Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi leo imegawa msaada wa madawati kwa shule ya sekondari Kangaye jijini Mwanza ikiwa ni sehemu zake za kuisaidia jamii. Pichani meneja wa masoko kanda ya ziwa Ally Maswanya akikabidhi mchango huo kwa uongozi wa Shule.
Meneja wa shughuli za kijamii Tunu Kavishe amesema kuwa Airtel mara baada ya kuona uhaba uliopo kwa shule nyingi nchini ili kuisaidia serikali kampuni yake imedhamiria kutoa zaidi vifaa mbalimbali vya elimu na kufundishia kama sehemu yake muhimu katika kuikwamua jamii.
Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata hiyo ya Nyakato bw. Josephat Manyerere: Ameishukuru sana Airtel kwa kuichagua Mwanza kama sehemu moja wapo ya kuinua elimu na amefurahishwa kusikia kuwa mpango huo kuwa ni endelevu kwani utapunguza uhaba wa madawati na nyezo za elimu kwa mashule.
Ni miaka saba sasa tangu Airtel ilipoanza mpango wake wa kusaidia nyenzo mbalimbali za elimu ikiwemo vitabu kwa shule za sekondari hapa nchini ambapo hadi sasa shule takribani 800 zimenufaika na mpango huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.