ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 16, 2024

BARAZA LA MADIWANI CHALINZE LAPITISHA MAPENDEKEZO YA BL.54.6 KWA MWAKA 2024/2025


NA VICTOR MASANGU CHALINZE 


HALMASHAURI  ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani hatimaye  imepitisha mapendekezo ya bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 54.6 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani  kwa ajili ya kujadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti.

Possi alibainishwa kwamba bajeti hiyo ambayo imeweza kugusa katika nyanja mbali mbali imepitia vikao mbali mbali vya kisheria pamoja na kuwahusisha madiwani kutoka kila kata kwa lengo keleta maendeleo.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba katika mapendekezo  ya bajeti hiyo fedha za ndani zitakuwa ni shilingi bilioni 17.3 luzuku kutoka serikalini kuu na matumizi ya kawaida ni bilioni 26.01.
"Mwenyekiti ninaomba baraza lako tukufu lipitishe mapendekezo ya bajeti hii ya bilioni 54.6 na kwamba itajumusha na mambo ya mishahara miradi ya maendeleo  pamoja na mahitaji mengine ya kiofisi,"alifafanua Possi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe.Hassan Mwinyikondo amewapongeza wataalamu pamoja na madiwani wote kwa kuweza kushirikiana kwa pamoja katika kuandaa mapendekezo ya bajeti hiyo.
Alisema kwamba kwamba hawezi kusita kuisifia bajeti hiyo kutokana na kuweza kugusa katika kila nyanja pamoja na kutoa fursa za maoni na mapendekezo ambayo yalikuwa yanatolewa kwa maslahi ya wanannchi.

"Kiukweli hii bajeti yetu imeweza kugusa kila nyanja  maana siku zote sisi madiwani kwa kushirikiana na madiwani tumekaa kuanzia asubuhi mpaka jioni nia na madhumuni kuyachukua mapendekezo yote ambayo yametolewa na kuyaingiza katika bajeti,",alisema Mwinyikondo.
Pia alisema kuwa bajeti hiyo itakwenda kuleta chachu kubwa ya mabadiliko katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itakuwa ni faida kubwa kwa wananchi wa chalinze.

Mwenyekiti huyo aliongeza kubwa lengo kubwa la kupendekeza bajeti hiyo ni kuhakikisha inakwenda kuokoa maisha ya wananchi wa chalinze pamoja na kuibua miradi mipya ya maendeleo.

"Waandishi wa habari nadhani mnajionea nyinyi wenyewe kwa hivyo yale mazuri yote ambayo tunayatekeleza ni vema mkayaandika kutokana na mambo mazuri ambayo tunayatekeleza,"alisema Mwinyikondo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash hakusita kuipongeza Halmashauri ya Chalinze kwa juhudi zake katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Mkuu huyo alisema amefarijika kuona madiwani na wataalamu mbali mbali wanafanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha kwamba wanaweka mipango ya kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia fedha za ndani.

Alisema mapendekezo ya bajeti hiyo yanatakiwa kusimamiwa ipasavyo ikiwa sambamba na kumsaidia Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ili aweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Nao baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wameungana kwa pamoja kupitisha mapendekezo ya bajeti hiyo ambayo wamesema itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi katika sekta mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.