TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Mcheza
sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye
mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na
ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro
Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila
mwaka.
Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi (3) |
Ujio
wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect
Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa
Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na
hadhi yake.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema
kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana
furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko
Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu,
wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie
niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi
ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri
kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza
nchini Marekani.
“Sasa
nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu
duniani uko Tanzania na sio Kenya”
alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika
kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz
ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard
Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park.
Mji
wa Moshi na viunga vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani
ambao wamekuja kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa
kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon
zilianzishwa na Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania
wa Tanzania nchini Misri.
Mbio
hizi zimejijengea umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi
zikiwa zimetolewa na Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya
milioni 5 likiwa limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani
wakati jarida la Forbes la Marekani lenye wasomaji wengi duniani limeipa nafasi
ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances
Boulevard”mwaka 2009.
Mbio
hizi hukimbiwa na watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima
Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon
zinajulikana kama 7 continental races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya
dunia.
Ratiba
ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto
yatima cha Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na
watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz
Disney mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani.
Siku
ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa
shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria
Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua
namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.
Imetumwa
na:
Grace Soka
Afisa
Uhusiano
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.