ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 7, 2018

MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 4,477



GSENGOtV

Rais John Magufuli amerejea kauli yake ya kuahirisha  maadhimisho ya sherehe za uhuru zinazofanyika Desemba 9 kila mwaka na kuagiza fedha zilizotengwa zielekezwe kujenga hospitali jijini Dodoma itakayoitwa Hospitali ya Uhuru.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 6, 2018 wakati akitoa salamu za siku ya Uhuru Ikulu, Dar es Salaam, Rais Magufuli pia ametoa msamaha kwa wafungwa 4,477 ambapo kati yao 1,176 wataachiwa huru siku ya maadhimisho hayo.

Novemba 20, 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alieleza kuwa Rais Magufuli ameagiza Sh995.182 milioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Majaliwa alitoa kauli hiyo alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa Lindi.

 “Ili kutekeleza mawazo ya waasisi wetu Serikali imeamua kuhamishia rasmi makao makuu ya nchi yetu jijini Dodoma na karibu wahusika wengi wameshahamia kule, nimebaki mimi ambaye nina mpango wa kuhamia hivi karibuni,” amesema Magufuli leo.

“Hii imefanya mahitaji ya huduma ya jamii ikiwamo afya katika jiji la Dodoma kuongezeka. Hivyo tumeamua kujenga Hospitali nyingine kubwa itakayosaidiana na hospitali ya Benjamini Mkapa na Hospitali ya Mkoa wa  Dodoma.”

Amesema hospitali hiyo itakayoitwa itasaidia kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za afya jijini hapo.

Kuhusu msamaha wa wafungwa amesema utawahusu wafungwa wagonjwa, wazee, wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa wajawazito, walioingia watoto wanaonyonya na wasionyonya  pamoja na wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili.

“Hali kadhalika nimeamua kwa wafungwa waliotumikia robo ya adhabu zao wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la theluthi moja linalotolewa kwenye kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya magereza Sura ya 58,’ amesema rais Magufuli.

MWILI UKIKAA SIKU 14 MOCHWARI SISI TUNAUZIKA

NJOMBE/GSENGOtV
Serikali Mkoani Njombe Imewataka Watanzania Kujenga Mazoea ya Kutembea na Nyaraka Zote Muhimu za Utambulisho Wao Pindi Wanapokuwa Safarini Ili Kurahisisha Mawasiliano Wakati Linapotokea Jambo Lolote Linalohitaji Mawasiliano ya Dharura.
Wito Huo Umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Kutoka Hospitali ya Rufaa Ya Kibena Mkoani Njombe Bwana Samson Sollo Wakati Akizungumza na Vyombo Vya Habari Juu Ya Mkazi wa Mmoja wa Songea Aliyefahamika Kwa Majina ya George Lutuhi Ambaye Amefariki Akiwa Anapatiwa Matibabu na Hakuna Ndugu Aliyejitokeza Hadi Sasa.
TAARIFA ZAIDI NA AMIRI KILAGALILA

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA YA SHARJAH IKULU LEO.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara   Wenye Viwanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi ya Sharja Bw.Abdallah Sultan Owais, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar Ikulu leo,akiwa na Ujumbe wake kulia Sheikh.Majid Faisal Khalid Al.Qasemi Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti w a Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda ya Sharjah,ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi, Bw.Abdallah Sultan Owais, wakiwa nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo Ikulu Zanzibar,7-12-2018.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanja Sharjah  ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi Bw.Abdallah Sultan Owais, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar, leo 7-12-2018.(Picha na Ikulu)

WAZIRI UMMY AZINDUA DAWATI LA JINSIA, UANZISHWAJI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA UTAMBULISHO WA SERA YA HAKI NA ULINZI WA MTOTO KATIKA JESHI LA MAGEREZA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili  kushoto), na Viongozi  Waandamizi  wa  Jeshi  la Magereza  wakikata utepe  kuashiria  Uzinduzi  wa  Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati) akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Benki ya NMB,ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo ya kifedha  katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA), ikiwa  ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa  na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.

Hayo yamesemwa na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua   Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo  jijini Dar es Salaam .

Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala  za Serikali, Mamlaka  za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.

“Leo nimefarijika  kuzindua dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza ni hatua nzuri kuelekea lengo la serikali kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo na kulinda haki za watoto, ni tumaini langu taasisi zingine zitaiga mfano huu ili tuweze kufikia dhumuni la serikali ya Awamu ya Tano kuona usawa wa kijinsia unakuwepo” alisema Waziri Ummy

Akizungumza katika Uzinduzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni aliwataka waratibu wa dawati hilo kuhakikisha wanasimamia haki hasa katika mashauri yanayowahusisha watoto na wanawake wajawazito waliopo magerezani na kuhakikisha ushirikiano unakuwepo kati ya wadau mbalimbali kuhusu ukaaji wa watoto magerezani

Pia amewataka viongozi wa Jeshi la Magereza kuhakikisha dawati hilo la jinsia linakua imara na madhubuti kwa kuweza kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu haki za motto aliyepo gerezani na akiahidi wao kama wizara kuhakikisha dawati hilo linadumu na kuweza kutoa matunda mazuri.

MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladslaus Mwamanga (katikati) akiongoza mkutano wa Wadau wa Maendeleo, Maafisa wa Serikali na TASAF kwenye ukumbi wa Mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau ,Serikali na TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa TASAF jijini DSM katika mkutano uliojadili utekelezaji wa Shughuli za Mfuko huo na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hapo mwakani.
Mmoja wa Watumishi wa TASAF,Shadrack Mziray akiwasilisha taarifa kwenye Mkutano wa Wadau ,serikali na TASAF jijini Dar es salaam.
Picha ya juu na chini menejimenti ya TASAF na ile ya Benki ya Dunia hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa TASAF, Serikali Na Wadau wa Maendeleo baada kuhudhuria mkutano wao wa pamoja jijini Dar es salaam.

Na Estom Sanga-DSM 

Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF uliojadili kwa kina utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unatekelezwa na Serikali kupitia TASAF umemalizika jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miezi sita , umefanyika kufuatia ziara ya washiriki hao katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na Unguja ambako walikutana na Walengwa wa Mpango huo na kujionea namna Walengwa wanavyoendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na Mpango huo kuboresha maisha yao. 

Miongoni mwa mambo yaliyofanywa katika mkutano huo ni pamoja na kuweka mkakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpangowa Kunusuru Kaya Maskini inayotarajiwa kuanza Mwezi Aprili hapo mwakani ambayo italenga zaidi katika kuwashirikisha Walengwa kufanyakazi za maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira. 

Akizungumza na Washiriki wa Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ametoa wito maalumu kwa wadau na maafisa wa Mfuko huo kufanya kazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya taifa ili lengo la serikali la kuwapunguzia kero ya umaskini wananchi liweze kufikiwa kwa ufanisi. 

Bwana Mwamanga amesema utekelezaji na mafanikio ya Mpango huo unategemea kwa kiwango kikubwa jitihada za pamoja hasa ikizingatiwa kuwa wananchi wanaolengwa ni wale ambao kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskinina wengine kukata tamaa jambo ambalo amesema linapaswa kukabiliwa kwa nguvu za pamoja. 

Kwa upande wake Kiongozi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Mohamed Muderis amepongezea jitihada za dhati zinazofanywa na Watumishi wa TASAF na wadau wengine katika kuwahudumia Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na hivyo kuleta hamasa ya dhati ya Walengwa kuuchukia umaskini. 

Aidha Bwana Muderis ametoa rai kwa watumishi hao kuendelea na kukamilisha kwa wakati maandalizi ya sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini inayotarajiwa kuanza mapema mwakani na kuzingatia kwa dhati maelekezo ya serikali . 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF upo kwenye maandalizi ya sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza huku mkazo ukiwekwa kuwawezesha walengwa kushiriki katika kazi za Ajira ya Muda, kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana,ujenzi wa miundombinu hasa katika sekta za elimu, afya ,maji na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.

RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCCA


 Jengo lililofungwa rada mpya kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio.

"Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?," amesema Mwakisasa.

Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania. Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi.

Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
 Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo.
 Mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye akieleza machache juu ya ujenzi huo wa rada mpya.
 Wanahabari waliofanya ziara katika mnara wa kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
 Mmoja ya wanamama muongoza ndege Bi. Mossy Kitang'ita akiwajibika.
Wanahabari wa vyombo mbali mbali wakipata maelezo kuhusu masuala yahusuyo usafiri wa anga.

Thursday, December 6, 2018

BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akizungumza waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya benki huduma ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70#. Kushoto ni Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akimuelekeza Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella jinsi ya kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa kuzindua huduma ya UBA Magic Banking ambayo mteja anaweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.



Ikiwa ni jitahada za kuendelea kuwa benki bora Barani Afrika kwa huduma za simu za mkononi na kuendelea kuendana na jinsi mtandao unapokuwa haraka na kuwa na bidhaa na huduma zilizo bora kabisa, benki ya UBA Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma nyingine bora ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70# kwa hapa Tanzania. 

Huduma hii ya Magic Banking itamfanya mteja kwa kutumia simu yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hii ya Magic Banking, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao UBA Bank Tanzania Asupya Nalingigwa alisema kuwa mbali na huduma ya Magic Banking kufanya kazi kwenye simu aina yeyote ile lakini huduma hii ni salama, ya haraka na nafuu na mteja haitaji kuwa na salio ili kufanya miamala. ‘Huduma ya Magic Banking inamfanya mteja kuweza kufanya miamala ya hadi TZS 1 milioni kwa siku kwa kutumia UBA Secure Pass ambayo inaongeza usalama kwa mtumiaji,’ alisema Nalingigwa. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji UBA Tanzania Usman Isiaka alisema kuwa huduma ya Magic Banking itamfanya kila Mtanzania mwenye simu iliyosajiliwa kufungua akaunti papo hapo. ‘Mteja anayetumia simu ya mkononi bila kujali anatumia mtandao ngani wa simu anaweza kufungua akaunti na sisi kwa kupiga *150*70# bila gharama yeyote, alisema Isiaka huku akiongeza kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Magic Banking ni moja ya lengo ya benki ya UBA kuweza kuwafikia mamilioni ya wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kuwaletea huduma ambazo ni rahisi, nafuu na za haraka zinazoendana na teknolojia. Vile vile tumelenga kufikisha huduma rahisi za kifedha kwa wananchi ili kuendana na matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), aliongeza Isiaka. 

Isiaka aliongeza kuwa benki ya UBA Tanzania imedhamiria kuboresha huduma za kifedha za kuzindua bidhaa na huduma zenye ubunifu ili kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa rahisi ya teknolojia. Ili kuweza kufanikisha yote haya tumewekeza rasimali nyingi na tuna uhakika tutaweza kuwafikia walengwa wetu, alisema AIsiaka. 

Uzinduzi wa Magic Banking umeenda sambasamba na kuzindua UBA Mobile banking App ya benki hiyo ambayo mteja anaweza kupakua kwa kupitia App Store na Play Store kwa watumiaji wa simu aina ya iPhone na Android. App hiyo itamuwezesha mteja kuweza kulipia huduma mbali mbali, kuangalia salio, kuomba cheque pamoja na kufanya miamala nyingine ya kibenki kwa kutumia simu zao za mkononi. 

Benki ya UBA Afrika imekuwa ikiongoza kwa huduma mbali mbali za kimtandao kwenye masoko yake ambayo yapo kwenye nchi 20 Barani Afrika. Kwa kutambua uwezo wake wa kutumia teknojia kwenye huduma za kifedha, benki ya UBA iliweza kushinda tuzo ya Best Digital Bank tuzo ambazo zilitolewa na Euromoney. 

SERIKALI KUIMARISHA UHUSIANO NA NCHI YA FALME ZA KIARABU

t-family: Arial, Helvetica, sans-serif;">Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad  Masauni, akizungumza   wakati   wa  Hafla  ya Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Ambapo aliahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akichagua  tiketi ya mchezo wa bahati nasibu iliyoendeshwa  wakati  wa  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za  Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu  Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni(wapili kulia) na Viongozi wengine wa Ubalozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu wakimkabidhi  Ali Suleiman Ali ,zawadi ya tiketi ya ndege  kwenda nchini Dubai na kurudi baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu iliyochezeshwa wakati  wa  Hafla  ya  Kusheherekea miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal (wapili kushoto), akiongozana na  Balozi  wa  Nchi  ya  Falme za  Kiarabu hapa  nchini, Khalifa  Abdulrahman  Mohamed  Al- Marzooqi (watatu kushoto), Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni (wanne  kushoto)  na  wageni waalikwa   wakitoka  nje  ya  ukumbi  baada  ya kumalizika  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa  la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Balozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu ,Khalifa Abdulrahman Mohamed Al- Marzooqi (kulia), baada ya kumalizika kwa Hafla ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za  Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

HII HAPA SIRI YA USHINDI KWA QUEEN ELIZABETH MISS WORLD 2018.



Mwakilishi wa Tanzania katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa dunia (Miss World), Queen Elizabeth Makune amefanikiwa kuingia katika orodha ya warembo mia moja watakao wania taji la mrembo wa dunia, fainali ikitarajiwa kufanyika Sanya nchini china Decemba 8 mwaka huu.

Ili kupata mshindi wa taji hilo kila mrembo atapigiwa kura kumuwezesha kuibuka mshindi,kamati ya Miss world imetoa tovuti maalumu na vyazo mbalimbali vya kupiga kura mtandaoni link kwa kila nchi kwaajili ya kumpigia kura mshiriki ane wakilisha nchi husika.

UKOSEKANAJI WA KUMBUKUMBU CHANZO CHA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA.



GSENGOtv

Wafanyabiashara mkoani Mwanza  wametakiwa kuweka kumbukumbu sahihi za biashara zao ili serikali iweze kupata kodi yake kikamilifu na kupunguza malalamiko kwa serikali katika makadirio ya ulipaji wa kodi.

Hayo yamebainishwa mkoani Mwanza na Mtaalam  kondi mamlaka ya mapato Tanzania TRASweetbert Igambisa katika wa klabu ya wafanyabishara waliokutanishwa na banki ya KCB.

Wednesday, December 5, 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME).

Bi. Lightness May, Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB akijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club 
pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa 

kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.



Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea 
kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa 

kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati 

yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli 
zao za kibiashara.


Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ilikusanya
wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa 
na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, 

uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa na 

KCB Bank ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya 
kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi, KCB Bank Mwanza, Nd. 
Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa 

kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika 

kukabiliana na changamoto za kibiashara. “Mtegemee semina kama 
hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri 
kibiashara” aliongezea Nd. Mzava.

Nd. Swetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi 
aliyealikwa na KCB Bank Tanzania mahususi kutoa mafunzo katika warsha 

hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa 

mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara 
zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali 
zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia 

watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao 

utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua 
wigo wa biashara zao. 

KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara 
wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia 

inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao 

hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa 
mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea 

katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi 

na Ethiopia.

Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii 
ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 

15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika 

Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, 
Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya 

KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua 

milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika 
kukuza sekta ya fedha nchini. 

Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania 
bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, 

Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es 

Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.


Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi 
ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea 

nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.