ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 23, 2017

MKUU WA MKOA WA TANGA APOKEA VIFAA TIBA KUTOKA KWA UZALENDO KWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - TANGA. Vifaa vilivyotolewa na wasanii na wachezaji hao katika uwanja wa Tangamano ikiwa ni Kampeni ya Uzalendo kwanza ni pamoja na Ultra Sound, mashine ya X- Ray, Wheel Chair, Magongo ya walemavu na craches. Shigella amepokea vifaa hivyo ikiwa ni moja ya Kampeni ya UZALENDO KWANZA ambayo inaongozwa na wasanii na wacheza mpira ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuchangia maendeleo ya nchi. Ambapo vifaa hivyo vinagawiwa katika hospitali za Ngamiani, Makorola, Pongwe na Mikanjuni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Vijana wazalendo wa UZALENDO KWANZA wakibeba vifaa Tiba ambavyo walitoa kwa ajili ya hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella aliwataka wasanii na wacheza mpira hao kuhakikisha wanatumia umaarufu walionao ili kuweza kuwavutia wawekazaji kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa nchi.

"Wasanii mnadhamana kubwa ya kuhakikisha mnatumia vema vipaji vyenu ili kuweza kusaidia juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda kwa wao kuvutia wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza katika nyanja mbalimbali." alisema "Ninatambua asilimia kubwa mlizunguka kwenye kampeni mkiwaomba watanzania wamchague Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na dhamira yake nzuri ya kuletea maendeleo lakini pia hivi sasa mnashirikiana naye kwenye sekta ya afya kwa kumuunga mkono kwa kutoa mchango wenu niwaambie huu ni uzalendo ambao ni msingi wa maendeleo ya Taifa" 

 "Kwa mfano Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na wazee wengine walipigania Taifa hii kwa sababu ya uzalendo na ndio maana mnaona Rais wetu namna anavyopambana kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa na kutunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae kwa lengo la kila mtanzania kuweza kunufaika nazo "
Wananchi wakifuatilia wakati halfa ya ugawaji wa vifaa tiba. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, akiwashukuru UZALENDO KWANZA kwa jinsi walivyoweza kujitoa kwa hali na mali vifaa tiba kwa hospitali za mkoa wa Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa akitoa msisitizo kwa wasanii wa Tanga kuwa na moyo kama wa UZANDO KWANZA wa kuweza kujitoa kwa moyo mmoja wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akieleza machache wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Kampeni ya UZALENDO KWANZA, Steven Mengele 'Nyerere' alisema uzalendo kwanza imemaua kuchangia vifaa tiba kwa hospitali ya Tanga na kwamba kampeni hizo zitaelekea mikoa mingine mbali mbali ikiwemo Lindi na Mtwara, Dodoma, Arusha, na Mwanza.
Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere akiwatambulisha baadhi ya wazanii ambao wanaunda UZALENDO KWANZA.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella akimtunza msanii wa UZALENDO KWANZA ambaye alikuwa akitoa burudani.
Meza kuu ikifuatilia tukio wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe. Thobias Mwilapwa na mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. Kutoka kulia ni mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa na mwishoni kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi.
Wasanii wa UZALENDO KWANZA akitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akisalimiana na Msanii Ruby ambaye ni mmoja ya wana UZALENDO KWANZA wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela, akiteta jambo na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere.
UZALENDO KWANZA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vifaa tiba.. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (wa kwanza kushoto), Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi (mwenye tisheti ya mistari) pamoja na Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere  wakati akipokea vifaa tiba kutoka kwa UZALENDO KWANZA ambao wametoa vifaa tiba.

GHOROFA MAARUFU MWANZA LABOMOLEWA KUPISHA UPANUZI WA BARABARA YA MAKONGORO

Mchakato wa kubomoa ghorofa Al-maarufu 'Ghorofa la Madaraka' lililoko barabara ya Makongoro, Misheni jijini Mwanza  unaendelea muda huu ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa shughuli hiyo jana, huku ulinzi ukiwa umehimarishwa vilivyo.

Pichani. hali ilivyokuwa mapema jana. 
Mmiliki wa awali wa Ghorofa hili anaitwa Madaraka na wala si Madaraka Nyerere

Ila kiukweli Ghorofa hilo lina Historia kubwa sana ktk jiji la Mwanza kwani limeweza kukwepa misukosuko ya mabonde na vizingiti vingi vya kubomolewa takriban miaka 22 sasa, ikiwa ni sanjari na ile ya kubomolewa kwa kituo cha mafuta Moil Mwanza kunako mwaka 2009.
 

Hatimaye Andiko limetimia.
BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOJIRI.






Friday, September 22, 2017

MAMBO 10 ALIYOFUNGUKA MBOWE LEO.


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo Septemba 22, 2017 amezungumza na vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam kuhusu hali ya Tundu Lissu na mengine yanayoendelea nchini kwasasa.

Hizi ni baadhi ya sentensi zilizonukuliwa kutoka kwenye hotuba yake ya leo.

"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Tundu Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii"- Mbowe

"Ni nani katika vyombo vya ulinzi na usalama, simjui lakini ni vigumu sana kusema tukio la ujambazi, hakuna ujambazi pale." Mbowe.

"Kama serikali inajiamini iko safi kabisa, waruhusu wachunguzi huru kama Scotland Yard waje wafanye uchunguzi kwani hatuna imani na Polisi"- Mbowe

"Mashine yetu Tundu Lissu itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%"-Mbowe

"Waziri Ummy Mwalimu anasema kwamba, serikali ipo tayari kumtibu Tundu Lissu mahala popote dunia, hapo unajiuliza, kwani Kenya si duniani?"- Mbowe

Freeman Mbowe: Spika amesema nimtumie barua, ili aseme kwamba nimemuomba wakati yeye alikuwepo hospitali, ajiandikie mwenyewe.

"Jaji Mkuu anasema uchunguzi utafanyika ndani, tunamwambia asubiri ushahidi Mahakamani, uchunguzi ni mambo ya Polisi"- Mbowe

Freeman Mbowe: Wabunge kutibiwa na serikali ni haki stahiki, Lissu amepata matatizo akiwa kazini.

"Hadi leo bado hatujapokea michango iliyochangwa na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"- Mbowe

Freeman Mbowe: Nawashukuru sana wanahabari mmeripoti tukio hili usiku kucha. Naomba muwe makini na habari pia zinazotolewa.

MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI KUGONGA NG'OMBE SHINYANGA.


#AjaliYaBASI: HUKO SHINYANGA:
Mtu mmoja amefariki na wengine zaidi ya 50 kunusurika baada ya basi la kampuni ya KIDIA ONE kupinduka usiku wa kuamkia leo September 22, 2017.


Basi hilo lililokuwa linatokea Jijini Dar-es-Salaam kuelekea Jijini Mwanza liligonga Ng'ombe majira ya saa sita katika eneo la Usanda kabla ya kupinduka.
NA: ENOS MAKEJA.

TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL 2017 LAFANA TUKUYU MBEYA

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wakicheza pamoja na wasanii wa kikundi cha Ngoma cha Wasonjo kutoka Ngorongoro, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. 
Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA GROUP)
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Masebe Rungwe, wakicheza jukwaani wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Keifo Kyela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana
 Meza kuu
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Keifo Kyela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana

 Mabalozi wa Tulia Trust wakijitambulia jukwaani
 Baadhi ya Mabalozi wa Tulia Trust wakiwa uwanjani hapo wakifuatilia burudani
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Kanengwa, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana
 Majaji wa shindano la ngoma Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, wakifuatilia burudani zilizokuwa zikiendelea jukwaani wakati wa Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Tandale, Tukuyu.
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Kanengwa, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa Tamasha hilo wakishuhudia burudani ya ngoma za asili jukwani katika Tamasha hilo.
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Lipango Mbozi Mkoa wa Songwe, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. 
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Lipango Mbozi Mkoa wa Songwe, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. 
 Wasanii wa kundi la kughani mashahiri ya Asili, Mwandurusa kutoka Kyela, wakighani mashahiri yao jukwaani wakati wa Tamasha hilo.
 Baadhi ya viongozi wakiwatunza wasanii baada ya kushuka jukwaani.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) akiwaongoza baadhi ya viongozi na wadau kucheza Kwaito jukwaani wakati wa Tamasha hilo.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akiwaongoza baadhi ya viongozi na wadau kucheza Kwaito jukwaani wakati wa Tamasha hilo.
 Mwanadada maarufu wa kuchezea mpira,Hadhara Charles, akionyesha umahiri wake jukwaani wakati wa Tamasha hilo.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akimtunza fedha mwanadada, Hadhara Charles, maarufu wa kuchezea mpira,baada ya kuonyesha umahiri wake jukwaani katika Tamasha hilo.
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Wasonjo kutoka Ngorongoro, wakicheza ngoma yao ya asili wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017.

 Waratibu wakimsindikiza msanii wa filamu nchini Senga, wakati akiwasili uwanjani hapo na 'kuchafua hali ya hewa' baada ya kuanza kufuatwa na wananchi kila alikopita kiasi cha kumzuia njia asipite kuingia eneo maalumu waliloandaliwa wasanii wenzake.