ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 14, 2024

TAHARUKI JESHI LA ZIMAMOTO LIKIZIMA MOTO JENGO LA NSSF TANGA

 

Mmoja wa watumishi wa NSSF Mkoa wa Tanga ambaye alipata majeruhi akibebwa kwa ajili ya kuwahishwa katika Hospitali leo




Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga akiteta jambo na baadhi ya wateja wa mfuko huo mara baada ya kutokea tukio hilo

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga kushoto akimsikiliza kwa umakini Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga Abrahaman Ntezidyo







Na Oscar Assenga,TANGA.

TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wateja na watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Tanga baada ya kuibuka kwa moto kwenye moja ya chumba kilichopo kwenye Jengo lao na hivyo kulazimika kuacha shughuli na kukusanyika eneo moja huku Jeshi la Zimamoto na Ukoaji likifika na kufanikiwa kuzima moto huo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uzimaji wa moto huo Kaimu Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga,Mrakibu wa Jeshi hilo Abrhaman Ntezidyo alitibitisha kutokea kwa moto huo ambapo alisema ulitokea saa 4.4o asubuhi.

Alisema kwamba walipataa taarifa za uwepo wa moto huo ambao ulianza saa nne na dakika arobaini asubuhi baada ya kupokea taarifa ya wito kutoka Jengo la NSSF kuwepo kwa moto kwenye jengo ambao ulitokea kwenye moja ya chumba cha ofisi.

Alisema kwamba katika jengo hilo kilikuwa na vitu kadhaa ikiwemo thamani za ofisi na waliopata hizo walipofika eneo la tukio kutokana na uwepo wa purukushani kutokana na taharuki hiyo mmoja wa watumishi wa mfuko huo alipata majeruhi kutokana na kupata mshutuko na alipelekwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo alisema kwamba chanzo chaa tukio hilo bado hakijafahamika lakini kwa sasa wanaendelea kufanyaa uchunguzi ili kuweza kubaini sabaabu zilizopelekea kutokea kwa moto huo katika moja ya chumba kwenye jengo hilo.

“Tunamshukuru Meneja wa NSSF kwa kutoa taarifa kwa wakati kwa Jeshi letu na tukio hilo kutokana na kuwahi kufika hakuna madhara makubwa kilichohusika ni chumba kimoja cha ofisi ambacho kimeungua vitu vichache kutokana na kuwahi kuzibiti moto usisambae maeneo mengine”Alisema

Alitoa wito kwa wananchi wanapopata matukio ya moto waweze kutoa taarufa kwa mapema ili nao waweze kufika kwa wakati na kuweza kufanya maokozi ambapo pia akitoa pole kwa Meneja na mfanyakazi aliyepata majeruhi apone na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Awali akizungumza,Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga alilishukuru Jeshi la Zimamoto na Ukoaji na vikosi vinavyohusika na majanga kuwahi kufika kwenye eneo la tukio kweli moto ulitokea na uliweza kudhibitiwsa kikamilifu.

Alisema lakini mfanyakazi mwenzao alipata madhara kidogo na kupelekwa Hospitali natukio hilo limetokea lakini wameweza kulihimili na ni njia mojawapo ya kuweza kuwa na utayari kuweza kuhimili majanga yanapojitokeza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.