|
Afisa Mifugo wa Wilaya ya Magu Dr.Faustine Msoke alianza warsha hiyo kwa kuainisha faida za mifugo katika warsha iliyoanza leo ikishirikisha wafugaji wa vijiji vya kata ya Kahangara na kufanyika katika kiwanda kipya cha kusindika nyama kilichopo Bugabu wilayani Magu mkoani Mwanza, chini ya ufadhili wa Alpha Choice. |
Katika kujadili mada isemayo 'Je ufugaji tunaojihusisha nao unafaa' Mambo mengi yaliibuliwa hapa na wafugaji hawa na iligundulika kuwa wengi wao:-
-Hawafugi vizuri ili kupata faida itakayowasaidia kuondokana na umasikini
-Kwa nini hawafugi vizuri ile hali wanataka faida:- Ukosefu wa malisho ni kikwazo, ongezeko la mifugo, ukosefu wa elimu ya ufugaji bora, Ukosefu wa mbegu bora nao ni tatizo.
|
Afisa Mifugo wa Wilaya ya Magu Dr.Faustine Msoke akiendelea kutoa darasa ndani ya warsha hiyo, kulia kwake ni Afisa Mifugo wa kata ya Kahangara Bi. Dinna Maurice Kasogela, na Zaid S. Mwinori ambaye ni Afisa Malisho wilaya ya Magu |
|
Pia wafugaji hawa ili waweze kutoa mazao bora na kujenga miili mizuri ya mifugo yao walipewa somo juu ya viini lishe sita vitakavyofanya mifugo yao kuwa na viwango sahihi, walifundishwa juu ya chakula cha ziada kwa ng'ombe mwenye mimba na anayenyonyesha pamoja na utunzaji wa ndama baada ya kuzaliwa hasa yule anaye poteza mama mara baada ya kuzaa. (mama wa ndama huyo anapo kufa wakati wa kuzaa) |
|
Wafugaji walipata nafasi kuuliza masali na kujadiliana. |
|
Bwana Anthony Nyingi ambaye nimeneja msaidizi wa Kampuni ya Alpha Choice akijibu maswali toka kwa wafugaji juu ya viwango halisi vya bei ya mifugo kutokana na uzito tajwa kama anavyoainisha ubaoni sambamba na bei ya mbuzi na kondoo. |
|
Mwenyekiti wa Warsha hiyo ambaye vilevile ni mfugaji bw. Paulo msambala mezani akigawa Karatasi zenye maelekezo tosha juu ya Ufugaji bora na Matunzo kwa mifugo pamoja na kanuni na mbinu za kumlinda mnyama dhidi ya maradhi na matibabu yake. |
|
Afisa Mifugo wa kata ya Kahangara Bi. Dinna Maurice Kasogela akiongoza msafara wa chakula kilichoandaliwa na Kampuni ya Alpha Choice kwaajili ya wafugaji wa kata yake kupata elimu. |
|
Wafugaji wa vijiji vya kata ya Kahangara wakiwa wamejumuika pamoja kwenye chakula na majadiliano chini kwa chini yakiendelea. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.