ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 17, 2018

KINONDONI, SIHA WAAAMUA.

ZOEZI la upigaji kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani katika baadhi ya maeneo, Tanzania Bara limeanza limeanza rasmi asubuhi hii ya leo tarehe Februari 17, 2018 ambapo majimbo mawili ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro yatakuwa kwenye mchakato wa kuwachagua wabunge wao baada ya waliokuwepo kujiuzulu.

Vile vile, uchaguzi huo utafanyika kwa Madiwani katika Kata nane Tanzania Bara na kuhusisha wapiga kura 355,131 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kutakuwa na vituo vya kupigia kura 867.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema leo asubuhi saa 2:00 huku wananchi wakijitokeza kuchagua viongozi wawakilishi wao na ulinzi ukiwa umeimarishwa na jeshi la polisi.

Katika Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia wa CCM anachuana na Salum Mwalimu wa Chadema ambapo Siha, Elvis Christopher Mosi wa Chadema akichuana na Dkt. Godwin Ole Mollel wa CCM.

Friday, February 16, 2018

HATIMAYE DR. SLAA APANGIWA KITUO CHA KAZI


Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli hatimaye hii leo  amemuapisha Dr. Wilbroad Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, tukio ambalo limefanyika mapema hii leo.

 

Si yeye tu Balozi Dkt. Slaa, bali pia ameapishwa Balozi Mboweto nao mapema hii leo wamesikika hivi wakila kiapo cha uaminifu mbele ya Rais Magufuli. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiashuhudia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kula kiapo kuwa mabalozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba akiongea machache baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Wilbrod Slaa baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Mohamed aliyeungana na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kushuhudia kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji (Mst) Harold Nsekela na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi na wakuu wa vyombio vya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa baada ya mabalozi hao kula kiapo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe 

Thursday, February 15, 2018

CONTE ARUSHIWA JEZI YA MAN UNITED KWENYE MKUTANO NA WANAHABARI.



 Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo siku ya Alhamisi meneja wa Chelsea, Antonio Conte amekabidhiwa jezi ya Manchester United na Pranksters iliyosainiwa na kocha wa Man United, Jose Mourinho.

Watangazaji wa kipindi cha Italia 1 satirical show Le Iene , Alessandro Onnis na Stefano Corti walifanikiwa kukamilisha zoezi hilo baada ya jezi hiyo kusainiwa na Mourinho mwezi uliyopita huko The Lowry Hotel Manchester.

Mjumbe aliyefikisha jezi hiyo alimuonyesha Conte pia kipande cha video kutoka kwa Onnis na Corti kinachoelezea.

“Antonioooo, tume kutumia mjumbe kukuwakilishia jezi iliyosainiwa na rafiki yako mpya Joseee Mourinhoooo. Ametuambia kuwa anakupenda tazama alichokiandika hapo mbele ya jezi na kutupatia tukupe, rafiki yako , Jos amesema.” Ujumbe wa video kutoka kwa Onnis na Corti.

“Unaweza kutuahidi kuwa mchezo ujao utakao cheza dhidi yake mtakubaliana kuwa marafiki?,  tuambie, Antonio urafiki wenu utadumu milele.”

Hata hivyo Conte ameonekana kusuasua kutoa majibu na kupokea jezi hiyo wakati wa mkutano huo mbele ya waandishi wa habari na kumtaka prankster kusubiri mpaka kumalizika kwa kikao hicho.

DANCER WA FM CADEMIA APANDWA MIZUKA NA KUVUA NGUO KWEUPEE USIKU WA VALENTINE MJINI ARUSHA


Sikukuu ya Valentine ndani ya mji wa Arusha ilikuwa fresh ile kinyama, lakini vituko havikukosekana tizama kideo hiki mpaka mwisho utapata majibu ya swali jeh Pesa ni sabuni ya Roho au Pesa Nyok**?

METDO TANZANIA IMEENDELEA NA ZIARA YAKE KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA NA USALAMA MAHALA PA KAZI KWA WACHIMBAJI WADOGO.



Asasi ya Mining and Environmental Transformation for Development Organization ( METDO Tanzania) imendelea na Ziara  yake kutoa Elimu ya Mazingira na Usalama mahala pa Kazi kwa Wachimbaji wadogo.

Lengo ni kuhakikisha wanafanya uzalishaji wakiwa salama na Mazingira  salama.

Serikali imekuwa ikipoteza kodi nyingi kwa wachimbaji wadogo hii ilitokana na kutoweka taratibu katika Halmashauri  zote Nchini. 

Tunaomba TRA , MADINI ,Wakusanyaji ushuru  wa Halmashauri na Wahusika wa Mazingira. 
Ili  mrabaha 6%* , Kodi TRA 5% na *Pato la Halmashauri *0.3%  kodi zote zikusanywe kwa Wachimbaji kwa wakati mmoja

 # Tuyatunze* Mazingira yatutunze,Tutumie Rasilimali zetu kwa ajili ya kuinua Uchumi wa Watanzania na kuijenga Tanzania

KIJANA WA MIAKA 19 AWAPIGA RISASI NA KUWAUA WATU 17 KATIKA SHULE MOJA YA SEKONDARI NCHINI MAREKANI.

 
WATU wasiopungua 17 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 kufyatua risasi katika skuli moja ya sekondari ya eneo la Parkland katika jimbo la Florida nchini Marekani.


Kwa mujibu wa polisi, muuaji huyo ambaye ameshakamtawa na ambaye amejulikana kwa jina la Nikolaus Cruz, alikuwa mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo lakini alifukuzwa kwa sababu ambazo hazijabainishwa za utovu wa nidhamu.
Cruz.
Ripoti ya Polisi imeeleza kuwa katika tukio hilo lililojiri hapo jana, Cruz kwanza alianza kufyatua risasi kutokea nje ya skuli kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi wanafunzi wa skuli hiyo ya Marjory Stoneman Douglas.
Maafisa wa hospitali katika jimbo la Florida wamesema hadi sasa watu 17 wamethibitika kuwa wameuawa na wengine 20 hadi 50 wamejeruhiwa, ambapo hali za baadhi ya majeruhi ni mahututi.

 Watu wakitolewa nje ya eneo la shule ya Marjory Stoneman Douglas baada ya mauaji hayo kutokea huku wengine wakijeruhiwa. (Photo by Joe Raedle/Getty Images)
 Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye yeye mwenyewe ni muungaji mkono wa sera ya uhuru wa kumiliki silaha nchini Marekani amesema kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuwa: haipasi mtu yeyote ajihisi hana usalama katika skuli za Marekani.


Kila mwaka maelfu ya watu huuawa na kujeruhiwa katika maeneo mbalimbali nchini Marekani katika matukio mbalimbali ya ufyatuaji risasi. Kwa mujibu wa ripoti rasmi kuna karibu silaha moto za mkononi milioni 270 hadi milioni 300 nchini Marekani, ikiwa na maana kwamba, kwa wastani kuna silaha moja moto kwa kila raia mmoja wa nchi hiyo.
Licha ya miito inayoendelea kutolewa kila leo na makundi ya kutetea haki za kiraia nchini Marekani, lakini kutokana na ushawishi wa lobi za viwanda vya utengezaji silaha, hakuna serikali yoyote ya nchi hiyo ambayo hadi sasa imeweza kutunga sheria ya kudhibiti uuzaji silaha kwa raia nchini humo.

Kikosi cha zimamoto na uokoaji kikiwa eneo la tukio kutoa msaada. (Photo by Joe Raedle/Getty Images)

BALOZI WA JAPAN AKABIDHI SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI KASENDA.

Kushoto  ni  Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa na mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi baada ya kukabidhi  soko la samaki la kimataifa la Kasenda  lililopo kata ya Mganza Wilayani Chato lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan. 


Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akizindua kwa kuweka jiwa la msingi kwenye mradi wa soko la samaki la kimataifa la kasenda pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato ,Mhandisi Joel Hari.

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida  akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakati wa hafra fupi ya kukabidhi soko la kimataifa la Samaki.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akibadilishana mawazo na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida  pamoja na mbunge wa jimbo la Chato Dk,Medard Kalemani.

Jiwe la msingi ambalo limewekwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida  kwenye soko la samaki la kimataifa la Kasenda.

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi(CCM)

Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida  akizungumza na wananchi baada ya shughuli ya kukabidhi na kuweka jiwe la msingi kwenye soko la samaki la kimataifa.

Muonekano wa soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilaya ya Chato mkoa wa Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi na Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaharu Yoshida  wakiweka saini kwenye vitabu vya wageni.


Na,Joel Maduka,Chato.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaharu Yoshida  kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita amezindua rasmi soko la kimataifa la uuzaji samaki la kasenda lililojengwa kata ya mganza wilayani chato mkoani hapa kwa hisani ya watu wa Japani.


Soko hilo lililopo kata ya Muganza lina jumla ya wafanyabiashara wa samaki zaidi ya 240 limegharimu jumla cha Shilingi milioni 320 za kitanzania hadi kukamilika kwake ukarabati uliohusisha pia ukarabati wa soko la zamani. 


Akikabidhi soko hilo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Balozi wa Japan nchini Tanzania mhe. Masaharu Yoshida amesema kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhia samaki na dagaa kutasaidia kuokoa mazao mengi kutoka ziwani hususan samaki na dagaa.

“Soko la samaki la Kasenda halikuwa na miundombinu ya kuhifadhia samaki ambapo zaidi ya tani 200 za samaki zilitupwa kila mwaka kutokana na kuharibika ambapo serikali” alisema Mhe Masaharu.


Wakati huo huo serikali ya Japan imesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Chato ya ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa moja kutoka Muganza hadi Kasenda mahali lilipo soko hilo kwa thamani ya shilingi milioni 197.


Waziri wa Nishati mhe.Dkt. Medard Kalemani ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chato ameishukuru serikali ya Japan kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania. Alisema serikali ya Japan kwa muda sasa imekuwa ikishirikiana na Wilaya ya Chato na hii inatokana  na uhusiano mzuri ulioanzishwa na mbunge wa Chato kwa wakati huo mhe. John Pombe Magufuli.


Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel  amewataka wananchi pamoja na uongozi wa soko kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ili kuhakikisha malengo ya uanzishwaji wa soko hilo yanatimia likiwemo suala zima la ukusanyaji wa mapato.


Mbali na kuhudumia soko la ndani ya nchi, soko hilo la kimataifa la Kasenda limekuwa likihudumia baadhi ya nchi za jirani kama vile Congo DCR, Rwanda, Burundi na Uganda.Ambapo  linakadiriwa kukusanya Zaidi ya shilingi milioni 140 kwa mwaka.

SAA 48 ZILIZOMNG'OA ZUMA MADARAKANI.

President of South Africa Jacob Zuma addresses the nation at the Union Buildings in Pretoria on February 14, 2018.
Jacob Zuma, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Urais. REUTERS
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake. Hatimaye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ajiuzulu
Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtakja ampe nafasi mamamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama.
Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi.
Mapema Jumatano, polisi walivamia nyumba ya familia tajiri ya Gupta ambayo Zuma ana uhusiano wa karibu nayo.

Zuma alijiuzulu kwa njia gani?

Alianza hotuba kwa kucheka na kufanya mzaha na waandishi wa hahari.
Baada ya kuwashukuru wale ambao amefanya kazi nao kwa miaka kadhaa, Bw Zuma alisena kuwa ghasia na migawanyiko ndani ya ANC imesabisha ajiuzulu.
"Hakuna maisha itapotea kwa sababu yangu wala ANC haiwezi kugawanyika kwa sababu yangu. Kwa hivyo nimefikia uamuzi wa kujiuzulu kama rais wa nchi mara moja," alisema
"Licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC.
"Ninapoondoka, niataendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini sawa na ANC, chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote."



Jacob Zuma ni Rais wa aina yake na mwenye utata kuwahi kutokea Afrika Kusini

YANGA SC 4-1 MAJIMAJI FC (MAGOLI YOTE) - 14/02/2018


Tazama mabao yote matano, Yanga ikiichapa Majimaji 4-1 katika dimba la Taifa DSM, mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara raundi ya 18. Mabao ya Yanga yamefungwa Papy Tshishimbi aliyefunga mabao mawili, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin.

WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za  Iparamasa pamoja  Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili  kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.

Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.

Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. 

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.
Na,Joel Maduka ,Chato

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi shirika la White City  Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini  Wilayani Chato.

Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana  kwa umeme kwenye  kata yake  na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.


 Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze  kuendesha  biashara  zao.


Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo  kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.

“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini  Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi  wa Shirika la White City  International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi  16 kwenye jumla  vijiji  220 vilivyopo  mkoani humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni  Sh Bilioni 78.56.

Wednesday, February 14, 2018

HIKI NDICHO WENGI HUFELI KWENYE ENTERVIEW LINAPOKUJA SUALA LA KUJIELEZEA - KAZI DARASA NA DR. JEMBE


Ilikuwa katika kongamano la ujasiliamali linaloitwa Chimbo lililofanyika Belmont Fairmont Hotel jijini Mwanza ambapo wadau mbalimbali walijitokeza na darasa likatolewa.

Hapa ilikuwa ni zamu yake Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege al-Maarufu Jembe ni Jembe.

Pamoja na kuzungumzia mengi Dr. Jembe aligusa kona hii adhimu ambapo wengi wetu huwa tunachemsha pindi linapokuja suala la mtu kuomba ajira na ukatakiwa kujieleza katika enterview.

HIVI ni wapi tunapochemsha.....?

MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA

Mawaziri kutoka Malawi mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa ajili ya majadiliano kuhusu masuala ya Nishati na mwenyeji wao Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kushoto ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa.
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Mawaziri kutoka Malawi (hawapo pichani).

Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Mawaziri kutoka Malawi. Kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini wa Malawi, Aggrey Masi.

Viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake wakiendelea na majadiliano. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ally Ubwa, Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi. Kutoka kulia ni Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Tanzania, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi mara baada ya kumalizika kwa majadiliano ya masuala ya Nishati.
Ujumbe kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.
Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.
Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.
Alisema umeme unaozalishwa nchini humo kwa sasa ni Megawati 140 pekee huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 17 kiasi ambacho alisema kimeshindwa kukidhi mahitaji.
“Sasa hivi tumebaki na megawati 140 peke yake, hali siyo shwari; suluhisho la haraka linahitajika ili kuweka mambo sawa. Imani yetu ni kwa Tanzania kutazama namna ya kusaidia katika hili,” alisema.
Alibainisha kwamba chanzo kikuuu cha uzalishaji wa umeme nchini humo ni maporomoko ya maji na kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, chanzo hicho kimeshindwa kuzalisha umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.
Aliongeza kwamba Serikali ya Malawi imeamua kuwa na vyanzo mbadala vya kuzalishia umeme ikiwemo Gesi Asilia hata hivyo alisema hakuna Gesi Asilia inayozalishwa nchini humo na kwamba matarajio yao ni kupata Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.
“Tumefarijika, tumepokelewa vizuri, lengo la ujio wetu ni kubaini uwezekano wa kupata Gesi Asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme,” alisema Masi.
Alisema kwamba baada ya tathmini waliyoifanya wamebaini kwamba chanzo cha haraka kinachoweza kuwasaidia kuvuka kwenye upungufu mkubwa wa umeme uliyoikumba nchi hiyo kwa sasa ni Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa tayari mwekezaji amepatikana ambaye atazalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kwamba atajenga mitambo yake kwenye eneo la Kalonga mpakani mwa Tanzania na Malawi.
Kwa upande wake Waziri Kalemani alisema suala hilo linaweza kujadiliwa baada ya wataalam wa Tanzania kujiridhisha uwezekano wake.
“Tupo tayari kushirikiana, kinachohitajika hapa ni majadiliano ya kitaalam na wataalam wetu waliopo hapa ili kuelewa mwelekeo,” alisema Waziri Kalemani.
Dkt. Kalemani aliwasisitiza wataalam hao kabla hawajafanya majadiliano wanapaswa kuelewa mambo makuu matatu ambayo wingi wa Gesi Asilia iliyopo kwa sasa, matakwa ya Sera ya Nishati na namna ambavyo Gesi hiyo inaweza kusafirishwa hadi huko Kalonga.
“Je tunayo gesi ya kutosha kugawana ama ni ya kutosha kwa matumizi yetu tu? Je Sera inaruhusu suala hilo? Na kama masuala hayo yanakubalika, Je ni vipi tutaifikisha hiyo Gesi huko mpakani?” alihoji Dkt. Kalemani.
Aliueleza ujumbe huo kuandaa mpango wa ombi lao kimaandishi pamoja na kuandika ombi rasmi na kuwasilisha katika utaratibu maalum wa Kiserikali ili majadiliano yafanyike.
Aidha, suala la Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe, Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana kupitia taarifa ya Tume ya Uendelezaji wa Bonde hilo ambayo inaundwa na nchi hizo mbili ili kubaini hatua za kuchukua kwenye kipengele cha kuzalisha umeme.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika bonde hilo ni pamoja na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 180 ambazo zitagawanya sawa kwa nchi hizo, kilimo cha umwagiliaji, (hekta 6,200) usambazaji wa maji kwa wananchi, ujenzi wa miundombinu ya jamii (bararabara, shule, na vituo vya afya).
Miradi mingine ni uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, uvuvi, utalii na uboreshaji wa mazingira, hususan kuimarisha kingo za mto ambao ni mpaka wa Tanzania na Malawi.