Thamsanqa Dyanty (kulia) akitoa utafsiri ya hotuba ya rais wa Marekani Barack Obama kwa walemavu wa usikivu wakati wa ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Nelson Mandela siku ya jumanne. |
Tizama utofauti wa utafsiri wa Thamsanqa Dyanty na utafsiri wa binti anayeonekana katika picha ndogo. |
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa. Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kulikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.