ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 15, 2010

NANI KTK MISS MAGU?

KUMEKUCHA MISS TANZANIA 2010, TENA SAFARI IMEANZA NA HAWA NDIYO WASHIRIKI TOKA WILAYA YA MAGU MKOANI MWANZA.

MITEMBEO, MAVAZI NA UTAMBUZI WA VIPAJI HAWA NDO WALIMU KTK MISS MAGU. NILIWAFUMA KATIKA KAMBI YAO YA MAZOEZI.

PARADE poz 2.KWA MUJIBU WA MRATIBU WA SHUGHULI HIYO MWANADADA NURJAN AMESEMA MISS MAGU ITAKAYOFANYIKA KESHO JUMAPILI 16MAY UKUMBI WA CCM MAGU, AMBAPO HUMO NDANI BURUDANI TOKA KWA WASANII DUDU BAYA NA JITAH MAN ITAPATIKANA KWA UBORA WA VIWANGO VYOTE.

TUZO ZA KILI 2010 NA MAPINDUZI YAKE.

MWANA USWAZI WA EATV MUSSA HUSSEIN AKIMKABIDHI TUZO JOE MAKINI TUZO YA WIMBO BORA WA HIP HOP, KUPITIA WIMBO WAKE WA STIMU ZIMELIPIWA.

MZEE YUSUPH WA JAHAZI MORDEN TAARAB ALBUM BORA YA MWAKA MUZIKI WA TAARAB na MTUNZI BORA.

SEAN KINGSTON TOKA NCHINI MAREKANI AKIMKABIDHI BWANA MISOSI TUZO YA WIMBO BORA WA RAGGA.

HASHEEM THABEET AKIMKABIDHI C PWAA TUZO YA VIDEO BORA YA MWAKA.

KAMA USIKU UNGALIKUWA WAMILIKISHWA BASI USIKU WA JANA ULIKUWA WAKE MSANII DIAMOND KWANI ALIFANIKIWA KUNYAKUA TUZO 3, HAPA AKIPOKEA TUZO YA MSANII ANAYECHIPUKIA IKITOLEWA NA MWANA FA.

Picha zote kwa hisani ya MTAA KWA MTAA.

Friday, May 14, 2010

BREAKING NEWS: KATIBU WA CCM KATA YA ISAMILO AUAWA.


NA: ALBERT G.SENGO; MWANZA

KATIBU WA CCM KATA YA ISAMILO JIJINI MWANZA Bi. BAHATI STEPHANO(49) AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU MARA BAADA YA KUVAMIWA OFISINI KWAKE NA KIJANA MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JUMANNE OSCAR (30).

TUKIO HILO LIMETOKEA LEO MAJIRA YA SAA SITA NA NUSU MCHANA OFISINI KWAKE MTAA WA NERA, MARA BAADA YA KIJANA JUMANNE OSCAR KUVAMIA OFISI HIZO NA KUMKUTA KATIBU HUYO NA MAJIBIZANO YA MANENO KUANZA HATIMAYE KIJANA HUYO ALICHOMOA KISU NA KUMCHOMA KIFUANI KUSHOTO NA KISHA TUMBONI.

MAMA HUYO KATIBU HUYO WA CCM KATA YA ISAMILO ALIFIA NJIANI AKIPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KUPATA HUDUMA.

MAUAJI HAYA YANAHUSISHWA NA SIASA KUTOKANA NA KUIBUKA KWA MAKUNDI YANAYOKINZANA NDANI YA CCM KUELEKEA KURA ZA MAONI ZA KUTAFUTA WAGOMBEA WA CHAMA HICHO TAWALA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU 2010.

AKITHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA BW. SIMON SIRO AMESEMA MARA BAADA YA KUFANYA UKATILI HUO KIJANA JUMANNE OSCAR ALITOKA OFISINI HUMO AKIKIMBIA KUELEKEA ZIWANI LAKINI KWA NGUVU ZA WANANCHI HATIMAYE ALIKAMATWA NA KUPELEKWA KITUO CHA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI.

MAREHEMU BAHATI ALIZALIWA KATIKA KIJIJI CHA BUSIRI WILAYANI UKEREWE MKOANI MWANZA NA AMEACHA WATOTO.

MWISHO:

TANZANIA HII HAPA DAKIKA YA MWISHO KWAKO KUPIGA KURA

SEAN KINGSTON AKIANGUSHA SAINI KATIKA CHUPA YA KILIMANJARO LAGER PINDI ALIPOTEMBELEA KIWANDA KINACHOTENGENEZA BIA HIYO CHA TBL.

SEAN KINGSTON LIVE IN DAR ES SALAAM.
Kilimanjaro Premium Lager tayari imemshusha Sean Kingston live in Dar, ataonekana kwa uzuri zaidi kwenye usiku wa tuzo za Kili 2010 leo tarehe 14/05/2010 akiwapa suport washindi wa Killi Music Awards, na tarehe 15/05/2010 ndani ya Diamond Jubilee, Sean Kingston anashuka stage na washindi wa 2010 killi Music Awards kwa show moja tu live na Bendi yake nzima kutoka States kwa Kiingilio cha shillingi 15,000 Tu Kwa Ticket za awali.

Ticket zimekwishaanza kuuzwa siku 5 kabla ya concert. Kwa wale watakao nunua Ticket Mlangoni Zitapatikana kwa shillingi 20,000 Tu. Tayari interviews za moja kwa moja ndani ya studio tofauti na sean Kingston zimefanyika.

ILI KUMPIGIA KURA MWANAMUZIKI WAKO TEMBELEA www.kilitime.co.tz

Thursday, May 13, 2010

KITU CHA MAJI BARIDI....

KAMONGO YUKO PALE, SATO PALE KATI NA KITU CHA SANGARA.
BAADA YA KUCHOKA KULA DAGAA LEO NAHAMIA KWENYE SAMAKI WAKUBWA....

MVUA

MVUA ZA MWISHO MWISHO.

MSIBA JIMBO LA BUSEGA.


BWANA NA BIBI ALOYSIUS GEORGE NTOBI WA PASIANSI NA MASANZA ONE WA MWANZA, WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BINTI YAO MPENDWA SEGA ALIPHONSINA GRACE NTOBI. KILICHOTOKEA TAREHE 11 May 2010 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO, MWANZA.
MWILI WA MAREHEMU UTAFANYIWA IBADA SIKU YA IJUMAA SAA TATU ASUBUHI PASIANSI ILONGAZALA NA BAADA YA IBADA UTASAFIRISHWA KWENDA NYUMBANI KWA WAZAZI WAKE MASANZA ONE MAGU MWANZA KWA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI 15MAY 2010 SAA NNE ASUBUHI

HABARI ZIWAFIKIE
NDG WOTE WA UKOO WA KULINDWA MASOTA, NA LYAMBA.
NGD WOTE WA UKOO WA KAPONGO, MAYALA MININGA NA KIGANGA
NDG KUTOKA JAMII YA WASILANGA WA UKEREWE NA NASSA.
WANACHAMA WA CCM NA VYAMA VYOTE VYA SIASA NCHINI.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Wednesday, May 12, 2010

TWALAA AU TWALIWA?



SUPU YA MBUZI NOW DAYS IMEPATA MASHABIKI WENGI HUKU IKIZIDI KUNYWEKA ILE MBAYA. TUKIWA NA ONGEZEKO HILI LA MABAA NA MAGROSARY MIJINI NA VIJIJINI, HALI HII INAPELEKEA MBUZI WAWILI HADI WANNE KUCHINJWA KWA SIKU KUHUDUMIA BAR 1 TU!
LAKINI HEBU JIULIZE MZAZI, PAMOJA NA YOTE HAYO MBONA MBUZI HAWAISHI WALA JAPO KUADIMIKA? SIYO KWAMBA KUNA MBINU MBADALA HAPA? MMMH!

TUINGIE DARASANI:- MBWA ANAZAA WATOTO SABA HADI KUMI NA MBILI KWA MPIGO ILE HALI MBUZI ANAZAA MTOTO MMOJA TU!
MBUZI ANALIKA ILE KINOMA KWENYE MABAA, KWA WANAOTAMBIKA, BIRTHDAY NA MASIKUKUU YOTE MBUZI NDIYO KITOWEO TEGEMEWA. LAKINI CHAKUSHANGAZA MBWA PAMOJA NA KUZALIANA KOTE HUKO ETI HAWAONEKANI MTAANI....! DUH!

UCHUNGUZI TATA USIO NA MBARATATA BALI VIMELEA VYA MKAMBWAMBWA UMEBAINI KUWA KATIKA MBUZI SITA WANAOCHINJWA NA KUUZWA MABUCHANI MBWA NI WANNE NA MBUZI WA UKWELI UKWELI NI WAWILI TU!
HUWEZI GUNDUA KWANI MAUNGO YA MBWA NA MBUZI HATA MAPAJA SEMBUSE MBAVU HUWEZI TOFAUTISHA. ETI MBWA AKICHINJWA UTUMBO WAKE HUTUPWA MBALI UKAFUKIWA HATA BUCHANI USIKANYAGE KWANI NI BALAA, ACHILIA MBALI KICHWA NA KWATO LADHA YA WANYAMA HAWA NI ILE ILE........

(MBONA WA.... WANAKULA MBWA? USIACHE KULA MBUZI.)

Tuesday, May 11, 2010

BGML YAZINDUA GAZETI LA JAMII:

- Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja mstaafu Bahati Matala,(kushoto), akifungua utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gazeti la jamii,"BUNAKOBA" linalotolewa Na Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, (BGML),kulia ni Afisa Mawasiliano wa BGML, Basil Mbakile na katikati ni mmoja wa viongozi wa kata ya Bugarama wilayani Kahama. Uzinduzi Huo ulifanyika Jumamosi tarehe 8 Mei 2010.

HABARI KAMILI:
Serikali imetoa changamoto kwa jamii inayoishi jirani na mgodi wa Bulyanhulu kujenga utamaduni wa kujisomea ili kupanua wigo wao wa uelewa.
Changamoto hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja mstaafu Bahati Matala, wakati akizindua gazeti la jamii la BGML linaloitwa”BUNAKOBA” mnamo Mei 8 2010.
Meja Matala amesema gazeti hilo ni kiungo muhimu katika kutoa habari mbalimbali kati ya mgodi na jamii na kwamba ni njia ya kuimarisha mahusiano mazuri baina ya pande hizo mbili.
“Ninatoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za BGML katika kubadilishana habari za kijamii, kiuchumi na utamaduni zinazohusu jamii na kuitumia fursa hii kujielimisha”, alisema Mkuu wa Wilaya.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi, Afisa Mawasiliano wa BGML, Basil Mbakile, alisema uamuzi wa kuanzisha gazeti la jamii ulifikiwa baada ya kutambua umuhimu wa kufikisha habari mbalimbali kwa jamii inayozunguka mgodi hasa zile zinazohusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na mgodi kwa jamii na pia wananchi wenyewe kutoa habari zinazowahusu hivyo basi kuboresha mawasiliano baina ya jamii na mgodi wenyewe.
“Tunaamini kwamba gazeti hili la jamii litasaidia kuwapatia wananchi habari sahihi juu ya shughuli za uendeshaji mgodi pamoja na miradi ya maendeleo kwa jamii, ambazo mara nyingi zimekuwa haziwafikii wananchi kwa usahihi,” alisisitiza Basil.
Alisema mbali ya kukusanya na kuandika habari za vijijini na zile zihusuzo mgodi, Idara ya Mawasiliano inaandaa utaratibu wa kushirikiana na vyombo vingine vya habari nchini, wizra, taasisi, mashirika ya umma, mashirika yasiyo ya kiserikali, (NGO), na wengineo katika tasnia ya habari ili kuhakikisha gazeti letu linapanua wigo wake wa habari na pia wananchi wanapata taarifa muhimu zinazowagusa.
Jina “BUNAKOBA” linamaanisha “Watu Watafutaji” kwa lugha ya Kisukuma. Gazei la BUNAKOBA linatayarishwa kwa pamoja na Idara ya Mahusiano na Jamii na Idara ya Mawasiliano ambalo litatolewa kila baada ya miezi minne na kugawiwa bure kwa wananchi.


- Pichani ni baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa gazeti hilo wakijisomea nakala ya kwanza ya gazeti.

AFISA POLISI IDARA YA UPELELEZI MWANZA AKWEAPIPA NA COCA COLA.

JOSEPH ALFRED MANGAPI, AFISA POLISI IDARA YA UPELELEZI MWANZA AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI MARA BAADA YA KUINASA TIKETI.

AFANDE JOSEPH (KULIA) AKIPOKEA MFANO WA TIKETI TOKA KWA MDAU WA COCA MAGINGA.

MASHAKA WANDERA WA GEITA (KULIA)NAE KULIKWEA PIPA.

RICHARD RUZWAHURA (KULIA)

ANTHON KAVISHE (KUSHOTO)NAYE KUKWEA PIPA.

HARUNA SALUM WA MUSOMA (KUSHOTO) NA LUNINGA YAKE.

LUNINGA NYINGINE HIYOOO YAENDA MUSOMA KWAKE RIZIKI MUSTAPHA(KUSHOTO).

HAPYBORZEY JACK FISH.

WADAU LEO NI BIRTHDAY YA MR. JACKSON NYAKUTONYA ALMAARUFU JACK MASAMAKI AKA JACK FISH WA MWANZA.
BLOG HII INAMTAKIA KILA LA KHERI MWANA 'JAIGORO' HUYU KATIKA KILA HATUA ZAKE ZA MAISHA, MUNGU AKUTANGULIE.
NISHAPATA TAARIFA KUNA ORDER YA KEKI YA SAMAKI KIWANDANI HADI MEZANI KWA MPISHI, SWALI NI KWAMBAAA.... SHANGWE LEO NI WAPI?

Monday, May 10, 2010

KICHAPO CHA SIMBA TOKA KWA WAARABU MASHABIKI MWANZA WAOMBOLEZA.


JIJINI MWANZA HAPA NI NYAMANORO PEMBEZONI MWA BARABARA IPANDAYO KAWEKAMO AMBAPO KUNA KIJIWE MAARUFU CHA BENDERA MBILI NA MLINGOTI MMOJA. TANGU KICHAPO CHA 5-1 BENDERA YA SIMBA IMEONEKANA KUPEPEA NUSU MLINGOTI.

@MBIO ZA KLABU ZA SOKA ZA TANZANIA KATIKA MICHUANO YA KIMATAIFA, ZILIMEFIKIA TAMATI MWISHONI MWA WIKI BAADA YA SIMBA, TIMU PEKEE ILIYOKUWA IMEBAKI KATIKA MICHUANO HIYO KUONDOSHWA KWA JUMLA YA MABAO 6-3 NA HARAS EL HODOUD YA MISRI.

MASHABIKI WANARUDIA MASWALI YALE YALE YASIYOKUWA NA MAJIBU MIAKA YOTE! TUTAENDELEA KUUMIZWA NA TIMU ZA WENZETU HADI LINI? LINI MWISHO WA MANYANYASO KWA TIMU ZETU? MIOYO INA UCHUNGU KUTOKANA NA MAUMIVU MAKALI YA KUBORONGA KWETU.

TUTAFANYAJE SASA!? ISHAKUWA, NATUOMBOLEZE SASA!

HUREE MIE NAMI SHABIKI!

MAMBO WADAU! NAITWA CATHBERT A.G.SENGO UMRI WANGU MWEZI JUNI 2010 NATIMIZA MIAKA MIWILI NASOMA CHEKECHEA.

JOTO LA UCHAGUZI MKUU KUMEKUCHA.


Joseph Kahungwa msomi aliyejitokeza kuwania ubunge jimbo la nyamagana kwa tiketi ya ccm.
JOTO LA UCHAGUZI LIMEENDELEA KUTANDA KATIKA ENEO LA KANDA YA ZIWA, BAADA YA KUONEKANA KUWA ULE UTABIRI WA REDET UNAENDA KUTIMIA YA KWAMBA THELUTHI MBILI YA WABUNGE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAWATACHAGULIWA.

ILI KUHAKIKISHA KILA MTU ANATUMIA VYEMA DAKIKA HIZI ZA LALA SALAMA VIKUMBO VIMEONEKANA DHAHIRI KATIKA KAMPENI ZISIZO RASMI KATI YA WAGOMBEA WATARAJIWA NA WALE AMBAO WANAOSHIKILIA NAFASI, KIGEZO KINAONEKANA WAZIWAZI IKIWA NI KUTOA MISAADA YA KIJAMII HALI INAYOONESHA NGUVU YA FEDHA KWA BAADHI.

PIA IMEBAINIKA KUWA BAADHI YA WAGOMBEA WATARAJIWA NA WAPAMBE WAO WAMEKUWA WAKIPIGA KAMPENI HADI VILIONI KWA KUTOA MISAADA ILI KUIHADAA JAMII KWAMBA WAPO NAO KATIKA SHIDA NA RAHA LENGO LIKIWA NI KUWINDA KURA ZA MAONI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

KATIKA JIMBO MOJA LA SHINYANGA, MGOMBEA M1 AMEONESHA KILA DALILI ZA KUTOA MSAADA WA MAGARI YA WAGONJWA KTK KATA ZA JIMBO LAKE, INGAWA TAYARI BAADHI YA WAPIGA KURA WAKE WAMEYAPONDA MAGARI HAYO HATA KABLA HAYAJAKABIDHIWA.
"MAGARI yenyewe yanatoa moshi balaa, sijui yatawezaje kuharakisha wagonjwa kwenda hospitali, alikuwa wapi mpaka sasa ndiyo aje na mikweche wakati wa uchaguzi ukikaribia?"

MKOANI MWANZA KATIKA JIMBO LA ILEMELA MBUNGE ALIYEPO DK. ANTHONY DIALLO HAJAONEKANA KUPATA UPINZANI MAKINI HADI SASA AMBAPO HUKO BUSEGA DK. RAPHAEL MASUNGA CHEGENI NAYE PIA INAELEKEA UPEPO UNAMPUNGIA KUTOKANA NA WAPINZANI WAKE KUTOJIPANGA MAPEMA.

WILAYA YA NYAMAGANA HOMA INAZIDI KUPANDA KWA KASI KWANII MH. MASHA KAKUTANA NA KISIKI KILICHOKWENDA SHULE JOSEPH KAHUNGWA PICHANI.... inaendelea

NDOMANAKE!

SIKU HIZI USAFIRI WA EXPRESS AKA DALADALA MWANZA KIMEO KWELI, WENYE KUWAHI WANAWAHI KWA MBINDE UKIJIFANYA MSTAARABU KWAKO UTAFIKA GIZA NENE. IMEFIKA WAKATI SASA MPANGO WA MAGARI MAKUBWA UTIZAMWE.

PALIKUWA PANACHANGAMKA KWELI HAPA.


JUA LA ASUBUHI.