Watu 12 wafariki dunia na wengine 22 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori la mizigo mkoani Iringa.
Lori likiwa limeacha njia mara baada ya kugongana na basi hilo la abiria la kampuni ya New Force katika jali mbaya iliyotokea hii leo mkoani Iringa.
Hali ilivyo mara baada ya ajali ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori la mizigo mkoani Iringa, ambapo jumla ya watu 12 wamepoteza maisha na 22 wamejeruhiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanae na wanne ni wanawake.
Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi na roli na hali zao siyo nzuri.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasili ambapo basi la Kampuni ya New Force aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF katika kijiji cha Mahenge wilaya ya Kilolo mkao wa Iringa katika barabara kuu ya Dar - Mbeya.
Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula, kilomita 45kutoka Iringa mjini.
TASAF YAJENGA STENDI YA MABASI LUNDUSI KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI KWA
WANANCHI
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songea
MRADI wa Ujenzi wa Stendi ya mabasi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) katika Kijiji cha Lundusi w...
58 minutes ago