ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 10, 2023

HALMASHAURI YA CHALINZE YAIBUKA KINARA WA KWANZA YAPATA NGAO YA UTAWALA BORA NCHI NZIMA

 VICTOR MASANGU/PWANI

 BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 9/2023.

Katika kutambua mchango na jitihada kubwa zinazofanywa na Halmashauri mbalimbali nchini, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeitunuku Ngao ya Ushindi wa Kwanza wa Tuzo ya Uutawala Bora, na matumizi mazuri ya fedha za Serikali kutokana na kukidhi vigezo vilivyowekwa.. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze HASSANI MWINYIKONDO wakati wa kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya kwanza kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai hadi Septemba mwaka 2023/2024.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo RAMADHAN POSS amebainisha kwamba mafanikio ambayo wameyapata kuibuka kidedea katika shindano hilo la utawala bora ni kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa idara zote.


Naye  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halma Okash amewataka madiwani na watendaji kuwabana baadhi ya watu ambao wanakwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi.


SIJALI MPWIMBWI,OMARY MSONDE NA TUNU MPWIIMBWI Ni madiwani wa Halmashauri ya Chalinze.

Halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeweza kuibuka kidedea na kupata tuzo hiyo ya utawala bora na kuwa ya kwanza katika halmashauri 184 nchi nzima.

BODI YA TASAC YAUNGA MKONO NA KUPONGEZA JITIHADA ZA TPA KUJENGA BANDARI YA KUHUDUMIA MZIGO MCHAFU KISIWA CHA MGAO

 











BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeunga mkono na kupongeza jitihada za Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kujenga Bandari ya kuhudumua mizigo Mchafu eneo la Kisiwa -Mgao.

Ujenzi huo unatarajiwa kufanyika katika kisiwa hicho kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma karibu na wananchi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Capt. Mussa Mandia akiwa katika ziara hiyo ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC chini ya usimamizi wa Bodi hiyo.

KAIMU NAIBU MRATIBU MKUU WA MASUALA YA UKIMWI WA PEPFAR NCHINI MAREKANI ATEMBELEA SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA KUPITIA UFADHILI WAO

 

KAIMU Naibu Mratibu Mkuu wa Masuala ya Ukimwi wa mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Ukimwi (PEPFAR) Dkt Rebbeca Bunnell na ujumbe wake wamefanya ziara ya kutembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Grace Magembe.

Akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo walitembelea shughuli zinazotekelezwa kupitia ufadhili wa PEPFAR kupitia kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Marekani (CDC) kinachosaidia upatikanaji wa baadhi ya huduma katika Hospitali hiyo huku akiridhishwa na huduma zinazotolewa.

Kupitia PEPFAR, CDC ilianza kusaidia Asasi ya Kiraia ya Gift of Hope Foundation mwaka 2019 ili kuwezesha huduma za kinga miongoni mwa vijana walioathirkka na matumizi ya dawa zaa kulevya na kusaidia upatikanaaji wa huduma za afya kwa watu wanaojidunga kutumia dawa za kulevya.

Hadi kufikia Octoba 2023,The Gift Of Hope Foundation imesaidia zaidi ya wapokea huduma 365 kupata Methadone katika kliniki ya waraibu wa dawa za kulevya (MAT) ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku wateja 22 wakiwa katika nyumba ya kusaidia kuacha matumizi ya dawa za kulevya (Sober House).

The Gift Of Hope pia imepanua huduma zake ili kutoa msaada wa kisaikolojia –kijamii na huduma za uhamasishaji,ikijumuisha kukaa kwa muda waa miezi mitatu katika Sober House kwa wapokea huduma wakati wanaahudhuria kliniki za MAT ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Katika ujumbe wake pia wametembelea kliniki ya tiba saidizi ya Methadone (MAT) na kupata taarifa juu ya huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) zikiwemo huduma za uchunguzi na matibabu ya kifua kikuu,homa ya Ini B na C na uchunguzi wa ukatili wa kijinsia.

Kliniki hiyo ya MAT ilianzishwa mwaka 2020 na hadi kufikia Septemba mwaka huu ilikuwa imewaahudumia jumla ya wapokea huduma 959 kati yao wanawake 27 na wanaume 932 ambapo hiyo ni kliniki pekee ya MAT mkoani Tanga.

“Kliniki hii inatoaa huduma za kina za kuzuia VVU pamoja na tiba matunzo, huduma za kifua kikuu, huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii na uibuaji wa watu wanaojidunga /kutumia dawa zaa kulevya ...The Gift of Hope ni mojawapo ya Asasi za Kiraia zinazoibua na kuunganisha wateja na matibabu katika kliniki ya MAT”

Dkt Bunnell pia ametembelea kliniki ya tiba na matunzo ya VVU (CTC) na kupata taarifa juu ya huduma jumuishi ya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU ikiwa ni pamoja na ujumuishaji wa huduma za uchunguziz wa saratani ya mlangio wa kizazi.

Ambapo hadi kufikia Octoba 2023 kituo hicho kilikuwaa na zaidi ya wapokea huduma 2,700 waliosajiliwa katika huduma za dawa zaa kufubaza makali ya VVU (ART).

Kwa kipindi cha Octoba 22 hadi Septembea 2023 wanawake 1,287 wanaopataa huduma zaa tiba na matunzo katika kliniki hiyo walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo 47 sawa ana asilimia 3.65 walibainika kuwa na viashiria vya awali vya saratani yaani VIA Positive,na 38 walitibiwa kwa tiba Mgandisho (cryotherapy) .

Ambapo wapokea huduma 23 walihisiwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na walifaanyiwa uchunguzi wa kina na kumi na sita kati yao walithibitishwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Ujumbe huo pia utaelezwa kuhusu shughuli za chanjo ya Human Papillomavirus (HPV) zinazofaanywa katika kituo hicho huku ikieleza walikuwa na wasichana 27 waliostahili kupata chanjo hiyo na walisimamia wasichana 26 kati yao 21 walikamilisha dozi tatu za HPV,wasichana watano wakiwa bado kwenye ratiba ya kupata dozi ya pili.

Kadhalika Dkt Bunnell amepataa fursa ya kuzungumza na vijana rika balehe wa kike na kiume wanaopatiwa huduma tiba na matunzo katikaa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ili kujifunza wanavyonufaika na afua zinazofadhiliwa na PEPFAR na CDC Hospitalini hapo.

Hata hivyo pia Dkt Bunnell ametembelea maabara hya Hospitali hiyo na kushuhudia uchakataji wa sampuli za damu iliyo kaushwa (DBS) na makohozi kwa ajili ya kipimo cha kifua kikuu na kuelezwa jinsi ambavyo sampuli za wingi wa VVU huchakatwa ili kusafirishwa kwa upimaji kwenye maabaraa husika.

Kwa sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga inapokea Ufadhili wa PEPFAR/CDC kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Healthe Promotion Support (THPS).
Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni Taasisi ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2011 kwa kufuatia Sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Na 24 hya mwaka 2002.

THPS inatekeleza kazi zake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu,Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto ,Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Afya huko Zanzibar.

Lengo la THPS ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watanzania ,kupitia uimarishwaji wa mifumo ya afya na jamii ili kutoa huduma bora za afya zikiwemo za VVU na UKIMWI,Kifua Kikuu,Kuzuia ukatili wa Kijinsia,Afya ya Mama na Mtoto ,Afya ya Uzazi na Afya ya Vijana  ikiwemo kuboresha mifumo ya maabara na Taarifa za Afya,Uviko 19 na Tafiti za Afya ya Jamii

Mradi wa CDC/PEPFAR Afya hatua (octoba 2021 hadi Septemba 2026) umelenga kutoa huduma jumuishi, katika vituo vya Afya (Kigoma, Pwani, Shinyanga na Tanga) na katika jamii (Kigoma, Pwani na Tanga) huduma za Kinga, matibabu na matunzo ya VVU zikiwemo huduma za kitabibu za Tohara kwa wanaume katika mikoa ya Kigoma na Shinyange na Programu ya Dreams kwa wasichana balehe na wanawake wadogo katika mkoa wa Shinyanga.

Wednesday, November 8, 2023

MBUNGE KIBAHA MJINI AZINDUA RASMI MRADI WA SHULE YA MSINGI MKOMBOZI KATA YA PANGANI


VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amezindua shule ya msingi na awali ya Mkombozi iliyopo kata ya Pangani na kuchangia madawati 20 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.

Katika halfa za uzinduzi wa shule hiyo  zimeudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,madiwani pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao walifika kushuhudia jinsi ya utekelezaji wa ilani unavyofanyika.

Mbunge Koka alisema kwamba lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inaweka mazingira bora katika kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za awali hadi za juu.
 


"Nimekuja hapa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa shule hii ya msingi na awali ya mkombozi hakika nimefarijika sana kwa hatua hii kwani watoto wetu watapata elimu kuanzia ngazi ya awali na msingi,"alisema Koka.

Aidha Koka alisema kwamba kwamba pamoja na kuzindua shule hiyo atahakikisha anaweka miundombinu mizuri katika shule hiyo kwa ambayo itawasaidia wanafunzi waweze kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu


Sambamba na hilo Mbunge huyo alibainisha kuwa anaweka mipango mizuri kwa kushirikiana na mamlaka husika katika kuweka huduma za msingi ikiwemo maji na umeme.


Pia alisema kwamba amechaguliwa kuwaongoza wananchi wa Jimbo la Kibaha mjini hivyo ataendelea kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Pia amechangia madawati 20 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao wasome katika mazingira rafiki na kuondokana kusoma katika hali ya msongamano.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Mkombozi Medard Rweyemamu alimpongeza Mbunge huyo kwa kuboresha zaidi sekta ya elimu.

Alisema kwamba msada wa madawati hayo waliyopatiwa yatakwenda kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hao kuondokana na changamoto ya kusoma kwa mlundikano.
Naye Diwani wa Kata ya Pangani Agustino Mdachi aliongeza kuwa kuzinduliwa kwa shule hiyo ni moja ya hatua kubwa katika kuwasaidia wanafunzi katika kupata elimu.

Aliongeza kuwa ana imani kukamilika kwa shule hiyo ya msingi na awali mkombozi kutaweza kuwaletea maendeleo katika kuwapatia watoto hao elimu.

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Pangani wameipongeza serikali ya awamu ya sita pamoja Mbunge Koka kwa juhudi za kuweka mazingira mazuri ya kuboresha sekta ya elimu na kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ya mkombozi.

Monday, November 6, 2023

RAIS SAMIA ATOA ML 252 UKARABATI WA DARAJA LA MTO MPIJI

 VICTOR MASANGU, PWANI


Wananchi wa Kata ya Pangani katika halmashauri ya mji Kibaha ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya adha kubwa ya kuvuka  katika daraja la mto Mpiji wanakabiliwa kuondokana na kero hiyo baada ya serikali kutoa fedha ambazo zitasaidia katika  ukarabati  wa miundombinu na kuzuia kingo kubomoka.


Hayo yamebainishwa na  Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibaha Samwelu Ndoveni akisema  kwamba tayari wamepokea kiasi cha shilingi milioni 252 kwa ajili ya kufanya matengenezo haraka zaidi  katika daraja hilo la Pangani.

INSERT..1 TV SAMWELI NDOVENI MENEJA WA TARURA WILAYA YA KIBAHA

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji ambaye amefika katika daraja hilo kujionea amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha hizo ambazo zitasaidia kuboresha  daraja hilo liweze kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi hiki cha mvua.


INSERT..2 TV SILVESTRY KOKA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amesema kwamba wananchi wa kata ya Pangani ambao wanatumia daraja hilo wamekuwa wakipata adha kubwa hasa katika kipindi cha mvua na kwamba fedha hizo zitakwenda kutumika kwa manufaa ya wananchi.

INSERT..3TV NIKSON SAIMONI MKUU WA WILAYA YA KIBAHA.

KOKA AUNGURUMA AMPA TANO RAIS SAMIA KWA KUMWAGA FEDHA UKARABATI DARAJA LA MTO MPIJI

 


VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali  kutoa kiasi shilingi milioni 252 kwa ajili ya ukarabati wa daraja la mto Mpiji ili liweze kuwasaidia wananchi wa kata ya pangani kuvuka kwa urahisi hasa katika kipindi hiki cha mvua.




Koka ametoa pongezi hizo wakati alipowatembelea wananchi wa kata ya pangani kwa lengo la kuweza kujionea hali halisi ya miundombinu wa daraja hilo pamoja na kuzungumza na wananchi ili kuwaeleza fedha ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya sita.

Koka ambaye pia aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimoni pamoja na wataalamu mbali mbali kutoka Tarura lengo ikiwa ni kuona namna ya kufanya ili kulitengeneza daraja hilo la muda liweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote.

"Kiukweli nipende kumpongeza kwa dhati Rais wetu wa awamu ya sita kwa kuweza kutukubalia kutupatia fedha hizi kiasi cha shilingi milioni 252 ambazo tayari zimeshakuja kwa ajili ya kukarabati baadhi ya maendeo ambayo yameharibika  ikiwemo kingo,mbao na sehemu nyingine,"alisema Koka.

Kadhalika Mbunge huyo alibainisha kwamba katika enjoy hilo daraja ambalo limejengwa kwa sasa ni la muda tu lakini  kitu ambacho wanachokifanya ni kufanya matengenezo kupitia fedha walizozipata ili wananchi waweze kupata fursa ya kupita kwa urahisi.

Aidha Mbunge huyo alisema lengo lake kubwa ni kushirikiana na mamlaka husika ikiwemo Tarura kwa ajili ya kuhakikisha hatua za haraka zinafanyika mapema ili kudhibiti uharibifu ambao unaendelea katika maeneo ya pembeni ya daraja hilo.

"Kimsingi kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kufanya upembuzi wa kina ili kulidhibiti daraja hili lisiweze kubomoka kwani ni kiunganishi muhimu sana kwa wakazi wa kata ya pangani na maeneo mengine ya jirani kwa wen zetu wa Dar es Salaam,"alisema .

Kwa upande wake   Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibaha Samwelu Ndoveni amekiri kupokea   kiasi cha shilingi milioni 252 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya  haraka zaidi  katika daraja hilo la mpiji ili lisiweze kuharibika zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon  alisema kwamba wananchi wa kata ya Pangani ambao wanatumia daraja hilo wamekuwa wakipata adha kubwa hasa katika kipindi cha mvua na kwamba fedha hizo zitakwenda kutumika kwa manufaa ya 

HATIMAYE MWANZA YAPATA VIJANA 22 WA SAFARI LAGER CUP SOCCER 2023

 NA ALBERT G SENGO/MWANZA

Zoezi la usaili wa Safari Lager Cup kwa jiji la Mwanza limefanyika leo kwenye kiwanja cha Nyamagana kuchakata na kung'amua vijana 22 kati ya zaidi ya vijana 380 waliojitokeza kwenye usajili uliofanyika Ijumaa ya Tarehe 3 na hatimaye Jumamosi ya Tarehe 4 kwenye viwanja hivyo kukawa na usaili kuwashindanisha vijana hao kujua nani na nani wanakwenda Jijini Dar es salaam ambako timu za washiriki wa mikoa ya Arusha, mbeya na Dar es salaam yenyewe zitakutana kushindana na hatimaye kutengeneza team ya wachezaji 22 cream ya Safari Lager Cup.