ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 23, 2011

MWANZA MPOOOooo!!!

Huu ndiyo ukumbi wa shughuli ya Miss Mwanza ndani ya meli ya Mv Umoja, shughuli itakayokwenda kupigwa leo usiku...

Jombaa Edgar Mapande akiwa na Mary pande za rock city kushuhudia harakati za kumsaka miss Lake zone.

Now days viunga vya burudani Mwanza ni Nowmaa!! Mahala hapa ni bustanini mwa hotel mpya yaitwa Victoria Palace.

Mabishost' Mary na Flora mbele ya mjengo wa Hotel Victoria Palace.

Ni kama dizaini flani Bismack Rock limeamishiwa kwenye himaya ya hotel hii.

Friday, July 22, 2011

TAMKO LA VIONGOZI WA DINI NA MADHEHEBU MBALIMBALI NCHINI LAFUKUNYUA MADHAIFU MENGI SEKTA YA MADINI.

Kamati ya viongozi wa dini na madhehebu mbali mbali inayojishughulisha na masuala ya kijamii, kiuchumi haki na uhifadhi wa mazingira iliyoundwa kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wanaoishi katika maeneo ambako serikali imewekeza katika sekta ya madini imeitaka serikali kuhakikisha kwamba shughuli za uchimbaji wa madini katika maeneo husika zinaendana na haki za binadamu. Kutoka kushoto ni Bishop Dr. Benson Bagonza (CCT), Arch Bishop Paul Ruzoka ambaye ni mwenyekiti na Sheik Salum Fereji BAKWATA.
Hayo yamesemwa Leo asubuhi na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora Paul Ruzoka wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya G & G jijini Mwanza.

Amesema katika ziara ya kamati hiyo ambayo inajumuisha wajumbe kutoka Afrika ya Kusini, Botswana, Zambia, Canada na Norway iligundua mapungufu mbalimbali yanayofanywa na wawekezaji katika sekta hiyo ukiwemo uchafuzi wa mazingira, unyanyasasi wa wananchi, ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi ya sheria za ardhi na kutokuwepo kwa mpangilio mzuri wa ulipaji fidia.

Amesema kamati hiyo ilibaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi na waathirika waliopisha shughuli za uchimbaji za mgodi wa madini ya dhahabu wa kampuni ya Geita Gold Mine hadi sasa hawajalipwa fidia baada ya kuondolewa katika makazi yao hadi sasa hawana makazi maalum ya kuishi wala hawajui nini hatma yao.

Askofu Luzoka amesema kwa upande wa Mgondi wa Nyamongo ulioko mkoani Mara, kamati hiyo imebaini kuwepo kwa uchafuzi mkubwa wa mazingira na wananchi ambao wanazunguka mgodi huo hawapati maji safi na salama licha ya uongozi wa mgodi huo kuweka magari ya matanki ya kusomba maji safi kwa ajili ya wananchi hao jambo ambalo waliitaka serikali kwa kushirikiana na uongozi wa mgodi huo kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

Aidha kamati hiyo imetoa ushauri kwa serikali kupitia wakuu wa wilaya na mikoa ambapo migodi hiyo inapatikana kuhakikisha kuwa shughuli zinazofanywa na migodi hiyo haziathiri mazingira ya mahali husika, sheria iliyotungwa hivi karibuni ya fidia ya ardhi pia iwaguse wale ambao walihusika na zoezi la uhamishaji wananchi ili nao waweze kupata fidia pamoja na serikali kuhakikisha kuwa fidia wanaolipwa wananchi husika inawanufaisha wananchi kwa kujenga nyumba bora za kisasa.

Pia kamati hiyo imeyaomba mashirika ya kimataifa ambayo yanahusika na haki za binadamu kuhakikisha kuwa wananchi ambao wanaishi karibu na migodi wanahakikishiwa usalama wa afya, maisha na mali zao na kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

Kamati hiyo inaundwa na wajumbe kutoka Baraza la Maaskofu wa katoliki Tanzania (TEC), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT) na wajumbe wake ni kutoka nchi za Afrika Kusini, Botswana, Zambia, Canada na Norway.

Thursday, July 21, 2011

MA-MISS LAKE ZONE NA LUNCH YAO MELINI LEO

Ndiyo hawa hapa.. Je ni nani kuchomoka na taji? Jibu jumamosi hii tr23....!


Second ofisa wa meli ya Victoria Godifrey Kalikayo akitoa maelezo kwa washiriki wa miss lake zone walipotembelea meli hiyo kujionea utendaji kazi.

Hii ndiyo dira kionyesha uelekeo kwa waongoza meli.

Mv Victoria ni meli yenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 200 na abiria 1200 inafanya safari zake ndani ya ziwa victoria kutoka Mwanza hadi Bukoba mkoani Kagera.

Baada ya kuzunguka na kuishuhudia jiografia melini humo warembo hao walipata fursa ya kupata chakula cha mchana.

Hizi ni safari za mwisho mwisho kwa warembo hao kuelekea siku ya jumamosi tupate kushuhudia kinyang'anyiro cha kumsaka Mnyange wa Miss lake Zone atakaye jumuika na washiriki wenzake toka kundini kwenye Miss Tanzania baadaye mwaka huu.

Je ni katika kundi hili....?

Wapishi sanjari na wahudumu wa hoteli ya melini humo.

MRISHO NGASA V/S MANCHESTER UNITED.

Seattle Sounders wamekubali kichapo cha mabao 7-0 toka kwa Manchester Utd, Wayne Rooney akifunga mabao 3, Michael Owen, Biram Mame Diouf, Park Ji Sung, Gabriel Obertan wakifunga bao moja moja.

Last night in Seattle he hit a 21-minute hat-trick that proved if there was any cobwebs from his summer holidays they have been very quickly blown away.

The last time we saw him scoring was in the Champions League Final at Wembley against Barcelona before 87,695 fans. This time it was in the less familiar surroundings of Seattle Seahawks NFL stadium CenturyLink Field in front a crowd of 67,052.

But Rooney would not mind if it was a park back in Croxteth before a man and his dog.
He just loves playing football and loves scoring goals — no matter where he is. Rooney came on as a substitute at half-time and within six minutes he was on target.

Nani was the supplier, sliding a ball across the box for Rooney to side-foot into the roof of the net.


Mtanzania Mrisho Ngassa aliyeingia dakika 12 za mwisho wa mchezo almanusura aifungie Sounders bao la kufutia machozi lakini mpira wake ulitoka juu ya lango la Manchester United.

Pichani Shaffih Dauda ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports Bar' akiwa kwenye pozi na miamba ya Mashetani wekundu.
Kwa habari zaidi tembelea www.shaffih.blogspot.com

Wednesday, July 20, 2011

AIRTEL YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA SEKONDARI KANGAYE

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi leo imegawa msaada wa madawati kwa shule ya sekondari Kangaye jijini Mwanza ikiwa ni sehemu zake za kuisaidia jamii. Pichani meneja wa masoko kanda ya ziwa Ally Maswanya akikabidhi mchango huo kwa uongozi wa Shule.

Meneja wa shughuli za kijamii Tunu Kavishe amesema kuwa Airtel mara baada ya kuona uhaba uliopo kwa shule nyingi nchini ili kuisaidia serikali kampuni yake imedhamiria kutoa zaidi vifaa mbalimbali vya elimu na kufundishia kama sehemu yake muhimu katika kuikwamua jamii.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata hiyo ya Nyakato bw. Josephat Manyerere: Ameishukuru sana Airtel kwa kuichagua Mwanza kama sehemu moja wapo ya kuinua elimu na amefurahishwa kusikia kuwa mpango huo kuwa ni endelevu kwani utapunguza uhaba wa madawati na nyezo za elimu kwa mashule.

Wanafunzi wa shule ya Kayange wawakilishi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na madawati yao.

Sehemu tu ya wanafunzi walio hudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.

Airtel mkombozi wa jamii, Airtel mkombozi wa Elimu nchini Airtel Oyee!

Meneja wa shughuli za kijamii Airtel Tunu Kavishe akishiriki zoezi la kuingiza madawati madarasani.

Ni miaka saba sasa tangu Airtel ilipoanza mpango wake wa kusaidia nyenzo mbalimbali za elimu ikiwemo vitabu kwa shule za sekondari hapa nchini ambapo hadi sasa shule takribani 800 zimenufaika na mpango huo.


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jackon Mbando akielekeza njia iendayo shule ya Sekondari Kangaye iliyoko kata ya Nyakato wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Tuesday, July 19, 2011

RAIS WA GUINEA ANUSURIKA KUUAWA.

Majeshi yanayomtii Rais wa Guinea Alpha Conde yamezuia shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana kwenye makazi yake kwenye mji mkuu, Conakry.Ripoti zinasema, milio ya risasi ilisikika mapema siku ya Jumanne na ufyatulianaji risasi ukafuatia ambapo mmoja wa askari wa usalama wa Bw Conde aliuawa. Bw Conde alitoa wito wa watu kutulia kupitia televisheni ya taifa kufuatia shambulio hilo.

Ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, yenye historia ya kufanya mapinduzi na mapigano ya kikabila naye alichukua madaraka mwaka 2010 baada ya nchi hiyo kuongozwa kijeshi kwa muda mrefu.

Waandishi wanasema, shambulio kwa rais huyo inaonyesha ukubwa wa changamoto zinazoikabili serikali mpya ya kiraia. Ijapokuwa harakati hizo zimepungua, Conakry bado iko katika hali ya wasiwasi, na watu wengi wanabaki nyumbani.

Majeshi ya usalama yameweka vizuizi karibu na makazi ya rais huyo, huku wakikagua magari.


Hisani ya BBC Swahili.

MISS LAKE ZONE KIKAZI NA KIJAMII ZAIDI.

Tukiwa na siku chache hatimaye siku itimu (23.JULY.2011) tupate kukishuhudia kinyang'anyiro cha miss lake zone 2011 warembo washiriki mwishoni mwa wiki walipata fursa ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea hospitali ya Sekou Toure iliyopo jijini Mwanza na kisha mengine yakafuata CHEKSHIA PICHAZZzzzz!Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 walishiriki kufanya usafi katika Hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.

Mrembo Lydia Fredric akifanya usafi katika moja ya wodi za wazazi katika hospitali ya mkoa ya Seketoure

Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 wakifurahi kumbeba mtoto.

Mrembo Jackline Dismas akikabidhi Mche wa sabuni kwa Mama mjamzito katika moja ya wodi za wazazi katika Hospitali hiyo ya Mkoa.

Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 pia walipata fursa ya kutembelea soko la Kimataifa la Mwaloni jijini mwanza, hapa wanaonekena wakiuliza maswali juu ya biashara ya dagaa na samaki mwa kukaushwa sokoni hapo.

Warembo wa Vodacom Miss Lake Zone 2011, wakipata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Mwaloni ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwaloni Mh. Novak Manoko mwenye shati jeupe.

Muongozaji kutoka Vodacom bi. Miriam, akitoa maelezo ya utendaji kazi wa ofisi ya Huduma za mawasiliano Vodacom Mwanza.

Baadaye Warembo wa Vodacom Miss Lake zone 2011 walielekea Kiwanda cha Bia TBL ambako walijionea shughuli mbalimbali za utengenezaji wa vinywaji vizalishwavyo na kampuni hiyo. Pichani wakiwa wamepozz na muandaaji wa shindano Bi. Clara.
Jumamosi ya tarehe 23 july 2011 nani kulinyakuwa taji?

Picha na THE BIG TOP TEN.

UKATILI GANI HUU? MWANAMKE AKATWA KIGANJA CHA MKONO AKATWA MAGOTI YOTE MAWILI NA MUMEWE.

Mwanamke mmoja mkazi wa Nyabiroga Songa Bunchari Bi. Agnes Chacha (25) amefyekwa kiganja chake cha mkono pamoja na magoti ya miguu yote miwili na mume wake na kukatika vibaya tukio likitokea jana usiku ambapo kwa hivi sasa amelazwa katika wod 6 hosptali ya wilaya ya Tarime akipata matibabu.

Akizungumza kwa uchungu na kulia kwa maumivu makali ya majera Bi Agnes amesema kuwa juzi majira ya saa mbili mume wake aitwaye Chacha Hamis alimkata kigaja chake na kutoroka kusiko julikana mara baada ya mwananke huyo kuchelewa kurejea nyumbani.

Bi. Agnes amesema kuwa alifika nyumbani hapo saa mbili usiku akitokea kwenye biashara yao ya duka ambayo iko katika senta kijijini hapo na alichelewa kwa sababu juzi ilikuwa ni siku ya soko hivyo wateja huwa wengi ambapo mara nyingi huwa wanachelewa hata wakati mwingine wakiwa na mume wake.

Agnes akihojiwa na Helena Magabe mwandishi wa Habari hii .
Akiendelea kuzungumza kwa majonzi ya maumivu makali amesema kuwa baada ya kufika nyumbani aliwaagiza watoto wake kumfatia unga wa muhogo kwa wifi yake ambapo watoto walimwambia kwamba wanaogopa kwani ulikuwa usiku hivyo akalazimika kubandika maji jikoni na kwenda mwenyewe.

Baada ya kutoka kwa wifi yake akiwa na unga wake alimkuta mume wake akiwa amekaa nje na panga lake mkononi ambapo alimwuliza sababu za yeye kufikia nje akiwa na panga na kuongeza kuwa mume wake alimwuliza kuwa alikuwa wapi naye akajieleza vizuri.

“ mimi nina mamba ya mwezi mmoja imenisababishia kuuchukia ugari wa mahindi ndio maana linifata mwenyewe licha ya kwamba ulikuwa usiku lakini mume wangu hakutaka kunisikiliza japo nilikuwa na unga akaanza
kunilazimisha niseme nilikuwa wapi na na nilikuwa na nani” alisema.

Akiendelea kusimulia amesema mumewe huyo aliendelea kumlazimisha kusema aliyekuwa naye ndipo atamsamehe naye bila hiyana mwanamke huyo akaamua kumtaja bwana Muhiri kijana ambaye mume huyo amekuwa akimlazimisha kuwa ni mpenzi wake baada ya kupata maneno ya watu.

Akifafanua amesema kuwa mume wake huyo aliwahi kufungwa kipindi cha vita ya koo na aliporudi uraiani watu walimwambia kwamba mke wake Bi Agnes alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muriri hivyo mume wake tangu hapo akamwekea kinyongo jamaa huyo ingawa anadai walikuwa wanakiiishi vizuri.

Miguu.
Amesema kuwa baada ya watoto wake kuona amekatwa kiganja na kiganja hicho kuruka mbali walipiga yowe hivyo watu wakakusanyika ambapo baada ya kuwa amepata fahamu alimkuta shemeji yake, wifi yake pamoja na mke mwenzake wakifanya jitihada za kupata gari kwajiri ya kumpeleka hosptali.

Licha ya Bi.Agnes kufanyiwa ulemavu wa maisha amesema kuwa akipona atarudi kwa mume wake kwa sababu akiolewa mke mwingine atanyanyasa watoto na kuongeza kuwa hawezi kupokelewa na mtu mwingine akiwa na mkono mmoja ikiwa ni pamoja na kukosa ajira yoyote akiwa katika hali hiyo.

Muuguzi wa zamu ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema waliokuwepo katika zamu usiku waligoma kumtibu wakitaka barua toka polisi ambapo na jana asubuhi baada ya kuona wauguzi wamembana sana
kusema ukweli alisimulia kisa kizima ambapo polisi walifika wodini hapo na kumchukuwa maelezo.

“ wifi yake alikuwa hapa alikuwa anaficha sana na ana mdomo sana lakini na sisi tukajua ni mume wake amemkata na kweli ni mume yaani matukio kama haya ni mengi sana hapa hivi ulkuwaga wapi jamani kufatilia watu wamekatwa mikono, miguu, hata wengine wawili walikuwa hapa ungewahi kidogo tu ungewakuta” alisema muuguzi huyo.

Baadhi ya wanawake walio kumbwa na sekeseke kama hili ni pamoja na Nyangi Wansama Ryoba mkazi wa Nyamongo (31) aliyekatwa mgongo na mume wake ambaye ameruhusiwa kuondoka jana na mwingine ni Deborah Lucas Jockson(38) mkazi wa Buhemba wilayani Trime ambaye amepigwa na kuumizwa vibaya maeneo ya nyonga na mbavu zake kiasi cha kutembelea upande mmoja.

Monday, July 18, 2011

ICT (Information Communication Technology) AWARENESS CAMPAIGN IN PAMBA SECONDARY SCHOOL IN MWANZA CITY.

Staff executive hamis fupi give out lecture about advantages to study abroad..

Students make follow up the seminer in detail


ICT consultant Mr Hudson Chegero from Kenya give lecture about ICT to students.

Pamba secondary students wants to share ideas about ICT.

Inter zepha Tanzania limited located in Mwanza city offers free ICT awareness in secondary schools .Inter zepha Tanzania limited dealing with ICT Solution, computer sales, Repair, maintenance, and admission (application)to study Abroad, started ICT campaign awareness in schools in Mwanza .

Aim of this campaign is to make awareness about technology in the 21 century. In this century technology is applicable everywhere and so, Inter zepha helps students in primary and secondary schools understand technology free of cost.
The company gives out assignment to the students to write an essay about role of ICT in formal education and the winner is awarded a new Acer mini lap top from Inter zepha Tanzania limited
Inter zepha Tanzania Limited like to say thanks to Pamba secondary management especially to Head master Mr Lugangika who gave permission to make hold the seminar, also we give thanks to all A-level students who attended the seminar.
by
Inter zepha Management.
pobox 3043
mwanza
Tel:+255 28 2541410
info@interzepha.com
www.interzepha.comNDOA YA J LO NA MARC ANTHONY SASA VIPANDE VIPANDE

Baada ya kuwa ndani ya ndoa na mahusiano mazuri kwa kipindi cha miaka saba, Hatimaye Jennifer Lopez na Marc Anthony wametangaza kutengana rasmi.

"We have decided to end our marriage. This was a very difficult decision. We have come to amicable conclusion on all matters," they said in a statement. "It is a painful time for all involved, and we appreciate the respect of our privacy at this time."
The couple are parents to three-year-old twins Max and Emme.

Crooner Anthony, 42, was conspicuously absent at Saturday's star-packed BAFTA Brits to Watch bash in L.A., where wife Lopez, 40, met Prince William and Duchess Kate with mom Guadalupe as her date.

Anthony and first wife Torres share sons Cristin, 10, and Ryan, 7. Lopez (who famously dated Sean Combs in addition to Affleck), had been married twice before: to restauranteur Ojani Noa (they split in 1998) and former backup dancer Cris Judd, to whom she was married from 2001 to 2003.


Just last year, they renewed their wedding vows for their sixth anniversary at their Hidden Hills, Calif. estate June 5. "We realized the bets in Vegas [on whether we'd make it] stopped at five years," Anthony joked to Us at the time. (The duo also renewed their vows in 2008, and playfully dirty-danced together at Us Weekly's Hot Hollywood bash in April 2010.)

And as recently as January, singer, actress and American Idol judge Lopez gushed on the Ellen DeGeneres Show about being a parent with Anthony. "As soon as I had the babies, I thought to myself, 'I want to do this a thousand more times...I love this. This is life."

Sunday, July 17, 2011

ARUSHA SERENGETI FIESTA NI KUCHA & KUCHWA

Hawa ni wasanii wa Arusha ambao wameonekana kufanya vizuri sana katika tamasha la Serengeti Fiesta 2011 ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha LEO.

Wakazi wa jijini Arusha ambao wamejitokeza katika tamasha Serengeti Fiesta 2011.

Mchizan Diamond kufunika jadi yake...!!

Mkali mpya kwenye sanaa mwanada-da-da Recho..

Tamasha hili la Serengeti Fiesta 2011 lilifanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ni mara ya kwanza kwa tamasha hilo kufanyika uwanjani na kuhudhuriwa na watu kibao kutoka pande za mji wa Arusha.

picha zote na blogu ya KAJUNA