ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 18, 2012

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MATEMBEZI KUCHANGIA AKINAMAMA WENYE MATATIZO YA FISTURA CCBRT

Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa (Finde your Moyo). Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.

Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria kuanza kwa matembezi hayo kwenye hoteli ya Golden Tulip kulia ni Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Dk. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa akizungumza na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.

Wakiwa katika mzungumzo kabla ya kuanza kwa matembezi hayo kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam ya kipolizi Suleiman Kova, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadji Mponda. Picha na www.fullshangwe.blogspot.com

Friday, February 17, 2012

WHITNEY KUZIKWA KESHO BOBBY AZUIWA KUMZIKA

Familia ya Whitney imewasikitisha maelfu ya mashabiki wa mwanamuziki huyo kutokana na kudai kuwa maziko yatafanyika kesho jumamosi kwa kuhusisha familia na wale watakaopewa mwaliko maalum tu.

Sehemu waliyopanga yafanyike mazishi hayo ina uwezo wa kuchukuwa watu 1,500 wakati awali kulikuwa na taarifa kuwa zoezi la kuuaga mwili lilikuwa lifanyike katika Ukumbi wa Prudential Center unaochukuwa watu 18,000.

Mume wa zamani wa marehemu, Bobby Brown ana uwezekano wa kukosa kuhudhuria maziko kwa kile kinachodaiwa kuwa familia haimuhitaji.


Bado kuna wingu kubwa la maswali likiwa limetanda juu ya kifo chake kwani watu wa karibu na marehemu wameeleza kuwa siku chache kabla ya umauti kumfika alisema anataka kuonana na Yesu na alikuwa akisissitiza juu ya hilo pia shoo yake ya Mwisho kuifanya alivaa nguo nyeusi tupu.

Peter Tatchell ambaye ni mtetezi wa haki za watu wa jinsia moja wenye uhusiano wa kimapenzi aliandika katika mtandao wake kuwa, Whitney aliwahi kuwa mmoja wao lakini alifanya hivyo kwa siri miaka ya nyuma.

HAMU YA USHINDI IMEENEA NCHI NZIMA

Yanga na Simba ziko katika kibarua kigumu kesho, kwa wale waliosafiri na Simba kwa lengo la kuisapoti twawaunga mkono tukiwa home.Shabiki wa Yanga akiwa amevalia jezi ya Niyonzima katika mitaa ya jiji la Mwanza.
Tuliobaki nyumbani hatuna budi kuiunga mkono Yanga kwa kuwa ndiyo timu ya Tanzania. Si sahihi hata siku moja kwa Watanzania kutumia nguvu zao kuiunga mkono timu ya Zamalek ambayo ni Adui wa Yanga kesho.

Hamu ya ushindi yapaswa kuenea nchi nzima kama shabiki huyu wa Yanga Afrika toka jijini Mwanza ambaye anaiombea kila la kheri ya timu yake ipate ushindi kwa mchezo wa kesho, sambamba na kuwatakia watani wao wa jadi Simba ambao nao wana kipute Kigali nchini Rwanda.

Mungu ibariki Tanzania.

CITY NA UNITED WATAMBA LIGI YA EUROPA

Mchezaji wa zamu Sergio Aguero alipata bao dakika za mwisho na kuiwezesha Manchester City, baada ya kufungwa, hatimaye kuweza kujikakamua na kupata ushindi wa magoli 2-1 ilipocheza na Porto ya Ureno, usiku wa Alhamisi, ikiwa ni mechi ya mkondo wa kwanza wa mechi ya ligi ya Europa, kati ya timu 32 ambazo bado zimo katika mashindano.

Licha ya Porto kutangulia kufunga Man City waliibuka na ushindi Porto, ikicheza katika uwanja wa nyumbani, ilikuwa imetangulia kwa kupata bao kupitia Silvestre Varela.

Man City walipata nafasi ya kusawazisha wakati Alvaro Pereira alijifunga mwenyewe kwa kuuelekeza mpira kwa bega hadi wavuni, kufuatia mkwaju kutoka Yaya Toure, mpira ambao alitazamia utamfikia Balotelli.

Manchester United wamo katika hali bora zaidi baada ya kupata mabao ugenini Katika mechi ya awali, Ashley Young na Javier Hernandez walifanikiwa kufunga magoli katika kipindi cha pili, na kuishinda Ajax magoli 2-0, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea katika mashindano ya ligi ya Europa.

Bao la pili Hernandez bila shaka litaisaidia sana United itakapoikaribisha Ajax katika uwanja wa Old Trafford kwa pambano la mkondo wa pili tarehe 23 mwezi huu wa Februari.

Licha ya kwamba vilabu mwamba vya Uingereza vimezoea zaidi ligi ya mabingwa na ambao inaheshimika zaidi kushinda Europa, meneja Ferguson ameelezea kwamba wao washatulia baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa, na sasa wanaonyesha ustadi wao kiufundi katika mashindano ya Europa.

Thursday, February 16, 2012

TOTO YACHARAZWA 2-0 DIMBA LA NYUMBANI

Timu ya soka ya Toto ya jijini Mwanza leo hii ikiwa nyumbani katika dimba lake la CCM Kirumba imezididi kujichimbia kaburi mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.Choki Abeid ambaye ni Kocha wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara kwa kusuasua kutokana na ukata unaoiandama kiasi cha wachezaji wake kucheza kwa kujitolea yaani bila mishahara amesema kuwa sababu za timu yake kupoteza mchezo huo muhimu ni wachezaji wake kukosa umakini na maandalizi mabovu lakini hata hivyo kocha huyo ana matumaini kuwa iwapo wadau watasikiliza kilio chao mambo yatabadilika na kujitengenezea mazingira mazuri kubaki ligi kuu.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar timu ambayo ilianza msimu wa pili ligi kuu kwa kichapo kocha wake msaidizi Patrick Mwangata anapinga timu yake kupata ushindi kwa kutegemea timu vibonde akisema kuwa Mtibwa ni moja kati ya timu zenye ushindani ligi kuu na hata matokeo katika msimamo wa ligi kuu zilizopita timu hiyo imekuwa ndani ya top four.

MZEE YUSUF AKARIBISHWA VALENTINE'S DINNER NA KUTUNIKIWA ZAWADI NYUMBANI KWA MISSY TEMEKE

Angalia Video ya Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, alivyokaribishwa rasmi valentines dinner, nyumbani kwa Missy Temeke, akishirikiana na Sophia Mmombasa, Salama Salma Jay Jay, Auntie Waheeda Margaret Gathesha, na Baadhi ya mabanati wa Wasington DC na kutunukiwa zawadi mbali mbali na wakaazi wa MD kwa hisani kubwa ya kutumbuiza siku ya Jumamosi ya Feb 5, 2012 ndani ya Washington DC Nchini Marekani. Daima tutamkumbuka Mzee Yusuf Al-batwa!! http://swahilivilla.blogspot.com/

WAFUNGWA 300 WATEKETEA KWA MOTO HONDURAS

Wanajeshi, polisi na waandishi wa habari wakijihami na machafuko yaliyotokea mara baada ya wananchi kuvamia gereza.
Takriban wafungwa 300 wameuwawa katika moto ulioteketeza jela moja nchini Honduras kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

Wananchi waliochachamaa walivunja geti la lango kuu la gereza na kuingia ndani.
Wengi wao waliteketea au kukosa hewa katika seli zao za jela ya Comayagua, kaskazini mwa mji mkuu Tegucigalpa.

Maafisa wa serikali wanasema imethibitishwa takriban 300 wamekufa lakini wengine 56 kati ya wafungwa 853 katika gereza hilo hawajapatikana na inadhaniwa wameteketezwa.


Jamaa wa wafungwa hao walipambana na polisi pale walipojaribu kuvamia jela hiyo wakitafuta maelezo zaidi ya majaaliwa ya watu wao.

Polisi walipaswa kufyatua risasi hewani na kutumia gesi ya kutoa machozi. Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha moto huo kama ulisababishwa na hilitalfu katika nyaya za umeme ama zilichochewa na ghasia za wafungwa.

Rais Lobo wa Honduras ameahidi uchunguzi kamili ulio wazi na kusema hillo ni janga lisilokubalika.

Alisema wakuu wa magereza wa kitaifa na wa eneo la moto huo watasimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea.


Wafungwa waliojeruhiwa.
Wafungwa wengine wanatibiwa majeraha makali ya moto kwenye hospitali mjini Tegucigalpa.

Wednesday, February 15, 2012

JIONEE TASWIRA USIKU WA VALENTINE GOLD CREST

Promota Dj Ally Coco kutoka Coco Entertainment akikabidhi zawadi ya Tiketi ya ndege kwenda na kurudi kupitia shirika la ndege la Fly 540 kwa mshindi wa droo ya usiku wa Valentine.

Mtu mzima King Kikii alizikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wake.

King Kikii alishirikiana na vijana wa Hill Way Band kumwaga burudani.

Ni wakati wa Kitambaa cheupe.

Meneja wa Gold Crest Hotel bi Elizabeth akitangaza washindi wawili aliojishindia zawadi ya kulala usiku mmoja hotelini hapo kupitia shindano la kucheza muziki.

Meza yetu kutoka kulia ni Wife, mie na shem Jackline.

Meza ya marafiki na dinner.

Mwanamuziki King Kikii, Dj Ally Coco na Meneja wa Gold Crest Hotel Bi. Elizabeth wakibadilishana mawazo.

Tuesday, February 14, 2012

MAANDALIZI YA VALENTINE LEO GOLD CREST MZ

VALENTINE MWANZA NA KING KIKII< Kutoka kushoto ni Promota Dj Ally Coco, Mwanamuziki King Kikii na mwimbaji Zed wakiwa katika maandalizi.

Ishasemwa kuwa ni Dinner and Dance na hivi ndivyo imemaanishwa.

Ni Valentine wandugu wapenzi.Wahi mapema ili hii iwe meza yako..

Ukumbi wa shughuli ndani ya Gold Crest katika hatua za awali upambaji leo....

Mdau kesha tupia saa nyingiiii...

Yaani ni maandari smart, safi, clean ikikusubiri wewe tu!!

Muhksin Mambo wa Star Tv akifanya mahojiano maalum na Mwandaaji wa Usiku wa Valentine utakaofanyika leo Gold Crest Hotel toka Coco Intertainment DJ Ally Coco.

Mwonekano wa mjengo wa Hotel Gold Crest nyakati za usiku hapa ndipo shughuli ya Valentine inayosubiriwa kwa hamu Mwanza inakwenda fanyika usiku wa leo....
!!!USIKOSE!!!

JINSI SIKU ILIVYOANZA LEO ME AND MY FAMILY

Upendo huanzia nyumbani kwa familia kisha kwa majirani na jamii kwa ujumla Leo asubuhi Queen wangu aliandaa keki kisha kila mmoja akajichukulia kipande chake huku wengine tukilishana kama kawazzzz!!!...

HAPPY VALENTINE 2 YOU ALL.

DOREEN HII NI TIME YAKO BANA.....!!!!

Leo ni siku ya kuzaliwa mwanadada Doreen Goodluck, Blogu hii na wadau wake wote yakutakia kila la kheri katika life, Inshahlah Mwenyezi azidi kukushushia neema kwa kila chema uombacho hatimaye uzime mishumaa 100 hivi na nini na nini...

'aaaah Hepi bazdeiiiiii'

Monday, February 13, 2012

WAPENZI WA DHATI KUJUMUIKA KESHO GOLD CREST KUSHEREHEKEA VALENTINE NA KING KIKII

Valentines with King kikii Special Dinner & Dance at Gold Crest Hotel Nyerere Hall From 7:00pm-on wards
King Kikii will be live on the Stage
Entrance 30,000 For Single
50,000 for Couples before
60,000 for Couples at the gate
COME AND ENJOY WITH KING KIKII (kitambaa cheupe) AT
GOLD CREST HOTEL

ZAMBIA WAIDUWAZA IVORY COST 2012

Zambia imechukua ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 7-8.Mchezo huo ulimaliza dakika 90 za kawaida, kabla ya kwenda muda wa ziada, na hadi katika mikwaju ya penati.

Awali nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alikosa penati ambayo ingeipa ushindi kabla ya kumalizika kwa dakika 90 za kawaida.

Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga ambapo Kolo Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.

Ivory Coast wataendelea kusubiri kunyakua kombe hilo, licha ya kuwa na wachezaji kadhaa wanaocheza Ulaya hasa katika Ligi Kuu ya England.

Tembo wa Ivory Coast walipoteza katika mchezo wa fainali mwaka 2006 dhidi ya Misri kwa mikwaju ya penati.

Lakini kwa Chipolopolo, ambao wamewahi kushika nafasi ya pili mara mbili, wamemaliza kwa ushindi kwa kuhanikizwa na vifo vya wachezaji wenzao mwaka 1993, baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja ilipochezewa fainali mjini Libreville.

Mara ya mwisho kwa timu hiyo kutoka Kusini mwa Afrika kufika fainali ilikuwa mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 wa nchi hiyo kupata ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Gabon.

Wakielekea katika mchezo wa fainali, wachezaji hao wa sasa walisema wanahisi nguvu kutokana na kukumbuka janga lililowapata wenzao.

Kwa kushinda mchezo wa fainali, wameonesha dhamira ya kuwashinda wapinzani wao ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi.

Sunday, February 12, 2012

WHITNEY HOUSTON HATUNAYE TENA

Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani Whitney Houston amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48, kwa mujibu wa Kristen Foster, mwandishi wake wa habari.

Kwa mujibu wa CNN, Houston alitangazwa kuaga dunia majira ya saa 3:55 p.m. PT at the Beverly Hilton Hotel. Sababu za kifo chake bado hazifahamiki, lakini kuna uvumi mkubwa ulioenea ukisema kuwa ni baada ya kubwia kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya.

Akiwa mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio makubwa duniani, pia aliwahi kuwa mcheza filamu, katika michezo kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.

Whitney´s Houston Last Song Video (Final Performance) Fani yake iliwahi kuzongwa na matumizi ya dawa za kulevya na maisha yake yenye matatizo katika ndoa na msanii Bobby Brown.