ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 4, 2017

ENEO LA PWANI LATOA WITO WA KUJITENGA NA ARDHI YA KENYA.

Eneo la Pwani latoa wito wa kujitenga na ardhi ya KenyaViongozi wa eneo la Pwani nchini Kenya wametoa mwito wa kutaka kujitenga eneo hilo na ardhi ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Gavana wa kaunti ya Mombasa, Ali Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Jeffa Kingi waliongoza wabunge 12 wa Pwani ya Kenya katika kutoa mwito huo jana Ijumaa.

Gavana Joho amesema "Huu ndio mwanzo wa kutimiza ndoto ya Wapwani ya kutaka kujitenga na Kenya".

Amesema tayari timu ya mawakili wa ndani na nje ya nchi wameanzisha mazungumzo na mchakato wa kuhakikisha kuwa kanda ya Pwani inajitenga na Kenya.

Ramani ya Kenya.
Gavana wa Kilifi kwa upande wake amesisitiza kuwa, katika safari yao hiyo ya kujitenga, watahakikisha kuwa hawatumii njia zisizo za kisheria na pia wataanza kupokea maoni ya wakazi wa eneo hilo kuhusu kadhia hiyo.

Jopo la wabunge wa Pwani ya Kenya limesema litawasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo, wa kutaka eneo hilo lipewe mamlaka ya kujitawala lenyewe.

Haijabainika iwapo hii ni moja ya mikakati ya mrengo wa upinzani wa NASA ulioapa kuanzisha uasi wa kiraia dhidi ya serikali, sambamba na kutaka wafuasi wao wasusie bidhaa na huduma za kampuni zinazoaminika kumilikiwa na viongozi wa chama tawala cha Jubilee, kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. CHANZO: PARSTODAY SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.