Blogger G. Sengo akiwa amembeba mtoto Winfrida Nicolaus aliyeunguzwa na mke wa baba yake mkubwa ambaye ni askari polisi, kwa madai ya kudokoa mboga. |
ALBERT G. SENGO.
MTOTO Winfrida Nicolaus ( miaka zaidi ya 8)ameunguzwa
vibaya na moto kwenye vidole vyake vya
Mkono wa kulia kwa kutuhumiwa kudokoa minofu miwili ya nyama kwenye sufuria na
mke wa Baba yake mkubwa ambaye ni Askari polisi Mkoani hapa maeneo ya Nyansaka
Wilayani Ilemela Jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea
katika Kituo cha Kuzuia na Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto Majumbani
kilichopo eneo la Kiloleli Wilayani hapa alipohifadhiwa na kupatiwa matibabu,
alisema kwamba mama yake huyo alimkamata na kumfunga kitambaa mkono wa kulia
kisha kummwagia mafuta ya taa na kuwasha kiberiti na kumchoma moto.
Kitendo hiki ni cha kinyama kisichokubalika kwa
jamii kutokana na hatua zilizochukuliwa na Mke wa Askari Polisi huyo cha kumfuata
mtoto Winfrida kijijini kwao na
kumchukua kuja kuishi naye kwa lengo la kumlea kumbe akija kumfanyia
ukatili na kumsababishia ulemavu wa mkono wake wa kulia ambao vidole vyote
vitano alivichoma moto kwa mafuta ya taa.
“ Alinishika na kusema eti nimedokoa nyama minofu
miwili niliposema sio mimi alinichapa fimbo kila sehemu na akanifunga kitamba
na kunimwagia mafuta ya taa na kunichoma na moto wa kiberiti nililia lakini
alikuwa nananifungia ndani ili watu wasinione” alisimulia mtoto huyo
Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha Foundation Karibu Tanzania Johanes Emmanuel (kulia). |
Naye Afisa Ustawi wa Jamiii Kituo cha Foundation
Karibu Tanzania Johanes Emmanuel alisema kuwa kutokana na kuzidi kwa kasi ya
ukatili Jijini Mwanza kutajwa kuongezeka kumepelekea Kituo hicho kupokea watoto
waliofanyiwa ukatili majumbani ambapo imevuka malengo kwa asilimia 25 ya mwaka
ya kutegemea kuokoa watoto 40 na sasa wanaokoa watoto na kupokea wapatao 100
kwa mwaka.
Afisa, Emmanuel tangu kuanzishwa kwa kituo hicho
mwaka 2011 kimeokoa zaidi ya watoto 120 waliounguzwa kwa moto na mpaka sasa
watoto 94 wamerudi makwao na 27 ndiyo walio bakia kituoni hapo wakiendelea na
matibabu na kusubilia kupewa elimu wazazi na walezi wao waliowafanya ukatili
jambo ambalo huwaogopesha watoto hao wakati wakiambiwa kuchukuliwa kurudi
majumbani mwao.
Picha za watoto waliokumbana na ukatili. |
“Ukatiili huu upo kwenye majumba na kitendo cha
watoto kufichwa majumbani baada ya kutendewa ukatili na kupatwa na majeraha
husababisha wengi wao kupata ulemavu wa kudumu kutokana na kutelekezwa kwa
kukosa Tiba ya haraka naya uhakika kwa majeraha waliyopata hali ambayo
huwachukua muda mrefu kupona hasa wanapochukuliwa na Kituo hiki kuanza
kufanyiwa utaratibu wa matibabu” alieleza.
Inasikitisha kwa mtoto huyu aliyekumbana na ukatili wa kucharangwa mikono kama ukataji muwa unavyokuwa. |
Aliongeza kuwa Kauli mbiu ya Kituo hicho inaeleza
kuwa “tunahitaji siku moja tuwe na Dunia huru dhidi ya Ukatili, watoto wawe
salama na waone dunia ni sehemu sala kuishi kwa furaha na amani na sio kufanyiwa
ukatili na kusababishiwa wao kuwa walemavu” imebainisha.
Afisa huyo ameitaka jamii kutambua sasa na kuanza
kuchukua hatua na kumgusa kila mmoja kuanza kulishughulikia kukabiliana nalo
ili kuwezesha kupunguza kasi na kumaliza kabisa kasi iliyoshamili ya ukatili wa
watoto majumbani jambo ambalo halina budi kutolewa elimu na taarifa kwa jamii
na viongozi wa serikali, vyama vya siasa na madhehebu ya dini maeneo mbalimbali
vijijini na Wilayani kote.
Jengo la kituo. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.