ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 2, 2020

KANISA LA TAG KILOLELI LASHIRIKI UTATUZI WA CHANGAMOTO YA MADARASA KILIMANI SEKONDARI


 Mchungaji msaidizi wa Kanisa la TAG Kiloleli wa tatu kutoka kushoto (mwenye fulana ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na walimu na baadhi ya waumini baada ya kumaliza kujitolea kupanga mawe na kumwaga zege kwenye vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani jana.




Walimu wa shule ya Kilimani Sekondari wakishirikiana na waumini wa Kanisa la TAG Kiloleli kusawazisha moja ya msingi wa chumba cha darasa kati ya sita yanayotarajiwa kujengwashuleni hapo jana.Mwenye fulana nyeupe mwalimu wa taaluma wa shule hiyo Athanas Manyika.
Akina mama ambao ni waumini wa kanisa la TAG Kiloleli wakijitolea kusomba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ye sekondari Kilimani jana.
waumini wa kiume wa kanisa la TAG Kiloleli wakijitolea kusawazisha kifusi kwenye moja ya Msingi wa vyumba vya madarasa ya Shule ye Kilimani sekondari yanayotarajiwa kujengwa shuleni hapo


1.Moja ya chumba cha darasa baada ya kumwagwa zege na waumini wa Kanisa la TAG kujitolea kufanya kazi hiyo jana ili kuwezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani ili yaweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajia kujiunga na shule hiyo wiki ijayo. Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

Muonekano wa chumba cha darasa baada ya waumini wa Kanisa la TAG kupanga mawe.

7. Moja ya chumba cha darasa baada ya kumwagwa zege na waumini wa Kanisa la TAG kujitolea kufanya kazi hiyo jana ili kuwezesha kujengwa kwa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Kilimani ili yaweze kutumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajia kujiunga na shule hiyo wiki ijayo. Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

WAUMINI wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) Kiloleli, wameguswa na kushiriki kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa inayoikabili Shule ya Sekondari Kilimani

Waumini hao wa jinsi zote jana walishiriki kujitolea kupanga mawe pamoja na kutoa tripu mbili za mchanga kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa  ili kutatua changamoto hiyo.

 Mchungaji msaidizi wa Kanisa hilo, Joseph Makala alisema ubinafsi umepunguza moyo wa uzalendo wa watu kujitolea kufanya shughuli za kijamii na kuifanya  jamii kushindwa kushiriki mambo yanayoihusu sababu ya  ubinafsi mkubwa uliopo kwenye maisha ya wanadamu,huku kila mmoja akijithamini  binafsi kuliko moyo wa kuwasaidia wengine.

Alisema  taasisi yao iliguswa baada ya kuambiwa watoto wanaoanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika Shule ya Kilimani Sekondari  hawana mahali pa kuingia kujifunzia kwa sababu ya uhaba wa vyumba vya madarasa usiowiana na idadi kubwa ya wanafunzi .

Mchungaji Makala alisema  Mkuu wa Shule  hiyo,alifikisha kilio cha changamoto ya shule na  hivyo kama taasisi ya dini wakaona washiriki ujenzi wa miundombinu  hiyo ili kuwezesha watoto kupata mahali pazuri pa kujifunza kwani sababu wanafahamu  wanahitaji kupata elimu wakiwa kwenye mazingira bora.

Makala alieleza baada ya kushikirishwa mioyo yao iliguswa wakaona washiriki kwa sehemu ambayo Mungu atakayowezesha ikizingatiwa taasisi hiyo ya dini ni sehemu ya jamii na inahusika na mahitaji ya jamii bila kujali imani za wanufaika.

“Methali inazungumza suala  elimu kuwa;Usimuache Elimu aende zake.Hivyo tukaona  watoto wetu wanahitaji kuwa na mahali pazuri pa kusomea na tuliguswa kama taasisi tukaona ni moja ya tunaoweza kushiriki baraka hizo ili kuhakikisha watoto wetu wanapata mahali pazuri pa kujifunzia, tuna wajibu huo kuwezesha watoto wetu wapate elimu,”alisema Makala.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo  taasisi hiyo imekuwa ikisistiza kama ambavyo  Bwana Yesu Kristo alivyotoa maisha yake kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine , vivyo hivyo jamii inawajibu huo na inatakiwa kujua kuwa inawajibika kuwasaidia watu wenye mahitaji na yawezekana sababu moyo wa ubinafsi umekuwa mkubwa kuliko wa kusaidia wengine.

Naye Mkuu wa shule hiyo Gerana Majaliwa, alisema wana changamoto  kubwa ya miundombinu ya madarasa,ingawa wanazitatua kwa fedha za serikalini huku wakishirikiana na  jamii pamoja na taasisi zingine kama Kanisa la TAG kuzipunguza.

Alishukuru jitihada za serikali kuendeleza elimu bure bila malipo lakini pia ushiriki wa wananchi katika kutatua changamoto za shule yao akiwemo Mbunge wa Ilemela Dk. Angeline Mabula,kwa kuwawezesha matofali 8,000,000 na mifuko 51 ya saruji.

“Kipekee hakuna taasisi iliyoakamilika, lazima ishirikiane na zingine wakiweo wananchi, tumeshirikiana na TAG ambao wamefanya kazi lakini pia tunakaribisha makampuni na wadau wengine wa maendeleo ili kusaidia kutatua changamoto na tunaamini ushirikiano huo utawezesha taaluma kukua,”alisema Majaliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi, Joseph Nyanda, alisema ili kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa wamepanga kujenga na kukamilisha vyumba vitatu kati ya sita Januari mwaka huu ili kuwezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza kupata mahali pa kusomea.

“Watoto wanaoingia kidato cha kwanza mwaka huu ni wengi na hatuna pa kuwaweka sababu vyumba vya madarasa havitoshi, hatuna msaada isipokuwa wazazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na taasisi za kijamii na taasisi za dini kama walivyofanya TAG Kiloleli.Pia  tulibahatisha mgawo wa matofali 4,000 kutoka kwenye kata lakini tukipata fedha za kujenga boma tutakamilisha mapema na kuwanusuru watoto hao,”alisema.

Aidha, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kawekamo, Maarufu Mohamed alisema ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule unafanywa kwa nguvu za wananchi na wazazi kuanzia msingi hadi boma kisha halmashauri kupaua na kuezeka ingawa mwitikio wa wananchi ni mdogo ambapo mbunge wa Ilemela amewezesha mifuko 51 ya saruji yenye thamani yash. 925,0000.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.