Saturday, October 22, 2011
SIASA
Friday, October 21, 2011
HABARI
Mazishi ya Kanali Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maafisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo.
Chini ya utamaduni wa Kiislam, maziko hutakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo. Lakini waziri wa mafuta wa Libya amesema mwili wa Gaddafi huenda ukahifadhiwa "kwa siku kadhaa".
Haifahamiki kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa Sirte, mji aliouawa siku ya Alhamis, au Misrata, mji aliopelekwa baada ya kufa, au mahala pengine.
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Muammar Gaddafi kinamaanisha shughuli za Nato nchini Libya zimefikia kikomo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa mamlaka nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi huyo. Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufanyika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.
Waziri wa mafuta Ali Tarhouni aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa "kwa siku kadhaa".
Friday, October 21, 2011
HABARI
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akifafanua jambo wakati wa mahojiano katika redio Clouds Fm iliyopo jijini Dar es Salaam. Pembeni yake yupo mtangazaji wa Clouds Fm Wasiwasi Mwabulambo.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati alipotembelea Clouds Media Group.
Tanzania ni nchi ya kuigwa- Waziri Membe
Watanzania wametakiwa kuuenzi Umoja, Upendo na Mshikamano ulipo Tanzania maana ndiyo sifa inayoiweka nchi katika historia.
Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati akifanya mahojiano katika redio Clouds iliyopo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa nchi za jirani wanatamani sana amani iliyopo mchini Tanzania, maana nchi nyingine huwa mpaka wapigane ndiyo amani ipatikane.
"Tanzania tunaonewa wivu kuhusu huu utaratibu wa kupeana vijiti vya uongozi, kijiti cha Mzee Nyerere akamkabidhi Mwinyi kwa amani na kura...kijiti cha Mzee Mwinyi akamkabidhi Mkapa na vile vile kijiti cha Mkapa akamkabidhi Kikwete hivi ndivyo inavyopaswa kufanyika siku zote," aliongezea Waziri Membe.
"Tunaposherehea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ni vyema tukatambua kuwa Tanzania ni nchi ya pekee na ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.
PICHA ZAIDI BONYEZA www.kajunason.blogspot.com
oYAaaaa! kArIbU kWEnYe pAtI lA kIkUbWa jUMaMosI hII!!!
Friday, October 21, 2011
BANGO
Mkurugenzi Wa Twanga Pepeta Katikati Asha Baraka Akiongea na waandishi wa Habari Kuhusu Uzinduzi na Ziara UK. Baada ya kufanya na Kumaliza uzinduzi wa albamu yao kabambe tarehe 6 Novemba 2011 ASET wakishirikiana na URBAN PULSE CREATIVE Wanatarajia kuwaburudisha wapenzi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta Nchini Uingereza mwishoni mwa Mwezi wa Novemba.
Show Hii Maalum ni kwa ajili ya kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Tarehe pamoja na maelezo ya Ukumbi yatafuatia mda sio mrefu. Hivyo wadau kaeni mkao wa Kula.
Friday, October 21, 2011
HABARI
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ilemela na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Amanzi ameyaomba mashirika, watu binafsi na wasamaria wema kujitokeza kutoa msaada wa vyakula kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha upepo katika Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela. Said Amanzi.
Amanzi ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akitoa tathimini ya uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo kwa waandishi wa habari na kuleta athari kubwa miongoni mwa wakazi wa Kata hiyo.
Miongoni mwa sehemu zilizoharibiwa vibaya na mvua hiyo ni pamoja na vyumba vinne vya madarasa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igombe, Jengo la Ofisi ya CCM na lile la Kanisa la Roman Katholiki.
Katika tukio hilo lililotokea usiku wa Oktoba 18 mwaka huu lililosababishwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali jumla ya kaya 322 zimeathirika kutokana na athari hiyo ya mvua na kimbunga na Inakadiriwa pia kaya zipatazo 45 hazina chakula kabisa, zinahitaji msaada wa haraka ikiwa ni pamoja na mahema na chakula hii ni kutokana na vyakula vyao kuharibiwa na mvua.
Jumla ya watu 14 wamjeruhiwa na wote wamekwishatibiwa katika Hosipitali ya Rufaa ya Bugando na wamekwisharuhusiwa.
Tayari hatua mbalimbali zimekwishachukuliwa kuwanusuru wakazi hao ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya tathimini ya kina ya athari hizo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
Thursday, October 20, 2011
HABARI
Kiongozi wa Zamani wa Libya, Muammar Gaddafi amekufa katika mateso ya majeraha baada ya kukamatwa karibu na Mji wake wa Sirte Juu imethibishwa na Afisa Mwandamizi wa Kijeshi wa Baraza la Taifa Mpito NTC leo.Taarifa kupitia vyombo vya habari.
Afisa huyo wa Baraza la Taifa Mpito, Abdel Majid Mlegta aliiambia Reuters awali kwamba Gaddafi alikamatwa na kujeruhiwa katika miguu yote kabla ya alfajiri leo wakati akijaribu kukimbia baada ya msafara wake kushambuliwa na ndege za kivita za NATO. 'Pia alipigwa risasi kichwani ,`alisema kiongozi huyo.
Majeshi ya upinzani nchini humo yakishangilia kifo cha Gaddafi.
Thursday, October 20, 2011
HABARI
Wednesday, October 19, 2011
MICHEZO
Wednesday, October 19, 2011
HABARI
Wakili Tundu Lisu akitoa maelezo ya mwenendo wa kesi hiyo huku mteja wake Mbunge Highness Samson (wapili kuia) akimsikiliza kwa makini.Kesi namba 12/2010 yakupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la ilemela mkoani Mwanza iliyompatia ushindi mbunge kupitia tiketi ya CHADEMA bw. Highness Samson imeahirishwa tena leo jioni katika mahakama ya rufaa jijini humo.Wakili T. Lisu (kulia) akiwa ameambatana na mteja wake mbunge H. Samson wakitoka kwenye ukumbi wa mahakama.Kati ya mashitaka tisa yaliyofunguliwa dhidi ya mbunge wa sasa wa Ilemela mashitaka nane yametupiliwa mbali na kubaki shitaka moja tu ambalo ni dai la watu wapatao laki moja na elfu kumi na nne kudaiwa kuzuiwa kupiga kura.Shitaka hilo lililosalia linaonekana kukosa nguvu kwani linafananishwa na kesi ya uchaguzi ya mwaka 1995 ya bw. Silvester Masinde na Pius Msekwa, ambapo Mahakama ya Rufaa Tanzania iliamuru kuwa kura ambazo hazikupigwa au hazikuhesabiwa kugawanywa kwa uwiano wa asilimia walizopata wagombea kwenye uchaguzi.Mashitaka nane yaliyofutwa ni pamoja na kufanyika kampeni kwenye vituo vya kupigia kura na makanisani siku ya kupiga kura, wafuasi wa chadema kuzuia watu wasipige kura, mgombea wa chadema na mawakala wake kutoa rushwa kwa kujenga visima kwa wapiga kura na kutoa vinywaji na vyakula kwenye misiba, mahela yalitolewa kwenye eneo la Manguruwe, mshtakiwa mbunge pamoja na mawakala wake walinunua shahada za wapiga kura, kulikuwa na mabadiliko ya vituo vya wapigia kura vituo vya soko la Kirumba na kwenye viwanja vya Furahisha, jingine ni kuwa kuna mawakala wa Sangabuye na Buhongwa hawakula kiapo cha kutunza siri.Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Fish' akiteta jambo na mh. mbunge na wakili wake mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ambapo inategemewa kusomwa tena Ijumaa hii 21oct2011.Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.