ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 12, 2013

TWENDE TUKALE WIKIENDI...

Eh bana wikiendi wapi wadau?
Tutatokaje?
Na nani?
Na tutaendaje?
Tuta kula nini?
Oyaaa wadau zingatieni ustaarabu...!!
Wikiendinjema.

SOMA KILIO CHA MACHOZI YA DAMU CHA BAADHI YA WANASAUTI MWANZA WAKILIA KUSALITIWA

By kijungu jiko View Post

Malisa Godlisten Rais wa Serikali ya WanafunziSAUTSO Chuo kikuu cha St Augustine umetudharirisha mpaka tunaona aibu sasa na vuguvugu la CHADEMA, tena tuliingia kwa mbwembwe kali kuwa tutakuwa wakombozi wa watu, waliotuchagua kwa kura nyingi richa ya kuwepo nguvu kubwa ya viongozi waliotangulia hasa Rais Bwana Cosmas Mataba na Anna Mushi, Spika wa Bunge Bw Maro Pius, na aliyekuwa Waziri mkuu Bw Leonard Mafuru, tukamchagua kijana huyu aliedaiwa machachari akitokea Baraza la vijana la CHADEMA yani BAVICHA kwa kishindo cha zaidi ya asilimia 75% licha ya hira za Mataba na Tume yake ya Uchaguzi, tukashinda uchaguzi kwa mbwembwe kabisa tukimtupilia mbali mgombea aliefadhiriwa kwa gharama kubwa na CCM Bwana Antony na Mgombea mwenza Bibie Alice, tuliingia huku wanafunzi wakiwa na matumaini makubwa ya kuona mabadiriko kufuatia manung’uniko ya serikari ilio tangulia ya Bwana Mataba, Maro na Mafuru kutuhumiwa kwa ufisadi, ubadhirifu Ngono na matumizi mabaya ya ofisi na kupeana madaraka ya SAUTSO (Maro na Mataba wanadaiwa kuongoza serikali hiyo ya 2011/2012 kwa ubia wa makubaliano maalum…. Source kinasa sauti cha siri kilichomrekodi Bwana Maro kwa siri na vijana wa CHADEMA nyumbani kwake Nganza). Tuliingia tukiwalaumu wenzetu waliotutangulia lakini kwa mtazamo wa haraka hakika wao na sisi wana unafuu mkubwa wa kukumbukwa, hakuna kilichofanyika wala kubadilika, Ahadi zote tulizo ahidi mpaka wakati huu tunapoelekea kufanya uchaguzi tena hakuna dalili kuwa tutafanya chochote,

Tumeshindwa kabisa kutekeleza ahadi zifuatazo:-
1. Tuliahidi kujenga kutuo cha polisi katika jamii hii ya watu zaidi ya 26,000 ili kupambana na vitendo vya ubakaji wa dada zetu katika maeneo tofauti ya vuinga vya chuo hiki tumeshindwa.
2. Tuliahidi kuhamia kwenye ofisi mpya za SAUTSO ili kuongeza ufanisi wa shughuri zetu mpaka sasa hivi haifahamiki mradi huo umeishia wapi.
3. Tuliahidi kupambana na matatizo ya mikopo kwa wanafunzi lakini hakika hivi sasa tuna matatizo makubwa katika idara ya mikopo kuliko hata wakati wa Mataba, mikopo inachelewa, majina yanachanganyika, na mpaka hivi sasa kuna watu hawajaona mkopo since waje mwezi September.
4. Tuliahidi kuanzisha utaratibu wa kutunza kumbukumbu za kudumu lakini hilo limeshindikana.
5. Tuliahidi kurekebisha miundo mbinu ambayo sio rafiki kwa wenzetu wenye changamoto ya viungo sijui tumeishia wapi.
6. Bunge limekuwa genge la malumbano, migawanyiko, makundi ya urais ujao, na mijadara ya miradi isiyotekelezeka,
7. Umeme madarasani bado na viongeza sauti bado ni kero.
8. Unyanyasaji wa kimapenzi umekithiri hasa kwa viongozi wa kike pale SAUTSO.
9. Kuna serikali ya siri ya Bw Tungaraza ndani ya serikali ya Bw Malisa,
10. Migawanyiko iliyotokana na maslahi binafsi na uroho wa fedha umezidi.
11. Ubadhirifu wa pesa umeongezeka na pesa zinaishia kwenye mikono ya mabosi wachache wa SAUTSO.
12. Bwana Malisa mwenyewe anaongoza kwa matumizi mabaya ya fedha za wanafunzi, amesafiri zaidi kwa Ndege hata zaidi ya Bwana Mataba na Serikali yake, hakai ofisini, hatekelezi majukumu ya SAUTSO kwa wakati, wanafuzi wanalaumu kuwa muda mwingi pamefungwa, na wasaidizi wake wana kauri mbaya hasa idara ya mikopo, Malisa yuko busy facebook mara sijui naenda Lunch, nimepoteza simu, mara sijui najiandaa kupanda ndege, mara sijui natoka wapi naenda wapi je hiyo ndio spirit ya wana BAVICHA.
13. Tuliahidi Basi la SAUTSO mradi umeishia hewani bila maelezo.
14. Funga kazi ni kitendo cha aibu cha maandalizi ya michezo ya Vyuo vya SAUT kule Morogoro hali ilikuwa ni ya aibu, michezo mibovu, hakukuwa na motisha, zawadi hovyo, ugomvi, mazingira magumu, nilibahatika kupata taarifa kuhusu michezo ya aina hiyo ambayo ilifanyika Mtwara wakati wa Bw Mataba, yani ni mara Elfu kumi Tamasha la Mtwara, kulikuwa na msisimko, watu wengi, zawadi nzuri, malazi safi, chakula kingi, matibabu, michezo mingi, na Ratiba ya kueleweka, yani kilichofanyika Morogoro hakikuwa tofauti na Kombe la mbuzi kwenye shule Fulani za kata.
15. Chini ya Uongozi wa Malisa na wenzake Umoja wa vyuo vya SAUT Umekuwa na picha mbaya, pesa zilitafunwa, watu wakapigana, zawadi zikaibiwa, makombe yakachanganyikana, mgeni rasmi kwa aibu kubwa akapigwa na maganda ya ndizi, mayai viza na kondomu zilizotumika ebu pata picha hali ingekuwa nihiyo kule Mtwara ambapo mgeni rasmi alikuwa ni VC KITIMA mwenyewe na wakuu wengine wa SAUT Tanzania nzima.

Aliyetuponza mpaka hapa ni mambo ni mengi ila TUNGARAZA ametuponza pia kwa kujaribu kuingilia kwa siri kila jambo, Vijana wa BAVICHA tuliohusika katika harakati za kukuweka madarakani tumeishiwa na imani kabisa tunahitaji mabadiriko ya vijana wajao katika nafasi hizi tulijitoa kwa moyo na maisha yetu mpaka hata kufikia hatua ya kuweka masomo yetu hatarini kwa kupambana na viongozi waliotangulia Bw Mataba na wenzie kufanikisha hili ila tumekatishwa tamaa.

TUMECHOKA NEXT TIME BAVICHA TUNATAKA MABADIRIKO TUNAIDHARIRISHA CHADEMA KWAKWELI

SERIKALI INATEGEMEA KUONA MABADILIKO YA KIMAENDELEO KWA WAFUGAJI: ASEMA MKUU WA WILAYA YA MAGU.

Mkuu wa wilaya ya Magu Jaquelline Liana akifunga Warsha ya siku tatu kwa mafunzo ya Ufugaji Bora kwa wafugaji wa kata za Kahangala Na Nyigogo wilayani humo, mafunzo yakidhaminiwa na Kampuni mpya ya usindikaji nyama iliyoamua kuwekeza wilayani humo ya Alpha Choice LTD .


Nae Mkurugenzi wa wilaya ya Magu Mwl. Naomi Nnko ameushukuru uongozi wa Alpha Choice LTD kwa kudhamini utolewaji mafunzohayo kwani kupitia mafunzo hayo si kwamba wafugajihaowatapata elimu bali pia kutaongeza mahusiaano na ukuzwajiwa pato la Halmashauri ya wilaya kwa maslahi ya uchumi wa Taifa.


Bi. Mary Mashulano ambaye ni Afisa Mifugo upande wa ukaguzi wa nyama akiwaonyesha wafugaji moja ya vifaa maalum vya kukatia pembe na kwato wakati wa warsha ya siku tatu ya elimu kwa wafugaji iliyofanyika katika kata ya Kahangara wilayani Magu mkoani Mwanza.


Mmoja wa wafugaji akiuliza swali ili kupata ufafanuzi juu ya matumizi ya zana zilizoonyeshwa kupitia warsha ya siku tatu ya wafugaji iliyomalizika jana wilayani Magu , ikishirikisha wafugaji wa vijiji vya Bugabu na Kahangara vilivyo katika kata ya Kahangara na kijiji cha Ilungu kilichopo katika kata ya Nyigogo.


Wafugaji wakijadiliana na kunakili masualamuhimu ya kuzingatia.


Bi. Mary Mashulano ambaye ni Afisa Mifugo upande wa ukaguzi wa nyama akitoa darasa kwa wafugaji juu ya kanuni zilizo bora katika kuhudumia wanyamakupitia warsha ya siku tatu ya wafugaji iliyomalizika kwa mafanikio makubwa jana wilayani Magu, ikidhaminiwa na Kampuni mpya ya Usindikaji nyama ya Alpha Choice, ikishirikisha wafugaji wa vijiji vya Bugabu na Kahangara vilivyo katika kata ya Kahangara na kijiji cha Ilungu kilichopo katika kata ya Nyigogo .


Mtaalamu kutoka Halamashauri ya wilaya ya Magu akikokotoa hasara za matumizi mabaya ya dawa za kutibu na kujikinga maradhi kwa wanyama wafugwao, katika warsha ya siku tatu ya elimu kwa wafugaji iliyofanyika katika kata ya Kahangara wilayani Magu mkoani Mwanza.


Maelekezo ya matumizi halisiya dawa yalitolewa na wataalamu hao.


Picha ya pamoja kwa viongozi na wana warsha wa mafunzo ya Ufugaji Bora kwa wafugaji wa kata za Kahangala Na Nyigogo wilayani humo, mafunzo yakidhaminiwa na Kampuni mpya ya usindikaji nyama iliyoamua kuwekeza wilayani humo ya Alpha Choice LTD ..

Friday, January 11, 2013

DALADALA YAUA ABIRIA WA PIKIPIKI IGOMA.


Askari wa usalama barabarani wakipima ajali iliyotokea leo jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW ambapo dereva wake (ambaye ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa) alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea, inasemekana kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.

Kijana aliyefariki  alitambulika kwa jina la Mayunga Clement Lufuta.


Marehemu Mayunga Clement Lufuta.


Pikipiki hiyo yenye namba za usajili T988 BDW eneo lake la mbele limezama kabisa uvunguni mwa daladala kiasi cha kuharibika vibaya.


Baada ya trafiki kufanya upimaji gari la abiria (daladala) linalofanya safari zake Buzuruga hadi Sumve liliruhusiwa kutoka barabarani na kupaki pembeni kwaajili ya taratibu nyingine kufanyika ikiwa ni pamoja na kuuondoa mwili wa kijana huyo pamoja na pikipiki iliyopata ajali ili kupisha shughuli nyingine za usafirishaji barabarani kuendelea. 


Pikipiki iliyopata ajali ikiondoshwa barabarani kwa amri ya trafiki.


Kisha mwili wa marehemu Mayunga Clement Lufuta ukatolewa barabarani kusubiri gari maalum kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando kuhifadhiwa.


Kujulikana kwa jina la marehemu huyo kumekuja mara baada ya askari wa usalama barabarani kumpekua na ndipo walipokuta walet yenye vitambulisho mbalimbali kikiwemo kitambulisho cha mpiga kura. 

Hiki ndicho kitambulisho kilichosaidia kumtambua marehemu.


Wananchi wakiwa wameuzunguka mwili wa Mayunga Clement Lufuta aliyepoteza uhai kwa ajali iliyotokea leo jioni majira ya saa 10:25 eneo la Igoma jijini Mwanza.

MCHUNGAJI DANIEL NA HOYCE MBOWE WANAWAALIKA KWENYE IBADA YA PILI YA KISWAHILI ITAKAYONYIKA BONN: UJERUMANI

Mchungaji Daniel Mbowe (nyuma) na na mbele
ni dada Eva Machangu wakati akisoma somo
katika ibada iliyofanyika hivi karibuni.
Mchungaji Daniel na Hoyce Mbowe, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika Jumapili hii tarehe 13.01.2013 .

Muda wa Ibada: Saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours).
Mahali: Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn
Anuani: Franz-Bücheler-Straße 10
53129 Bonn
Ibada hii ya Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.
Mchungaji Hoyce Mbowe akitoa mahubiri katika ibada ya kwanza iliyofanyika Bonn, Ujerumani.
Mawasiliano: dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com
Wote mnakaribishwa: Karibuni tumwabudu na tumsifu Mungu wetu.

Thursday, January 10, 2013

CHEREKO CHEREKO LA HARUSI YA PROSPER NA MARYSTELLA

Bwana harusi Prosper Makene na mkwe Marystella Munissy wakiingia katika ukumbi wa Gedeco, Geita baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa katoliki la mtakatifu Bikira Maria wa Fatima lililopo Geita Mkoani Geita juzi. Bwana harusi ni mfanyakazi wa gazeti la The Guardian na Bibi harusi ni mfanyabiashara.

Bwana harusi Prosper Makene akimlisha keki mkewe Marystella Munissy baada ya ya kufunga pingu za maisha katika kanisa katoliki la mtakatifu Bikira Maria wa Fatima lililopo Geita Mkoani Geita juzi. Bwana harusi ni mfanyakazi wa gazeti la The Guardian na Bibi harusi ni mfanyabiashara.

Bwana harusi Prosper Makene akiwasalimia ndugu na jamaa katika ukumbi wa Gedeco uliopo mjini Geita, Mkoani Geita baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa katoliki la mtakatifu Bikira Maria wa Fatima lililopo Geita Mkoani Geita juzi. Bwana harusi ni mfanyakazi wa gazeti la The Guardian na Bibi harusi ni mfanyabiashara.

Bibi harusi Marystella Munissy akipewa dhawadi ya biblia takatifu na mama mkwe wake Mary Makene baada ya kufunga ndoa na Prosper Makene katika kanisa katoliki la mtakatifu Bikira Maria wa Fatima lililopo Geita Mkoani Geita juzi. Bwana harusi ni mfanyakazi wa gazeti la The Guardian na Bibi harusi ni mfanyabiashara.


PICHA ZOTE: RENATUS MASUGULIKO

MABONDIA DEO NJIKU NA OMARY RAMADHANI KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA February 14Rais wa PST Emanuel Mlundwa katikati akiwa na mabondia Deo Njiku kushoto na Omary Ramadhani  Dar es salaam jana baada ya kusaini mkataba wa kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese. 
Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkataba kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese.
www.superdboxingcoach.blogspot.com 

Wednesday, January 9, 2013

ALPHA CHOISE (RAFIKI WA MKULIMA) WATOA MAFUNZO YA SIKU 3 KWA WAFUGAJI WILAYA YA MAGU


Afisa Mifugo wa Wilaya ya Magu Dr.Faustine Msoke alianza warsha hiyo kwa kuainisha faida za mifugo katika warsha iliyoanza leo ikishirikisha wafugaji wa vijiji vya kata ya Kahangara na kufanyika katika kiwanda kipya cha kusindika nyama kilichopo Bugabu wilayani Magu mkoani Mwanza, chini ya ufadhili wa Alpha Choice. 


Katika kujadili mada isemayo 'Je ufugaji tunaojihusisha nao unafaa' Mambo mengi yaliibuliwa hapa na wafugaji hawa na iligundulika kuwa wengi wao:-
-Hawafugi vizuri ili kupata faida itakayowasaidia kuondokana na umasikini 
-Kwa nini hawafugi vizuri ile hali wanataka faida:- Ukosefu wa malisho ni kikwazo, ongezeko la mifugo, ukosefu wa elimu ya ufugaji bora, Ukosefu wa mbegu bora nao ni tatizo.
  
Afisa Mifugo wa Wilaya ya Magu Dr.Faustine Msoke akiendelea kutoa darasa ndani ya warsha hiyo, kulia kwake  ni Afisa Mifugo wa kata ya Kahangara Bi. Dinna Maurice Kasogela, na Zaid S. Mwinori ambaye ni Afisa Malisho wilaya ya Magu  


Pia wafugaji hawa ili waweze kutoa mazao bora na kujenga miili mizuri ya mifugo yao walipewa somo juu ya viini lishe sita  vitakavyofanya mifugo yao kuwa na viwango sahihi, walifundishwa juu ya chakula cha ziada kwa ng'ombe mwenye mimba na anayenyonyesha pamoja na utunzaji wa ndama baada ya kuzaliwa hasa yule anaye poteza mama mara baada ya kuzaa. (mama wa ndama huyo anapo kufa wakati wa kuzaa)


Wafugaji walipata nafasi kuuliza masali na kujadiliana.


Bwana Anthony Nyingi ambaye nimeneja msaidizi wa Kampuni ya Alpha Choice akijibu maswali toka kwa wafugaji juu ya viwango halisi vya bei ya mifugo kutokana na uzito tajwa kama anavyoainisha ubaoni sambamba na bei ya mbuzi na kondoo.
Mwenyekiti wa Warsha hiyo ambaye vilevile ni mfugaji bw. Paulo msambala mezani akigawa Karatasi zenye maelekezo tosha juu ya Ufugaji bora na Matunzo kwa mifugo pamoja na kanuni na mbinu za kumlinda mnyama dhidi ya maradhi na matibabu yake. 


Afisa Mifugo wa kata ya Kahangara Bi. Dinna Maurice Kasogela akiongoza msafara wa chakula kilichoandaliwa na Kampuni ya Alpha Choice kwaajili ya wafugaji wa kata yake kupata elimu. 


Wafugaji wa vijiji vya kata ya Kahangara wakiwa wamejumuika pamoja kwenye chakula na majadiliano chini kwa chini yakiendelea.


HILI NDILO KERO LA WAVUVI TANZANIA


Ingawa uvuvi ni mojawapo ya vyanzo vikuu vya mapato kwa watu wanaoishi kando kando ya Ziwa Tanganyika, matukio ya ujambazi yamekuwa yakitishia usalama wa wavuvi na wasafiri katika ziwa hilo Magharibi mwa Tanzania.
Polisi wanasema kazi yao inakuwa ngumu kutokana na ukosefu wa vitendea kazi na wamiliki kuajiri raia wa kigeni kinyume cha sheria.
Mwaka jana askari mmoja alipigwa risasi na kuawa katika mapambano na majambazi.
Mwandishi wa BBC Hassan Mhelela amefanya ziara Kigoma hivi karibuni alikotuandalia taarifa ifuatayo.
SHUKURANI KWA BBC SWAHILI.

BREAKING NEWS: BUS LA BUNDA EXPRESS LAUWA ENEO LA MAGU MWANZA

Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge Basi la abiria la 'Bunda express" lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza muda wa saa mbili asubuhi hii limepata ajali mbaya kwenye eneo hilo.

Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.


Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri.


Chanzo cha ajali kinatajwa kuwa ni mwendo kasi wa busi hilo.


Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao. 


Mpaka tunaenda mitamboni idadi ya watu waliopoteza maisha ni wawili na 36 majeruhi,
Watu 24 waliopata majeraha makubwa wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza
Na majeruhi 12 wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Magu. 


Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.


Baadhi ya nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu.

Hali ya baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na maji.


Barabara hali ya hewa na mazingira.