Silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji kwa ukaribu zaidi. |
Silaha hiyo iliyotengenezwa kienyeji, risasi zilizokamatwa na RB ya polisi. |
JESHI la Polisi Mkoani Mwanza
limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa tukio la ujambazi wakiwa na silaha
moja ya kienyeji ikiwa na risasi sita za Short-gun na kukili kufanya uhalifu na
kumuua mlinzi mmoja na kumjeruhi mwingine kwa kumpiga nondo kichwani maeneo ya
Busweru kona Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Liberatus Barlow akizungumza ofisini kwake amesema kuwa jeshi hilo
limefanikiwa kuwakamata majambazi hao wanaohusishwa na tukio lililotokea
Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku katika maeneo ya maduka mawili
Busweru kona Kata ya Busweru Wilayani Ilemela ambapo watuhumiwa walimuua mlinzi
mmoja Mwita Chariya(40) na kumjeruhi mwingine Mwita Wambura wote wakiwa wakazi
wa Mabatini Wilayani Nyamagana.
Kamanda Barlow amesema kuwa baada ya
tukio hilo jeshi la polisi liliunda kikosi kazi na kuanza msako wa kuwatafuta
wahusika wa tukio hilo huku wakipokea ushirikiano wa raia wema kwa kutumia
falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi ambapo mnamo Septemba 26 mwaka huu
majira ya saa 7:30 walianda mtego na kufanikiwa kumkamata moja kati ya
watuhumiwa Jonathan Fredrick mkazi wa Nyakato jijini Mwanza akiwa
nyumbani kwake.
Mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa
aliwataja wenzake nalo jeshi la polisi likaweka mtego mwingine na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wengine wawili walio salia Mkubwa Rajab na Jonathan
Athuman wote wakazi wa Mabatini.
Watuhumiwa hao licha ya kukiri
kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo hilo la
kuua mlinzi waliwaonyesha mahala walipoficha silaha hiyo iliyotengenezwa
kienyeji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.