ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 19, 2018

MBELE YA MAGUFULI, KASEJA AKWAMISHA NJOZI ZA SIMBA KUCHUKUWA UBINGWA BILA KUFUNGWA

Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiinua Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu kabla ya kumkabidhi Nahodha wa Simba SC, John Bocco (wa pili kulia) 

RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI SIMBA KOMBE BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA KAGERA SUGAR…AWAAMBIA; “KABORESHENI KIWANGO CHENU…KIMATAIFA BADO”


Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, John Pombe Joseph Magufuli amewakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC wakitoka kufungwa 1-0 na Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


Na kabla ya kuwakabidhi Kombe hilo, Rais Magufuli akawaambia Simba SC hajaridhishwa na kiwango cha mchezo wao na akawataka wakakiboreshe kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewapongeza Simb SC kwa kufikia kutwaa la ubingwa wa Ligi Kuu bila ya kupoteza mechi kabla ya kufungwa na Kagera leo.

Rais Dk. John Magufuli akimkabidhi Kombe Nahodha wa Simba SC, John Bocco leo 

Wachezaji wa Simba SC wakifurahia na Kombe lao ubiongwa wa Ligi Kuu

“Mimi huwa ninafuatilia ligi mbalimbali, nilifuatilia hadi juzi timu ambazo zilikuwa zimechukua ubingwa bila kufungwa, zilikuwa zimebaki mbili, Barcelona na Simba, Jumapili iliyopita Barcelona wakafungwa na leo Simba nao wamefungwa,”alisema Rais Dk. Magufuli kabla ya kuwakabidhi Kombe hilo Simba SC.

Rais amesema kwamba anawapongeza Simba SC kwa sababu pia wamepitia kipindi kirefu bila kuchukua ubingwa na akasema anazipongeza na timu nyingine zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu huku akiwatania SImba; “Nashukuru hakuna timu iliyokwenda FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) kudai pointi za mezani msimu huu,”.

Aidha, Rais Magufuli aliyewapongeza Kagera Sugar kwa kuonyesha mchezo mzuri leo pia alisema Simba SC nayo ilijitahidi na kudhihirisha wao ni mabingwa.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa Florentina Zablon wa Dodoma aliyesaidiwa na Jesse Erasmo wa Morogoro na Mashaka Mwandile wa Mbeya, bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Edward Christopher Shijja kwa kichwa dakika ya 84 akimalizia krosi ya Japhet Makalai kutoka upande wa kulia.

Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi akapoteza nafasi ya kuisawazishia Simba SC dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida kufuatia mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Juma Kaseja.

Florentina Zablon aliwapa Simba penalti hiyo baada ya Okwi mwenyewe kuangushwa na kiungo mkongwe wa Kagera Sugar, George Kavilla.

Simba SC inabaki na pointi zake 68 baada ya kucheza mechi 29 na itakwenda mjini Songea kukamilisha msimu kwa kumenyana na wenyeji Maji Maji Mei 28 Uwanja wa Maji Maji. Kagera Sugar inafikisha pointi 34 katika mechi ya 29, ingawa wanabaki nafasi ya 10.

Kikosi cha SimbaSC kilikuwa; Said Mohamed Nduda, Nicholas Gyan/Muzamil Yassin dk46, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, James Kotei/Salim Mbonde dk50/John Bocco dk70, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, John Bocco, Shiza Kichuya,

Kagera; Juma Kaseja, Suleiman Mangoma, Abdallah Mguhi, Juma Nyoso, Mohamed Fakhi, Peter Mwalyanzi, Japhet Makalai, Ally Ramadhani/George Kavilla dk58, Japhery Kibaya/Paul Ngalyoma dk79, Edward Christopher, Atupele Jackson/Omar Daga dk32.

PICHA ZOTE NA BINZUBEIR

MWANZO MWISHO WERRASON JUU YA JUKWAA NCHINI KENYA [ KOROGA FESTIVAL]GSENGOtV
Werrason gave a high energy performance at Two Rivers Mall during the 22nd edition of Koroga Festival.
Here is footage from the event.

CONTE ASEMA UTATA ULIOJITOKEZA KATI YAKE DHIDI YA JOSE MOURINHO NI MATUKIO YALIYOPITA.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema atamsalimia Jose Mourinho kwa mkono watakapokutana Chelsea wakikabiliana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley leo Jumamosi.

Mameneja hao wawili wamekuwa na uhasama kila klabu zao zinapokabiliana Ligi ya Premia.

Lakini jana Ijumaa, Conte alisema: "Kesho, nitamsalimia kwa mkono na sote wawili tutafikiria kuhusu mechi."

"Si muhimu yale yaliyopita awali. Kuna uhusiano wa kawaida kati yangu naye."

Uhasama kati ya wawili hao ulianza Oktoba 2016, msimu wa kwanza wa Conte ligi kuu England pale Mwitaliano huyo alimpomshambulia Mourinho akisherehekea baada ya Chelsea kuwalaza United 4-0.

januari, Conte alimweleza Mreno huyo kama "mwanamume mdogo" baada ya kurushiana maneno kupitia vyombo vya habari.

Conte anatarajiwa na wengi kuondoka Chelsea majira ya joto na alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, aliwachezea wanahabari na kusema: "Ninaweza kusema kwa kweli kwamba mechi hii itakuwa yangu ya mwisho, msimu huu.

"Kwangu na wachezaji, itakuwa mechi yetu ya mwisho. Kisha, kama mjuavyo vyema sana, nina mkataba na nimejitolea kwa klabu hii."

Mourinho alikataa kuzungumzia mustakabali wa Conte akisema: "Hadi iwe rasmi kwamba Antonio ameondoka, sijui. Kwa kweli, mkiniuliza kama nafuatilia hili - ni hamu tu ya kutaka kujua.
"Kuhusu mechi ya kesho (Jumamosi), iwapo itakuwa mechi yake ya mwisho au la, sifikiri hilo litabadilisha mtazamo wake kwa mechi hii na hamu yake ya kutaka kushinda."

Mourinho alipoulizwa kuhusu heshima kati yake na mashabiki wa Chelsea, alisema: "Kitu pekee ninaweza kusema kuhusu mashabiki wa Chelsea ni kwmaba tangu siku yangu ya kwanza 2004 hadi siku ya mwisho nilipofutwa miaka kadha iliyopita, waliniunga mkono kikamilifu," alisema Mourinho, 55, aliyeshinda vikombe vinane akiwa Stamford Bridge.
"Waliniunga mkono kila siku. Waliniunga mkono kila mechi, waliniunga mkono haa siku nilipofutwa - mara mbili, moja 2008 na miaka kadha iliyopita.

"Hilo sitalisahau kamwe kwa sababu walifanya kile ambacho ninaamini mashabiki wazuri hufanya, ambacho ni kumuunga mkono meneja wao hadi siku ya mwisho.
"Kuhusu mashabiki wa Chelsea, hilo sisahau: walikuwa wazuri sana."

Mourinho ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi Chelsea baada ya kushinda mataji matatu vipindi viwili alivyokuwa Stamford Bridge mwaka 2005, 2006 na 2015.

KIAPO CHA MAHARUSI | ROYAL WEDDING: HARRY AND MEGHAN EXCHANGE VOWS

   GSENGOtv  
Imekusongezea matukio yaliyojiri sanjari na yale yaliyojiri hii leo kwenye harusi ya mjukuu wa himaya ya Malkia Elizabeth. 

Katika harusi hiyo maandalizi muhimu yote yalifanywa na kukamilika mapemaa, ulinzi ukizingatiwa kila sekunde kwaajili ya kuhudumia wageni takribani 2500 waliodhuru jijini London kushiriki shughuli hiyo wakiwemo marafiki wa karibu wa Meghan kutoka nchini Marekani na Canada, pamoja na askari na marafiki wa karibu wa Harry .

Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.

Wawili hao walifunganishwa katika ndoa mbele ya Malkia na wageni 600 waliokuwemo ndani ya kanisa la St George, katika Windsor Castle.

Bi Markle alikuwa amevalia vazi la harusi lililoshonwa na fundi mbunifu wa mitindo Mwingereza Clare Waight Keller.

Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.

Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.
George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.

Mwanamfalme Harry na Meghan Markle baadaye walipitia kwenye mji wa Windsor kwa msafara kwa kutumia kigari maalum cha kuvutwa na farasi.

Harry, ndiye aliyeyemsindikiza Bi Markel kwenda kwenye madhabahu baada ya babake Thomas kushindwa kuhudhuria harusi hiyo kutokana na sababu za kiafya.

Mkesha wa harusi, Mwanamfalme Harry, 33, aliambia umati wa watu Windsor kwamba anajihisi "mtulivu" na kwamba Bi Markle, 36, anajihisi "vyema sana".

Katika kiapo chake cha ndoa, Bi Markle hakuahidi "kumtii" mume wake. Mwanamfalme Harry ameamua kuwa na pete ya ndoa.

Wageni 600 walifuatilia harusi hiyo, ambayo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, katika kanisa la St George.

Umati wa watu wakiungana na waandishi wa habari kutoka maeneo mengi duniani wamlikusanyika Windsor kwa sherehe hii kubwa.

Inakadiriwa kwamba watu hadi 100,000 walikuwa kwenye barabara za mji huo.
Watu wa kawaida 1,200, wengi ambao wametambuliwa kwa juhudi zao za hisani katika jamii, walialikwa kuhudhuria harusi hiyo Windsor Castle.

Bi Markle alikuwa na mabinti 10 wapamba harusi na wavulana, wote wa chini ya miaka minane, wakiwemo Mwanamfalme George na Bintimfalme Charlotte.

Bi harusi alilakiwa na Mwanamfalme Charles, ambaye alimtembeza hadi kwenye madhabahu.

Wakati wa ibada, wawili hao walikula kiapo kila mmoja akijitoa kwa mwenzake na kusema: "kwa mema, kwa mabaya, kwa ujatajiri, kwa umaskini, kwa ugonjwa na kwa afya, kukupenda na kukuenzi, tangu kifo kitutenganishe."

Friday, May 18, 2018

HRW: WATU 15 WALIUAWA WAKATI WA KAMPENI ZA KURA YA MAONI BURUNDI; MATOKEO YA AWALI YATANGAZWA.


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kwa akali watu 15 waliuawa wakati wa kampeni za kura ya maoni ya kuifanyia marekebisho katiba huko nchini Burundi.
Ida Sawyer, Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika eneo la Afrika ya Kati amesema leo Ijumaa katika taarifa kuwa, wamenakili kesi 15 za mauaji wakati wa kampeni hizo, mbali na kesi sita za ubakaji.
Kadhalika shirika hilo la kutetea haki za binadamu limenakili kesi nane za watu kutekwa nyara wakati wa kampeni hizo. 
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, baadhi ya maafisa wa serikali walisikika hadharani wakitoa mwito wa 'kuhasiwa wafuasi wa upinzani' waliokuwa wakipinga kufanyika kura hiyo ya maoni.

Rais Nkurunziza akipiga kura jana Alkhamisi

Kura hiyo ya maoni ilifanyika jana Alkhamisi chini ya mazingira ya taharuki na wasi wasi, haswa baada ya kuenea habari za kushambuliwa wanaharakati wa upinzani waliokuwa wakipinga kufanyika zoezi hilo.
Matokeo ya kura hiyo ya maoni yanasubiriwa leo Ijumaa, na iwapo kwa uchache asilimia 50 ya wapiga kura wataunga mkono mabadiliko hayo ya katiba, watakuwa wamemsafishia njia Rais Pierre Nkurunziza ambaye amekuwako madarakani tokea mwaka 2005, kusalia uongozini hadi mwaka 2034.
Mwandishi wetu Hamida Issa ametuandalia ripoti maalumu kuhusu matokeo ya awali ya kura hiyo ya maoni.

JUSTINE BIBER NA 'MAVIPAJI' YAKE.Justin Bieber and Questlove Drum-Off

HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 150 ZILIZOKUWA ZIKIINGIA KWENYE MIFUKO YA WAJANJA KILA MWEZI


GSENGOtV

Baada ya kudhibiti mianya ya kupiga fedha, mchezo unaosemekana ulikuwa ukifanywa na baadhi ya wahudumu na viongozi wasio waaminifu, wakitafuna fedha za mapato ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, hatimaye hospitali hiyo imefanikiwa kukomboa zaidi ya shilingi milioni 150 kwenye makusanyo ya kila mwezi, fedha zilizokuwa zikiliwa na wajanja wachache.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella wakati akipokea msaada wa vitanda 40 na magodoro yake, uliotolewa na Exim Bank kama mwendelezo wa kampeni ya benki hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa jamii.

Kupitia ripoti ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Sekou Toure, Dr. Rutachunzibwa Thoma, aliyoipenyeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, inaonesha kwa sasa hospitali hiyo inakusanya wastani wa shilingi za Tanzania milioni 200, kwa mwezi ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa ikikusanya milioni 40 hadi 50 tu kwa mwezi.


 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Sekou Toure, Dr. Rutachunzibwa
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Watu na taaluma zao.
Benki ya Exim imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Hospitali hiyo ya Sekou Toure imekuwa ya kumi kupokea msaada baada ya Hospitali nyingine za mikoa mbalimbali hapa nchini kunufaika na mapango huo wenye lengo la kutoa vitanda na magodoro 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

BALOZI WA TANZANIA VATICAN USO KWA USO NA PAPA FRANCIS

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi jana Mei 17, 2018 aliwasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu, Papa Francis.
Balozi Possi pia anaiwakilisha Tanzania katika maeneo tisa ikiwemo mji wa Vatican.
Katika hafla hiyo, pia Dkt. Possi alikutana na Jumuiya ya Watanzania waishio mjini Vatican, ambapo aliwataka kutumia nafasi zao kuhakikisha Tanzania inadumu katika umoja na amani.

SERIKALI KUTOA MASHINE ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA WADOGO KUANZIA JULAI MOSI

Serikali imesema kuanzia Julai mosi mwaka huu, kupitia Mamlaka ya Mapato nchini- TRA itaanza kutoa mashine za risiti za kielektroniki-EFD kwa wafanyabiashara wadogo nchi nzima.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo aliyeishauri serikali kutoa mashine za EFD bure kwa wafanyabiashara wadogo.
“Tumeanza utaratibu wa kufikia wafanyabiashara wote, na hata kwanza mashine hizo hazikutolewa bure wafanyabiashara wakubwa walipewa kwa mkopo, kwa hivyo tuna mpango kupitia TRA ifikapo Julai 1, 2018 kutoa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogo,” amesema.
Amesema awamu hii serikali itaacha kutumia mawakala katika kugawa mashine hizo ili kuondoa mzigo wa bei kwa wafanyabiashara wadogo.
“TRA itaanza kutoa yenyewe mashine hizi na kuacha kutumia mawakala kitendo kilichoongeza gharama. TRA ikianza kutoa ghrama zitapungua,” amesema Dkt. Kijaji.

Thursday, May 17, 2018

MWANAMUZIKI WA SUPER KAMANYOLA ALIYETOKA KWA MUUMINI MWINJUMA AFUNGA NDOA

GSENGOtV
Saa kadhaa jumatano ya tarehe 16 May 2018 kabla ya kuingia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwanamuziki Aboubakari Mangegeka wa bendi ya Super Kamanyola yenye maskani yake Villa Park Resort jijini Mwanza amefunga ndoa na Bi. Swaumu.

Ndoa ya Kiislamu imefungwa Mji Mwema jijini hapa nao marafiki wengi wakihudhuria shughuli hiyo licha ya wengi kupewa taarifa za kama vile surprise.

Mangegeka aliye na ulemavu wa kuona na mwenye kipaji cha uimbaji ambaye awali kabla ya kujiunga na bendi hiyo alikuwa akifanya kazi na bendi ya Muunini Mwinjuma Double M Sound, anadai moja kati ya vitu vilivyomvutia kwa Bi. Swaumu na hata kuamua kumuoa ni sauti ya mvuto aliyonayo binti huyo, vingine siri yake mazee.  
WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AZINDUA COPA UMISSETA MJINI BUKOBA

 Waziri Mwakyembe akigawa vifaa vilivyotolewa na Coca-Cola kwa moja ya mwakilishi wa mmoja wa shule za sekondari.
 Waziri Mwakyembe akikagua moja ya timu wakati wa hafla ya uzinduzi.
 Wadau wa Umisseta katika picha ya pamoja na Waziri Mwakyembe.
 Waziri Mwakyembe akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo. Pembeni ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Said Kiganja.
 Waziri Mwakyembe akiongea na wanafunzi waliohudhuria.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhandisi Richard Ruyango akiongea wakati wa hafla hiyo.
Waziri Mwakyembe akipiga penati  kuashiria uzinduzi huo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta mjini Bukoba.

Akizindua mshindano hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema michezo ni burudani, inaleta undugu, umoja na upendo hivyo h aina budi kuienzi siku zote.

"Nawaomba vijana mpende michezo maana ni burudani na ilateta afya kwa watu wa rika zote, mkizingatia hivyo hakutakuwa na watu wenye magonjwa ya ajabu ajabu," amesema.

Mashindano hayo yalipambwa na shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Kaitaba na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa michezo na wanzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Said Kiganja.

Wednesday, May 16, 2018

YANGA SC YAGAWANA POINTI NA RAYON SPORT.


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imepata pointi ya kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya sare ya bila kufungana na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa Kundi D uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.


Kwa sare hiyo, Yanga inaendelea kushika mkia kwenye kundi hilo, nyuma U.S.M. Alger yenye pointi nne kileleni, Gor Mahia, Rayon pointi mbili kila moja baada ya mechi mbili za awali.


Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Angola, Helder Martins De Carvalho aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Ivanildo Meirelles De O Sanche Lopes na Wilson Valdmiro Ntyamba, kwa mara nyingine udhaifu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga uliiathiri timu.


Yanga ilikuwa inacheza vizuri kuanzia nyuma ikipitisha mashambulizi yake pembezoni mwa Yanga, lakini mipira  kila ilipofika mbele ilichukuliwa na wachezaji wa Rayon kwa urahisi.

Winga chipukizi, Yusuph Mhilu ameendelea kuonyesha ubora wake kikosini Yanga, lakini nafasi zote alizotengeza hazikutumiwa vizuri na mshambuliaji Mzambia Obery Chirwa.


Dakika ya 83 Chirwa alikosa bao la wazi baada ya kugongesha mwamba wa juu kufuatia kazi nzuri ya Mhilu na hapo hapo kocha Nsajigwa Shadrack akamtoa na kumuingiza majeruhi wa muda mrefu, Mrundi Amissi Joselyn Tambwe.


Mara mbili Rayon walitumbukiza mipira kwenye nyavu za Yanga, mara moja kila kipindi, lakini wakati walifanya hivyo kimakosa.


Kipindi cha kwanza mchezaji wa Rayon aliuchukua mpira uliotoka nje na kuutumbukiza nyavuni na kipindi cha pili mfungaji alikuwa amezidi. 


Ikumbukwe mechi ya kwanza Yanga ilianza vibaya kwa kufungwa mabao 4-0 Mei 6 na U.S.M. Alger Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers, Algeria wakati Rayon ililazimishwa sare ya 1-1 na Gor Mahia siku hiyo mjini Kigali.


Michuano ya Kombe la Shirikisho inasimama sasa kupisha Fainali za kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi na Yanga watakamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.


Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.


Timu mbili za juu kutoka kila kundi katika makundi yote manne, zitakutana katika hatua ya Robo Fainali na baadaye Nusu Fainali itakayozaa Fainali. 


Kikosi cha Yanga kilikuwa; Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko/Raphael Daudi dk66, Yusuph Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chirwa/Amissi Tambwe dk84, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk88.


Rayon Sport; Eric Ndayishimiye, Gabriel Mugabo, Thierry Manzi, Mutsinzi Yannick, Shassir Nahimana, Sadam Nyandwi, Ismaila Diarra/Christ Mbonsi dk73, Pierre Kwizera, Mugisha Francois na Manishimwe Djabel/Kevin Muhire dk57.

HAPA NDIPO NINAPOKETI NIWAPO JIJINI MWANZA.GSENGOtV
Upo msemo usemao 'Hujafika Mwanza kama hujafika Villa Park Resort' naam huu msemo unamaanisha kwani idadi kubwa ya wageni wanaofika jijini hapa imekuwa desturi pindi wanapo wauliza wenyeji wao sehemu gani kwaajili ya kujinafasi, kula na kuburudika jibu halikosi kutaja kiunga hiki cha burudani.

Sasa Villa Park Resort imefanyiwa ukarabati na kuwa na muonekano mpya wakisasa zaidi.

WAKANDARASI DAR WAUNGANA NA MAKONDA WAOKOA MABILIONI YA FEDHA ZA SERIKALI.

Zaidi ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali za Dar es salaam Bure kama sehemu ya kuunga mkono jitiada za Mkuu wa mkoa huo  Paul Makonda.

Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda kufanya ziara usiku na mchana na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo.

Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka  kwa Meneja wa TARURA Wilaya kwaajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo.

Aidha  Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo Bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya pesa za serikali.

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.

MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA VYA UPASUAJI KUTOKA UBALOZI WA KUWAIT.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI, zitaipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji wa Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI) jana tarehe 15 Mei, 2018.

“ Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru Mheshimiwa Balozi wewe binafsi na Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano ambao mnaendelea kuipatia Serikali yetu ya awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali za maendeleo lakini hasa hasa katika sekta ya afya” alishukuru Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alisema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo leo wamesaidia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo vitaiwezesha Taasisi kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Makamu wa Rais amlisema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa watakaopata huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi, kufikia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka zaidi.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile  amesema Tanzania iatendelea kuimarisha uhusiano na nchi ya Kuwait kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada haswa msaada inayohusu sekta ya afya.

Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem alisema kuwa Wananchi wa Kuwait wana mapenzi makubwa na Watanzania na kuahidi wataendelea kutoa msaada.

DAR ES SALAAM KUMEKUCHA, RAIS MAGUFULI ASHUSHA NEEMA.*

 Na Zephania Mandia wa G.sengo TV.

Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wameendelea kula Matunda ya serikali ya awamu ya tano baada ya Rais Dr. John Magufuli kutoa zaidi Shilingi Billion 250 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi Mkakati ya kuziwezesha Halmashauri za jiji hilo kujiendesha zenyewe ili kupunguza utegemezi wa fedha kutoka Serikali kuu. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema miongoni mwa miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mabasi ya Mikoani Mbezi Luis kitakachogharimu zaidi ya shilingi Billion 50 ambacho ujenzi wake utaanza Mwezi June na kuchukuwa miezi 18 kukamilika. 

RC Makonda amesema jengo hilo litakuwa na gorofa tano ambapo kituo hicho cha kisasa kitakuwa na uwezo wa kuchukuwa Mabasi 200 na Maegesho magari 300 (Underground parking) ambapo ndani kituo kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Hotel, Hostel, Shopping Mall,Maduka, Migahawa, sehemu za mapumziko, Kituo cha Polisi, Bustani, Bank, Vyoo vya kisasa pamoja na Ofisi za kampuni za Magari. Aidha RC Makonda amesema miradi mingine ni Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu litakalogharimu shilingi Billion 16, Kituo cha Mabasi Chamanzi Mkondogwa, Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti yenye thamani ya Billion 8.5 itakayokuwa na uwezo wa kuchinja Ng'ombe 1,000 kwa siku hali itakayoondoa uagizwaji wa Nyama Nje ya nchi kwaajili ya kuuzwa kwenye Hotel na Supermarket ambapo kukamikika kwa mradi huu utawezesha wazawa kupata soko la nyama la uhakika, Ujenzi wa Soko la Mburahati Billion Billion 2.7 kituo cha Daladala Tuangoma, Soko la Kibada Billion 14 pamoja na miradi mingine mingi ikiwemo Fukwe za Coco, Ujenzi wa Shopping Mall na miradi mingine lukuki inayofanywa na Rais Magufuli kwenye Mkoa wa Dar es salaam.

RC Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kwa dhamira njema ya kusaidia kutatua kero za wananchi ambapo amewasihi wananchi wa Dar es salaam kukaa mkao wa kula kwa kuchangamkia fursa za ajira zitakazotolewa kwenye miradi hiyo. 

HUU NI UPENDO WA DHATI WA RAIS MAGUFULI KWA  WANANCHI WAKE.