Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati alipotembelea Clouds Media Group.
Tanzania ni nchi ya kuigwa- Waziri Membe
Watanzania wametakiwa kuuenzi Umoja, Upendo na Mshikamano ulipo Tanzania maana ndiyo sifa inayoiweka nchi katika historia.
Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati akifanya mahojiano katika redio Clouds iliyopo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa nchi za jirani wanatamani sana amani iliyopo mchini Tanzania, maana nchi nyingine huwa mpaka wapigane ndiyo amani ipatikane.
"Tanzania tunaonewa wivu kuhusu huu utaratibu wa kupeana vijiti vya uongozi, kijiti cha Mzee Nyerere akamkabidhi Mwinyi kwa amani na kura...kijiti cha Mzee Mwinyi akamkabidhi Mkapa na vile vile kijiti cha Mkapa akamkabidhi Kikwete hivi ndivyo inavyopaswa kufanyika siku zote," aliongezea Waziri Membe.
"Tunaposherehea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania ni vyema tukatambua kuwa Tanzania ni nchi ya pekee na ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.
PICHA ZAIDI BONYEZA www.kajunason.blogspot.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.