ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 13, 2013

ILI KUJENGEWA UWEZO WADAU WA MRADI WA UWAJIBIKAJI WA JAMII FORUM SYD WAKUTANA JIJINI MWANZA HII LEO.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza Bi. Mary Tesha akizindua mpango wa Mpya wa Mradi wa Uwajibikaji wa Jamii wa Forum SYD mbele ya wadau mbalimbali wanaofanyakazi na mradi. Wengine katika picha kushoto ni Meneja Mradi wa Forum SYD nchini Tanzania Wawa, na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa wilaya ya misungwi Bi. Naomi Nko pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karagwe. 
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza Bi. Mary Tesha akimkabidhi kabrasha la mpango wa mpya wa Mradi wa Uwajibikaji wa Jamii wa Forum SYD, Meneja Mradi wa Forum SYD nchini Tanzania Wawa, mbele ya wadau wa mpango huo waliohudhulia semina ya kujengewa uwezo iliyofanyika katika Hoteli ya Victoria Prince jijini Mwanza. 
Wadau wa masualaya uwahia jambo toka kwa wawasilishaji mada. 
Washiriki wa semina hii ya ForumSYD ni kutoka maeneo ya mradi ambayo ni pamoja na wilaya ya Magu, Ukerewe na Karagwe.  
Akizindua mpango huo mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza Bi. Mary Tesha amewaagiza watendaji waliopo katika maeneo ambayo mradi huo unatekelezwa kushirikiana na wananchi ili walengwa waweze kunufaika na fedha zilizotengwa kwaajili yao katika kipindi cha 2013 hadi 2018.
"Uzuri wa Mfumo huu unapima uwezo wa jamii kutambua haki zao ili kutekeleza wajibu wao kwani kabla kufanyika kazi elimu hutolewa kisha unafuata utekelezaji" Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza Bi. Mary Tesha akizungumzia mfumo ndani ya mpango mpya uliozinduliwa hii leo na Forum SYD jijini Mwanza.
Wadau wakisikiliza kwa makini kinachojiri kwenye semina hii.
Mkurugenzi wa wilaya ya misungwi Bi. Naomi Nko akizungumza na washiriki wa semina hii ya ForumSYD ambao wanatoka maeneo ya mradi ambayo ni pamoja na wilaya ya Magu, Ukerewe na Karagwe.
Wakifuatilia hatua kwa hatua ni sehemu ya washiriki wa semina hii ya ForumSYD kanda ya ziwa.
Wadau nao walipata fursa kuchangia kwa kubainisha changamoto au pengine ushauri juu ya nini kifanyike ili kuboresha.
Sauti ya mdau ikipaza kwa washiriki sanjari na meza kuu.
Kwa mijibu wa Meneja wa Mradi wa Forum SYD nchini Tanzania Godfrey Wawa unaofadhiliwa na serikali ya Sweeden mpango huo uliozinduliwa jijini Mwanza umelenga zaidi makundi yaliyosahaulika na jamii kama vila walemavu na waathirika wa virusi vya Ukimwi.
Shirika hilo limefikia uamuzi wa kuzindua mpango huo baada ya kuthibitika kuwa kumekuwepo na baadhi ya matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu zinazo wanyima haki wananchi kushirikishwa katika maamuzi mbalimbali yanayo husu maisha yao, mazingira ambayo yanasababisha miongoni mwao kutopata kabisa haki za msingi.
Shirika la Forum SYD Tawi la Tanzania linalotekeleza wajibu wake chini ya mwamvuli wa serikali ya Sweden lilijitambulisha Afrika Mashariki miaka 30 iliyopita na kuanza utekelezaji wa miradi yake mnamo mwaka 1982.

TAMASHA KUBWA LA UJASILIAMALI LINALO DHAMINIWA NA TIGO LAANZA LEO JIJINI MWANZA

Mtoa mada wa Tamasha la Ujasiliamali James Mwang'amba akiwasilisha mada katika siku ya kwanza ya Tamasha hilo leo, ambapo litafanyika tena kesho (jumamosi) kisha kumalizika siku ya Jumapili chini ya udhamini wa TIGO, Benki ya NMB na Street University.   
Mtoa mada wa Tamasha la Ujasiliamali James Mwang'amba akiwasilisha mada katika siku ya kwanza ya Tamasha hilo leo, ambapo litafanyika tena kesho (jumamosi) kisha kumalizika siku ya Jumapili.  
Tamasha hili lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha. Watoa mada wengine ambao wataonekana tena kesho na keshokutwa viwanjani hapa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.


Akizungumza na Umma wa wana Mwanza, Mc wa Tamasha la Ujasiliamali linalofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kutarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili ya tarehe 15 Dec 2013 chini ya udhamini wa TIGO, Benki ya NMB na Street University.   


Kwa upande wa burudani leo tume koshwa kiroho zaidi na kwaya mbalimbali za jijini Mwanza pamoja na msanii wa muziki wa Injili Edson Mwasabwite (PICHANI) 
Siku ya Jumapili burudani itang'arishwa zaidi na wasanii Fid Q, H. Baba, Young Killer, Jitta Man na Mr. Two aka Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson Mwasabwite.
Edson Mwasabwite.
Mzikilize  James Mwang'amba ambaye ni mtoa mada wa Tamasha la Ujasiliamali akizungumza na waandishi wa habari. BOFYA PLAY.

KULALA KIDOGO MCHANA

 Je, umewahi kulemewa na usingizi baada ya chakula cha mchana? Hiyo haimaanishi kwamba hukulala vyakutosha. Ni kawaida kusinzia wakati wa mchana kwa sababu joto la mwili hupungua wakati huo. Kwa kuongezea, hivi majuzi wanasayansi wamegundua kwamba kuna protini inayoitwa hypocretin, au orexin, inayotengenezwa na ubongo ambayo hutusaidia kuwa macho. Kuna uhusiano gani kati ya hypocretin na chakula?

 Tunapokula, mwili hutengeneza homoni inayoitwa leptin ambayo hutufanya tuhisi tumeshiba. Lakini homoni hiyo huzuia utengenezaji wa hypocretin. Yaani, kadiri leptininavyokuwa nyingi kwenye ubongo, ndivyo hypocretin inavyopungua na tunahisi usingizi zaidi. Labda hiyo ndiyo sababu katika nchi fulani watu hulala kidogo baada ya kula chakula cha mchana.

VIONGOZI WA VYUO VIKUU NCHINI WAKUTANA JIJINI MWANZA NA KUJADILI MASUALA YA AJIRA.

Mhadhiri Mwanzamizi wa Uchumi ambaye pia ni Mtafiti na Mshauri mwelekezi toka Chuo Kikuu Mzumbe Dr. Honest Prosper Ngowi akitoa mada katika semina ya viongozi wa vyuo vikuu nchini waliokutana katika ukumbi wa jengo jipya la huduma ya maradhi ya Saratani  jijini Mwanza kujadili masuala ya fursa na upatikanaji ajira.
Ni sehemu ya wahudhuriaji wa semina ya viongozi kutoka vyuo vikuu vya mikoa mbalimbali hapa nchini waliokutana katika ukumbi wa jengo jipya la huduma ya maradhi ya Saratani  jijini Mwanza kujadili masuala ya fursa na upatikanaji ajira.
Ni sehemu ya wahudhuriaji wa semina ya viongozi kutoka vyuo vikuu vya mikoa mbalimbali hapa nchini waliokutana katika ukumbi wa jengo jipya la huduma ya maradhi ya Saratani  jijini Mwanza kujadili masuala ya fursa na upatikanaji ajira.
Kwa umakiiiini... yale yanayojiri.
Mhadhiri Mwanzamizi wa Uchumi ambaye pia ni Mtafiti na Mshauri mwelekezi toka Chuo Kikuu Mzumbe Dr. Honest Prosper Ngowi akitoa mada katika semina ya viongozi wa vyuo vikuu nchini waliokutana katika ukumbi wa jengo jipya la huduma ya maradhi ya Saratani  jijini Mwanza kujadili masuala ya fursa na upatikanaji ajira.
Kwa upande wake Rais wa TAHILISO Amon Chakushemeire, anasema kuwa changamoto kuu katika ajira kwa wahitimu nchini ni Takwimu, "Kama nchi hatujawa na 'DATA BASE' sehemu ambapo unaweza ukaenda ukaona kwamba mfano wahitimu wa shahada ya Sheria labda 6000, lakini soko la sheria la Tanzania linahitaji wanasheria 4000 ili hata wanafunzi wanaotoka kidato cha sita wanapokuja kuamua kusoma sheria wawe na taarifa kuwa wanakwenda kusomea kitu hali yake katika soko kiko hivi au vile"

Kisha akaongeza "Tulitegemea ukienda Wizarani taarifa hizo utazikuta kwamba wangapi wamechukuwa ajira nchini Tanzania lakini bado tunatatizo kubwa la Takwimu"
"Taasisi zinazo waandaa watu wanaopaswa kuingia kwenye soko la ajira na Taasisi zitakazo ajiri hawana mawasiliano mazuri, kila mmoja anatembe njia yake"

"Kwa hiyo Taasisi zinazo waandaa watu watakao ajiriwa haziwasiliani na yule atakaye waajiri ili aweze kuwaambia yeye angependa kupata mtu ambaye ana stadi zipi ili wanapokuwa wakiandaa mitaala waweze kuandaa mtu ambaye wanauhakika atakwenda kuuzika"
Katibu mtendaji wa TAHILISO Donati Sulla akizungumza na wanasemina kutoa miongozo.
Semina hii ni zaidi ya darasa.
Kwa nchi za Afrika tatizo la ajira hususani Tanzania hili lilipaswa kuwa liwe dogo nalisiwe kubwa kuliko nchi za Ulaya kwa sababu tuna rasilimali nyingi tuna mashamba (ardhi yenye rutuba), mito, migodi vyanzo vya nishati kama gesi na kadhalika kuliko hata nchi za Ulaya lakini limekuwepo kutokana na sababu za kihistoria kama ilivyokuwa miaka ya 1970 hadi miaka ya 80 ambapo mtu alikuwa akihitimu anasubiri kupangiwa sehemu ya kwenda kufanya kazi hivyo kukawa hakuna ubunifu wa kuvumbua vitega uchumi vingine vitakavyo toa ajira kwa umma wa sasa unaoongezeka siku baada ya siku.
Picha ya pamoja Mgeni rasmi Ally Msaki ambaye ni Mkurugenzi wa Ajira Wizara ya Kazi na Ajira (wa 5 kutoka kulia) ambaye alikuja kumwakilisha Waziri wa Kazi na Ajira, akiwa na Uongozi wa juu TAHILISO na wawezeshaji mada za ukosefu wa ajira.
Picha ya Pamoja.
The second.
Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Cha KUHASS Bugando Mussa Mdede, ambaye pia ni rais mwenyeji wa mkutano huo akizungumza na vyombo vya habari. 
Mhitimu kutoka Chuo Cha Mtakatifu Agustino kitivo cha Elimu ambaye pia  ni Kamishna wa TAHILISO Kanda ya Ziwa Bi. Consolata Michael akizungumza na wanahabari. 

MTAFSIRI WA LUGHA YA ALAMA MSIBA WA MANDELA KUMBE ALIKUWA MZUGAJI...!

Thamsanqa Dyanty (kulia) akitoa utafsiri ya hotuba ya rais wa Marekani Barack Obama kwa walemavu wa usikivu wakati wa ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Nelson Mandela siku ya jumanne.
Tizama utofauti wa utafsiri wa Thamsanqa Dyanty na utafsiri wa binti anayeonekana katika picha ndogo.
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbu kumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa akidanganya kwa miaka mingi na imekuwa itoa watafsiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa. Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kulikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.

Thursday, December 12, 2013

TAMAA ZA MALI NA UMASIKINI ZASABABISHA WAZAZI KUOZESHA MABINTI ZAO MAPEMA KATIKA KIJIJI CHA DODOMA MKOANI SIMIYU.

Mratibu wa safari ya uelimishaji toka Shirika la KIVULINI iliyopewa jina la 'Caravan Route' Bi. Hadija Liganga akitoa uelimishaji kwa wanakijiji wa Dodoma wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambapo katika kijiji hiki baadhi ya wazazi walikiri kuwalazimisha kuwaozesha mabinti zao katika umri mdogo ili wajipatie mali.
Kundi la sanaa la Babatan toka jijini Mwanza lilikuwa chachu katika kutoa elimu kupitia sanaa ya maigizo ambapo lililenga changamoto kubwa zilizopo katika eneo husika na kuigiza yanayojiri kisha kuchanganua nini kifanyike kuleta mabadiliko. 
Macho mbele huku wengine wakirekodi yanayojiri... watoto sanjali na wazazi wao katika kijiji hiki cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamevutiwa sana na elimu inayotolewa na Caravan Route kuhusu masuala ya elimu ya kijinsia.  
Igizo lililo sisimua toka kwao BABATAN.
Mabinti wanaoolewa katika umri mdogo wamejikuta katika manyanyaso kutoka kwa waume zao kutokana na  ukosefu wa elimu ya kujitambua na uelewa mdogo wa haki zao hivyo wamekuwa wakikubali kutii hata yale yaliyo wazi yenye unyanyasaji wakidhani kuwa wao ni watu wa chini na ni haki yao kufanyiwa matendo hayo mabaya. alifunguka mwanamama Veronica Stephen. 
Baadhi ya wazazi wa kijiji cha Dodoma wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kusaka mali na chakula kwaajili ya kuzilisha familia zao, kwa maana hiyo basi wengi hukimbilia kuwaoza mabinti zao mara tu wanapomaliza darasa la saba kama njia mbadala ya kujipatia mali kama ng'ombe na nafaka za chakula ambazo hutolewa kama sehemu ya mahali. Afunguka Bi. Maria.
Mzee Matius Doto asema mfumo dume ndiyo chanzo cha unyanyasaji kwa jiamii nyingi kijiji cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Amekiri kuozesha binti yake akiwa na umri wa miaka 16 kutokana na hali ya uchumi wa familia yake, kitendo ambacho kwa sasa anakijutia. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)
Joseph Sayayi naye alikiri kumwachisha mwanae shule na kumwozesha kutokana na kutojua umuhimu wa elimu kwani naye hakusoma. 
Wazee wa kijiji cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoa mpya wa Simiyu wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikiendelea toka kwa timu ya wadau wa Caravan Route waliojikita katika mpango wa kutoa elimu kwa vijiji, kata na wilaya zilizo athiriwa na ukatili pamoja na unyanyasaji wa kijinsia Kanda ya ziwa.
Hakika wananchi wa kijiji hiki walivutiwa sana na masomo na ushauri uliokuwa ukitolewa na timu Caravan Route.
Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo safari kuelekea kijiji kingine iliwadia, ambapo njiani changanoto za barabara kujaa maji na njia kutopitika ziliikabili timu ya waelimishaji Caravan Route, na hapa ilibidi chombo chetu cha usafiri kipige STOP kuyapisha maji.
Barabara ilikuwa haionekani...Hata hivyo daadaye safari iliendelea...kukifikia kijiji kingine kujionea changamoto...ITAENDELEA.