ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 9, 2012

BREAKING NEWS: HENRY MATATA (CHADEMA) AWA MEYA MPYA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA, NAIBU WAKE NI SWILA DEDE (CCM)


Habari za sasa toka chumba cha uchaguzi zinamtaja diwani aliyepitia vigingi vingi huku akiwaburuza wenzie kortini mara kadhaa akidai haki zake mh. Henry Matata wa kata ya Kitangiri Ilemela jijini mwanza ameukwaa umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ... 



Awali licha ya wajumbe wenzake wote kupitia CHADEMA (madiwani wenzie)  kususia kushiriki uchaguzi huo wakidai kupewa maelekezo kutoka makao makuu kwamba wasishiriki, wajumbe waliobaki ni madiwani wa tano wa CCM na mmoja wa CUF ambao jumla yake sita, walikuwa na sifa ya kukamilisha idadi kuuhesabu uchaguzi huo kuwa wa halali hivyo Sheria na kanuni ikaruhusu uchaguzi kuendelea. 
 
Amini usiamini Henry Matata (CHADEMA) akashinda kwa 100% akizoa Kura zamadiwani wote 6.

Naibu wake akiwa  Swila Dede (CCM) ambaye ni diwani wa kata ya Sangabuye.



Jeh! CHAMA KINAMTAMBUA MATATA KAMA MGOMBEA?

Kwa mujibu wa barua ya CHADEMA ya tarehe 08/11/2012 iliyosainiwa na Katibu wa chama hicho wilaya ya Ilemela John Anajus na kutumwa kwenda kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi, chama hicho kiliwasilisha majina ya wagombea wa umeya na naibu wake ambao kwa mujibu wa barua hiyo waliopendekezwa walikuwa ni;
1. Henry Mtinda Matata nafasi ya meya
2. Marrieta Chenyenge nafasi ya naibu meya  

Pia sehemu ya barua hiyo ilisisitiza kuwa Uchaguzi ulizingatia kanuni pia maelekezo ya mahakama ya hakimu mkazi ya 14/09/2012 n1 5/11/2012 kwamba mchakato wowote ule wa ugombea umeya lazima mgombea diwani Henry Matata ahusishwe hivyo uteuzi huo ulizingatia sheria za nchi na maamuzi ya mahakama na ndiyo maana Matata ameshiriki uchaguzi huo uliosusiwa na wenzake madiwani wa CHADEMA.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.