Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo
akizungumza na wananachi na baaadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki cha Mkongoma
kiichopo Wilayani Kisarawe. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha chaki Geofrey
Mkongoma akitoa risala fupi kwa mgeni
rasmi mara baada ya kiwanda hicho kuwekea
jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani .
Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe Happines Seneda akizungumza na wananchi waliofika katika
sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha chaki.
Baadhi ya viongozi wa halmshauri ya Wilaya ya
Kisarawe wakiwa katika halfa hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda
hicho cha chaki.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, KIRASAWE
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa serikali ya awamu ya
tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda,Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wawekezaji wote kuhakikisha wanaachana
kabisa na tabia ya kukwepa kulipa kodi na
badala yake watimize wajibu wao ipasavyo bila ya kuvunja sheria na taratibu za
nchi ili kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.
Injinia Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika
kiwanda cha chaki kinachoendelea kujengwa katika awamu ya kwanza katika kijiji
cha Msanga zalala kata ya Msimbu Wilayani Kisarawe na kuhudhuriwa na viongozi
mbali mbali wa , serikali, madhehebu ya dini pamoja na watendaji wa serikali za vijiji na vitongoji.
Pia Mkuu huyo alibainisha kuwa katika uwekezaji wa viwanda
katika Mkoa wa Pwani baadhi ya maeneo bado yanakabiliwa na changamoto ya
kutokuwa ni nishati ya umeme wa uhakika pampja na kuwepo kwa mioundimbinu
mibovu ya barabara hivyo ameagiza mamlaka zote zinazohusika kulifanyia kazi
suala hilo ili kuweza kuwavutia wawekezaji wengine.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda alitoa wito kwa wananchi
wengine kutumia fursa zilizopo katika kujifunza mambo mbali mbali ya
ujasiriamali na kuanzisha viwanda vidogo
vidogo kwa lengo la kuweza kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuwa
na uchumi wa kati pamoja na kuwapa nafasi zaidi wawekezaji ambao ni wazawa ili
waweze kutoa fursa za ajira kwa vijana.
Awali Mkurugenzi
mtendaji wa kiwanda hicho cha chaki Geofrey Mkongoma akisoma taarifa yake ameiomba serikali ya
awamu ya tano kuweza kuwapa fursa ya kipekee wazawa wa
Tanzania katika suala zima la
uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vidogovidogo huku akitaja akisema changamoto
kubwa ni suaala la umeme wa uhakika.
Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaunga mkono
juhudi za serikali ya wamu ya tano katika kuwa na uchumi wa viwanda hivyo
ataendelea kushirikiana bega kwa began a wadau wengine kwa lengo la kuweza
kufanikisha malengo aliyojiwekea ya kuweza kutoa fursa za ajira kwa wazawa
pamoja na kuongeza uzalishaji wa chaki.
“Hiki kiwanda kilianza tangu mwaka 2013 na kwa sasa kama
mnavyoona mimi nimeshaajiri wafanyakazi
wapatao 38. Ambao ninawalipa kutokana na kiwanda hiki cha chaki hivyo kitu
kikubwa ninachokiomba kwa serikali ni kutoa sapoti kubwa zaidi kwa wawekezaji
ambao ni wazawa ili waweze kuendelea kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuweza
kukuza uchumi wa nchini,”alisema Mkurgenzi Mkongoma.
Nao baadhi ya wakinamama ambao wanafanya kazi katika kiwanda
hicho cha chaki akiwemo Tedy Mzingula na Shoboa Msagasa wamesema kuwa
kipato wanachokipata kinaweza kuwabadilisha kwa kiasi kikubwa katika suala zima
la kujikwmau kimaisha kutokana na kuendesha familia zao ikiwemo kuwasomesha
watoto walionao pamoja na kuwahudumia mahitaji madogo madogo.
“Sisi kwa kwli kama wafanyakazi wa kiwanda hiki tunapenda
kumshukuru Mkurugenzi wetu kwa kuweza kupenda katika hali na mali, na kutokana
na kufanya kazi hii fedha ambayo tunaipata inatusaidia kwa kiasi kikubwa katika
kuendesha familia zetu, kwani wengne tuna watoto ambao tunawasomesha na maisha
yanaendelea lakini kikubwa ni serikali kumsaidia kuweza kupata umeme,”walisema.
KIWANDA hicho cha chaki ambacho kinajulikana kwa jina
la Mkongoma Chalk Factor kilianzishwa
mnamo mwaka 2013 ambapo kwa sasa kina jumla ya wafanyakazi zaidi ya 38 wakiwemo
vijana pamoja na wakinamama kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo ya
Kisarawe.