ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 8, 2012

WAKAZI WA TABORA WAPAGAWISHWA NA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012

Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.

Anaitwa Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangwaka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo
 .
Nikki Mbishi akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabota.
watu walivyojutokeza wingi kwenye tamasha la Serenegeto Fiesta
Pichani kulia ni Daffih Dauda Dauda anbaye abaemamai ghetto
Wakazi wa mji wa Tabora wakiwa ndani ya uwannja wa Ally Hassan Mwinyi wakati tamasha la Serengeti Fiesa lilipokuwa linaondoka
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua mashine,na kulia kwake ni Hamza Balla,
Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012,Supa Nyota Ney Lee akitumbuiza jukwaani.
Msanii Recho akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa madens wake
Msanii mahri wa muziki wa kizazi kipya,Ben Paul akionesha kipaji chake ch a kuimba.

Palikuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.
Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku
Mbunge wa Tabora Mjini,Mh Afeni Rage akisoma moja ya namba ya aliyebahatika kuibuka na bajaji,kulia kwake ni Mkuu wa utafiti wa Clouds .TV,Bwa.Ruge Mutahaba.
NI full mzuka mwanzo mwisho kwa mashabiki.
Sir Juma Natura akikamua usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 202

Watu walikuwa kibao.

Hamza Balla na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.

Friday, September 7, 2012

VIDONDA VYA TUMBO, KANSA, UZAZI NA KUTOKA DAMU BILA MPANGILIO KWA AKINA MAMA NA TIBA ZA ASILI KWA MAGONJWA SUGU SASA LIVE KWENYE MAONYESHO UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA

Jeh unajua kwa nini unasumbuliwa na maumivu mbalimbali katika mwili wako?
Jibu liko ndani ya viwanja vya Maonyesho ya Biashara Nyamagana jijini Mwanza katika banda la Dr Top Manyota, ambapo utakutana pia na Dr. Yustas Nyakubaho Nyakujanga kutoka Ngara mkoani Kagera.

Daktari wa tiba asili, dawa ambazo zimeweza kusaidia wengi Dokta  Yustas Nyakubaho Nyakujanga kutoka Ngara mkoani Kagera akitambulisha mawasiliano yake kwa wananchi kuweza kumpata kirahisi.

Ndani ya banda hili kuna dawa mbalimbali za kuondosha sumu mwilini, dawa za kutatua maumivu ya meno na jino lililotoboka, maradhi sugu, asaz, kurejesha nguvu kwa miguu iliyopalalaiz, chango la uzazi na kadhalika. 

Ni mojakati ya dawa za ajabu zilizo na uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali yaliyoshindikana... Karibu uepukane na kuumwa kusikosikia dawa za hospitali upate virutubisho vya mwili wako uboreshe afya.

Soma mwenyewe....

Dr. top Manyota akitambulisha moja kati ya dawa zake kulia kwake kashika dawa ya kuamsha miguu iliyoparalaiz  na kushoto kwake kashika dawa ya asaz zote zikiwa na maelezo tosha, wadau hawa wakipatikana ndani ya uwanja wa maonyesho wa biashara Nyamagana jijini Mwanza, yakitaraji kumalizika jumapili hii.  
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nao kupitia 0763 735662

NAFASI ZA KAZI MWANZA NA BUKOBA


 JOB ADVERTISEMENT 
1. THERE IS A CHANCE FOR HOTEL MANAGER WITH MINIMUM QUALIFICATION OF ADVANCED DIPLOMA IN HOTEL MANAGEMENT WITH WORK EXPERIENCE OF NOT LESS THAN FIVE YEARS.

2. AN ACCOUNTANT WITH AT- LEAST A DIPLOMA IN ACCOUNTING WITH EXPERIENCE OF NOT LESS THAN TWO YEARS IN THAT FIELD, AND SHOULD BE ABLE TO USE ACCOUNTING PACKAGE SUCH AS TALLY, MYOB PASTEL ETC.

ALL APPLICATIONS SHOULD BE SENT ELECTRONICALLY VIA denmahs@yahoo.com or dlwampama@yahoo.com

Contact phone is 
+255767026172/0787026172

NANI KUTWAA TAJI LA REDD'S MISS KINONDONI 2012, SEPT 14?

Jeniffer Manu.
Mwatumu Mustapha.

Zulfa Vuai.

Diana Hussein.
Kudra Lupatu.

Nahma Saidi.

Brigitter Alfred.

Ester Mussa.

Judith Sangu.

Hawa ni baadhi tu ya warembo watakaoshiriki katika kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kinondoni 2012.

MAREHEMU ELISHA PAUL AZIKWA KIJIJINI KWAO

Mchungaji wa kanisa la Anglican akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Elisha Paul aliyefariki tarehe 4/09/2012 katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Watu wa karibu na marehemu Elisha Kulwa ambaye ni mmoja kati ya vijana wanaharakati walifurika na kuhudhuria mazishi hayo yaliyofanyika kijiji cha Misasi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.




Dada wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa kaka yake.


Wingu zito la majonzi lilitanda kwa ndugu jamaa na marafiki waliofika kwenye safari ya mwisho ya marehemu Elisha Kulwa.

Hali ilikuwa tete kwa ndugu zake wa karibu.
Safari kuelekea makaburini...

Mwili katika ibada kuilaki nyumba yake ya milele.


Picha ya pamoja kwa familia makaburini.

Sister Rodha Ndamanyhilu katikati akiwa na ndugu wakaribu wa marehemu Elisha Kulwa.

Na gari letu la homu.."Furahini katika bwana tena nasema furahini" 

Mr & Mrs Isaac Ndamanyhilu wakiwa na watoto wao kwenye shamba la familia ambako ndiko alizikwa marehemu mpendwa wao Elisha Paul ambaye ni mdogo wake bw. Isaac. 
Mie na katotoo na kwa chati ni my sis Rodha.

Thursday, September 6, 2012

AIRTEL ANNOUNCES AY AS AIRTEL ARTIST'S AMBASSADOR FOR 2012 - 2013

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (shoto) akimkabidhi msanii Ambwene Yessayah* (*AY) simu aina ya Sumsung Galaxy mara baada ya kumtangaza AY kuwa Balozi wa Airtel kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania, *AY sasa kushiriki shughuli zote za kijamii za Airtel nchini. *Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi. Hafla ya hiyo ilifanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini Dar es salaam.  

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kati) akimtangaza msanii Ambwene Yessayah* (*AY) (shoto) kuwa Balozi wa Airtel Tanzania kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania kwa mwaka 2012 -2013, *AY sasa atashirikiana na Airtel katika  shughuli zote za kijamii za Airtel nchini*kwa lengo la kufaidisha taifa letu hasa sekta ya ELIMU. Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi. Hafla ya hiyo ilifanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini Dar es salaam 


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtangaza Balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013 ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea katika kushirikiana na wasanii nchini ili kufanya shughuli mbalimbali za kijamii. 

AY ni msanii mahiri nchini kwenye muziki wa kizazi kipya aliyejipatia heshima na kuvuta hisia za wapenda burudani wengi pale anapokuwa jukwaani, AY alijulikana zaidi baada ya kuachia album yake ya kwanza iliyobeba wimbo mkali wa ‘Raha kamili” na kufanya apendwe zaidi kitaifa na kimataifa kuanzia mwaka 2001

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeingia makubaliano na msanii AY kuwa Balozi wetu wa mwaka huu, lengo letu ni kuendelea kuwa karibu zaidi na wasanii wetu nchini na pia kufanya nao shughuli za kijamii ili kufaidisha taifa letu kwa kuwa wasanii wetu ni mahiri zaidi na wote tunafahamu  AY ni msanii mkongwe na anayejituma, hivyo tunaamini  ushirikiano huu utaweza kutimiza malengo yetu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhudumia jamii kupitia miradi mbali mbali ya jamii inayoendeshwa na Airtel pamoja na kuiwakilisha Airtel kwa kuwa Balozi mzuri”

“Sasa AY atakuwa ni msanii wa pili kuingia mkataba kama huu ambapo mwaka uliopita alikuwa Ali Kiba. Tulimtangaza Ali kiba kuwa  Balozi wa Airtel mwaka jana na ameshirikiana na Airtel kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kuitangaza Airtel kupitia matangazo ya radio, Luninga, Mabango na Mabandiko lakini pia alifanikiwa kuiwakilisha nchi yetu kwenye wimbo wa Hands Across the World alioimba na wasanii wengine wa kimataifa akiwemo R. Kelly katika kundi la One8 kwa udhamini wa Airtel na kufaulu sana kubainisha umahiri wa wasanii wa Tanzania kwenye mataifa mengine makubwa kupitia kazi yake nzuri aliyofanya ndani ya wimbo huo”aliongeza Mmbando.

AY ni msanii mwenye umahiri wa hali ya juu pale anapokuwa jukwaani, AY ameshafanikiwa kufanya matamasha ya kimataifa huko USA, UK, Spain, Dubai, Burundi, Rwanda, Ethiopoa, Malysia, India, Russia, Afrika ya kusini, Kenya na Uganda ikiwa ni pamoja na kufanya nyimbo nyingi na wasanii wengi wa kitaifa na kimataifa 

Wasanii waliowahi kufanya nyimbo na AY ni pamoja na Chameleon, Ngoni(Uganda), Amani, Nameless, Jua Cali (Kenya), P.Square, J.Martins (Nigeria)wengine ni msanii wa kimataifa Ms.Trinity, Sean  Kingston anayewika Jamaica pamoja na  Lil Romeo wa USA.

Vilevile AY ni msanii wa kwanza wa kiume nchini Tanzania kutunukiwa tuzo ya KORA mwaka 2005, na kupata pia tuzo ya MTV MAMAs ya 2009 pamoja na kutunikiwa France Awards mwaka 2010. Na hivi sasa amechaguliwa katika kuwania tuzo za Channel O katika vipengele vitatu; Video bora ya Africa, Video bora ya mwaka na mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka.****

Kwa upande wake Ambwene Yessayah kama balozi wa Airtel alisema “kwa kushirikiana na Airtel nitakuwa nikifanya shughuli za kijamii, hususani katika kuchangia ukuaji wa Elimu nchini. Pamoja na Airtel tutashirikisha vyombo na taasis nyingine ikiwemo vyombo mbalimbali vya Habari ili kuweza kufanikisha yote hayo. Kwa Kushirikiana na Airtel tutaandaa maonyesho mbalimbali ya burudani kwa ajili ya wateja wetu na hii itatangazwa hivi karibuni”.

“Na kwa kuanza kama balozi wa Airtel napenda kuwaomba na kuwaimiza Watazania wenzangu kuweza kuchangia mradi ambao tumeshauanzisha wiki tatu zilizopita tukishirikiana na BAMVITA katika kuchangia vitabu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum. Kampeni hii ya ushirika na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu, na Watanzania tunaweza kuchangia kwa kutuma neno *“Vitabu*” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS tutakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 itakayoingizwa yote katika mradi huu.” 

“Vile vile wadau wengine wote wataweza kuchangia kwa kupitia huduma ya Airtel Money ambapo jina la fumbo ni *VITABU* au kutuma michango yao kwenda namba 0788041361. Hivyo basi ningependa kuwahamasisha watanzania wote kuchangia kiasi chochote mtakachoweza pia unaweza kuchangia zaidi ya mara
moja.”