Airtel yazindua Minara ya Mawasiliano inayotumia umeme wa Jua
. kupunguza changamoto za umeme vijijini
. kurahisisha mawasiliano madhubuti
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua
minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua katika kijiji
cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya
mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji
wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za
uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake
nchini.
Akiongea wakati wa
uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga
Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza
kukabili changamoto za mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji
wa uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo
awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na mawasiliano
thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa kupitia Mtandao na
huduma ya Airtel money huduma za kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na
kuwawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama
nafuu na bila usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama
za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na
kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwa Mpululu
Naye mkazi wa kata ya
Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji
kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel.
Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo
kuwafanya wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano.
Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli
mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.
Akiongea kwa niaba ya
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando
alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya diesel na generator
kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia umeme wa nishati ya jua ambao
utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji ambazo
zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia
watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na
wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi
nikulinda huduma hizi na kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu
ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata gharama za
uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye viwango vya juu kwa
gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”
Kampuni ya Airtel katika
kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga mitambo ya umeme wa sola
katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa
mengine mingi. Mpaka sasa Airtel imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia
nguvu za jua katika mkoa wa iringa Iringa vijijini. Mpaka sasa Airtel inaongoza
kwa kutoa huduma zenye wigo mpana na ina vijiji na miji 50 zaidi.