VICTOR MASANGU, PWANI
Wananchi wa Kata ya Pangani katika halmashauri ya mji Kibaha ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya adha kubwa ya kuvuka katika daraja la mto Mpiji wanakabiliwa kuondokana na kero hiyo baada ya serikali kutoa fedha ambazo zitasaidia katika ukarabati wa miundombinu na kuzuia kingo kubomoka.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibaha Samwelu Ndoveni akisema kwamba tayari wamepokea kiasi cha shilingi milioni 252 kwa ajili ya kufanya matengenezo haraka zaidi katika daraja hilo la Pangani.
INSERT..1 TV SAMWELI NDOVENI MENEJA WA TARURA WILAYA YA KIBAHA
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji ambaye amefika katika daraja hilo kujionea amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha hizo ambazo zitasaidia kuboresha daraja hilo liweze kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi hiki cha mvua.
INSERT..2 TV SILVESTRY KOKA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amesema kwamba wananchi wa kata ya Pangani ambao wanatumia daraja hilo wamekuwa wakipata adha kubwa hasa katika kipindi cha mvua na kwamba fedha hizo zitakwenda kutumika kwa manufaa ya wananchi.
INSERT..3TV NIKSON SAIMONI MKUU WA WILAYA YA KIBAHA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.