ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Showing posts with label SANAA. Show all posts
Showing posts with label SANAA. Show all posts

Sunday, August 11, 2024

MBUNGE KOKA KUANZISHA KLINIKI MAALUMU YA KUKUZA VIPAJI KWA WASANII

 


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuibua vipaji vya wasanii wa fani mbali mbali ameweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuanzisha kliniki maalumu ambayo itaweza kuwapa fursa vijana waweze kuonyesha vipaji walivyonavyo ili waweze kutambulika zaidi kutokana na kazi wanazozifanya.

Koka ameyasema hayo wakati wa semina elekezi  ambayo imewakutanisha wasanii mbalimbali wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa lengo la kuweza kukutana kwa pamoja ikiwa pamoja na kubadilishana mawazo na kupeana uwezo, ujuzi ,mahalifa na mbinu ambazo zitaweza kuwasaidia kufika mbali katika sanaa ambayo wanaifanya.


Koka alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuona namna ya kuendelea kuwakutanisha kwa pamoja wasanii mbali mbali wa Jimbo lake na kuwaweka katika Kliniki ya pamoja ambayo itaweza kuwapa fursa ya kuonyeha uwezo na vipaji walivyonavyo.

“Nafahammu katika Jimbo langu kuna vijana wengi ambao wana vipaji vya aina mbali mbali kwa hivyo nitashirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha katika kuanzisha Kliniki maalumu ambayo itaweza kuwapa fursa zaidi vijana kuweza kuonyesha uwezo ambao walionao na kikubwa zaidi lengo ni kuweza kuwafanya vijana wetu waweze kufika mbali zaidi,”alisema Koka.

Kadhalika Koka aliongeza kwamba mbali na kuanzisha Kliniki hiyo  maalumu ya kukuza vipaji hivyo vya wasanii amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa kuwasaidia baadhi ya vifaa mbali mbali ambayo vitaweza kuwasaidia kuwa na studio yao ya kisasa ambayo itakuwa ni mkombozi katika kufanya kazi zao mbali mbali za mziki.


Kwa wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amesema  kwamba lengo lake kubwa ni  kushirikiana bega kwa bega na wasanii wa Wilaya ya Kibaha kuwatengenezea  mfumo mzuri ambao utawasaidia katika kuwatangaza zaidi ikiwa pamoja na kwenda nao katika vituo mbali mbali kwa ajili ya kuweza kufanya mahojiano.

Naye Mwenyekiti wa wasanii  waigizaji Wilaya Jumanne Kambi amempongeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa maamuzi yake ya kuweza kuanzisha Kliniki hiyo ya wasanii ambayo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji vyao.


Tuesday, November 30, 2021

WAZIRI BASHUNGWA -TAMASHA LA KIHISTORIA LATUA MBEYA

 


Na. John Mapepele, WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Filamu nchini inatarajia kwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru wake kufanya tamasha kubwa la kihistoria la utoaji wa tuzo mbalimbali za filamu ambalo litafanyika Disemba 18, 2021 jijini Mbeya.

Akizungumza na kwenye Mkutano wa Waandishi wa   wa habari jijini Mbeya, Novemba 29, 2021 Mhe. Bashungwa amesema sababu kubwa ya kufanyia kilele cha tuzo hizi jijini Mbeya ni kutambua uwepo wa wanatasnia ya filamu pamoja na wasanii katika mikoa na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam ili kuamsha ari ya kufanya kazi za sanaa na hatimaye kujipatia ajira na kipato kitakacho boresha maisha yao.

  “Tamasha hili linakwenda kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko maeneo hayo katika uwanja huu wa filamu na Sanaa kwa ujumla kupitia idadi kubwa ya wapenzi wa filamu watakaokuwa wanafuatilia tukio hili ndani na ncje ya nchi yetu.”. Amefafanua

Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, imedhamilia kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya sanaa na Filamu ndyo maana imekuwa na miokakati mbalimbali ya kuboresha tasnia hiyo  ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo za filamu kwa wanatasnia ya filamu hapa nchini kwa lengo la kutambua mchango wa wahatasnia hao.

“Kwa mwaka huu wa fedha, Mhe. Rais ametenga kiasi cha Sh. Bilioni 1.5 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni ambao niliuzindua tarehe 22 Novemba 2021. Mfuko huo utatoa mikopo na kuwezesha programu mbalimbali za kuendeleza Sanaa nchini ikiwemo filamu” amefafanua Mhe. Bashungwa

Akifafanua zaidi Mhe. Bashungwa amesema  katika  kuboresha  kazi za sanaa na Filamu nchini Novemba 22,  2021, alizindua  Mfumo wa kidijitali utakaokuwa unatumiwa na Taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA, ambazo ziko chini ya Wizara yake.

Ametaja baadhi ya faida za mifumo hiyo kuwa ni pamoja na kurahisha utendaji wa Taasisi hizo katika kuwahudumia wasanii kwa kutia huduma kwa haraka,kuwarahisishia wasanii wote nchini na hata nje ya nchi kupata huduma kokote walipo bila kufika katika ofisi hizo, ambazo ni BASATA, BODI YA FILAMU na COSOTA na kutunza kumbukumbu za wasanii na kuleta wepesi wa kuwatambua kokote walipo ili kurahisisha utoaji huduma kwao kama vile mafunzo mbalimbali ya Sanaa ambayo Taasisi hizi zimekuwa zikiyatoa.

“Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha nguvu na mchango mkubwa wa Tasnia ya Filamu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi. Sekta ya burudani inayohusisha filamu imefanya vizuri katika nyanja za Kiuchumi, kwa mfano, mnamo mwaka 2018 Sekta hii iliongoza kwa ukuaji wa kasi ya zaidi ya 13%, ambapo ilishika nafasi ya tatu mwaka 2019 kwa ukuaji wa kasi ya 11%. “ amesisitiza Mhe. Bashungwa

Wednesday, September 20, 2017

KAMANDA MUSILIMU AIPONGEZA PUMA ENERGY KWA KUWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOCHORA PICHA BORA ZA ATHARI ZA USALAMA BARABARANI

 Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mwanafunzi Nasri Mwema  akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu 
  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu  na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu  katika mashindano hayo
 Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili  wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea


 Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa sh. mil. 2.

 Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo
Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao

Friday, June 30, 2017

WASHIRIKI WA SHINDANO LA BONGO STYLE WAENDESHEWA SEMINA KUHUSU PICHA,MITINDO NA UANDISHI WA FILAMU

Bi. Joyce Msigwa ambaye ni Mratibu wa Faru Arts and Sports Development Organization (FASDO) akitoa maelezo kwa washiriki wa  'Bongo Style Competition'  2017, kuhusiana na asasi ya FASDO
Mwezeshaji Bw. Erick Chrispin akitoa semina kwa washiriki wa Bongo Style namna ya kujiongoza wenyewe katika maswala ya Fedha,Muda na uongozi.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Bongo Style 2017, wakiwemo wapiga picha,waandishi wa miswada ya Filamu na wabunifu wa mitindo upande wa mavazi wakiwa wanafanya zoezi waliopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (ambaye hayupo pichani)
Baadhi ya Washiriki wa Bongo Style Competition 2017 wakiwa wanafanya kazi waliyopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (hayupo pichani) baada ya kumaliza semina yake.
 Mkufunzi na Mtaalam wa maswala ya Picha Bw. Iddy John akitoa somo juu ya maswala ya picha kwa washiriki wa Shindano la Bongo Style kundi la  Picha
Mbunifu maarufu wa Mitindo ya mavazi Martin Kadinda akitoa somo kwa washiriki  kundi la mitindo
Washiriki wa kundi la  Ubunifu wa mitindo upande wa  mavazi wakipewa vitendea kazi.
Bi. Christina Pande(aliyesimama) ambaye ni Mtunzi na muongozaji wa Filamu, akiwapa darasa vijana ambao wapo katika kundi la Uandishi wa  miswada ya Filamu shindano la Bongo Style 2017.
Picha zote na Fredy Njeje.

Monday, November 9, 2015

WASHIRIKI 20 WA SHINDANO LA BONGO STYLE WAENDELEA KUJIFUA


 Washiriki wa shindano la Bongo style kwa upande wa picha wakimsikiliza kwa makini mtaalam wao Sameer Kermalli(wa tatu kulia) akitoa maelekezo wakati wa mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki kwa upande wa picha wakiwa wanasikiliza kwa makini somo
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani , akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.
Baadhi ya  Washiriki kwa upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanachakalika kuandaa kazi zao mbalimbali

Mbunifu wa Mavazi Martini Kadinda akiwapa somo washiriki upande wa ubunifu wa mavazi.
  Washiriki  wa ubunifu wa mavazi wakiendelea na kazi
Hawa ni washiriki kwa upande wa kupiga picha wakikamilisha moja ya mazoezi waliyopewa(Picha kwa hisani ya Washiriki upande wa wapiga picha)
 Baadhi ya Washiriki upande wa kupiga picha wakiwa mtaani wakiwa katika mazoezi waliyopewa kuyafanya na mtaalam wao Sameer Kermalli
 Baadhi ya washiriki wengine kwa upande wa Kupiga picha  na ubunifu wa  mavazi wakisikiliza kwa makini somo ambalo linatolewa na mtaalam ambaye hayupo pichani.
 Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanasikiliza kwa makini maelekezo wanayopewa na Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda ambaye hayupo pichani
 Muda wa mapumziko 
 Muwezeshaji kutoka Wiki Loves Africa akitoa somo juu ya upigaji picha kwa washiriki ambao hawapo pichani.
 Tunukiwa Daudi (Aliyesimama) akitoa somo juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na Faida zake
Baadhi ya washiriki upande wa kupiga picha wakifurahia jambo

IKIWA ni siku ya tano tangu Washiriki 20 wa Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na asasi isiyo ya Kiserikali ya Faru Arts and Sport   Development Organization (FASDO), ikiwahusha Wapiga picha na wabunifu wa mavazi wenye umri kati 19-25 walioingia rasmi kambini tarehe  5.11.2015,ambapo tangu tarehe hiyo  washiriki hao  wameendelea kujifua zaidi huku wakipewa kazi mbalimbali za ubunifu na masomo mengine ikiwa ni sehemu ya shindano hilo. Wakiwa kambini washiriki hao wamepata nafasi ya kujifunza mambo mapya ambayo walikuwa hawayafahamu.

Fainali hizi zinatarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2015 ndani ya ukumbi wa 
Alliance Francaise Jijini  Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa upande wa picha wamekili kuwa walikuwa wanaona kama wanafahamu vema kupiga picha lakini baada ya kupata somo wamegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu na mengine walikuwa wanayafanya lakini bila kujua kuwa walikuwa sahihi, Pia waliongeza kuwa wanashukuru kuwapata wataalam ambao wameweza kuwaonesha ni jinsi gani wanatakiwa kuwa wapiga picha wazuri.

Nao washiriki wa ubunifu wa mavazi wameshukuru kupata wataalam ambao wamekuwa wakiwapa maelekezo mengi ambayo  yalikuwa ni chachu kwao kwasababu kila mmoja kwa upande wake wamejifunza mambo mapya mengi na kuona kuwa kumbe sio lazima kuwa na ubunifu wa aina moja ya mavazi lakini wanaweza wakawa na aina nyengine nyingi kulingana na mazingira waliyopo na kuishukuru Fasdo kwa kuwakutanisha.

Mwalimu na mtaalam wa kupiga picha Sameer Kermalli amekili kuwa tangu darasa lianze washiriki hao wamekuwa na uelewa wa haraka na yeye kupata nafasi ya  kuwaelekeza mbinu mbalimbali za kupiga picha na kanuni mbambali za upigaji picha, washiriki hao wamekuwa wasikivu na wameongeza ubunifu zaidi jambo ambalo limemtia moyo mtaalam huyo.

Kwa upande wa Mbunifu wa mavazi Martin kadinda alisema kuwa washiriki wapo vizuri na kila mbunifu anakitu chake cha kipekee ambacho yeye anafanya mfano wapo wale ambao wanabuni nguo zao kwa kutumia kitenge tu, wengine wanatumia vitu vya asili, nguo za kisasa, nguo ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuvaliwa na zenginezo, aliwashauri kuwa wasiegemee katika kitu kimoja tuu au aina moja ya mavazi lakini wawe na ubunifu na kubadilika kila wakati kwa sababu mitindo inakwenda ikibadirika.
  
 Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande  alipata nafasi ya kutembelea kambini na kujionea jinsi washiriki wanavyojituma katika kazi zao na maandalizi ya shindano hilo yanavyo kwenda " Ninachukua nafasi hii kwa niaba ya Fasdo kuwapongeza washiriki wote mliofanikiwa kuingia katika shindano hili la Bongo style ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo zaidi wa kile ambacho mlikuwa mnafanya na sasa kipate kuwa zaidi" aliongea Chande na kuongeza kuwa kuna ushindani mkubwa na shindano linafuata vigezo vyote vya ushindani na washindi watakuwa wamekidhi vigezo hivyo.

Sunday, November 8, 2015

PAPAA WEMBA AFANYA MAAJABU KWENYE TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVALS 2015

DSC_1032
Mwanamuziki nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha ya kuwa na uri wa miaka 66, kwa kupiga shoo ya aina yake usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015 linaloendelea ndani ya viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo-Tanzania.

Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliweza kupanda jukwaani akiwa na bendi yake na kupiga nyimbo zaidi ya tano zilizokonga nyoyo mashabiki lukuki waliofurika ndani ya viwanja hivyo vya Mwanakalenge mjini hapa.

Papaa Wemba ambaye anatamba kwa muda mrefu na wimbo wa “Show Me The Way” ameweza kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa dansi kutoka DRC Congo kufika Tanzania kwa mara ya pili sasa kwa vipindi tofauti huku watanzania wengi wakionyesha kumkubali na kufuatilia muziki wake mara kwa mara.

Baada ya shoo hiyo Papaa Wemba aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono katika muziki wake ambapo alieleza kuwa tamasha hilo la Karibu Music Festival licha ya kuwa change kwa kufanyika mwaka wa pili, huko linakoelekea litakuwa kubwa zaidi na kuwa maarufu.

Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliimba nyimbo zaidi ya nne huku akiimba pia vibao kadhaa vilivyowahi kutamba miaka ya nyuma pamoja na nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya.
Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. 

Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
DSC_1025
Papaa Wemba akiimba jukwaani kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
DSC_1099
Papaa Wemba akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
DSC_1027
Wanenguaji wa Papaa Wemba wakishambulia jukwaa kwa style ya aina yake ambao walikuwa kivutio katika tamasha hilo..
DSC_1083
Sebene likiendelea jukwaani..
DSC_1102
Host wa tamasha la Karibu Music Festival 2015, Mc Lulu akipata kuimbisha mashabiki waliofurika katika tamasha hilo kwa kuimba sambamba na Papaa Wemba (Hayupo pichani) kibao cha "Show Me the way"..
DSC_1087
Papaa Wemba katika ubora wake..
DSC_1130
DSC_1030
Dansa akifanya yake jukwaani..
DSC_1063
DSC_1080
Papaa Wemba..
DSC_1090
Mwenyekiti wa tamasha la Karibu Music Festival, Amarido Charles (kushoto) akiwa pamoja na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Bodenim 'Bo' katika viunga vya tamasha hilo viwanja vya Mwanakalenge..