ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 10, 2012

JIJI RAFIKI NA MWANZA LAKABIDHI MRADI KWA WAVUVI WA DAGAA ZIWA VICTORIA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akibonyeza swichi ya taa za kuchaji zinazotumia umeme wa solar kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa uvuvi wa karabai zinazotumia nishati ya jua, kushoto kwake ni rais wa Umoja wa majiji rafiki (jiji la Housberg na jiji la Mwanza) Michael Shorfa's toka nchini Ujerumani na kulia kwake ni mjumbe aliyeambatana na rais huyo, pembeni kabisa ni kiongozi wa BMU Luchelele iliyopo kata ya Mkolani ambao utakuwa ni wa majaribio kabla ya kuenea maeneo mengine kanda ya ziwa Victoria.

MSONDO NGOMA YAKABIZIWA VYOMBO NA KONYAGISAID MABELA AKIPOKEA  KUTOKA KWA DAVID MGWASA


Na Mwandishi Wetu 

BENDI kongwe nchini ya Msondo Ngoma music band  imekabidhiwa vifaa vya muziki na kampuni ya Konyagi Dar es Salaam 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Konyagi nchini, David Mgwasa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania na kuifanya msondo kuwa imara katika kutoa burudani kwa watanzania.

"Msondo ni bendi kongwe tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 imesimama imara katika kutoa burudani ya uhakika kwa watanzania sanjari na kutumia nyimbo zake katika kuelimisha, kufunza jamii ya watanzania walio wengi," alisema Mgwasa.

Alisema watu wengi kwa kuwepo bedndi ya msondo wamewezakupata mafunzo mengio kupitia nyimbo zao ambazo nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa watanzania.


Hivyo alisema kuwa kwa kuwapatia vifaa hivyo, Msondo itakuwa moto wa kuotea mbali katika kutoa burudani ya uhakika hali itakayofanya bendi nyingine kwa wasindikizaji katika tasnia ya muziki wa dansi nc?hini.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Maalim Gurumo alisema kuwa kwa sasa wanadeni kwa Watanzania na kampuni ya Konyagi katika kutoa burudani ya uhakika baada ya kupatiwa vifaa hivyo.

"Tunaamini baada ya leo kupata vifaa hivyo tutatoa burudani ya uhakika sanjari na kukijenga vyema kikosi chetu kwa lengo la kukiimarisha," alisema Gurumo.

Kiongozi wa bendi hiyo Said Mabela alitoa shukrani wa kampuni ya konyagi kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kutoa burudani safi kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla.

"Tunashukuru kampuni ya Konyagi kutupatia vifaa vya muziki ambavyo kwetu ilikuwa ni vigumu kwa kipindi hiki kuvipata, hivyo tunaamini tutafanya tutaendela kuwa vinara katika kutoa burudani nchini," alisema Mabela.

Ofisa Habari wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo akiamini kuwa vijana wake watafanya vizuri zaidi katika ushindanio wa muziki huo nchini.

Pia aliwaomba wadau wengine wa muziki nchini kujitokeza  kuisaidia Msondo ili kuijengea uimara katika ushindi wa muziki huo nchini ili kuendelea kuwa bendi bora na ya kuigwa nchini. 

WANAMZIKI WA BENDI YA MSONDO NGOMA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KONYAGI

FLAVIANA MATATA RECEIVE 10,000 USD FROM DIAMOND EMPOWERMENT FUNDTanzanian born supermodel Flaviana Matata received a 10,000 USD donation from Diamond Empowerment Fund for her Flaviana Matata Foundation. It is a foundation that supports young girl's education in Tanzania.The donation will give more opportunities to girls who cannot afford to pay for their school fees.  Flaviana Matata  is a part of Russel Simmons Charity Projects and is a Diamond Angel of D.E.F.
Diamond Empowerment Fund (D.E.F.), is an international non-profit organization co-founded by Russel Simmons to support educational empowerment programs and initiatives in African nations where diamonds are a natural resource like in Tanzania. Countries like Tanzania,Botswana and South Africa are part of Russel Simmons and his Diamond Empowerment Project 
DEF’s envisions a future for these countries to be strong, stable, economically prosperous and socially empowered
Flaviana Matata who is Miss Universe Tanzania 2007 is currently pursuing her modelling career  in United States.
Russell Simmons is the third richest figure in hip hop, having a net-worth estimate of $340 million as of April 2011. Russell Simmons and Rick Rubin founded the pioneering hip-hop label Def Jam and created the clothing fashion lines called Phat Farm, Argyleculture, and American Classics.

TAMASHA LA SIMAMA KATAA UBAKAJI WA WATOTO LAFANA JIJI DAR

Naibu Katibu Mkuu Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mheshimiwa Anna Maembe akizungumza katika tamasha la Simama Awareness, lililofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar. Tamasha hilo lililoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali iitwayo Tanzania Alliance Peoples Organisation likiwa na lengo kupinga ubakaji kwa Watoto... ujumbe usemao, SIMAMA KATAA UBAKAJI WA WATOTO.

Mwakilishi wa Ustawi wa Jamii Kinondoni, Fransisca Makoye akitoa somo kwa watoto waliohudhuria tamasha hilo.

Mtoto wa shule ya msingi Hekima ya jiji Dar es Salaam akieleza machache kwa watoto wenzake, pembeni yake ni Mwakilishi wa Ustawi wa Jamii Kinondoni, Fransisca Makoye na mshereheshaji Zainab.

Watoto wakifuatilia tamasha.

Wanahabari toka kituo cha television ya TBC1, wakifanya mahojiano na watoto.

Meza kuu wakifuatilia.

Inspector Prisca Komba wa Kituo cha Polisi Osterbay  mwakilishi kutoka polisi

Walimu wa Shule ya msingi Hekima wakifuatilia kwa makini.

Nyimbo toka shule ya msingi Hekima.

Picha ya Walimu, Wanafunzi, Waandaaji pamoja na mgeni rasmi. PICHA ZOTE NA CATHBERT ANGELO- KAJUNASON BLOG.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA AELEZA WALIVYOJIFICHA MAKABURINI BAADA YA KUFANYA MAUAJI

Abdurahman Ismail aka Dulla (28) ambaye ni mkazi wa Mkudi Ghana jijini Mwanza ambaye ni mdogo wa watuhumiwa  Muganyizi Michael Peter aliyedaiwa kumfyatulia risasi marehemu Barlow alieleza jinsi walivyo tekeleza unyama wao na kwenda kuficha radio call na funguo za gari kwa kutupa katika tankila maji taka katika eneo la Nyashana kwenye nyumba ambayo haina mahusiano yoyote na hao watuhumiwa bali kwa lengo la kuhakikisha vitu hivyo havipatikani kabisa.

Watuhumiwa wawili waliofungwa pingu wakiwa wameshikiliwa na makachero wa jeshi la polisi waliovalia kiraia wakiwaonyesha kwenye shimo la maji taka eneo ambalo walitupa Radio call pamoja na funguo za gari la aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlowpo. 

Hawa ni watuhumiwa wawili kati ya saba wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kutoka kushoto ni Abdurahman Ismail aka Dulla (28) ambaye ni mkazi wa Mkudi Ghana jijini Mwanza na Amos Abdalah (32) mkazi wa mji mwema Wilayani Ilemela ambaye pia aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha mwaka 2006 katika gereza la Butimba, kabla ya kukata rufaa na kushinda mwaka 2010 ambapo aliachiliwa huru. 
Watu hao walitumbukiza radio call hiyo na funguo za gari kupitia bomba linaloonekana kulia la kupitishia hewa ya maji taka na hapa ni harakati za kutindua mlango wa shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la  mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza (RCO) Joseph Konyo akijiandaa kuchungulia ndani ya shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la  mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Shimo lenyewe.


Picha ya ndani ya shimo hilo..

Radio call kabla haijafanyiwa usafi...

Funguo za gari  zikifanyiwa usafi..

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza (RCO) Joseph Konyo akionyesha betri ya radio call iliyotenganishwa na radio call yenyewe wakati akizungumza na vyombo vya habari ikiwemo blog ya G. Sengo

Hivi ni baadhi ya vitu vilivyokamatwa nyumbani kwa watuhumiwa hao vikiwemo vyeti vya kughushi, pasipoti  na picha za utambulisho wa kughushi wa kipolisi, simu zaidi ya nne zenye laini zake na laini nyingine za ziada kwa mitandao tofauti, sare za moja kati ya makampuni ya ulinzi Mwanza, kofia zenye nembo ya jeshi la Polisi na kadhalika...

Panga na nondo ni moja kati ya vielelezo...

Sare za moja kati ya makampuni ya ulinzi....

Tv, sub woofer ambavyo vinatajwa kuwa ni mali ya wizi vikiwa sambamba na buti na viatu hivi ni sehemu tu ya vielelezo vilivyonaswa kwa watuhumiwa hao.

Friday, November 9, 2012

BREAKING NEWS: HENRY MATATA (CHADEMA) AWA MEYA MPYA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA, NAIBU WAKE NI SWILA DEDE (CCM)


Habari za sasa toka chumba cha uchaguzi zinamtaja diwani aliyepitia vigingi vingi huku akiwaburuza wenzie kortini mara kadhaa akidai haki zake mh. Henry Matata wa kata ya Kitangiri Ilemela jijini mwanza ameukwaa umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ... Awali licha ya wajumbe wenzake wote kupitia CHADEMA (madiwani wenzie)  kususia kushiriki uchaguzi huo wakidai kupewa maelekezo kutoka makao makuu kwamba wasishiriki, wajumbe waliobaki ni madiwani wa tano wa CCM na mmoja wa CUF ambao jumla yake sita, walikuwa na sifa ya kukamilisha idadi kuuhesabu uchaguzi huo kuwa wa halali hivyo Sheria na kanuni ikaruhusu uchaguzi kuendelea. 
 
Amini usiamini Henry Matata (CHADEMA) akashinda kwa 100% akizoa Kura zamadiwani wote 6.

Naibu wake akiwa  Swila Dede (CCM) ambaye ni diwani wa kata ya Sangabuye.Jeh! CHAMA KINAMTAMBUA MATATA KAMA MGOMBEA?

Kwa mujibu wa barua ya CHADEMA ya tarehe 08/11/2012 iliyosainiwa na Katibu wa chama hicho wilaya ya Ilemela John Anajus na kutumwa kwenda kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi, chama hicho kiliwasilisha majina ya wagombea wa umeya na naibu wake ambao kwa mujibu wa barua hiyo waliopendekezwa walikuwa ni;
1. Henry Mtinda Matata nafasi ya meya
2. Marrieta Chenyenge nafasi ya naibu meya  

Pia sehemu ya barua hiyo ilisisitiza kuwa Uchaguzi ulizingatia kanuni pia maelekezo ya mahakama ya hakimu mkazi ya 14/09/2012 n1 5/11/2012 kwamba mchakato wowote ule wa ugombea umeya lazima mgombea diwani Henry Matata ahusishwe hivyo uteuzi huo ulizingatia sheria za nchi na maamuzi ya mahakama na ndiyo maana Matata ameshiriki uchaguzi huo uliosusiwa na wenzake madiwani wa CHADEMA.


OBAMA AMWAGA MACHOZI MBELE YA TIMU YAKE YA KAMPENI YA UCHAGUZI
The morning after he won re-election, an emotional President Barack Obama credited his youthful staff of several hundred with running a campaign that will "go on in the annals of history." "What you guys have accomplished will go on in the annals of history and they will read about it and they'll marvel about it," said Obama told his team Wednesday morning inside the Chicago campaign headquarters, tears streaming down his face.

MAPINDUZI MAKUBWA UCHAGUZI WA MZFA YAFANYIKA MWENYEKITI APETA, KADUTU AUKWAA UWAKILISHI VILABU KWA ASILIMIA 100


Na ALBERT G. SENGO MWANZA
MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza(MZFA) Jackson Songora ametetea nafasi yake kwa miaka mingine  minne baada ya kuchaguliwa tena na wajumbe wapatao 17 kati ya 30 wa mkutano mkuu wa chama hicho Mkoani humo.

Uchanguzi huo umefanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambapo awali wagombea mbalimbali walijinadi kwa  wajumbe wa mkutano huo ili kuwashawishi kuweza kuwachagua katika nafasi walizomba ikiwemo ile ya Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu, Katibu msaidizi, Mweka Hazina na Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Mjumbe mwakilishi wa Vilabu na Mjumbe wa kamati ya udendaji.

 Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi huo Richard Mgabo (pichani aliyesimama) nafasi ya Mwenyekiti iliyokuwa na wagombea wawili ambapo  Jumbe Maghati na Jackison Songora walichuana vikali.. Hapa mwenyekiti wa uchaguzi huo anaweka mambo hadhalani..... Bofya play.Ikafuata nafasi ya Katibu mkuu wa MZFA …..Bofya Play.

Nafasi ya Mweka hazina ilikwenda kwa Jeremiah Tito Mahinya.
Nafasi iliyokuwa na upinzani mkali ya Mjumbe wa Mkutano mkuu wa TFF ambapo kura ilibidi kurudiwa kwa wagombea wawili ambao kura zao ziligongana awali katika duru la pili ili kumpata mshindi wa nafasi hiyo Mshindi alikuwa  Vedastus  Lufano aliyepata kura 16 dhidi ya kura 11 za Samwel Nyara aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.
Vedastus  Lufano

Kadutu.

Nayo nafasi ya Mjumbe  Mwakilishi wa vilabu ikatangazwa..... Bofya Play


Nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ilikuwa na mgombea mmoja Domiti Chisena aliyepata kura 16 za ndiyo na kura 13 za hapana ndiye ametawazwa mshindi kwa nafasi hiyo.


Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya mkutano mkuu TFF Deo J. Lyatto 

Moses Kaluwa.
MATOKEKEO YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA MZFA.
TAREHE: 08 NOVEMBER 2012

Thursday, November 8, 2012

NGOMA AFRICA BAND GROWING STRONGER AND STRONGER IN EUROPE!


Ngoma Africa Band, a German based Tanzanian band is now one of the oldest and most successful Africans bands in Germany.

Many African bands in Europe hardly survive for more than a year. Yet Ngoma Africa Band, founded by Ebrahim Makunja aka Ras Makunja in 1993, is still growing stronger.
The band plays "Bongo Dance", which is a unique combination of traditional and modern Tanzanian rhythms with  Soukous and Rumba. All theirs songs are in Kiswahili.

Ngoma Africa Band has released several successful hits including “Mama Kimwaga” (Sugar Mummy), “Anti-Corruption Squad” and “Apache wacha Pombe” (Stop over drinking).

In 2010 Ngoma Africa Band released a single in praise of Tanzania’s President Jakaya Kikwete. The song titled “Jakaya Kikwete 2010” praises Mr. Kikwete’s good leadership skills and commitment to fight corruption.

On 12th August 2012, Ngoma Africa Band received the International Diaspora Award (IDA) at the International African Festival Tubingen 2012, Germany, for their hard work in promoting East African music throughout Europe.

Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tubingen 2012 said Ngoma Africa Band was also chosen for the Award because of their creative performance on stage. It’s difficult to resist dancing at their concerts, she said.

This year the band released a new CD titled "Bongo Tambarare" featuring "Supu ya Mawe" and "Uhuru wa Habari". The new release is already dominating air waves in Tanzania.

"Supu ya Mawe" advices the listeners to work hard and be patient while pursuing their objectives in life. It also appeals for generosity towards the needy.

"Uhuru wa Habari" praises African journalists who are bold enough to speak out the truth in environments where freedom of speech is quite limited.

Ngoma Africa Band is famous for staging thrilling shows in festivals in different parts of Europe. The band’s joyful female dancers, wearing traditional costumes and dancing vigorously to their tunes, always leave fans asking for more.
 
Ngoma Africa Band is composed of talented young musicians including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, Said Vuai, Matondo Benda, Jonathan Sousa, A-Jay, Richard Makutima, Bedi Beraca "Bella" and Jessy Ouyah.

For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visit  
By Stephen Ogongo Ongong’a
                                                                                                                                                                     

TANZANIA NA ZAMBIA SASA KUPAMBANA KWENYE MASUMBWIWAPENZI WA MCHEZO WA MASUMBWI MNATAHALIFIWA KUWA KUTAKUWA NA MCHEZO WA NGUMI WA KIMATAIFA KATI YA ZAMBIA NA TIMU YA TAIFA YA BOXING YA TANZANIA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI YA TAREHE 10,11,2010 KATIKA UKUMBI WA DDC KARIAKOO KUANZIA SAA KUMI KAMILI.

 NJOO UBURUDIKE NA NGUMI SAFI KUTOKA KATIKA MATAIFA MAWILI TOFAUTI MPAMBAO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA KINGILIO MLANGONI ITAKUWA NI 5000 KWA KILA MTU MPAMBANO SI WAKUKOSA KWANI UMEANDALIWA VEMA NA ULIKUWA UKISUBILIWA KWA HAMU, HIVYO SHIME WATANZANIA KUJITOKEZA KUIPA SAPOTI TIMU YA NGUMI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KUHAKIKISHA  MABONDIA WA TANZANIA WANAFANYA VIZURI KWA KUJA KUTOA MCHANGO WAKO WA KUJA KUWASHANGILIA.

 MGENI RASMI SIKU HIYO NI MBUNGE WA KINONDONI IDDI AZANI AMBAYE KWA SASA YUPO BEGA KWA BEGA NA TIMU HIYO KUAKIKISHA INAFANYA VIZURI  KATIKA MCHEZO WA NDONDI MASUMBWI MAWE.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.
”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. 

Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali. 


DVD YA MANNY PAQUAIO ALIYOPIGWA KIUTATA IPO INAPATIKANA
 
DVD YA FLOYD MAYWEATHE MPAMBANO WAKE WA MWISHO KABLA YA KWENDA JELA NAYO INAPATIKANA KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA 0713 406938,0787 406938,0754 406938 NA 0774 406938 AU FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU FIKA KLABU YA ASHANTI ILALA AU AMANA

WATU MAARUFU KUPANDA JUKWAANI KATIKA ONYESHO LA KANGA LITAKALOFANYIKA 23 NOVEMBER HII.Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.

Watu Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo itapelekwa kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani kwa ajili ya kumalizia ujenzi.

MHASHAMU BABA ASKOFU BALINA KWA SASA ANAAGWA JIJINI MWANZA, KUZIKWA SHINYANGA JUMAMOSI


Msafara ulioubeba mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiingia katika himaya ya Kanisa kuu la Bugando jijini Mwanza leo kwaajili ya kutoa nafasi kwa wakazi wa mkoa huu kutoa heshima zao za mwisho 

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukishushwa toka kwenye gari tayari kufikishwa eneo maalum la ibada kanisani hapa 

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiingizwa ndani ya kanisa kuu la Bugando kwaajili ya ibada ya heshima za mwisho kwa wakazi wa Mwanza.

Padre wa Parokia ya Kanisa Katoliki Bugando Padre Alfred Lwamba ameongoza mapokezi ya ibada ndogo ya kupokea mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina. 

Watu mbalimbali pamoja na watumishi wa mungu kutoka ndani na nje ya jiji hili wamehudhuria ibada hii.

Upande wa akina mama.

Upande wa akina baba.

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiwa tayari kwaajili ya kuagwa katika Kanisa kuu la Bugando jijini Mwanza

Kisha baada ya ibada fupi ulianza utaratibu wa waumini, masista na mapadre kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina.

Heshima za mwisho zikiendelea....

Kimya kimetawala hapa, huku sauti za taratibu za uimbaji zikisikika.....

Wanavyuo waliomfahamu aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina nao wamejumuika kanisani hapa.

Kanisa 

Msafara wa kutoa heshima za mwisho uko hadi nje...