Saturday, March 3, 2018
MABINGWA TIMU YA IRINGA UNITED KUUWAKISHA MKOA WA IRINGA KWENYE LIGI YA MABINGWA WA MIKOA
Saturday, March 03, 2018
No comments
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi kombe kampteni wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na
mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi
kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa
njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa
wamefungana goli moja moja
mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na
mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi mchezaji bora wa mashindano
Razack Kibuga ambaye ametoka katika timu ya Iringa United
Baadhi ya wadau na mpira wa mikuu mkoani Iringa wakiwa wapo sambamba na kiongozi wa Iringa United walipokuwa wakifuatilia kwa ukaribu mechi katika ya Iringa United na Mtwivila City kutoka kushoto anaitwa Frank Lyimo kutoka kituo cha TV cha IMTV ,Ally Msigwa ambanye ni mkurugezi mtendaji wa Iringa Football Academy na anayefuata ni Steve Lihawa mtangazaji wa kipindi cha michezo cha radio Ebony fm iliyopo mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
TIMU ya
Soka ya Iringa United imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Iringa
baada ya kuibuka na ushindi penati 3 - 1 dhidi ya Mtwivila Fc.
Katika
mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Samora timu ya Mtwivila Fc walikuwa wa
kwanza kupata bao dk 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari David Mwanga baada
uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kuponyokwa na mpira na
kumpita tobo.
Mchezo
huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha
ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila
walikuwa wakiongoza bao 1.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha
kufika fainali ya ligi ya Mkoa kwa Mtwivila wakitaka kuongeza huku Iringa
wakitaka kurudisha.
Mchezaji
bora wa mechi ya nusu fainali Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya
kusawazisha goli katika dk 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana.
Mara ya
dakika 90 kumalizika ndipo hatua za kupigiana matuta ilipowadia ambapo timu ya
Mtwivila fc ilikosa penati 3 na Iringa United kupata penati 3 dhidi ya 1.
Kutokana
na ushindi huo timu ya Iringa United imejinyakulia jezi seti moja, mipira
miwili huku timu ya Mtwivila wakiondoka na jezi na mpira mmoja.
Mchezaji
bora wa mashindano hayo aliibuka Razack Kibuga wa Iringa United aliyeondoka na
zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa
United aliyepata sh.50000
Katika
mchezo huo mgeni rasmi alikuwa mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa soka
Mkoani hapa Feisal Abri Asas ambaye alikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa
Iringa united, Ahmed Kivike.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi kombe hilo Feisal alisema kuwa anatarajia kudhamini ligi ya
Mkoa mwakani kwa kuwa mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa.
Wakati
huo huo ya soka ya Mkimbizi fc imefanikiwa kushika nafasi ya tatu ya ligi ya
mkoa baada ya kuwafunga timu ya soka ya Mshindo fc mabao 5 - 4.
Katika
mchezo huo mkali uliopigwa majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Samora
timu ya Mshindo 'wabishi wa mjini' itabidi wajilaumu kwa kuwa hadi kipindi cha
kwanza walikuwa wanaongoza goli 3 - 2 kwa magoli yaliyofungwa na Michael Chader
dk za 8,17 na 23.
Magoli
ya Mkimbizi fc yalifungwa na Said Kaliumi aliyefunga magoli matatu katika dk za
10 na 29 na 53.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kwa Mshindo Fc kufunga goli la nne kupitia Michael
Chader katika dk 50 lililodumu hadi dk ya 53 ambapo Mkimbizi Fc walijipatia
goli kupitia kwa Said Kaliumi.
Mkimbizi
Fc wakiwa nyuma kwa goli mbili walikuja kwa kasi na kuanza kufunga katika
dk za 64 na 70 na kufanya matokeo kuwa 5 - 4
Kwa
ushindi timu ya mkimbizi imefanikiwa kuwa Mshindi wa tatu katika ligi ya Mkoa
na kuondoka na zawadi ya jezi seti moja.
MAUAJI YA WANAJESHI WA TZ NCHINI CONGO DRC, UCHUNGUZI WABAINI HAYA.
Timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa,iliyokuwa inachunguza kiini cha kuuwa walinzi wa amani 15 wa Tanzania huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa mwaka jana,imesema tukio hilo linadhihirisha “mapungufu” ya jinsi gani askari wa Umoja huo wanavyopatiwa mafunzo.
Ikiwasilisha ripoti yao hapo jana, timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ilisema imegundua mapungufu pia kwenye mfumo wa utoaji amri, uongozi pamoja na ukosefu wa vikosi vya uwezeshaji kama vile vya anga, wahandisi na ujasusi.
Katika shambulio hilo la Desemba 7 kwenye mji wa Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini, wanajeshi 15 wa Tanzania waliuawa na wengine 43 kujeruhiwa katika tukio linalotajwa kuwa baya zaidi kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini DRC tangu mwaka 1999.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, waasi wa jeshi la ADF la nchini Uganda ndio waliohusika na shambulio hilo.
MAMA AZIMIA MAZISHINI BAADA YA WANAWE WANNE KUFARIKI KWA AJALI YA MOTO WILAYANI SENGEREMA
WATOTO wanne wa familia moja ya katika mtaa wa Geita kata ya Nyatukala wilayani Sengerema wamefariki dunia baada ya chumba walichokuwa wamelala kuwaka moto.
Akizungumzia ajali hiyo mkuu wa wilaya ya SENGEREMA mh EMMANUEL KIPOLE amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa tarehe 27/2/2018 majira ya saa tano na baada ya timu ya ulinzi na usalama kufika eneo la tukio imebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mshumaa.
SHAVU LA WIMBO WA KOMBE LA DUNIA KWA DIAMOND PLATNUMZ KUIPAISHA TENA TANZANIA
Wimbo huo umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.
Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka Machi16 mwaka huu.
JANA Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June mwaka huu
NAIBU WAZIRI MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL KILICHOKO MKOANI TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018.
NA K-VIS BLOG/Khalfan
Said, TANGA
NAIBU
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.
Antony Mavunde amekitoza faini ya shilinhgi milioni 35 (milioni thelathini na
tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange Mkoani
Kilimanjaro.
Mhe.
Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya
Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado
hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
Naibu Waziri Mavunde, alikuta wafanyakazi wa kiwanda hicho ambacho
kina mashine nyingi na kutokana na mfumo wa utendaji kazi wake, kinatoa
kelelenyingi hawakuvaa vifaa vya kujikinga na madhara kazini, (protective
gears).
Mhe. Mavunde aliwakuta baadhi yao wakiwa wamevaa kandambiloi,
wengine hawana vifaa vya kuziba masikio kujihami na kelele, pamoja na vifaa
vingine.
Hatua hiyo ilimkasirisha Mhe. Navu Waziri na kumuagiza Afisa wa
OSHA, kuchukua hatua mara moja ambapo kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi
milioni 35 kwa kukiuka Sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo pamoja na
mambo mengine inasisitioza usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi kuvaa vifaa
vya kujihami.
Aidha Mhe. Mavunde ambaye kabla ya kufika Mkoani Tanga,
alitembelea mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kilimanjaro, ameuagiza uongozi wa
kiwanda hivho kuondoa kasoro hizo mara moja.
Sambamba na hilo, Mhe. Mavunde amesema, serikali haitabadili
msimamo wake wa kuwafikisha mahakamani waajiri wote ambao bado hawajatekeelza
takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi, (WCF) kwani kwa kutofanya hivyo wanakabiliwa na adhabu mbalimbali
ikiwemo kupelekwa mahakamani ambapo mwajiri atakayepatikana na hatia
atalazimika kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi Milioni 50,000,
(Milioni Hamsini), au kifungo kisichopungua miaka mitano (5) au vyote kwa
pamoja.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao bado
hawajajisajili na WCF na ambao hawafuati sheria ya ajira na mahusiano kazini,
mkoani Tanga Ijumaa Machi 2, 2018, Mhe. Mavunde alisema.
“Si jambo zuri kwa waajiri kutekeleza matakwa hayo ya kisheria
hadi wanapoona kiongozi wa serikali amewafikia, hii siyo sawa, na kuonya kuwa
ni muhimu waajiri wakatambua kuwa zama zimebadilika, hakuna kichaka cha
kujificha, vichaka vyote vinawaka moto hivi sasa.” Alisema.
Mhe. Mavunde pia aliwatahadharisha waajiri ambao wamejisajili kwa
kupeleka taarifa za uongo kuhusu shughuli zao ikiwa ni pamoja na idadi ya
wafanyakazi wao na viwango vya malipo ya mishahara ya wafanyakazi hao, kwani
kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai.
Naibu Waziri ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Aira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alilotoa
mwishoni mwa mwaka jana, la kuwataka waajiri kutoka sekta rasmi (umma na
binafsi) Tanzania Bara, kutekeleza takwa la kisheria linalowataka kujisajili na
kutoa michango Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
“Kama nilivyowaeleza wenzenu kwenye mikoa niliyotembelea ya
Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro na leo hapa Tanga ninarudia tena, nia ya
serikali ni kuwaondolea mzigo wa gharama waajiri, ya kuwahudumia wafanyakazi
wao wanapopatwa na madhara wakati wakitekeelza majukumu yao ya kikazi, na
badala yake wajibu huo uchukuliwe na serikali kupitia Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi”.
Tunataka ninyi waajiri mjikite zaidi kwenye shughuli zenu za
msingi za kufanya biashara na uwekezaji, na jukumu la kuwahudumia wafanyakazi
wanapodhurika kazini tuachieni sisi serikali, alisisitiza Mhe. Antony Mavunde.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, Mkoa wa Tanga una jumla ya waajiri 769
na kati ya hao, ni waajiri 413 tu ndio wamejisajili, huku wengine 356, bado
hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye
Mfuko.
Naibu Waziri akitembelea kiwanda hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018.
Nabu Waziri Mavunde, akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, wakati walipotembelea kiwanda bhicho cha PPTL.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (katikati), akizungumza na Mkuu wa Kituo cha Afya, Tumaini Health Centre kilichoko Chumbageni Mkoani Tanga, Sister Flora Mushi, (kulia), ambapo alibaini bado mwajiri huyo hajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuagiza afikishwe mahakamani kwa kosa hilo la jinai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter.
Naibu Waziri na ujumbe wake, wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe.Martin Shigela, (katikati), mwanzoni mwa ziara yake aliyoifanya mkoani humo Machi 2, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa, (kushoto), akizungumza na Naibu Waziri Mabunde, (watatu kulia), Bw. Anselim Peter, (wapili kulia) na Kamishna wa Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde, akiwa na Bw. Anselim Peter, wakati wa ukaguzi huo.
Mhe. Mavunde akisalimiana na Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde akisalimiana na Bw. Anselim Peter (kulia).
Mhe. Mavunde akizungumza kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu, shule ya Sir John iliyoko Ras Kazoni Mkoani Tanga. Katikati ni Bw. Anselim Peter na Bi. Rehema Moyo.
RPC MWANZA, ASISITIZA ASKARI WAKE KUEPUKA UBAMBIKAJI KESI
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi amewasisitiza askari kuepuka ubambikaji kesi kwa wananchi, rushwa na ubabaishaji pia akiwataka askari kufanya kazi kwa utii, nidhamu na maadili kama ambavyo Jeshi la Polisi Tanzania linavyoelekeza. Hayo yamejiri tarehe 28/02/2018 wakati Kamanda Msangi alipokutana na askari wa Wilaya ya Sengerema katika ukaguzi anaoendelea kuufanya katika Wilaya na Vikosi vyote hapa Mkoani Mwanza.
Amewataka askari kukomesha vitendo vya ubabaishaji kwa wananchi na ubambikaji kesi kama vipo, mfano kesi ya madai inabadilishwa kuwa kesi ya jinai jambo ambalo linanyima haki wananchi na kuchafua sifa nzuri ya Jeshi la Polisi. Hivyo ubabaishaji wa aina hiyo uepukwe na yeyote atakaye bainika anafanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo Kamanda Msangi amewataka askari wa kila kitengo kusimama vyema katika nafasi zao, ambapo alisema kila askari akiwa vizuri katika utendaji kazi hakutakuwa na malalamiko yeyote toka kwa wananchi hivyo ni jukumu la kila askari kuhakikisha dhamana aliyopewa na serikali ya kulinda wananchi pamoja na mali zao anaisimamia vizuri bila ubabaishaji wa aina yeyote ile.
Pia aliwataka askari wawe na utaratibu mzuri wa upokeaji, utunzaji na uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi, kwani katika baadhi ya vituo vya Polisi lipo tatizo la utunzaji wa vielelezo hivyo hataki kuona tatizo hilo linaendelea kuwepo. Vilelele aliwataka Maofisa wa Polisi wa Wilayani hapo kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria za uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi.
Hata hivyo alisema hategemei kuona mlundikano wa vielelezo katika vituo vya Polisi ambavyo vimekaa vituoni mwaka mmoja au zaidi. Kwani madhara yake vinaweza kuharibika, kupoteza ubora au kupotea alafu baadae liwe deni kwa Jeshi. Hivyo aliwataka askari kutekeleza maamuzi ya mahakama haraka juu ya uondoshaji wa kielelezo/vielelezo baada ya kesi kumalizika mahakamani.
Kwa upande wa upelelezi alisema kumekuwa na tatizo la kuchelewesha upelelezi wa kesi nyingi. Jambo ambalo linawanyima wananchi haki. Hivyo alimtaka Mkuu wa Upelelezi Wilayani hapo kushughulikia suala hilo mapema lisiwepo katika himaya yake ili haki ipatikane haraka bila uonevu wa aina yeyote.
Pia aliwapongeza askari wa Wilaya hiyo kwa utendaji mzuri wa kudhibiti uhalifu, aliwataka waongeze juhudi kwa yale maeneo yenye vibaka na uhalifu mwingine mdogomdogo kwani anaamini wanaweza. Ushirikiano ulipo na Viongozi wa ulinzi na usalama Wilaya, Wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama udumishwe ili Sengerema iwe salama zaidi kwani amani ikiwepo maendeleo yatapatikana zaidi.
Amewataka askari kukomesha vitendo vya ubabaishaji kwa wananchi na ubambikaji kesi kama vipo, mfano kesi ya madai inabadilishwa kuwa kesi ya jinai jambo ambalo linanyima haki wananchi na kuchafua sifa nzuri ya Jeshi la Polisi. Hivyo ubabaishaji wa aina hiyo uepukwe na yeyote atakaye bainika anafanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Pia aliwataka askari wawe na utaratibu mzuri wa upokeaji, utunzaji na uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi, kwani katika baadhi ya vituo vya Polisi lipo tatizo la utunzaji wa vielelezo hivyo hataki kuona tatizo hilo linaendelea kuwepo. Vilelele aliwataka Maofisa wa Polisi wa Wilayani hapo kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria za uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi.
Hata hivyo alisema hategemei kuona mlundikano wa vielelezo katika vituo vya Polisi ambavyo vimekaa vituoni mwaka mmoja au zaidi. Kwani madhara yake vinaweza kuharibika, kupoteza ubora au kupotea alafu baadae liwe deni kwa Jeshi. Hivyo aliwataka askari kutekeleza maamuzi ya mahakama haraka juu ya uondoshaji wa kielelezo/vielelezo baada ya kesi kumalizika mahakamani.
Kwa upande wa upelelezi alisema kumekuwa na tatizo la kuchelewesha upelelezi wa kesi nyingi. Jambo ambalo linawanyima wananchi haki. Hivyo alimtaka Mkuu wa Upelelezi Wilayani hapo kushughulikia suala hilo mapema lisiwepo katika himaya yake ili haki ipatikane haraka bila uonevu wa aina yeyote.
Pia aliwapongeza askari wa Wilaya hiyo kwa utendaji mzuri wa kudhibiti uhalifu, aliwataka waongeze juhudi kwa yale maeneo yenye vibaka na uhalifu mwingine mdogomdogo kwani anaamini wanaweza. Ushirikiano ulipo na Viongozi wa ulinzi na usalama Wilaya, Wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama udumishwe ili Sengerema iwe salama zaidi kwani amani ikiwepo maendeleo yatapatikana zaidi.
Friday, March 2, 2018
JINSI ARSENAL WALIVYOKUTANA NA KIPIGO CHA MBWA MWIZI TOKA KWA CITY.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema klabu hiyo ilishindwa na klabu iliyo bora zaidi kwa sasa Uingereza baada yao kulazwa 3-0 kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja na Manchester City Alhamisi.
Gunners walikuwa wamelazwa 3-0 na City katika fainali ya Kombe la Carabao Jumapili.
Mechi ya Ligi ya Premia kati ya timu hizo mbili iliyochezwa Alhamisi iliamuliwa katika dakika 33 za kwanza kutokana na mabao ya Bernardo Silva, David Silva na Leroy Sane.
Gunners walipoteza nafasi ya kukomboa bao moja kipindi cha pili pale mchezaji waliyemnunua £56m, Pierre-Emerick Aubameyang, aliposhindwa kufunga mkwaju wa penalti kipindi cha pili.
WANAFUNZI 400 WA LYAMUNGO SEC WATIMULIWA BAADA YA KUMFANYIZIA MWALIMU WAO WA NIDHAMU
WANAFUNZI zaidi ya 400 wa kidato cha 5 katika shule ya sekondari ya Lyamungo iliyoko wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa masomo kwa muda wa siku 17 mara baada ya kufanya vurugu ya kuvamia nyumba ya mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo Mwalimu Safarani Rasini na kuharibu nyumba ya mwalimu huyo zikiwemo mali za shule.
Nini chanzo?....Ungana na mandishi wetu Fatma Seif kutoka eneo la tukio.
WATUHUMIWA MAUAJI YA KIONGOZI WA CHADEMA WADAKWA.
Watu 13 wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa makosa mawili tofauti wakiwemo 11 kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kifo cha Diwani wa CHADEMA huku wengine wawili raia wa Kenya wakishikiliwa kwa tuhuma za utapeli wakijifanya wao ni (TRA).
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema baada ya tukio la kuuwawa kwa Diwani wa Kata ya Namwawala wilaya ya Kilombero Godfrey Luena, Jeshi la Polisi mkoani humo liliendesha msako wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo ambapo mpaka sasa jumla ya watu 11 wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Katika hatua nyingine, watu nwawili ambao ni raia wa Kenya wanashikiriwa na polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli kwa kujifanya ni mawakala wa mamalaka ya mapato nchini.
Thursday, March 1, 2018
LUKAKU SASA CHINI YA JAY-Z
Straika wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku amejiunga na Roc Nation Sports iliyopo chini ya kampuni ya Roc Nation inayomilikiwa na msanii wa muziki nchini Marekani, Jay-Z.
Nyota huyo wa Man United, Lukaku ameposti picha katika mitandao yake ya kijamii zinazomuonyesha akikaribishwa katika familia hiyo ya michezo huko New York.
Jay-Z alianzisha kampuni ya Roc Nation kwaajili ya burudani kabla ya kutanua wigo zaidi hadi kufikia Roc Nation Sports na Lukaku kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga kutoka ligi kuu ya Uingereza.
Roc Nation Sports ni sehemu ya kampuni ya Roc Nation ambayo imeanzishwa na Jay – Z mwaka 2013 kwa kushirikiana na Shirika la kukuza vipaji vya michezo (Creative Artists Agency) huku ikiwa na lengo la kuenua na kukuza vipaji huko Los Angeles na California.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anakuwa wa pili kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu baada ya beki wa Bayern Munich, Jerome Boateng kujiunga na familia hiyo yenye maskani yake nchini Marekani.
KUHUSU 'ROC NATION SPORTS'
Roc Nation Sports is the sports management division
of Roc Nation, an entertainment company founded by Jay-Z.
The Sports branch was launched in 2013 and proclaims its
mission is to aid the careers of athletes on and off the field.
Commercial deals, media relations and 'brand strategy' are
all listed as areas Roc Nation Sports helps develop with their
clients.
Notable clients include:
Kevin Durant,
Dez Bryant,
Jerome Boateng,
Miguel Cotto,
Romelu Lukaku
Subscribe to:
Posts (Atom)