ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 19, 2011

RAIS WA GUINEA ANUSURIKA KUUAWA.

Majeshi yanayomtii Rais wa Guinea Alpha Conde yamezuia shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana kwenye makazi yake kwenye mji mkuu, Conakry.Ripoti zinasema, milio ya risasi ilisikika mapema siku ya Jumanne na ufyatulianaji risasi ukafuatia ambapo mmoja wa askari wa usalama wa Bw Conde aliuawa. Bw Conde alitoa wito wa watu kutulia kupitia televisheni ya taifa kufuatia shambulio hilo.

Ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, yenye historia ya kufanya mapinduzi na mapigano ya kikabila naye alichukua madaraka mwaka 2010 baada ya nchi hiyo kuongozwa kijeshi kwa muda mrefu.

Waandishi wanasema, shambulio kwa rais huyo inaonyesha ukubwa wa changamoto zinazoikabili serikali mpya ya kiraia. Ijapokuwa harakati hizo zimepungua, Conakry bado iko katika hali ya wasiwasi, na watu wengi wanabaki nyumbani.

Majeshi ya usalama yameweka vizuizi karibu na makazi ya rais huyo, huku wakikagua magari.


Hisani ya BBC Swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.