ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 3, 2018

SHAVU LA WIMBO WA KOMBE LA DUNIA KWA DIAMOND PLATNUMZ KUIPAISHA TENA TANZANIA


Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz anatarajiwa kushiriki katika wimbo maalumu wa Kombe la Dunia nchini Russia. Wimbo huo utakuwa unawakilisha bara la Afrika.

Wimbo huo  umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.

Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka Machi16 mwaka huu.

JANA Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June mwaka huu

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.