Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto)
akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta
katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam jana.
Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa
Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel
Fursa Lab” Dar es Salaam jana.
Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar
Kampuni
yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es
Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara
ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo
hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo
hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu
na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia
kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama
na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara
kwa kutumia technologia za kisasa
Akiongea
kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo
awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni
bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii
itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na
hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.
Waalimu
wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii
inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania,
aliongeza Matinde.
Hata
hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa washaanza
yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale wanafunzi ambao
walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika ni chukua hatua ya
ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao waweze kuwa kwenye nafasi ya
kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema Matinde.
Matinde
aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana
wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema
maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani vijana kuongeza ujuzi
na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.
Kwa
upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “ Tayari
tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama. Tuhahakisha kuwa
walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao waanze kutoa mafunzo na elimu
kwa wanafunzi.
Jengela
alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa
watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects” msingi
wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali
Bado
tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha
vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www. airtelfursa.com au
kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama