Akizungumza baada ya kumaliza kuhojiwa jana jijini Dar es Salaam, Jacob alisema, alitoa utetezi wake kuwa hakufanya kikao isipokuwa alitembelewa na wageni wa chama, lakini kama wanaona anastahili kuwajibishwa wafanye hivyo.
Kadhalika Jacob alisema alitoa ushaidi wa matumizi mabaya ya ofisi za umma, yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nimewaeleza Sekretarieti kuwa, pia CCM, kimekuwa kikifanya vikao vyake Ofisi za Ikulu na wamenieleza hakuna aliyewahi kulalamika. Hivyo nimelazimika kuandika barua ya malalamiko juu ya kitendo hicho,” alisema.
Kuhusu shauri lake la vyeti feki aliloliwasilisha mahakamani Mhe. Boniface amefunguka "Nikiwa hai nikiwa mfu ningependa shauri lifike kwenye baraza la maadili"
Kuitwa na kuhojiwa kwa Jacob na Sekretarieti hiyo kumetokana na kitendo chake cha kumkaribisha ofisini kwake Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.