Awa kivutio
mazoezini" "Gazeti moja laumbuka kwa propaganda za Simba"
"Kisa eti ametekwa na Simba"
Hatimaye aliyekuwa beki wa kutumainiwa wa klabu ya Simba katika msimu
uliopita Kevin Yondan "Vidic" leo amekata mzizi wa fitina baada ya kuanza rasmi
mazoezi katika uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya klabu ya Yanga na kuwa
kivutio katika mazoezi hayo.
Kipenzi hicho cha Yanga kiliwasili majira ya saa tatu kasoro dakika kumi
asubuhi, ambapo mara baada ya kushuka katika gari mashabiki waliofurika katika
mazoezi hayo walipomuona ghafla walimshangilia kwa vifijo na nderemo huku
akielekea uwanjani akiwapungia mashabiki hao mikono.
Vidic ambaye ana mapenzi makubwa na klabu ya Yanga, leo ameripotiwa na
chombo kimoja cha habari kuwa eti alitekwa hapo jana na klabu ya Simba na
kudaiwa kushiriki katika mazoezi na timu yake hiyo ya zamani.
Kelvin
Yondan
Mchezaji huyo ambaye kila kukicha timu yake hiyo ya zamani ikiendelea
kumuota kwa mazuri aliyowafanyia amekuwa gumzo kwa kipindi hiki cha usajili
ambapo timu yake mpya ya Yanga ikiendelea kufanya kufuru ya usajiri ambao
unatarajiwa kumalizika Julai 15 Mwaka huu.
Yondan hivi karibuni aliwashukuru wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba
kwa ushirikiano aliokuwa akiupata wakati akiitumikia timu hiyo,aliweka bayana
mara baada ya kumwaga wino kuichezea Klabu ya Yanga kuwa Simba isihangaike na
yeye kwakuwa hana mpango tena wa kuichezea klabu yake ya zamani.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanachama mmoja wa klabu ya Simba kwa
jina maaraufu (Kobe) muda mfupi uliopita wakati
www.youngaficans.co.tz ikiwa mitamboni aliwasili katika mazoezi ya timu ya Yanga
yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Kaunda kwa ajili ya kutaka kuhakikisha
juu ya uvumi wa beki Kevin Yondan kuwa yupo katika mazoezi.
Mara baada ya kumshuhudia mchezaji huyo akifanya mazoezi mwanachama huyo
aliangua kilio uwanjani hapo huku mashabiki wa Yanga wakishangilia na kumnunulia
maji ya matunda pamoja na uji.
Wachezaji wengine walioanza mazoezi leo ni pamoja na kiungo wa timu ya
Taifa Frank Domayo aliyekuwa JKT Ruvu na mshambuliaji wa timu ya Taifa Saimon
Msuva aliyekuwa Moro United.
Naye Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Fredy Felix Minziro amesema kikosi
chake chote kinatarajiwa kukamilika mara baada ya wachezaji Haruna Niyonzima
aliyekuwa na timu ya Taifa lake(Rwanda) na Rashid Gumbo anayeumwa malaria
watakapojiuunga na kikosi hicho.
Habari kwa hisani ya
http://www.youngafricans.co.tz