GSENGOtV
Hatimaye mwili wa Mzee Julius Kakono Mabula umezikwa hii leo jijini Mwanza katika makaburi ya RC Parokia ya Kirumba jijini Mwanza.
Majonzi na simanzi vimetawala tangu kanisani kwenye ibada ya kuuaga mwili wa marehemu hata makaburini wakati wa kuupumzisha mwili wa marehemu Julius Makono Mabula aliyekuwa mume wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na hata vyama mbalimbali vya siasa wameshiriki katika hatua zote za safari hiyo ya mwisho ya mzee huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na hata katika kanisa la Roman Katoliki Mwanza.
Kwaheri....
This Photo Credit by ABC Studios Mwanza.
Picha enzi za uhai wake Marehemu Julius Mabula.
Katika kukamilisha ibada familia ya marehemu Julius Mabula ilijumuika pamoja na kufunga kwa sala iliyoongozwa na kanisa.
Jiografia ya umati uliojitokeza kanisani kushiriki ibada.
Kwaya ikihudumu katika sala ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Julius Mabula.
Ibada ikiendelea.
Nyimbo mbalimbali ziliimbwa.
Ibada ya mazishi katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.
Ibada ya mazishi katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi komred Angelina Mabula akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mumewe Julius Mabula mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika hii leo jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi komred Angelina Mabula akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu mumewe Julius Mabula mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika hii leo jijini Mwanza.
Watoto na wajukuu wa wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika hii leo ni katika viwanja vya makaburi ya Rc Kirumba Mwanza.
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Nishati na madini Dkt. Medard Kalemani akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mwanasheria mkuu mpya wa serikali Dkt Adelardus Kilangi akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ambaye pia alimwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Busega Raphael Chegeni, akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa na makada wa kada mbalimbali CCM wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakuu wa mikoa mbalimbali wakiongozwa na mwenyeji wao mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (kulia mwenye shati jeupe na madoa meusi) wakiendelea na zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Waheshimiwa wakuu wa wilaya nao wamehudhuria hapa.
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Mhe. James Bwire akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkurugenzi wa wilaya ya Ilemela Paul Wanga (kushoto) na Waheshimiwa wengine katika zoezi la kuweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Marry Tesha akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Kwa pamoja waheshimiwa wakiweka mashada.
Kwa pamoja viongozi wa madhehebu mbalimbali, makanisa na misikiti wakiweka mashada.
Kanisa Katoliki parokia ya Kirumba.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Juma Nature akimpa mkono wa pole mama Angelina Mabula mara baada ya kumalizika shughuli za mazishi.
Hatua za mwisho ndugu, watoto, jamaa na marafiki wa familia katika kaburi la marehemu Julius Mabula.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akiwasha mshumaa kwenye kaburi la marehemu Mzee Julius Mabula.
Sala ya shukurani mara baada ya kukamilika kwa mazishi.