ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 14, 2015

MTEMVU ACHANGIA KIKUNDI CHA SANAA TSH. MILIONI 3

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas  Mtemvu achangia Kikundi  cha Sanaa cha K & S Alt Vision cha Temeke Jijini Dar es Salaam,  Pesa Taslim Tsh. Milion 3 (PICHA ZOTE NA KAMISI MUSSA)
Mtemvu akizungumza jambo na kikundi cha Sanaa na  Viongozi wao
Msemaji wa kikundi hicho, Saba Habibu akizungumza jambo kabla ya kupokea pesa hizo

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas  Mtemvu (kulia) akimkabidhi msemaji wa kikundi  cha Sanaa cha K & S Alt Vision cha Temeke Jijini Dar es Salaam,  Pesa Taslim Tsh. Milion 3,  Saba Habibu,  kwa maandalizi ya kuandaa Filamu inayoitwa Kwanini Rafiki Yangu? ambapo leo wanaanza safari kwenda  Mkoa wa Pwani Bagamoyo katika Kijiji cha Kaole ambapo wataweka kambi kwa ajili ya kazi hiyo, wa Pili kulia ni Diwa wa Kata ya Kilakala, Amiri Osama na watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kikundi hicho, Edwin Mgoli
Msemaji wa kikundi hicho, Saba Habibu akitoa shukurani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  kwa niaba ya kikundi hicho
Diwani wa Kata ya Kilakala Amiri Osama akitowa shukurani kwa niaba ya kikundi hichokwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu Dar es Salaam.
Mtemvu katika Picha ya pamoja na Kikundi cha Sanaa cha K& S Alt Vision.

MSEMAJI wa kikundi hicho akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho cha Sanaa cha K& S Alt vision  mara baada ya kupokea Pesa Tsh. Milioni 3 toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke,
 Abbas Mtemvu, Saba Habibu, alisema anamshukuru Mtemvu kwa moyo wakujitolea

 Mtemvu anamoyo wa dhati na ukizingatia amepita katika kipindi kigumu cha mpito hakuweza kuwaangusha kwakuwa na msimamo wa kuwasaidia, aliendelea kusema  Saba Habibu, 

Mtemvu alikuwa akimsihi msemaji huyo kama mwanaye wa kumzaa kwamba ahadi yake ataitimiza kama alivyo itowa kwa kundi lake ipo palepale haijalishi popoteatapokuwa ataitowa kwa kukamilisha ahadi yake kwani aliitowa kwa ridhaa yake na moyo wake yeye kama yeye atawasaidia,

 kauli hiyo iliendelea kunipa faraja  msemaji wa kikundi hicho Saba Habibu alisema na akiendelea kusema, hata hivyo anawashukuru Wasanii wenzake kwa kumuamini wakati alipokuwa akifanya mawasiliano na Mtemvu. msemaji huyo alisema,
tumeomba na tumefarijika kwa msaada huu na tunamuahidi hatutomuangusha kwa kile tulichokiomba tutakifanyia kazi kwa nguvu zao zote na kwauadilifu mkubwana kwa unyenyekevu mkubwa hadi kufikia malengo yao na mwisho akasema Mungu awaongoze.

Diwani wa Kata ya Kikalaka, 
akizungumza kwa kumpongeza kwa moyo wake anao endelea nao kwa kusaidia vikundi vingi na haijawahi tokea kwa Mbunge mwenyekusaidia vikundi vingi kama mwenzetu, rafikiyetu, kaka yetu, ambaye amesaidia Vikundi vingi na vijana wengi kwa kuwasaidia kwa hali na mali na kuwa begakwabega na kumtia moyo na kumuombea Dua kwa mwenyeezi mungu ili aweze kuwasaidia vijana wa temeke

Diwani huyo akasema, waswahili husema  kutowa ni moyo wala si utajiri na wala si tajiri sana bali nikuwa na moyo kuwasaidia vijana wetu wa Jimbo la Temeke, 

Hivyo tuzidi muombea Dua kwa mwenyeezi Mungu ampe maisha marefu na mungu amjalie aweze pata riziki na maisha mema na tutaendelea kumkumbuka daima dumu. (Amin) 

ILIVYOKUWA MECHI YA TAIFA STARS NA ALGERIA LEO 14 NOV 2015


Mambo Ya Samatta Uwanjani

Mambo ya Samatta sio ya kitoto licha ya mpira kuwa wa moto kwelikweli kwa timu zote mbili za Taifa stars na timu ya Algeria.

Stars 1 Algeria 0 DakikaYa 43

Mgagaa na upwa hali wali mkavu bwana, baada ya dakika kadhaa za utulivu Tanzania inajipatia goli la kwanza kupitia mchezaji Mwinyi Haji katika dakika ya 43;

Stars 2 Algeria 0

Mbwana Samatta wacha kabisa habari yake, hebu ona alivyokuwa akipiga mpira kwa kujiamini mwishoe aipatia Tanzania goli la 2;

Stars, Algeria Watoka Draw

Na dakika 90 za kandanda zimefikia ukingoni huku timu zote zikiwa na mabao sare ya 2 kwa 2;

Algeria 2 Stars 2

Huku ni kukosa bahati kwa mechi ya leo au? Angalia hali ilivyo dimbani kipindi cha kwanza. Hebu toa tathmini yako binafsi.

Friday, November 13, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI

1 na 1B:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko. Picha na OMR

2:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

3:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. Picha na OMR

4:- Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu. Picha na OMR

5 na 5B:- Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

6:- Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.

7:- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

8:- Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

11:- Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

12:- Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Kimara, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

13:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 13, 2015. Picha na OMR

UZINDUZI WA USHIRIKA WA MAMA NA BABA LISHE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA.

Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya Ya Mama na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Said Said (wa pili toka kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam. 

Lengo la jumuiya hiyo kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali, kutoa fursa kulinda haki za ajira na kuzitafutia ufumbuzi na kuondoa tatizo la ajira kupitia tasnia hii ikiwa ni kumtambua mama na baba lishe kama sehemu ya maisha ya kila mmoja wetu, kwani kila mtanzania anaufahamu umuhimu wa mama na baba lishe na takwimu zinaonyesha asilimia 50% ya wanzania waishio mijini hupata huduma ya chakula. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Mhonzu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Mama Lishe wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Waaandishi wa habari wakufuatia mkutano huo.

KWANINI WASANII TOKA ARUSHA WAMEITEKA HIP HOP KWA SASA NA SI MWANZA...?

LEO JEMBE FM ndani ya kipindi cha HIT ZONE imekutanisha Rock City Finest Hip hop artists and R&B Singer ....Koyo MC, Mirror wa Ryhmes, Biznea na Alvix.... Hosted by 93.7 presenters @MbabaVc @Nattyebrandy na @ChrissTheDj

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA KUWATAKA KUBUNI MIRADI MBALIMBALI YA KUONGEZA MAPATO NDANI YA JESHI HILO.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo (Kushoto), akisalimiana na Maofisa  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Braiton Manyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, taarifa ya ujenzi la Jengo laa  linalotarajiwa kuwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizoko TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza  na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizopo TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wa tatu kutoka kulia waliokaa),akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea makao Makuu ya Jeshi hilo na Ofisi zilizopo Tazara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).


Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya  Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI,WASIMAMISHWA KAZI NI BAADA YA KUKWAPUA ZAIDI YA MILIONI 70

Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani) .
Baadhi ya iongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.
Wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame .
Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.
Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame ,Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi.
Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha  mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.

VODACOM YAPELEKA SOMO LA ICT SHULE ZA SEKONDARI VIJIJINI.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Vodacom,Tanzania wakiwa katika ofisi za Mkuu wa Shue ya Sekondari Shimbwe iliyopo kata ya Uru wilayani Moshi vijijini ambako walifika kwa ajili ya kujionea uwekwaji wa programu za kujifunzia katika Kompyuta mpakato zilizotolewa shuleni hapo na Vodacom.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali na Learning In sync Tanzania,Lisa Wolker akitoa maelezo kwa Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini Henry Tzamburakisi kuhusiana na Programu maalumu zilizowekwa katika Kompyuta mpakato zilizotolewa na odacom.
Wafanyakazi wa Vodacom,Kana ya Kaskazini wakisikiliza kwa makini maelezo ya Lisa Wolker (hayupo pichani).
Baadhi ya Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kama msaada wa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini ,Henry Tzamburakisi akizungumza jambo na mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine alipotembelea darasa la Kompyuta shuleni hapo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Learning Insync  akijaribu kuunganisha nyaya katika darasa la kompyuta lilopo shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakisi (kushoto) akiwa katika darasa la Kompyuta katika shule ya Shimbwe Sekondari ,wengine ni baadhi ya walimu katika shule hiyo ambao wamepatiwa mafunzo ya kompyuta.
Lisa Wolker akitoa maelekezo kwa walimu na wanafunzi.
Walimu na wanafunzi katika shule hiyo wakisikiliza kwa makini.
Mafunzo juu ya matumizi ya Programu maalumu ya kufundishia na kujifunzia yakiendelea katika darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Shimbwe.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Tzamburakisi akielekeza jambo kwa wananfunzi.
Jumla ya Kompyuta 30 zimetolewa na Vodacom kupitia mfuko wa Vodacom Foundation kwa shule ya sekondari Shimbwe ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa wataalamu wanao toa mafunzo ya matumizi ya Programu maalumu za kufundishia katika shule hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.