kunakuwa na magari machache hivyo kuepusha adha ya msongamano wa magari inayojitokezwa nyakati za pilika, mazungumzia mchana.

Barabara halisi kama inavyoonekana ipo kwenye matengenezo kufikia kiwango cha lami hivyo inayotumika kwa sasa ni ya muda mfupi imechongwa tu kwa katapila pembeni yake.

HALI HALISI
Aidha wameiomba serikali kuidhibiti mapema hali mbaya ya barabara hiyo kabla mvua zaidi kunyesha hali inayoweza kusababisha zoezi la ukarabati kuwa gumu zaidi, Mpaka sasa maeneo yaliyoathiriwa vibaya na mvua hizo ni pamoja na Katesh na Dareda.

Benki ya Maendeleo ya Afrika imetenga shilingi bilioni 210 kukamilisha ujenzi wa barabara hii ulioanza mwaka 2008 na unaotegemewa kukamilika mwezi wa 8 mwaka huu, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kugharamia ujenzi wa barabara zetu kwa nia ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, kuondoa umaskini na kuboresha hali ya maisha .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.