Kwa upande wake Rais wa TAHILISO Amon Chakushemeire, anasema kuwa changamoto kuu katika ajira kwa wahitimu nchini ni Takwimu, "Kama nchi hatujawa na 'DATA BASE' sehemu ambapo unaweza ukaenda ukaona kwamba mfano wahitimu wa shahada ya Sheria labda 6000, lakini soko la sheria la Tanzania linahitaji wanasheria 4000 ili hata wanafunzi wanaotoka kidato cha sita wanapokuja kuamua kusoma sheria wawe na taarifa kuwa wanakwenda kusomea kitu hali yake katika soko kiko hivi au vile"
Kisha akaongeza "Tulitegemea ukienda Wizarani taarifa hizo utazikuta kwamba wangapi wamechukuwa ajira nchini Tanzania lakini bado tunatatizo kubwa la Takwimu" |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.