ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 16, 2018

WANAFUNZI 70,904 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo,  Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya Sanaa na biashara. Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Waziri Jafo alisema jumla ya wanafunzi 11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.