ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 21, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA LISHE NA VIRUTUBISHO (ICN1) ROME ITALIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kushoto) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy. Picha na OMR
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho. Picha na OMR
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. Picha na OMR
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA KUHUSU LISHE NA VIRUTUBISHO JIJINI ROME, ITALIA NOVEMBA 21, 2014

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Novemba 19, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la 
Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome Italia. 

Mkutano huu umefanyika ikiwa ni miaka 22 baada ya mkutano wa kwanza maarufu kwa jina la ICN1 kufanyika katika jiji la Rome na kuazimia kuwa, upo umuhimu wa kuhakikisha binadamu wanapata Lishe bora yenye virutubisho ili kusadia kujenga afya ya binadamu duniani. Mkutano huu wa pili pia umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi wa Kudumu wa Italia katika Umoja wa Mataifa Gianni Ghisi aliyesoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Italia Giorgio Napolitano ambapo alifafanua kuwa Rome inawakaribisha wawakilishi wan chi mbalimbali na kwamba inatamani kuona mkutano huu unatoka na majibu ya tatizo la lishe duni kwa watu wa mataifa mbalimbali. 

Katika siku ya ufunguzi pia hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon iliwasilishwa pamoja na uzoefu wa masuala ya Lishe kutoka Italia ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia Paolo Gentiloni aliwasilisha hotuba yake huku akiwakaribisha washiriki wa mkutano huu wa ICN2 katika jiji la Rome na kufafanua kuhusu matarajio ya Italia katika mkutano wa sasa ukilinganisha na ule uliofanyika miaka 22 iliyopita.

Akiwasilisha taarifa ya Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wa Maendeleo ambao wamekuwa wakichangia katika sekta za Afya na Kilimo na akafafanua kuwa Tanzania imepiga hatua tangu ICN1 na sasa inahitaji kuona mkutano huu unatoka na maamuzi yanayotekelezeka ili kuwasaidia wananchi wa mataifa mbalimbali hasa watoto na akina mama wajawazito kuwa na uhakika wa lishe bora yenye virutubisho.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo vingi vilitokana na lishe duni na kwamba serikali ya Tanzania inaendelea kulipatia msukumo suala la lishe na virutubisho kwa wananchi wenye uhitaji ili kujenga taifa lenye afya na lenye watu wenye uwezo wa kusaidia nguvu zao katika kuleta maendeleo.

Akizungumza siku ya pili ya Mkutano huo Baba Mtakatifu Fransis alisema haki ya chakula bora si tu kuwa imetolewa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu bali pia ni haki inayoashiria utu na ambayo haipaswi kutolewa kama zawadi kwa wanadamu. 

Papa Fransis aliendelea kusema kuwa, katika dunia ya sasa masuala ya chakula, lishe na mazingira yametokea kuwaunganisha binadamu wa mataifa yote sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma na akazitaka serikali za dunia kuhakikisha zinapunguza utupaji wa vyakula sambamba na kuongeza mikakati ya kuhakikisha kila mwanadamu anapata lishe bora.

ICN2 inatazama pia kuhakikisha kuwa nchi zinakuwa na mikakati ya kupunguza utapiamlo na kwamba chakula kinachopatikana kiwe kile kilichoboreshwa ama kuongezewa virutubisho ili kusaidia jamii zinazokabiliwa na matatizo kama utapiamlo kuepukana nayo 
na hivyo kuwa na kizazi chenye afya bora na chenye uwezo wa kutumika katika uzalishaji ama katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Margareth Chan, Mkurugenzi wa WHO aliueleza mkutano huo kuwa suala la lishe ni mhimili katika kufanya jamii inayoweza kukabiliana na magonjwa huku pia Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva akifafanua kuwa, shirika lake linautumia mkutano huu unaoshirikisha nchi 172 kutoa mwongozo kwa dunia kuhusu jambo hili muhimu katika maisha na hasa sasa ambapo tunaelekea kukamilika kwa Malengo ya Milenia na kuanza malengo mapya.

Katika mkutano huo, licha ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Tanzania pia iliwakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid pamoja na Waziri wa Mifugo Dkt. Titus Kamani sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim. 

Sambamba na kuhudhuria mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi Italia na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa sambamba na kukutana na Mkurugenzi wa FAO ambaye alionesha furaha yake kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepitia na kuahidi ushirikiano zaidi katika masuala ya Kilimo. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais na ujumbe wake umeondoka kurejea nyumbani Tanzania tayari kuendelea na shughuli nyingine za Kitaifa leo Ijumaa Novemba 21, 2014.
 
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
                       Rome, Italia
                 Novemba 21, 2014

IJUMAA IMERUDI TENA TUKUTANE THAI VILLAGE...!!

DSC_0016
Majembe ya Skylight Band yakiporomosha burudani kwa mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mkongwe kwenye muziki wa dansi Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo na Sam Mapenzi.
DSC_0087
Pichani juu na chini ni mashabiki nao wakijibu mapigo ya sebene lililokuwa likiporomoshwa na majembe ya Skylight Band.
DSC_0089
Mashabiki wa Skylight Band wakijinoma na muziki mzuri kwa kujinafasi ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0121
Usishangae kumuona Sony Masamba kavua shati na kubaki na vest..ilikuwa ni patashika na nguo kuchanika...Joniko Flower akisongesha burudani.
DSC_0030
SAM MAPENZI.....Kuna watu hatari, wenye mapenzi zenye siri kali…Letu nalo lina jua kali, penzi letu serikali…Wajua nakupenda, malaika.......ANETH KUSHABA AK47:......Kuna wengi walafi, fimbo zao haziui mbali…Wengi wao wajidai, mimi kwako no, sitawai…Mmm take me, nitembee nawe….Baby take me, nitembee nawe... bonge moja la kolabo njoo ulishuhudie mwenyewe kwa macho yako.
DSC_0059
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wake wanapata furaha na tabasamu nyusoni mwao, usikose usiku wa leo ndani ya Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
DSC_0021
If I should stay…..I would only be in your way…..So I'll go but I know…I'll think of you every step of the way…..And I... will always love you, ooh….Will always love you…You….My darling, you.......Mmm-mm...si mwingine ni Bela Kombo katika hisia kali za kuteka mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village, tukutane baadae kwa play list kali na nyimbo kali zilizoenda shule.
DSC_0115
Hashim Donode akifanya yake huku akipewa sapoti na mwanadada Bela Kombo.
DSC_0093
DSC_0133
Mashabiki nao walicharukaje sasa.....palikuwa hapatoshi uwanjani.
DSC_0140
Mdau MO Tajiri naye alikunwaje na burudani akaamua kutoa kibulungutu na kuanza kutunza kuanzia wapiga vyombo mpaka waimbaji.
DSC_0143
MO Tajiri akiendelea kumwaga manoti kwa waimbaji wa Skylight Band.
DSC_0177
Sehemu ya umati uliofirika kushuhudia burudani ya Skylight Band Ijumaa iliyopita ni balaaaa.
DSC_0198
Burudani ikiendelea.
DSC_0183
DSC_0154
Huku burudani ikiendelea alikuwa anazaliwa Mkurugenzi wa Skylight Band Sultan Gijegije, ambapo wadau na mashabiki wa Skylight Band walimpongeza kwa kumwogesha vinywaji vya kila aina mwilini mwake kama inavyoonekana pichani.
DSC_0156
Birthday boy Sultan Gijegije akiendelea kuogeshwa na vinywaji mbalimbali.
DSC_0162
Swahiba wake wa karibu MO Tajiri akimpongeza Sultan Gijegije kwa kutimiza miaka kadhaa ndani ya bata la Skylight Band Ijumaa iliyopita.
DSC_0168
Team WANAMANYOYA ukodak ulihusika na birthday boy Sultan Gijegije.
DSC_0045
Mdau Rakim Kent (kushoto) akipata ukodak na Mratibu wa Skylight Band Lubea Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.
DSC_0189
Birthday boy Sultan Gijegije Rais wa Wanamanyoya akipata ukodak na Divas wa Skylight Band Bela Kombo na Aneth Kushaba.
DSC_0192
Birthday boy Sultan Gijegije akiwa na baharia LEMUTUZ (wapili kushoto) pamoja na Eddievied.
DSC_0200
Mtangazaji wa Clouds Radio Ben Kinyaiya akipata Ukodak na birthday boy Sultan Gijegije.
DSC_0204
Na sebene likachezeka na hapo ndio mahali pake... hawa jamaa ni noumaa wakiamua kuwa madansa watafunika sana.
DSC_0213
Backstage nako palinoga sana...!
DSC_0147
Si mwingine anaitwa Customer care akishow love na murembo mkali ndani ya Thai Village Masaki Ijumaa iliyopita.
DSC_0222
Wadau wakipata Ukodak.
DSC_0224
Wabebez wakali kama hawa ndani ya Skylight Band ni Ijumaa hii pia ndani ya Thai Village.
DSC_0229
Pichani ni Hashim Donode wa Skylight Band akipata Ukodak na mashabiki wake.
DSC_0232
Wadau wa Skylight Band wakishow love na ukodak.

KAMPUNI YA PAN AFRICAN ENERGY YATOA MSAADA WA MIFUKO 1500 YA SARUJI KWA WILAYA YA KILWA.

Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki (kwanza kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) msaada wa saruji 1,500 yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Lindi ili kuwezesha ujenzi wa maabala 59 katika shule zake za sekondari zipatazo 24. Pembeni wanaoshuhudia ni viongozi wa halmashauri hiyo na wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy. Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki Novemba 17, 2014 katika kiwanda cha Saruji cha Kilwa, Lindi. (Picha zote na Cathbert Kajuna.)
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya Peter Amosi Malekela akizungumza machache.
Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule ya sekondari Mtanda ambapo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya Maabala inayojengwa kwa msaada wa Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya mradi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo.
Mradi.
Moja ya Hospitalli ya Nangurukuru ikiwa imekwosha tayari kwa.
Mazungumzo ya hapa na pale.
Mazungumzo ya hapa na pale.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) akiongea na wageni wake waliomtembelea ofisini kwake.
Msafara ukielekea eneo la tukio.
Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy imetoa msaada wa mifuko 1500 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa ili kuwezesha ujenzi wa maabala katika shule zake za sekondari.

Akikabidhi msaada huo Andrew Kashangaki, Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa kampuni hiyo alisema wao wametoa msaada huo ili kuweza kutimiza lile agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzitaka kila shule za sekondari kuwa na maabala ifikapo Novemba 30, 2014.

“Kampuni yetu imewekeza huku hivyo ni vyema kuendeleza eneo ambalo limewekeza ikiwa ni kutoa huduma kwa jamii inayotuzunguka likiwemo suala la elimu bora na afya kwa ujumla ndiyo maana umeona leo tumekabidhi msaada wa mifuko hii ya saruji,” alisema Bw. Kashangaki.

Bw. Kashangaki alisema kampuni yao, mbali na Aliongeza kuwa mbali na utoaji wa msaada huo, kampuni ya Pan African Energy alishajenga hospitali katika eneo la Nangurukuru ambao imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa huko.
Pia alishukuru halmashauri ya Wilaya hiyo kwa uaminifu iliyouonyesha kwa kuanza kutumia saruji hizo kama zilivyokusudiwa.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa, Peter Malekela aliishukuru kampuni hiyo kwa kile walichotoa ambacho kwa kiasi kikubwa kimesaidia kuleta maendeleo katika wilaya yao jambo linaloleta faraja kwa wananchi.

Bw. Malekela alisema saruji waliyoipata waliigawanya kwa shule 24 za wilaya hiyo ambazo jumla ya maabala 59 zinahitaji, ambapo shule ya Kikanda, Kandawale, Miguruwe, Kiranjeranje, Nakiu, Likawale, Kikole, Pande, Mtanga, Njinjo, Namayuni, Kibata hizi zote zinahitaji maabala tatu (3) na mgao wa mifuko 76 ya saruji kila moja.

Nyingine ni shule ya sekondari Miteja, Mpunyule, Matanda, Songosongo, Dodomezi, Kivinje, Mibuyuni, Kipatimu, Alli Mchumo, Migumbi, Kijumbi hizi nazo zinahitaji maabala 2 kila moja na zinapata mgao wa mifuko 51 kila moja. Shule ya mwisho ni Kila yenyewe inahitaji maabala moja na imepata mgawo wa mifuko 25 ya saruji.

“Kila tunapopita tumekuwa mabalozi wenu wazuri kusema yale mazuri ambao mmekuwa mkiyafanya kwa wilaya yetu, tokea kampuni hii imeingia maendeleo ya eneo hili yanaonekana tofauti na zamani. Tunawaomba muendelee na moyo huu wa kujitolea na tunaalika makampuni mengine yaje tuijenge Kilwa yetu,” Alisema Bw. Malekela.

FM ACADEMIA YAMOTO BAND NA BARBANAS KUWASHA MOTO 'USIKU MWEUPE' JIJINI DAR

Mkurugenzi wa Blog ya Wananchi, William Malecela akiongea wakati wa onesho maalum liitwalo 'Usiku Mweupe' utakaofanyika ukumbi wa Escape One jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' Yamoto Band na Barbanas, kesho watakuwa na onesho maalum liitwalo 'Usiku Mweupe' litakalofanyika kwenye ukumbi wa Escape One, uliopo mikocheni Dar es Salaam.

Mratibu wa onesho hilo Wiliam Malecela, alisema kuwa kila kitu kipo vizuri ambapo onesho hilo litaanza saa 3, usiku.

Alisema kuwa dhumuni la kufanya onesho la pamoja kwa bendi hizo na msanii huyo anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya ni kutaka kuuinua muziki wa dansi ambao umeonekana kufifia.

Malecela alisema kuwa katika usiku huo mweupe umeangalia umri wa kila mdau wa muziki, kuanzia miaka 18 mpaka 50 kwa sababu kuna muziki wa kizazi kipya na bendi ya muziki wa dansi.
"Kwanza tumeangalia muziki wa dansi kama unapotea ni bora tuanze kuurudisha kwa kufanya onesha la pamoja na vijana hawa ambao kwa sasa ni moto wa kuotea mbali, vile vile tumeamua kuunganisha watu wa lika lote waje kushuhudia burudani safi"alisema Malecela.

Alisema ana amini kila mpenzi wa muziki atapata burudani safi na kukumbuka usiku huo maalum.

Malecela alisema kuwa wamejipanga kwa kuweka ulinzi wa aina yake, ambapo kila atakayekuja atakuwa salama.
Meneja wa Serengeti Platinum, Elihuruma Ngowi (Kati) akiongea machache.
Waandishi wa Habari.
"Tumejipanga kila sehemu hata suala la ulinzi, tumeomba kupata ulinzi wa kutoka, kwa kila atakayekuja atapenda, maana atakaa mpaka anaondoka akiwa yupo vizuri"alisema Malecela.
Alisema katika onesho hili viingilio ni shilingi 20,000 na 10,000.
Limedhaminiwa na Serengeti Platinum, CXC Africa,Clouds FM,Jambo Leo, Smart, Blogu ya Wananchi, Udaku Special na Domo Cosmetics.