ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 4, 2020

KUTOPANDA MADARAJA KWA WALIMU TATIZO LINASABABISHWA NA BAADHI YA MAAFISAUTUMISHI WENYE ROHO ZA NYOKA



KATIKA kuwatoa shaka waalimu kuhusu malalamiko yao ya kutopanda madaraja, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemeni Jafo ametoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha walimu wanaostahili kupanda madaraja wanapandishwa madaraja. Waziri Jafo ametoa kauli hiyo katika Tamasha la utoaji TUZO ZA UMAHIRI KATIKA ELIMU MKOA WA MWANZA zilizoanzishwa na wadau wa elimu mkoa huo kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha na kuongeza kiwango cha ufaulu kimkoa. "Daraja halipandishwi na Magufuli, hapandishi Mama Samia wala Majaliwa, wala Jafo, mchakato wa madaraja unaanzia kwenu wenyewe, iweje leo Afisa Utumishi katika Halmashauri fulani anashindwa kuweka katika bajeti yake ya makisio ya Mwaka, kwamaba watumishi fulani watapanda madaraja?" Alihoji Waziri Jafo na kuongeza..... "Wewe Afisa Utumishi leo hii watu wamepewa barua ya kupanda daraja lakini kwenye makisio ya mshahara mtu hayupo, halafu tunahamisha lawama kusema Serikali imeshindwa kupandisha watu madaraja, kumbe kuna watu tunaokaa nao wanaroho kama za nyoka. Ni matatizo ya baadhi ya Maafisa Utumishi wanaoshindwa kupanga utaratibu wa watu kupanda madaraja kutokana na sababu zao binafsi" Halmashauri ya Jiji la Mwanza imekuja na wazo hilo ili kufikia malengo yake iliyojiwekea kwa Shule zake kwa miaka ijayo kuongoza katika chati ya ufaulu kitaifa. Ikumbukwe kwamba Halmashauri ya Jiji la Mwanza/Wilaya ya Nyamagana imekuwa Mshindi wa pili Kimkoa kwa matokeo ya Elimu Msingi Darasa la Saba Mwaka 2019-2020, Ya Nne katika matokeo Kitaifa huku shule zake mbili za Serikali zikiwa ndani ya Kumi Bora na baadhi ya Shule zake binafsi zikiwa ndani ya Tano Bora. Kwa matokeo hayo Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeona ipo sababu ya kutia hamasa kwa Waalimu na watendaji Sekta ya Elimu, kusherehekea na kutoa tuzo kwa wanafunzi na shule zilizo ongoza sanjari na kuweka mkakati kuhakikisha Halmashauri hiyo inakuwa ya kwanza kwenye matokeo yajayo. Tuzo za Elimu Mkoa wa Mwanza zinaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ofisi ya Mbunge na Wadau mbalimbali wa Taasisi za Kifedha, Watu, Mashirika Binafsi na Wafanya Biashara waliojitokeza kuweka chachu katika zawadi na udhamini. KAULI MBIU INAYOSHIKA MKAKATI HUO NI 'MWANZA KUWA WA KWANZA INAWEZEKANA'

Thursday, January 2, 2020

JEH WAISLAMU WANAPASWA AU HAWAPASWI KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA?


Shekhe Hassan Kabeke ni Sheikh wa mkoa wa Mwanza anajibu hoja hiyo kwa mifano ya Hadithi za Quran Tukufu, Ni katika kusanyiko la kusherehekea mwaka mpya 2020 iliyofanyika Tahere 01/Januari/2020 katika viwanja vya ofisi za BAKWATA zilizopo kata ya Mirongo wilayani Nyamagana jijini hapa, ambapo viongozi hao wa Baraza na baadhi ya waumini walijumuika kunywa na kula chakula cha pamoja na watoto yatima wanaolelewa na baadhi ya vituo vya kiislamu.

KANISA LA TAG KILOLELI LASHIRIKI UTATUZI WA CHANGAMOTO YA MADARASA KILIMANI SEKONDARI


 Mchungaji msaidizi wa Kanisa la TAG Kiloleli wa tatu kutoka kushoto (mwenye fulana ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na walimu na baadhi ya waumini baada ya kumaliza kujitolea kupanga mawe na kumwaga zege kwenye vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani jana.




Walimu wa shule ya Kilimani Sekondari wakishirikiana na waumini wa Kanisa la TAG Kiloleli kusawazisha moja ya msingi wa chumba cha darasa kati ya sita yanayotarajiwa kujengwashuleni hapo jana.Mwenye fulana nyeupe mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Athanas Manyika.
Akina mama ambao ni waumini wa kanisa la TAG Kiloleli wakijitolea kusomba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ye sekondari Kilimani jana.
waumini wa kiume wa kanisa la TAG Kiloleli wakijitolea kusawazisha kifusi kwenye moja ya Msingi wa vyumba vya madarasa ya Shule ye Kilimani sekondari yanayotarajiwa kujengwa shuleni hapo


1.Moja ya chumba cha darasa baada ya kumwagwa zege na waumini wa Kanisa la TAG kujitolea kufanya kazi hiyo jana ili kuwezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani ili yaweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajia kujiunga na shule hiyo wiki ijayo. Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

Muonekano wa chumba cha darasa baada ya waumini wa Kanisa la TAG kupanga mawe.

7. Moja ya chumba cha darasa baada ya kumwagwa zege na waumini wa Kanisa la TAG kujitolea kufanya kazi hiyo jana ili kuwezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani ili yaweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajia kujiunga na shule hiyo wiki ijayo. Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

WAUMINI wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) Kiloleli, wameguswa na kushiriki kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa inayoikabili Shule ya Sekondari Kilimani

Waumini hao wa jinsi zote jana walishiriki kujitolea kupanga mawe pamoja na kutoa tripu mbili za mchanga kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa  ili kutatua changamoto hiyo.

 Mchungaji msaidizi wa Kanisa hilo, Joseph Makala alisema ubinafsi umepunguza moyo wa uzalendo wa watu kujitolea kufanya shughuli za kijamii na kuifanya  jamii kushindwa kushiriki mambo yanayoihusu sababu ya  ubinafsi mkubwa uliopo kwenye maisha ya wanadamu,huku kila mmoja akijithamini  binafsi kuliko moyo wa kuwasaidia wengine.

Alisema  taasisi yao iliguswa baada ya kuambiwa watoto wanaoanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika Shule ya Kilimani Sekondari  hawana mahali pa kuingia kujifunzia kwa sababu ya uhaba wa vyumba vya madarasa usiowiana na idadi kubwa ya wanafunzi .

Mchungaji Makala alisema  Mkuu wa Shule  hiyo,alifikisha kilio cha changamoto ya shule na  hivyo kama taasisi ya dini wakaona washiriki ujenzi wa miundombinu  hiyo ili kuwezesha watoto kupata mahali pazuri pa kujifunza kwani sababu wanafahamu  wanahitaji kupata elimu wakiwa kwenye mazingira bora.

Makala alieleza baada ya kushikirishwa mioyo yao iliguswa wakaona washiriki kwa sehemu ambayo Mungu atakayowezesha ikizingatiwa taasisi hiyo ya dini ni sehemu ya jamii na inahusika na mahitaji ya jamii bila kujali imani za wanufaika.

“Methali inazungumza suala  elimu kuwa;Usimuache Elimu aende zake.Hivyo tukaona  watoto wetu wanahitaji kuwa na mahali pazuri pa kusomea na tuliguswa kama taasisi tukaona ni moja ya tunaoweza kushiriki baraka hizo ili kuhakikisha watoto wetu wanapata mahali pazuri pa kujifunzia, tuna wajibu huo kuwezesha watoto wetu wapate elimu,”alisema Makala.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo  taasisi hiyo imekuwa ikisistiza kama ambavyo  Bwana Yesu Kristo alivyotoa maisha yake kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine , vivyo hivyo jamii inawajibu huo na inatakiwa kujua kuwa inawajibika kuwasaidia watu wenye mahitaji na yawezekana sababu moyo wa ubinafsi umekuwa mkubwa kuliko wa kusaidia wengine.

Naye Mkuu wa shule hiyo Gerana Majaliwa, alisema wana changamoto  kubwa ya miundombinu ya madarasa,ingawa wanazitatua kwa fedha za serikalini huku wakishirikiana na  jamii pamoja na taasisi zingine kama Kanisa la TAG kuzipunguza.

Alishukuru jitihada za serikali kuendeleza elimu bure bila malipo lakini pia ushiriki wa wananchi katika kutatua changamoto za shule yao akiwemo Mbunge wa Ilemela Dk. Angeline Mabula,kwa kuwawezesha matofali 8,000,000 na mifuko 51 ya saruji.

“Kipekee hakuna taasisi iliyoakamilika, lazima ishirikiane na zingine wakiweo wananchi, tumeshirikiana na TAG ambao wamefanya kazi lakini pia tunakaribisha makampuni na wadau wengine wa maendeleo ili kusaidia kutatua changamoto na tunaamini ushirikiano huo utawezesha taaluma kukua,”alisema Majaliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi, Joseph Nyanda, alisema ili kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa wamepanga kujenga na kukamilisha vyumba vitatu kati ya sita Januari mwaka huu ili kuwezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza kupata mahali pa kusomea.

“Watoto wanaoingia kidato cha kwanza mwaka huu ni wengi na hatuna pa kuwaweka sababu vyumba vya madarasa havitoshi, hatuna msaada isipokuwa wazazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na taasisi za kijamii na taasisi za dini kama walivyofanya TAG Kiloleli.Pia  tulibahatisha mgawo wa matofali 4,000 kutoka kwenye kata lakini tukipata fedha za kujenga boma tutakamilisha mapema na kuwanusuru watoto hao,”alisema.

Aidha, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kawekamo, Maarufu Mohamed alisema ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule unafanywa kwa nguvu za wananchi na wazazi kuanzia msingi hadi boma kisha halmashauri kupaua na kuezeka ingawa mwitikio wa wananchi ni mdogo ambapo mbunge wa Ilemela amewezesha mifuko 51 ya saruji yenye thamani yash. 925,0000.


Wednesday, January 1, 2020

MWANZA YAUKARIBISHA MWAKA KWA KUOMBEA AMANI UCHAGUZI MKUU 2020.



Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblis of God (TAG) Mwanza Isaac Mgwao amewaomba watanzania kuwanamoyo wa maombi kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa ajili ya nchi yetu. Akisoma Risala katika mkesha huo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Askofu Philipo Magwano amemwomba Mungu ili Taifa hili linapoingia kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020 Mungu alisaidie ili chaguzi zote zifanyike katika misingi ya haki. Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkesha huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuhamasisha waumini wao kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAWAKILI NJE YA OFISI ZA NIDA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akifatilia Uingizwaji wa Taarifa za Wananchi waliotoka sehemu mbalimbali mkoani Morogoro na  kufika  Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),zilizopo eneo la Tungi-Mfuruni mkoani hapo  ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kujipatia kitambulisho hicho kwa wananchi nchini kote.Wapili kulia ni Afisa Usajili wa NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Mkoa wa Morogoro,James Malimo(aliyenyoosha mkono),akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),aliyefika Ofisi ya NIDA zilizopo eneo la Tungi-Mfuruni kuona zoezi la uandikishaji na utolewaji wa vitambulisho linavyoendelea. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), akifatilia Uingizwaji wa Taarifa za Wananchi waliotoka sehemu mbalimbali mkoani Morogoro na  kufika  Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),zilizopo eneo la Tungi-Mfuruni mkoani hapo  ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kujipatia kitambulisho hicho kwa wananchi nchini kote.Wapili kulia ni Afisa Usajili wa NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo.
Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),wakitoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro na vitongoji vyake waliofika katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Tungi-Mfuruni kujipatia namba na vitambulisho.
Masauni apiga marufuku Mawakili  Nje ya Ofisi za NIDA
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amepiga marufuku watu wanaojiita mawakili na kuwatoza wananchi kiasi cha  fedha kinachozidi shilingi Elfu Kumi  wakidai ni ada ya kupewa nyaraka mbadala ya cheti cha kuzaliwa ikiwa ni hitajio la msingi kwa wananchi wanaofika ofisi mbalimbali nchini za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)
Akizungumza baada ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Morogoro walioitaka Serikali kuweka bayana kama kupata vitambulisho vya taifa lazima ulipe hela,Naibu Waziri Masauni alisema vitambulisho hutolewa bure hakuna haja ya kulipa gharama yoyote huku akipiga marufuku wananchi kutozwa fedha nje ya ofisi za NIDA
“Kuanzia sasa kila Ofisi ya NIDA itakuwa na mawakili wa serikali wataohusika na kuandaa pamoja kuhakiki nyaraka mbalimbali za wananchi wanaokuja kwa ajili ya vitambulisho vya taifa na ninatoa maelekezo kwa nchi nzima katika ofisi za NIDA kuwaondoa watu wanaowaandalia wananchi nyaraka hizo kwanza hatuwatambui kama ni maafisa sheria sahihi au la na wanaweza kuwathibitisha watu ambao sio raia wakapata vitambulisho kama raia” alisema Masauni
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema wao kama mkoa wako tayari kuleta mawakili wa serikali katika ofisi hizo za NIDA huku akiwaasa wananchi kwenda sehemu sahihi wanapofika kutafuta vitambulisho katika ofisi hizo.
“Serikali ipo kuhakikisha zoezi la utolewaji namba na vitambulisho vya taifa linamalizika ndani ya siku 20 zilizoongezwa na Rais Magufuli na kama mkoa tunayafanyia kazi maelekezo ya Naibu Waziri Masauni na kuanzia kesho mawakili wa serikali watakuwepo hapa kuhakiki na kutengeneza nyaraka za serikali kwa wananchi” alisema RC Sanare
Nae Afisa Usajili wa  NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo amesema katika Mkoa wa Morogoro na Wilaya zake jumla ya vitambulisho 347,466 kati ya 849,436 vimezalishwa huku maombi 237.236 yakikwama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo waombaji kukosa vigezo vya uraia,mihuri ya wadau na viambata.

UPINZANI WASHINDA URAIS GUINEA BISSAU.


Kiongozi wa upinzani Umaro Sissoco Embalo ameshinda urais nchini Guinea Bissau baada ya kupata asilimia 53.55 ya kura zote, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (CNE) imetangaza.

Mshindani wake Domingos Simoes Pereira, kiongozi wa chama tawala (PAIGC) amepata asilimia 46.45 katika uchaguzi huo wa marudio.


“Ninamtangaza Umaro Sissoco Embalo kuwa mshindi wa uchaguzi huu wa marudio,” amsema Rais wa CNE, Jose Pedro Sambu

Embalo anachukua uraia kutoka kwa Jose Mario Vaz aliyechukua madaraka mwaka 2014 akiwa na matumaini ya kuituliza nchi hiyo ambayo imeandamwa na mapinduzi na mauaji ya viongozi tangu ilipopata uhuru mwaka 1974.

Lakini katika kipindi hicho ilikabiliwa na nguvu ya Bunge.

CNE imesema watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 72.67, sawa na ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa Novemba 24, ambapo Pereira alishinda kwa asilimia 40.1 dhidi ya asilimia 28 za Embalo.

Tuesday, December 31, 2019

TANZANIA: MAMA WA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA AFARIKI.

Mama mzazi wa mwandishi wa habari Erick Kabendera



Mama wa mwandishi wa habari aliye mahabusu nchini Tanzania Erick Kabendera amefariki dunia, familia imethibitisha.

CHANZO:- BBC Swahili.
Bi Verdiana Mjwahuzi (81) amefikwa na umauti katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumanne.
Alipelekwa hospitalini hapo siku ya Jumamosi wakati hali yake ikiwa mbaya. Hata hivyo kufikia mapema jana taarifa zilisema hali yake ilikuwa ikiendelea kuimarika.
Kabendera yupo rumande akikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi.
Hivi karibuni mama Verdiana Mjwahuzi (81) alimuomba Rais John Magufuli kumsamehe mwanae.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bi Verdiana alisema mwanae Kabendera ni nguzo muhimu ya ustawi wa familia yake.
"Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma. Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake," alisema Bi Verdiana.

Mwandishi Erick Kabendera
Erick Kabendera alikamatwa mwezi Julai 2019 na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kuongoza kikundi cha uhalifu. Mashtaka ambayo mawakili wake wameyakana.
Tayari mawakili wake wamefungua majadiliano na mkurugenzi wa mashtaka wa serikali (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha.
Wakati Kabendera anakamatwa, tayari afya ya mama yake ilikuwa dhoofu.

Kabendera ni mtoto wa saba kuzaliwa kati ya watoto nane wa Bi Verdiana.
Alisema pamoja na kuwa mdogo kati ya wanae, Kabendera ni mtoto ambaye mara tu anaposikia mama yake anaumwa hukimbia mara moja aidha kumpatia matibabu au kwenda kumuona nyumbani kwake.
"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi," alisema Bi Verdiana.
Alimuelezea mwanae kwamba hana hulka ya kusema watu vibaya, asiyependa anasa na mchapa kazi. Bi Verdiana ana amini kwamba mashtaka dhidi ya Kabendera yanatokana na kazi zake za uandishi wa habari.

Bi.Verdiana

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," alisema Bi Verdiana huku akibubujikwa machozi.
Bi Verdiana pia alieleza masikitiko yake ya kushindwa kwenda kumsalimia mwanae aliyeko rumande.
"Kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi," alisema Bi Verdiana kwa uhuzuni. 

Monday, December 30, 2019

POLISI MWANZA YAKANUSHA KUTEKWA KWA MAKADA WAWILI CHADEMA YATOA ONYO.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali zikidai kutekwa kwa wanachama wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Muliro amesema siku ya Desemba 29, Mwaka huu Majira ya 15:00 Mtaa wa Mahina Kata ya Mahina wilayani Nyamagana kulipatikana taarifa toka kwa raia wema kuwa kumeonekana watu wawili waliohisiwa kuwa siyo watu wema wakiwa karibu na Hoteli ya Paradise na kuingia nyumba jirani iliyokuwa karibu na hoteli hiyo. Kamanda Muliro, amesema baada ya kupatikana taarifa hizo jeshi la polisi lilifanya ufuatiliaji wa haraka na kufika eneo hilo na kuwakamata watu hao wawili, ambao katika mahojiano ya awali walikataa kutoa utambulisho wao kuwa wamefika maeneo hayo kufanya shughuli gani.

Aidha Muliro kazungumzia suala la ulinzi na usalama kwa mkoa wake wa Mwanza na kutoa rai na tahadhari kwa wananchi. ZAIDI FUATILIA VIDEO HAPO JUU.


MCHEZAJI WA YANGA ATAKAYEFANYA VIZURI MECHI DHIDI YA SIMBA KUCHOMOKA NA ZAWADI NONO TOKA GSM


Kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi, Kampuni ya GSM Group, ambao ni moja ya wadhamini wa Yanga inatarajia kutoa zawadi ya godoro kwa mchezaji wa klabu hiyo atakayeibuka nyota wa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, alisema wameamua kutoa zawadi hiyo ili kuwapa morari wachezaji wa Yanga.

Alisema wao kama wadhamini wa Yanga ni wajibu wao kuhakikisha timu hiyo inawapa raha mashabiki wake kwa kushinda mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.

"Kuelekea mechi ya kukata na shoka kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga, GSM Group kupitia godoro chapa GSM, tutatoa zawadi nono kwa mchezaji bora wa timu ya Yanga wakati wa mechi Yanga  na Simba kwa  kumzawadia godoro la nchi 5x6x8," alisema.

Aliendelea kwa kusema, "Tunaamini zawadi hii itawaongezea wachezaji morali ya kupambana kuiwezesha Yanga kupata ushindi na hivyo kuwapa raha mashabiki wao na kuendelea kupata matokeo chanya kwa mechi zingine zijazo,".

CHUO KIKUU INDIA KUFUNDISHA MADAKTARI MASUALA YA UCHAWI.

File photo of Ayurvedic doctors being trained by surgeons at Mumbai hospital in 2008Haki miliki ya picha
Chuo maarufu nchini India kimeanza kutoa kozi ya ngazi ya cheti kwa madaktari jinsi ya kutibu wagonjwa wanaopatwa mapepo au huyaona.
kozi hiyo ya miezi sita katika chuo kikuu cha Banaras Hindu (BHU) kwa mji wa kaskazini wa Varasanasi, kozi hiyo itaanza mwezi Januari.
Na pia kozi hiyo itakua inatolewa na kitengo cha afya ya akili na magonjwa yasiyo ya kawaida.
Msemaji wa chuo aliambia shirika la habari la India kuwa kitengo cha masomo ya uchawi kimeanzishwa.
''Kitengo hicho kinaitwa Bhoot Vidya na kunajihusisha na magonjwa yasiyo ya kawaida ama matatizo ya akili'' anasema Yamini Bhushan Tripathi mkuu wa kitengo hicho.
Aliongeza pia Chuo hiki ndo chuo cha kwanza kuanzisha kozi ya namna hiyo ambayo itafundisha masomo ya utabibu wa majini, mapepo na mizimu.
Matibabu yatatolewa kwa njia ya dawa za asili, miti shamba na masaji.
Kwa mujibu wa utafiti wa 2016 wa kitengo cha magonjwa ya akili (Nimhans) karibu asilimia 14 ya watu nchini India ni wagonjwa wa akili na mwaka 2017 shirika la afya duniani WHO inakadiria asilimia 20 ya Wahindi wanaweza kupatwa na msongo wa mawazo katika kipindi fulani katika maisha yao.
Lakini kuna chini ya wagonjwa 4,000 wa akili huwa wanaenda hospitali kupatiwa matibabu rasmi, kuna uelewa mdogo sana juu ya afya ya akili.
Lakini pia kutokana na unyanyapaa kusambaa sana , wagonjwa wachache ndio wanaenda hospitali wengi huenda kwa waganga wa kienyeji na kudhani kuwa watatibiwa matatizo yao ya akili.
Wengi wameonesha kulidhihaki tangazo hilo katika mitandao ya kijami, baadhi wameuliza serikali ya India je vipaumbele vyake vikwapi?
Taarifa ya kuwa chuo hiko cha serikali kitaanza kutoa kozi hiyo imepokelewa kwa maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wengi wakiuliza ni namna gani kozi hiyo itatolewa?

6 WAFARIKI KATIKA AJALI DODOMA.


Watu sita wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Coaster na lori eneo la Kisasa jijini Dodoma usiku wa kuamkia leo Desemba 30, 2019.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dk, Ernest Ibenzi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Wakati huo huo naye Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto amesema watu wengine 12 wamejeruhiwa.

Sunday, December 29, 2019

ALIYEUA MKE KWA SHOKA AKAMATWA 'KININJA' MAFICHONI AKITOKEA KENYA! / 'DOG STAILI' YATUMIKA!


Jeshi la Polisi Wilayani Arumeru lina mshikiia *Moses Latiaeli Pallangyo* almaarufu kama Moses Lebaba anayejishughulisha na nyimbo za injili, Kwa tuhuma za Kumuua kwa shoka Mwanamke alietambuliwa kwa Majina ya *Marry Richard Mushi* mkazi wa kijiji cha *Kilinga Wilayani Arumeru* aliyeuawa kwa kupigwa na shoka leo Tarehe 25/12/2019 Majira ya mchana na mwanaume aliyekuwa akiishi naye, Katika kijiji cha Kiinga Wilayani Arumeru

MKULO ASEMA HANA MPANGO WA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KILOSA, MOROGORO 2020


Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Morogoro Mustafa Mkulo (pichani) ameshangazwa na baadhi ya watu kudai anataka kugombea ubunge katika jimbo la Kilosa huku akikanusha hana mpango wowote wa kugombea nafasi hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro katika salamu za mwaka mpya wa 2020 ikiwa ni sehemu ya kawaida yake kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka, Mkulo amesema ajabadilisha maamuzi yake ya kutogombea nafasi ya ubunge  na kushangwazwa na baadhi ya watu kudai anataka kuombea tena nafasi hiyo.

“Kuna watu wamekuwa wakidai nataka kugombea tena ubunge Kilosa hizi ni habari za uongo sina mpango wa kugombea ubunge sehemu yoyote ile hapa nchini “ amesema Mkulo.

Mkulo amesema bado anajivunia katika miaka 10 ya ubunge jimbo la Kilosa kwa kutekeleza ilani ya chama kwa kipindi hicho na Wana-Kilosa kuridhika na utendaji wake.

Aidha Waziri waziri huyo mtaafu wa Fedha amesema ataendelea kuwa mwanachama na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo amefafanua kuwa pamoja sio mbunge na wala hafikirii kugombea nafasi hiyo lakini ataendelea kutoa mawazo yake kwa CCM na hata kusaidia wasiojiweza kwa niaba ya CCM ili chama kiweze kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo.

Katika salamu zake za mwaka 2020 Mkulo amesema anafurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli na anaunga na wanaCCM wengi kutomuingilia katika katika uchaguzi wa kipindi cha pili ya miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025  ili aweze kutekeleza kwa ufasaha mipango ya kimaendeleo alioicha katika awamu ya kwanza.

“Huu ni utaratibu wangu wa kila mwaka kutoa salaumu za mwaka mpya  tangu nikiwa mbunge na sasa ni wakati wa kusema ukweli Rais Magufuri kwa miaka minne amefanya mengi mazuri anahitaji pongezi kutoka kwa Watanzania hasa katika kupandisha uchumi na kuboresha miundombinu ya nchi hii” amesema Mkulo.

Mustafa Mkulo ni Mbunge Mstaafu ambaye aliongoza kwa miaka 10 katika jimbo la Kilosa ambapo pia katika kipindi hicho alishika nafasi ya Waziri wa Fedha na kuacha kugombea mwenyewe kwa hiari yake katika uchaguzi  2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mbunge wa sasa Mbaraka Bawaziri ambapo amesema  maamuzi yake ya kuacha kugombea ni kutoa nafasi wa wanaCCM wengine kuchangia mawazo yao katika kuliletea maendeleo jimbo la Kilosa.

BODI YA FILAMU TANZANIA TOENI ELIMU YA MAADILI YA TAALUM KWA WASANII.


 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto) akitoa maagizo kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ya kutoa  elimu kwa wadau wa tasnia ya filamu kuzingatia maadili ya kitaaluma wapoigiza kulingana taaluma mbalimbali ilikuzipa kazi zao mvuto, (watatu kulia) ni Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
 Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa kwanza kulia) akimweleza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto)  mpango wa bodi  kuwa na pragramu ya kuanzisha filamu bora ya mwezi itakayooneshwa kwa siku moja katika kumbi za sinema kote nchini leo alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kupata taarifa za uendeshaji wa shughuli taasisi hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo (wa kwanza kushoto) akitoa ushauri kwa Bodi ya Filamu Tanzania kutumia tovuti yake wakati wa kutangaza filamu bora ya mwezi ili kutangaza tovuti hiyo mbele ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto)  leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za bodi.
 Afisa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Simon Peter akitoa taarifa ya utekelezaji na majukumu ya Kitengo cha Maendeleo ya kazi za Filamu mbele ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (hayupo pichani)  leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za bodi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akizungumza mara baada ya kikao  cha ufuatiliaji wa shughuli za Bodi ya Filamu Tanznia leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo (wa kwanza kulia) pamoja na Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa pili kulia).



Bodi ya Filamu Tanzania toeni elimu ya Maadili ya Kitaaluma kwa Wasanii
Na Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam
29/12/2019
Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amegiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania kuhakikisha unatoa mafunzo kwa wadau wa tasnia ya filamu katika kuzingatia maadili ya kitaaluma.

Dkt.Possi ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli zao pamoja na uandaaji wa  Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Bodi ya Filamu na Michezo yakuigiza.

“Kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya kazi za filamu kukosa uhalisia katika maigizo ya kitaaluma haswa pale wanapoigiza kuhusu taaluma mbalimbali mfano  Madaktari,Wanasheria au Wahandisi na hii inapelekea kupoteza mvuto wa filamu hizo,”alisema Dkt.Possi.  

Akiendelea kuzungumza Dkt.Possi alisistiza kuwa bodi inapashwa kuandaa mradi utakaosaidia wadau watasnia hiyo kupata elimu na pia kuipaisha tasnia hiyo katika nyanja mbalimbali  ikiwemo ngazi za kimataifa na kuimarisha uandaaji wa kazi hizo kwa kuwa na viwango vyenye ubora.

Nae Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo alisema kuwa Bodi inampango wa kuanzisha programu  ya kuwa na filamu ya mwezi ya kitanzania ambapo filamu hiyo itapigiwa kura na watanzania na baada ya kushinda itazinduliwa katika Majumba ya Sinema nchini na kwenye vingamuzi kadhaa nchi nzima na kuonyeshwa siku moja katika muda mmoja lengo ikiwa ni kuzitafutia masoko filamu za kitanzania na kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu.

“Bodi inampango wa Kuanzisha Kanzi Data ya Waandaji wa kazi za Filamu,Wasambazaji,Waigizaji,Waongozaji na Waandishi wa Miswada ya Filamu lengo likiwa kupata takwimu zao, ili kuwa na njia rahisi ya kuweza kuwasaidia kiuchumi wadau hawa ili angalau waweze kupata bima ya afya au kuwasaidia kupata mikopo,”alisema Dkt.Kilonzo.

Pamoja na hayo nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo aliishauri  Bodi kutumia tovuti yake katika kipindi cha kupigia kura filamu bora ya mwezi ili kuweza kuitangaza tovuti hiyo kwa wananchi.