Katibu wa Iringa Press Club (IPC),Tukuswiga Mwaisumbe akiongea na mwandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yatakayofanyika siku ya tarehe 03 / 05 / 2019
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WAANDISHI wa habari mkoani
Iringa wametakiwa kuacha kuandika habari kama maafisa habari wakati
kunachangamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi ambazo zinahitaji kutafutiwa
ufumbuzi wa kina.
Akizungumza na blog hii Katibu wa
Iringa Press Club (IPC),Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa waandishi wengi
waandika habari za mialiko kuliko kuandika habari za kichunguzi ambazo zinatija
kwa taifa kwa maendeleo ya nchi.
“Kwetu waandishi wa habari
tumekuwa tukisubilia kupewa habari na viongozi mbalimbali na ndio maana
tumekuwa tunaandika wanachotaka wao lakini sio waandishi hapo zamani tulikuwa
tunauwezo wa kuhoji kutokana na changamoto za wananchi” alisema Mwaisumbe
Mwaisumbe alisema kuwa jukumu
kubwa la waandishi wa habari ni kukusanya na kuzichakata na kuzichapisha habari
na kumekuwa na changamoto kubwa ni kukusanya habari kutokana sheria mbalimbali
ambazo zimetolewa hivi karibuni.
Kuna sheria kandamizi kwa
waandishi wa habari ambazo zinasababisha waandishi wa habari kuwa maafisa
habari kutokana na sheria zifuatazo,Sheria ya mitandao ya kijamii,sheria ya
takwimu,sheria ya upatinaji wa habari na sheria ya huduma kwa vyombo vya habari
“Sheria hizi zimekuwa kikwazo
kwa waandishi wa habari kutokana na kanuni zake jinsi zilivyo na zinavyofanya
kazi mfano sheria ya huduma kwa vyombo vya habari inamruhusu kama wa polisi
kuchukua vifaa vya habari na kukaanavyo hadi atakapo maliza uchuguzi wake hizo
ndio changamoto zilizopo” alisema Mwaisumbe
Mwaisumbe alisema kuwa
mwandishi wa habari ni kiungo muhimu katika ya wananchi na viongozi mbalimbali
kwa kuwa anachujukumu na kufichua changamoto za wananchi na kuzifikisha kwa
viongozi kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Mwandishi anajukumu la kutafuta
changamoto za wanachi na kuzifikisha kwa viongozi kwa namna ambavyo anafanya
kazi kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto hiyo,na ndio maana ya mwandishi
kuwa daraja kati ya wananchi na serikali.
Mwaisumbe alisema kuwa kwa
mfumo uliopo hivi sasa imekuwa vigumu mno kumpata kiongozi hasa viongozi wa
kiserikali kujibia zile kero ambazo umezifumbua kwa wananchi kwa hiyo ni
changamoto kubwa kwa waandishi katika kipindi hiki.
“Unaweza ukamtafuta kiongozi
furani kujibia kero za wananchi huwezi kupata huo muda labda ajisikie yeye
lakini kiongozi huyo akiwa na shida na vyombo vya habari atawaita kwa muda wake
tena kwa kujisia yeye mwenyewe huu ndio mfumo ambao tunao hivi sasa” alisema Mwaisumbe
Mwaisumbe alimalizia kwa
kuwasema kuwa kwa sasa habari za radio,televiseni na magazeti kwa sasa habari
zote zinahabari zote zinazofanana kutokana na sheria zilizopo ambazo zinamfunga
mwandishi kutanua wigo wake wa uandishi
“Kama nilivyosema hapo awali
kuwa habari nyingi hivi sasa hazina radha ile inayotakiwa kwa walaji wa habari
hivyo ipo siku taaluma hii itakufa kwa kuwa wanaofanya habari za kichunguzi
hazipo tena” alisema Mwaisumbe
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.