ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 14, 2013

PAMBA YASHINDA 1-0 DHIDI YA TOTO LIGI DARAJA LA KWANZA

Pamba Sport Club.

Toto Africans.

PAMBA YASHINDA 1-0 DHIDI YA TOTO LIGI DARAJA LA KWANZA

NA. ALBERT G. SENGO: MWANZA

Timu ya soka ya Pamba ya jijini Mwanza imeanza vyema safari yake kuelekea ligi kuu mara baada ya kuifunga Toto Africans bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi C, Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uliochezwa dimba la CCM Kirumba.

Pamba ilipata bao hilo la ushindi katika dakika ya 5 tu kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Paschal Liponda mara baada ya kupokea mpira wa krosi ya winga machachari Mathius Wandiba.

Dakika 90 zinamalizika zikishuhudia Pamba wakitoka kidedea na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Toto.
- Athuman Bilali ambaye ni Kocha wa Toto Africans anazungumza na Sports Xtra juu ya kichapo kwa timu yake.


- Naye Kocha wa Timu ya Pamba Kazimoto Muzo alikuwa na haya ya kusema.

MH. LOWASSA ASIMIKWA KUWA CHIFU WA UNYANYEMBE MKOANI TABORA.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa katika vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na Machifu kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.


MAHASIMU WAWILI PAMBA NA TOTO KUUMANA CCM KIRUMBA HII LEO.

Pamba iliyojenga heshima ya soka la Mwanza, itarejea?
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
LIGI Soka daraja la kwanza Tanzania bara inataraji kuanza rasmi kutimua vumbi LEO Jumamosi ya tarehe 14 sept 2013 kwa makundi yote matatu nchini.

Tuelekee kundi C ambapo zaidi litazihusu timu za Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati.

Katika michezo minne, miwili kati yake itakayopigwa inaonekana kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa kwanza ni wa pale mjini Shinyanga kati ya Mwadui Fc V/s Stand United na wa pili ni ule utakaochezwa dimba la CCM Kirumba ukihusisha mahasimu wawili wa Jiji la Miamba, Wana Kawekamo (Pamba Fc) V/s Wana Kishamapanda (Toto Africans)...   


 Zaidi sikiliza mahojiano ya A.G. Sengo wa Sports Xtra na Maafisa habari wa timu za Toto na Pamba, Kwa kubofya play hapo kulia.

MH. LOWASSA AKUTANA NA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU MKOANI TABORA NA KUTEMBELEA CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Tabora,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini,mchana wa leo Septemba 13,2013.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Tabora waliofika kumlaki alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora mchana wa leo Septemba 13,2013.
Msafara wa Pikipiki (maarufu kama Boda Boda) Mkoani Tabora ukiwa barabarani wakati wa kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora leo,ambapo alitembelea Ofisi za Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora wakati alipokitembelea Chama hicho jioni ya leo Septemba 13,2013.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Waziri Kipusi.
Mwenyekiti wa Chama Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora,Waziri Kipusi (kushoto) akisoma taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa juu ya mwenyendo wa Chama hicho pamoja na malengo yake.ambapo Mh. Lowassa ameahidi kuwapatia pikipiki tatu,ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwenye Chama hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kwenye mkutano wake ya Waendesha Boda Boda wa Mkoa wa Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Watoto waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora leo,Septemba 13,2013.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo na Watoto Chipukizi waliokuwepo nje ya Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye kipaza sauti) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Vyo mbali mbali Mkoani Tabora,waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Utumishi,Mkoani Tabora leo Septemba 13,2013.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tabora Mjini,Seif Gulamali akizungumza machache mbele ya Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora leo.
Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh. Athuman Kapuya akijibu moja ya Maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Wanafunzi hao wa Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora waliokuwa wamefurika kwa wingi ndani ya Ukumbi wa Chuo cha Utumishi Mkoani humo,kumsikiliza Mh. Lowassa.
Baadhi ya wanafunzi hao kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora,wakiuliza maswali.
Baadhi ya wanafunzi hao kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora,wakiuliza maswali.
Baadhi ya wanafunzi hao kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora,wakiuliza maswali.
Wanafunzi kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora kusanyikoni.

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA YAFANYIKA MKOANI DODOMA

Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.

Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.


Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
  
Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
 
Mwakilishi wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.


Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya  mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.


Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.
 
Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
 
Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

Friday, September 13, 2013

AUNGUZWA VIDOLE NA MAMA YAKE MKUBWA KISA KUDOKOA MBOGA.


Blogger G. Sengo akiwa amembeba mtoto Winfrida Nicolaus aliyeunguzwa na mke wa baba yake mkubwa ambaye ni askari polisi, kwa madai ya kudokoa mboga.
ALBERT G. SENGO.
MTOTO Winfrida Nicolaus ( miaka zaidi ya 8)ameunguzwa vibaya na moto  kwenye vidole vyake vya Mkono wa kulia kwa kutuhumiwa kudokoa minofu miwili ya nyama kwenye sufuria na mke wa Baba yake mkubwa ambaye ni Askari polisi Mkoani hapa maeneo ya Nyansaka Wilayani Ilemela Jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika Kituo cha Kuzuia na Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto Majumbani kilichopo eneo la Kiloleli Wilayani hapa alipohifadhiwa na kupatiwa matibabu, alisema kwamba mama yake huyo alimkamata na kumfunga kitambaa mkono wa kulia kisha kummwagia mafuta ya taa na kuwasha kiberiti na kumchoma moto.

Kitendo hiki ni cha kinyama kisichokubalika kwa jamii kutokana na hatua zilizochukuliwa na Mke wa Askari Polisi huyo cha kumfuata mtoto Winfrida kijijini kwao na  kumchukua kuja kuishi naye kwa lengo la kumlea kumbe akija kumfanyia ukatili na kumsababishia ulemavu wa mkono wake wa kulia ambao vidole vyote vitano alivichoma moto kwa mafuta ya taa.

“ Alinishika na kusema eti nimedokoa nyama minofu miwili niliposema sio mimi alinichapa fimbo kila sehemu na akanifunga kitamba na kunimwagia mafuta ya taa na kunichoma na moto wa kiberiti nililia lakini alikuwa nananifungia ndani ili watu wasinione” alisimulia mtoto huyo

Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha Foundation Karibu Tanzania Johanes Emmanuel (kulia).
Naye Afisa Ustawi wa Jamiii Kituo cha Foundation Karibu Tanzania Johanes Emmanuel alisema kuwa kutokana na kuzidi kwa kasi ya ukatili Jijini Mwanza kutajwa kuongezeka kumepelekea Kituo hicho kupokea watoto waliofanyiwa ukatili majumbani ambapo imevuka malengo kwa asilimia 25 ya mwaka ya kutegemea kuokoa watoto 40 na sasa wanaokoa watoto na kupokea wapatao 100 kwa mwaka.

Afisa, Emmanuel tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2011 kimeokoa zaidi ya watoto 120 waliounguzwa kwa moto na mpaka sasa watoto 94 wamerudi makwao na 27 ndiyo walio bakia kituoni hapo wakiendelea na matibabu na kusubilia kupewa elimu wazazi na walezi wao waliowafanya ukatili jambo ambalo huwaogopesha watoto hao wakati wakiambiwa kuchukuliwa kurudi majumbani mwao.
Picha za watoto waliokumbana na ukatili.

“Ukatiili huu upo kwenye majumba na kitendo cha watoto kufichwa majumbani baada ya kutendewa ukatili na kupatwa na majeraha husababisha wengi wao kupata ulemavu wa kudumu kutokana na kutelekezwa kwa kukosa Tiba ya haraka naya uhakika kwa majeraha waliyopata hali ambayo huwachukua muda mrefu kupona hasa wanapochukuliwa na Kituo hiki kuanza kufanyiwa utaratibu wa matibabu” alieleza.

Inasikitisha kwa mtoto huyu aliyekumbana na ukatili wa kucharangwa mikono kama ukataji muwa unavyokuwa.
Aliongeza kuwa Kauli mbiu ya Kituo hicho inaeleza kuwa “tunahitaji siku moja tuwe na Dunia huru dhidi ya Ukatili, watoto wawe salama na waone dunia ni sehemu sala kuishi kwa furaha na amani na sio kufanyiwa ukatili na kusababishiwa wao kuwa walemavu” imebainisha.

Afisa huyo ameitaka jamii kutambua sasa na kuanza kuchukua hatua na kumgusa kila mmoja kuanza kulishughulikia kukabiliana nalo ili kuwezesha kupunguza kasi na kumaliza kabisa kasi iliyoshamili ya ukatili wa watoto majumbani jambo ambalo halina budi kutolewa elimu na taarifa kwa jamii na viongozi wa serikali, vyama vya siasa na madhehebu ya dini maeneo mbalimbali vijijini na Wilayani kote. 


Picha hizi zinaonyesha madhara ya ukatili kupitia vipigo, kumwagiwa maji ya moto, kuchomwa moto, kufanyiwa ukatili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali na kupigwa na vitu vizito sehemu mbalimbali za mwili.  

Jengo la kituo.

MSHINDI WA NYUMBA YA PILI AIRTEL YATOSHA APOKEA CHETI CHA USHINDI RASMI

Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmmbando (kushoto)  akimkabidhi cheti Mshindi wa Nyumba wa Airtel Yatosha bi. Anna G.Lyimo mkazi (kulia) wa  Dar Es Salaam  akishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga.

 Mshindi wa Nyumba wa pili wa Airtel Yatosha  bi. Anna G. Lyimo akionyesha cheti chake alichokabidhiwa na Meneja wa uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kulia), wakishuhudiwa na Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kushoto)

Meneja wa uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio la makabidhiano kukamilika.

Dar es Salaam Septemba 12 , 2013 Mshindi wa nyumba ya pili ya Airtel Yatosha yenye thamani ya shilingi milioni 65/- amekabidhiwa cheti cha ushindi leo ikiwa ni uthibitisho maalum  mbele ya wanahabari ambapo ni muda mfupi  baada ya mshindi huyo kuibuka mshindi kupitia droo kubwa ya mwisho wa mwezi iliyochezeshwa wiki iliyopita

Airtel Tanzania kupitia promosheni hiyo imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake zikiwemo pesa taslim pamoja na nyumba 3 Akizungumza kwa furaha Mshindi wa nyumba hiyo ya pili Bi Anna Gustav
Lyimo ambae ni mkazi wa Dar es salaam alisema “namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha  kuwa mshindi wa nyumba ya Airtel Yatosha,

Nilipopigiwa nilijua ni matapeli, mpaka siku ya pili nilipopigiwa  kwa mara ya pili na Airtel ndipo nilipojua si utapeli” “Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii  kwani imenirahisishia mipango
yangu ya kuanza ujenzi wa Nyumba mwishoni mwa mwaka huu.  ,” alisisitiza Bi, Lyimo

“Ninawashauri wateja wengine wa airtel kuendela kutumia huduma ya Airtel yatosha ili na wao waibuke washindi kama mimi” alimalizia kusema Bi Anna Lymo
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema “makabidhiano ya cheti hiki ni taratibu za awali ambapo hivi karibuni mshindi huyu atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam”

“Airtel tutaendelea kutoa zawadi bora kwa wateja wetu nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali tulizonato” “Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo bado tunatoa zawadi za pesa taslim kila siku kwa wateja mbalimbali wa Airtel nchi nzima. Njia ni rahisi tu! Jiunge sasa na vifurushi mbalimbali vinavyo patikana kupitia Yatosha na utapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda,” alisema Mmbando.
 
Kujiunga na vifurushi hivyo mteja anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote cha Wiki, Siku au Mwenzi.


Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha  imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 60 kwa wateja wake kupitia promosheni hii ambapo Promosheni hii  inadumu kwa siku 90 toka ianze, hadi sasa bado kuna nyumba moja kati ya tatu zilizopo Kigamboni itashindaniwa kwa mwezi huu.

MASANJA ALIVYOKANDAMIZA KWENYE MAZISHI YA KULOLA.

Emanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji akizungumza na kusanyiko lililojitokeza kwenye mazishi ya Askofu wa EAGT hayati Moses Kulola aliyefariki na kuzikwa kwenye eneo la wiwanja vya kanisa la EAGT Bugando jijini Mwanza. 
Mbali ya kuwa mchekeshaji mahiri, Masanja Mkandamizaji ana karama ya uinjilisti, akitambulika kama Mchungaji wa kanisa la Mito ya Baraka. Katika mazishi ya Askofu kulola, Masanja alipata nafasi ya kuimba (kwani ana album ya muziki wa Injili) katika ufafanuzi wa moja ya nyimbo zake alisema  "Hakuna mstari kwenye Biblia usemao 'baada ya kifo ni kesi', bali kuna unaosema 'baada ya kifo ni hukumu'," Kisha akaongeza... "Kuna tofauti kati ya kesi na hukumu, kesi unasomewa na kujitetea na mengineyo ya kutafuta ushahidi, lakini hukumu ni kwamba mambo yoooote yamejulikana na sasa kinachobakia ni kusalimika ukarejea uraiani au kukutana na kifungo"

"Ingekuwa baada ya kifo  ni kesi hakuna Mtanzania angeenda motoni kwani Watanzania ni mafundi kwenye kujitetea hivyo Mungu aliliona hilo....."(Bofya play kumsikiliza.)

Thursday, September 12, 2013

BATA LA BIRTHDAY YA DJ K-FLIP

Flash...

Mwaaaaah...!!

Tost...!!

Wuuuuu...!!!

Tishaaaa...!!

Poz..

Crazy hour...!!

Per Moko..

Haiwezekani.

Show up...!!

Frees..!

Hands Up..!!

You are not alone..