NA VICTOR MASANGU CHALINZE
Friday, February 16, 2024
BARAZA LA MADIWANI CHALINZE LAPITISHA MAPENDEKEZO YA BL.54.6 KWA MWAKA 2024/2025
NA VICTOR MASANGU CHALINZE
Wednesday, February 14, 2024
TAHARUKI JESHI LA ZIMAMOTO LIKIZIMA MOTO JENGO LA NSSF TANGA
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga akiteta jambo na baadhi ya wateja wa mfuko huo mara baada ya kutokea tukio hilo
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga kushoto akimsikiliza kwa umakini Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga Abrahaman Ntezidyo
Na Oscar Assenga,TANGA.
TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wateja na watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Tanga baada ya kuibuka kwa moto kwenye moja ya chumba kilichopo kwenye Jengo lao na hivyo kulazimika kuacha shughuli na kukusanyika eneo moja huku Jeshi la Zimamoto na Ukoaji likifika na kufanikiwa kuzima moto huo.
Alisema kwamba walipataa taarifa za uwepo wa moto huo ambao ulianza saa nne na dakika arobaini asubuhi baada ya kupokea taarifa ya wito kutoka Jengo la NSSF kuwepo kwa moto kwenye jengo ambao ulitokea kwenye moja ya chumba cha ofisi.
Alisema kwamba katika jengo hilo kilikuwa na vitu kadhaa ikiwemo thamani za ofisi na waliopata hizo walipofika eneo la tukio kutokana na uwepo wa purukushani kutokana na taharuki hiyo mmoja wa watumishi wa mfuko huo alipata majeruhi kutokana na kupata mshutuko na alipelekwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo alisema kwamba chanzo chaa tukio hilo bado hakijafahamika lakini kwa sasa wanaendelea kufanyaa uchunguzi ili kuweza kubaini sabaabu zilizopelekea kutokea kwa moto huo katika moja ya chumba kwenye jengo hilo.
“Tunamshukuru Meneja wa NSSF kwa kutoa taarifa kwa wakati kwa Jeshi letu na tukio hilo kutokana na kuwahi kufika hakuna madhara makubwa kilichohusika ni chumba kimoja cha ofisi ambacho kimeungua vitu vichache kutokana na kuwahi kuzibiti moto usisambae maeneo mengine”Alisema
Alitoa wito kwa wananchi wanapopata matukio ya moto waweze kutoa taarufa kwa mapema ili nao waweze kufika kwa wakati na kuweza kufanya maokozi ambapo pia akitoa pole kwa Meneja na mfanyakazi aliyepata majeruhi apone na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Awali akizungumza,Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga alilishukuru Jeshi la Zimamoto na Ukoaji na vikosi vinavyohusika na majanga kuwahi kufika kwenye eneo la tukio kweli moto ulitokea na uliweza kudhibitiwsa kikamilifu.
Alisema lakini mfanyakazi mwenzao alipata madhara kidogo na kupelekwa Hospitali natukio hilo limetokea lakini wameweza kulihimili na ni njia mojawapo ya kuweza kuwa na utayari kuweza kuhimili majanga yanapojitokeza.
Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa yazindua promosheni ya Swahiba "Langu Lako"
WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUFANYA UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO MARA KWA MARA
Na Oscar Assenga, TANGA.
DAKTARI Mwandamizi wa Magonjwa ya Kinywa na Meno katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Dkt Onesmo Ezekiel amewashauri wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa kinywa na meno mara bili kwa mwaka ili kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kukutana nayo ikiwemo ya kung’oa jino
Dkt Onesmo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Kinywa na Meno Katika Hospitali hiyo aliyasema hayo leo wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema uchunguzi huo wanaweza kufanya bila hata kuumwa kwa sababu magonjwa ya kinywa na meno katika hatua za awali hayana dalili zozote.
Alisema ila dalili zinaanza kujitokeza wakati ugonjwa unakuwa tayari upo kwenye hatua za mbele zaidi hivyo unapokwenda daktari ukiwa na maumivu na kukuangalia kama kuna uwezekano wa kuzuia magonjwa ya kinywa na meno unakuta tayari umeshaathiri eneo kubwa na hivyo kuwa na uchaguzi mmoja wa kung’oa jino.
“Lakini niwaambie kwamba dalili za meno ukiziwahi kwenye hatua za awali inakuwa rahisi kufanya matibabu na gharama zake zinakuwa ni rahisi vyenginevyo utakwenda kwa daktari ukiwa na maumivu makubwa zaidi na hivyo kuwa na uchaguzi wa kungo’a jino”Alisema
Hata hivyo Dkt Onesmo alisema kwamba magonjwa hayo yanaathiri watoto na watu wazima hivyo kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanazingatia suala la usafi wa kinywa na meno vizuri wasimamiwe watumie dawa ya mswaki yenye madini ya floride,calcium na karafuu .
“Lakini mswaki wanaoutumia usizidi zaidi ya miezi mitatu kwa sababu baada ya miezi hiyo unashindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi huku asisisitiza umuhimu wa jamii kuhakikisha wanatunza vinywa vyao kwa kuzingatia kufanya usafi mara kwa mara”Alisema
Akizungumza kuhusu kitengo cha huduma ya Afya ya Kinywa na Meno katika Hospitali hiyo Dkt Onesmo alisema wanatoa huduma zinazohusiana na magonjwa ya kinywa na meno kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu mpaka saa tisa na nusu mchana.
“Pia wakati mwengine tunatoa huduma siku za wikiendi linapokuwa limejitokeza suala la uhitaji na kitengo chetu kina vitengo kadhaa ndani yake ambapo tunatoa huduma za meno bandia,kuziba meno,kusafisha meno,kufanya matibabu ya mzizi wa jino na kungarisha jino “Alisema
Alisema pia wakati mwengine wanalazimika kwenda chumba cha upasuaji inatpokea kuna mahitaji mfano wanapotokea wagonjwa wenye uvimbe ambao unahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa au wagonjwa wa ajali ambao matibabu yao ili kuweza kuwatibu wanapaswa kwenda chumba cha upasuaji.
“Tunafanya upasuaji mdogo ambao hauhitaji mgonjwa kulazwa bali isipokuwa ikiwekewa ganzi katika eneo husika anaweza kufanyiwa huduma hizo na kuruhusiwa“Alisema.
Hata hivyo alisema kwamba hospitali hiyo inapokea inapokea wagonjwa kutoka wilaya zote za mkoa huo na wanapata matibabu hapo na wachache wanalazimika kuwapa rufaa kwendfa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumzia magonjwa yanayowatesa wananchi wengi,Dkt Onesmo alisema magonjwa hayo ni kutoboka kwa meno ambao zaidi ya nusu ya wagonjwa ni tatizo kubwa na wengine ni fizi kutoka damu na yamekuwa yakiathiri watu wa umri zote.
“Kuanzia vijana,watoto hadi wazee wa jinsia zote wanakaribiana huku kundi jingine ni wale wanaopata ajali za kuvunjika taya la chini na la juu au yote mawili pamoja au kung’oka meno kwa ajili ya ajali ambazo zinahusisha bodaboda ambao wamekuwa wamelewa”Alisema
Tuesday, February 13, 2024
LOWASSA AAGWA DAR ES SALAAM.
Salaam za rambirambi zinaendelea kumiminika katika eneo la Karemjee ambako waombolezaji wamekusanyika kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwanasiasa huyo aliyezipamba siasa za Tanzania kuanzia ndani ya chama cha CCM na hata pale alipokwenda chama kikuu cha upinzani Chadema wakati wa harakati za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kila anayepanda jukwaani amekuwa akitoa saalam na kumwelezea kiongozi huyo kuwa mtu aliyeziishi enzi zake na kutenda mambo kwa umakini mkubwa.
Lowassa alikuwa mvumilivu
Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba amekumbusha namna alivyokuwa ameshibana na kiongozi huyo akisema Lowassa alikuwa mtu mwenye misimamo na aliyependa kuchapa kazi kwa umakini mkubwa.
"Lowassa alikuwa mvumilivu sana na mimi niliendelea kuwa na uhusiano huo popote alipokuwa, alipokuwa katika CCM, alipokuwa katika serikali alipokuwa katika Chadema, aliporudi hata CCM, uhusiano wetu ulikuwa kama kaka na mdogo wake,"alisema Warioba.
Akizungumza wakati akitoa salamu zake za rambirambi, makamu wa rais Dkt Philip Mpango amesema taifa limempoteza kiongozi aliyekuwa hodari na aliyedhubutu katika kila jambo. Mbali na kutoa pole kwa familia ya kiongozi huyo, makamu wa rais pia alisema hiki siyo kipindi kigumu kwa familia pekee bali kwa taifa zima.
"Kwa kweli ni mmoja wa watoto mahiri sana wa mama Tanzania ambaye alijitoa kwa dhati kulitumikia taifa letu kwa moyo wake wote. Mheshimiwa Lowassa alitumia vyema karama ambazo alijaliwa na mwenyezi Mungu kuwatumikia Watanzania," alisema Mpango.
Wakati wa uhai wake, Lowassa alishika nyadhifa mbalimbalimbalindani ya CCM mpaka serikalini. Aliingia katika baraza la mawaziri wakati wa awamu ya pili ya utawala wa Rais Ally Hassan Mwinyi akiendelea hivyo mpaka wakati wa utawala wa hayati Benjamin Mkapa.
Alijiuzulu kama Waziri Mkuu
Aliteuliwa kuwa waziri mkuu wakati wa utawala wa awamu ya nne wa Jakaya Kikwete nafasi ambayo alidumu nayo kwa kipindi kifupi cha miaka miwili tu, akilazimika kujiuzulu baada ya kuandamwa na kashfa ya Richmond.
"Nadhani tatizo ni uwaziri mkuu kwamba ionekane waziri mkuu ndiye amefanya haya…ionekane kwamba waziri mkuu ndiye amefanya haya tumwondolee heshima au tumwajibishe ..mheshimiwa spika nimetafakari sana kwa niaba ya chama change, kwa niaba ya serikali yangu nimeamua kumwandikia barua rais ya kumwomba niachie ngazi," alisema Lowassa wakati huo.
Lowassa atazikwa mwishoni mwa wiki jimboni kwake Monduli mkoani Arusha, mazishi ambayo yataongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa yuko ziarani Vatican.
"KIFO CHA LOWASSA HAKIWEZI KUSITISHA KUDAI HAKI ZA WATANZANIA" KUELEKEA MAANDAMANO YA CHADEMA MWANZA
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
KUELEKEA Alhamisi ya tarehe 15 mwezi Februari 2024 siku ambayo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeiteuwa kuwa ya kufanyika maandamano ya amani jijini Mwanza, napata nafasi ya kufanya mahojiano na wadau wa chama hicho waliopo kwenye maandalizi katika viwanja vya Furahisha. 1. Jeh ni ajenda zipi CHADEMA wanakwenda nazo katika maandamano yao jijini Mwanza? 2. Mnafanya Maandamano haya wakati Taifa likiwa kwenye simanzi ya kuondokewa na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa, ambaye pia mnamo mwaka 2015 alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, pengine hamuoni ingekuwa busara kupisha kwanza hilo liishe kisha mkaendeleza ajenda zenu? 3. Pengine inawezekana Maandamano yenu yakaingiza hoja Mpya ya kuenzi Demokrasia kama mnavyosema ama mtabaki na hoja zile zile ambazo mmekuwa mkizinadi?