ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 5, 2014

WATU ZAIDI YA 35 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI ILIYOTOKEA LEO MKOANI MARA


Picha na habari kwa hisani ya Ahmad Michuzi, Musoma.
Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa. 
 Ajali hiyo mbaya ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya matukio ya ajali ya barabarani yakihusisha mabasi kuwahi kutokea kwa mwaka huu, imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma wakati moja ya mabasi hayo yakiovateki gari lingine. 
Baadhi ya mashuuhuda wakitizama basi la J4 Express  lililogongana na basi la mwanza coach halipo pichani na wengine wakitoa  msaaada wa kuokoa majeruhi toka katika basi hilo
Gsengo blog inawapa pole wafiwa, tupo pamoja kwenye kipindi cha majaribu makubwa, tunamwomba Mwenyezi Mungu atupe nguvu na uvumilivu. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.