Wanajeshi, polisi na waandishi wa habari wakijihami na machafuko yaliyotokea mara baada ya wananchi kuvamia gereza. |
Wananchi waliochachamaa walivunja geti la lango kuu la gereza na kuingia ndani. |
Maafisa wa serikali wanasema imethibitishwa takriban 300 wamekufa lakini wengine 56 kati ya wafungwa 853 katika gereza hilo hawajapatikana na inadhaniwa wameteketezwa.
Jamaa wa wafungwa hao walipambana na polisi pale walipojaribu kuvamia jela hiyo wakitafuta maelezo zaidi ya majaaliwa ya watu wao.
Polisi walipaswa kufyatua risasi hewani na kutumia gesi ya kutoa machozi. Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha moto huo kama ulisababishwa na hilitalfu katika nyaya za umeme ama zilichochewa na ghasia za wafungwa.
Rais Lobo wa Honduras ameahidi uchunguzi kamili ulio wazi na kusema hillo ni janga lisilokubalika.
Alisema wakuu wa magereza wa kitaifa na wa eneo la moto huo watasimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea.
Wafungwa waliojeruhiwa. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.