ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 13, 2019

ALICIOUS KUTUA MWANZA PASAKA


🛑.....P A S A K A ... hii #JembeDjz kufanya makamuzi chumbani #CLUBvillagE ya #VillaParkResort + Moto zaidi ni pale sebuleni penye #LIVEband safari hii @queenalicios huyu hapa.
.
.
@jembefm itaruka #LIVe toka eneo la tukio. Tag mafrendZ zako waibuke PASAKA hii #VillaParkResort Mwanza #MbeleMbeleYao
@jembenijembe
@kikotifredy
@gijegije
@rama.maganga
@mwakad25
@mansourjumanne
@nattyebrandy
@mustafakinkulah
@deejay_coolcutz
@chrissthedj
@salim_kikeke
@sullybonzo
@ally_jembe_ni_jembe
@danya_juniour
@djaroarungu
@djmike_beatz
@djscorpion
@myna_400
@mkabesah
@eddievied
@kabago
@fauxmundele
@chouchoumaxino
@officialivonakamuntu 🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑🛑

'SIMBA ALIWA NA MAMBA' MAZEMBE vs SIMBA 4 - 1 MAGOLI YOTE 13/04/2019


 SAFARI ya Simba SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika imefikia tamati leo baada ya kuchapwa mabao 4-1 na wenyeji, Tout Puissant Mazembe katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali jioni ya leo Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa matokeo hayo Simba SC inatolewa kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi ya wiki iliyopita mjini Dar es Salaam, hivyo kushindwa kurudia rekodi yake ya mwaka 1974 kufika Nusu Fainali. 

Katika mcheze wa leo uliochezeshwa na refa Janny Sikazwe, aliyesaidiwa na Romeo Kasengele wote wa Zambia na Berhe Tesfagiorgis O'michael wa Eritrea, hadi mapumziko TP Mazembe walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Lakini ni Simba SC waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili tu kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyemlamba chenga kipa Muivory Coast, Sylvain Gbohouo baada ya pasi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na kufunga kiulaini.

Mazembe ikasawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa beki wake Mzambia Kabaso Chongo aliyemalizia pasi ya mshambuliaji Jackson Muleka baada ya kona iliyochongwa na Tressor Mputu.

Na Meschak Elia akaifungia Mazembe bao la pili dakika ya 38 kwa shuti la mguu wa kushoto akitumia makosa ya beki Mburkinabe wa Simba SC, Zana Coulibaly.
Kipindi cha pili, kocha Mbelgiji wa Simba SC, Patrick Aussems akaanza na mabadiliko mfululizo akiwatoa beki Mganda Juuko Murshid na kiungo Muzamil Yassin na kuwaingiza kiungo Mzambia Clatous Chama na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Hayakuwa mabadiliko yenye manufaa kwa timu, kwani yaliwasaidia Mazembe kupata mabao mawili zaidi, wafungaji Tessor Mputu dakika ya 62 na Muleka dakika ya 75, huku kipa Aishi Salum Manula akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo zaidi ya hatari.

Simba SC inarejea Dar es Salaam usiku wa leo kuelekeza nguvu zake kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili iweze kutetea taji lake na kupata tena nafasi ya kucheza michuano ya Afrika msimu ujao. 

Kikosi cha TP Mazembe kilikuwa; Sylvain Gbohouo, Joseph Ochaya, Issama Mpeko, Chongo Kabaso, Kevin Mondeko, Nathan Sinkala, Miche Mika, Rainford Kalaba/Koffi Christian dk76, Meschak Elia, Jackson Muleka na Tressor Mputu/Glody Likonza dk85.

Simba SC; Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Juuko Murshid/Clatous Chama dk53, Jonas Mkude, James Kotei, Muzamil Yassin/Meddie Kagere dk46, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi/Rashid Juma dk71 na John Bocco.

Shirika la Amref lazindua Mradi wa Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Amref Health Africa- Tanzania kwa kushirikiana na Serikali mkoani Mwanza, limetambulisha mradi wa usafi wa mazingira (Pro Poor Wash Enterprise Project Mwanza), utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili katika Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Mradi huo unaofadhiliwa na Jiji la Madridi nchini Hispania ulitambulishwa jana ukilenga kuwafikia takribani wananchi 50,000 hususani vijana na wanawake wanaotoka katika jamii maskini kwa kuwawezesha kukua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa kuzalisha bidhaa mbadala ikiwemo mkaa kutokana na taka ngumu na vinyesi.

Afisa Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira na Afya (WASH) kutoka Shirika la Amref Health Africa-Tanzania, Mhandisi James Mturi alisema mradi huo utasaidia kuondoa taka katika maeneo ya makazi ya wananchi, kuongeza kipato kwa vijana na akina mama pamoja na kupunguza milipuko ya magonjwa.

Akizugumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya alisema mradi huo utasaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa jiji la Mwanza wa mwaka 2004 wa kusimamia taka ngumu, kuboresha vyoo, kusimamia na kuondoa taka katika maeneo ya makazi.

Akiwasilisha mada kwa wadau waliohudhuria utambulisho wa mradi huo, Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene alisema Jiji hilo huzalisha zaidi ya tani 800 za taka ngumu kwa siku ambapo asilimia 74 tu ya taka hizo ndizo hukusanywa na kupelekwa dampo hivyo mradi huo utasaidia kupambana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira.

Naye Meneja Msaidizi- Usafi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Salim Lossindilo alisema asilimia 66 ya wakazi wa Jiji la Mwanza hawajajiunga na mfumo wa majitaka na kwamba zaidi ya asilimia 20 hawana vyoo huku zaidi ya asilimia 90 ya vyoo vikiwa nje ya mtandao wa majitaka wa MWAUWASA.

Katika kutekeleza mradi huo, elimu kuhusu masuala ya utunzaji wa mazingira itatolewa kwa wananchi hadi ngazi ya Kaya ikiwemo ujenzi wa vyoo bora, kujiunga na huduma ya majitaka (kuondoa vinyesi) pamoja na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kibiashara ikiwemo gesi na mkaa kwa kutumia taka ili kuwaimarisha wananchi kiuchumi huku wakiboresha mazingira yao.
Afisa Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira na Afya (WASH) kutoka Shirika la Amref Health Africa-Tanzania, Mhandisi James Mturi akizungumza kwenye kikao cha utambulisho wa mradi wa Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akizungumza kwenye kikao cha utambulisho wa mradi huo.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Wadau waliohudhuria kikao hicho wakimsikiliza Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene  wakati akiwasilisha mada.
Meneja Msaidizi- Usafi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Salim Lossindilo akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Mradi wa Huduma Jumuishi za Kifedha Huboresha Usafi wa Mazingira na Afya (FINISH FORT), Christopher Ndangala akiongoza kikao hicho.
"Energizer time"
Wajumbe wakifurahia "Energizer Session"
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia mada.
Viongozi kutoka Shirika la Amref Health Africa- Tanzania wakiwa kwenye kikao hicho.
Viongozi kutoka Shirika la Amref Health Africa- Tanzania wakiwa kwenye kikao hicho,
Wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi zinazohusika na masuala ya mazingira walioshiriki kikao hicho.
Tazama BMG Online TV hapa chini

TUPO TAYARI KUKABILIANA NA TISHIO LOLOTE LITAKALOJITOKEZA - JENERALI MABEYO.



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali  Venance Mabeyo amesema kuwa hali ya usalama kwenye nchi ni shwari na wakati wote wapo tayari kukabiliana na matishio yoyote yatakayojitokeza.
Jenerali Mabeyo ameeleza hayo leo wakati wa hafla ya  uzinduzi wa mji wa kiserikali uliojengwa Ihumwe mkoani Dodoman ambao unazinduliwa  na Rais wa Tanzania, John  Magufuli.

“Hali ya usalama kwenye mipaka yetu ni shwari, ndani ya nchi yetu JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vya wengine liko tayari kuwalinda wananchi na mali zao, wakati wote tupo tayari kukabiliana na matishio yoyote yanayojitokeza," amesema.

Kuhusu ujenzi wa nyumba na ofisi za Serikali, Jenerali Mabeyo amesema kwa kiasi kikubwa kazi hiyo imefanywa na vijana wa JKT na imefanyika kwa miezi mitano.
Rais Dkt.Magufuli anazindua Mji mpya wa Serikali Uliojengwa Mtumba Jijini Dodoma ambapo unahusisha ofisi za Wizara mbalimbali za Serikali n.k

SEKTA YA AFYA NI NYETI HAIPASWI KUINGILIWA NA WANASIASA - RC Mnyeti


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema sekta ya afya ni nyeti isiyopaswa kuingiliwa na Wanasiasa ila Madaktari na wauguzi wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwemo kuzuia vifo vya mama na mtoto.

Mnyeti aliyasema hayo mjini Babati, wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, madaktari na wauguzi kwenye uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama.

Alisema kazi ya viongozi ni kusimamia utekelezaji na madaktari na wauguzi wafanye kazi zao kwa vitendo huku wakitumia lugha nzuri pindi wanapotoa huduma kwa wagonjwa.

Alisema wataalamu wa afya wanapaswa kutimiza wajibu wao katika uwajibikaji na kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga waweze kuwa watu wazima.

“Kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza jukumu lake ikiwemo kupatiwa huduma bora ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto pamoja na kutoa elimu kuanzia ngazi ya jamii,” alisema Mnyeti.

Alisema kwa mujibu wa sera za afya nchini, huduma za uzazi hutolewa bure ila kuna baadhi ya maeneo malalamiko ya mama wajawazito kudaiwa fedha yamekuwa yakitolewa.

“Halmashauri na wengineo kasimamieni hilo inawezekana suala la kuwatoza fedha wajawazito au wa mama waliojifungua halipo kwetu ila lichunguzwe na kufanyiwa kazi,”  alisema Mnyeti.

DAWASA KUFUFUA VISIMA VYA PEMBEZONI KWA MJI DAR ES SALAAM NA PWANI

Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya (mwenye kofia) akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kushoto) mara baada ya kutembelea mradi wa Kisima cha Maji cha Gezaulole kichojengwa kwa muda mrefu na kimekuwa kikitoa huduma kwa watu wachache tu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha ramani ya mtandao wa maji utakavyokuwa wakisambaziwa wananchi na Gezaulole.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha genereta inayotumika kufua umeme kwa ajili ya kusambazia wakazi wa Gezaulole.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasha mashine.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionyeshwa mashine zilizokuwa zikitumika kuvuta maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha kisima cha maji kinachotumika kusambazia wakazi wa Vijibweni, Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja  akitoa maelekezo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza mchakato wa kuvifufua na kuvirejesha visima vilivyojengwa na  Serikali na kuachwa kwa muda mrefu bila kutumika kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa pembezoni mwa mji.

Akizungumzia mchakato huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuna maeneo ambayo hayana mtandao wa maji ya bomba kwahiyo wameamua kuvifufua visima vilivyojengwa muda mrefu na serikali au wahisani ili viweze kuhudumia wananchi wa maeneo hayo na yaliyokaribu.

Amesema, kuna kisima kilichopo Gezaulole na Vijibweni tayari wameshaanza kuvifanyia tathmini na vinatarajia kuanza kutoa maji kwa wananchi wa maeneo hayo na yaliyokaribu nao.

“Visima hivi vilijengwa kwa muda mrefu sana, katika maeneo ambayo hayana mtandao wa DAWASA tumeamua kuwapelekea huduma ya maji kwa kutumia visima hivi ambavyo maji yake ni safi na salama,”amesema Luhemeja.

“Ninapoongelea asilimia 85 ya wananchi wanaotumia maji safi na salama ndani ya mkoa wa Dar es Saalaam namaanisha na huduma hii ya visima, na lengo letu ni kuhakikisha kuwa ifikapo Juni 2020 tunataka Watu wote wawe wanapata maji,”

Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa amesema bado wanaendelea na tathmini ya kufahamu visima hivyo vina uwezo wa kuhudumia wananchi wa ngapi pamoja na kujenga tenki la kuhifadhi la maji.

Nao Wananchi wa eneo la Gezaulole wamefurahi kuona wanatarajia kupata maji safi na salama kwakuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wanatumia maji ya visima ambapo ni vifupi na kuhatarisha maisha yao kiafya hususani ifikapo kipindi cha mvua, visima huchafuka na kuchanganyika na udongo.

Kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam unapata maji Lita Milion 502 kutoka kwenye vyanzo vya Ruvu juu, Ruvu Chini na Mto Kizinga.

Ziara hiyo itaendelea tena kesho kwa kutembelea miradi mingine ikiwemo maunganisho mapya ya wateja, mradi wa Maji Chalinze na Miradi mingine inayoendelea kujengwa kwa kutumia fedha za ndani za DAWASA ambapo takribani Bilion 3 zinatumika kila mwezi.

Friday, April 12, 2019

HALMASHAURI YA IRINGA YAPOKEA MSAADA WA GARI KUTOKA KWA SHIRIKA LA IBO

Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota Hiece na mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.   Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa kwenye gari hilo aina ya Toyota Hiece baada ya kukabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
 Gari aina ya Toyota Hiece lilokabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Iringa wakifurahia kupokea kwa msaada wa Gari hilo

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
 
HALMASHAURI ya wilaya ya Iringa imepokea msaada wa gari aina ya Toyota Hiece kwa ajili ya wanafunzi wa elimu maalumu katika shule ya msingi Kipera kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la IBO lililoko nchini Italy kwa ufandhili wa wadau kama Waldesian Church,Emilia-romagna Region,Ferrara Town,Helpicare na Nyumba ya Ali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Gari hilo mwakilishi wa IBO Iringa DC, Paola Ghezzi alisema kuwa shirika lisilo la kiserikali la IBO limekuwa likijishughulisha na elimu maalumu kwa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.

“Shirika hili linafanya kazi na halmashuri ya Iringa kwa kusaidia watoto wenye changamoto hizo hapo juu kwa lengo la kuwasaidia kiuchumi na kuwawezesha kupata mahitaji yao kama ilivyo kwa watoto wengine wanaopata mahitaji yote muhimu” alisema Ghezzi

Ghezzi alisema kuwa shirka hilo tayari limeshasaidia ujenzi wa jiko la shule ya msingi Kipera yenye watoto mchanganyiko na watoto wenye ulemavu  na ujenzi huo bado unaendelea katika shule hiyo kwa lengo la kutoa hudumu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo.

“Tumefanikiwa kujenga Ramps katika shule nne za halmashauri ya Iringa ambazo ni Ismani,Idodi,Ihehelo na Tungamalenga kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupita bila kupata usumbufu wowote ule” alisema Ghezzi

Aidha Ghezzi alisema kuwa shirika hilo limefanikiwa kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya arobaini (40) kwa kuwaongezea maarifa kwa ajili ya kufundisha elimu maalumu kwa wanafunzi wanahitaji elimu hiyo katika halmashauri ya Iringa katika kata za Idodi na Ismani tayari washapewa mafunzo.

“Tumefanikiwa kutoa semina na maonesho kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu maalumu kwa kata ya Ismani ambapo shirika limefanikiwa kutoa elimu hiyo kwa jamii hadi hivi sasa” alisema Ghezzi

Akipokea gari hilo aina ya Toyota Hiece mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa aliwakikishia shirika la IBO kuwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa katika halmashauri hiyo utatumika kama ulivyokusudiwa na miradi yote itatunzwa kikamilifu.

“Mmetusaidia sana miradi mingi hivyo sisi tunaahidi kutunza na kuthamini miradi na uwepo wenu katika halmashauri hii ambapo mmetusaidia kuwaokoa watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu” alisema Mhapa

Mhapa alisema kuwa imekuwa vigumu mno kumlea mtoto mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu na mtoto mwenye ulemavu kwa kuwa inahitaji uangalizi mkubwa mno ila shirika la IBO limetusaidia kulea watoto hao.

“Namna ilivyo tabu kumlea mtoto mwenye mahitaji maalumu,mtoto mwenye mazingira magumu na mtoto mwenye ulemavu,wakina mama mnajua ilivyo kuwa kazi ngumu hivyo tunaomba kutoa shukrani zetu kwa wadau ambao wanatusaidia kulea watoto hao” alisema Mhapa

Mhapa alimalizia kwa kuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa kuhakikisha wanawaandikia barua ya shukrani kwa shirika la IBO kwa kuasiadia miradi mbali mbali ambayo imekuwa ikiwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu,watoto wenye mazingira magumu na watoto wenye ulemavu.

Lakini Mhapa aliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali kwa kuwa bado halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za watoto hao na nyingi zinazoshabiana na changamoto hizo hivyo mkipata kitu tunaomba mtukumbuke ili tuendelee kutatua changamoto hizo.

KATIBU WA IPC:WAANDISHI WA HABARI ACHENI KUWA MAAFISA HABARI

Katibu wa Iringa Press Club (IPC),Tukuswiga Mwaisumbe akiongea na mwandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yatakayofanyika siku ya tarehe 03 / 05 / 2019


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WAANDISHI wa habari mkoani Iringa wametakiwa kuacha kuandika habari kama maafisa habari wakati kunachangamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa kina.

Akizungumza na blog hii Katibu wa Iringa Press Club (IPC),Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa waandishi wengi waandika habari za mialiko kuliko kuandika habari za kichunguzi ambazo zinatija kwa taifa kwa maendeleo ya nchi.

“Kwetu waandishi wa habari tumekuwa tukisubilia kupewa habari na viongozi mbalimbali na ndio maana tumekuwa tunaandika wanachotaka wao lakini sio waandishi hapo zamani tulikuwa tunauwezo wa kuhoji kutokana na changamoto za wananchi” alisema Mwaisumbe

Mwaisumbe alisema kuwa jukumu kubwa la waandishi wa habari ni kukusanya na kuzichakata na kuzichapisha habari na kumekuwa na changamoto kubwa ni kukusanya habari kutokana sheria mbalimbali ambazo zimetolewa hivi karibuni.

Kuna sheria kandamizi kwa waandishi wa habari ambazo zinasababisha waandishi wa habari kuwa maafisa habari kutokana na sheria zifuatazo,Sheria ya mitandao ya kijamii,sheria ya takwimu,sheria ya upatinaji wa habari na sheria ya huduma kwa vyombo vya habari 

“Sheria hizi zimekuwa kikwazo kwa waandishi wa habari kutokana na kanuni zake jinsi zilivyo na zinavyofanya kazi mfano sheria ya huduma kwa vyombo vya habari inamruhusu kama wa polisi kuchukua vifaa vya habari na kukaanavyo hadi atakapo maliza uchuguzi wake hizo ndio changamoto zilizopo” alisema Mwaisumbe

Mwaisumbe alisema kuwa mwandishi wa habari ni kiungo muhimu katika ya wananchi na viongozi mbalimbali kwa kuwa anachujukumu na kufichua changamoto za wananchi na kuzifikisha kwa viongozi kwa lengo la kutatua changamoto hizo.

Mwandishi anajukumu la kutafuta changamoto za wanachi na kuzifikisha kwa viongozi kwa namna ambavyo anafanya kazi kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto hiyo,na ndio maana ya mwandishi kuwa daraja kati ya wananchi na serikali.

Mwaisumbe alisema kuwa kwa mfumo uliopo hivi sasa imekuwa vigumu mno kumpata kiongozi hasa viongozi wa kiserikali kujibia zile kero ambazo umezifumbua kwa wananchi kwa hiyo ni changamoto kubwa kwa waandishi katika kipindi hiki.

“Unaweza ukamtafuta kiongozi furani kujibia kero za wananchi huwezi kupata huo muda labda ajisikie yeye lakini kiongozi huyo akiwa na shida na vyombo vya habari atawaita kwa muda wake tena kwa kujisia yeye mwenyewe huu ndio mfumo ambao tunao hivi sasa” alisema Mwaisumbe

Mwaisumbe alimalizia kwa kuwasema kuwa kwa sasa habari za radio,televiseni na magazeti kwa sasa habari zote zinahabari zote zinazofanana kutokana na sheria zilizopo ambazo zinamfunga mwandishi kutanua wigo wake wa uandishi

“Kama nilivyosema hapo awali kuwa habari nyingi hivi sasa hazina radha ile inayotakiwa kwa walaji wa habari hivyo ipo siku taaluma hii itakufa kwa kuwa wanaofanya habari za kichunguzi hazipo tena” alisema Mwaisumbe